Wednesday, 27 March 2013

Re: [wanabidii] Dk. Slaa atajwa kumtuma Saanane kummaliza Zitto Kabwe

Taarifa kama hii imejaa utoto, upungufu wa kupangilia habari japo ya uwongo! Imejaa uswahili uswahili (umbea umbea vile, yaani mtu ambaye lazima aseme hata kama hana point), na inaonyesh tabia hasa ya source yenyewe/mtoa taarifa. Yaani Zitto Kabwe tunayemjua anusurike kifo cha sumu chenye ushahidi kama uliotajwa wa wazi wazi (kama muongo huyu anavyojaribu kufanya ionekane hivyo), halafu anyamaze kimya kwa mwaka mzima sasa?

Na gazeti nalo limekurupuka mno kuufanya uchafu huu kama habari. Limeonyesha upeo mdogo na kujikosesha thamani mbele ya wasomaji wake.

Kama siasa zemejaa upuuzi kiasi hiki, ni heri watu wapelekwe shule kwanza, wafundishwe na maadili ya mila na dini zao kabla hawajaruhusiwa kuwa ktk jukwaa lolote la kuwapa fursa ya kutapika hivi mbele ya watu wazima wenye akili zao!

AIBU!


Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Airtel Tanzania.

-----Original Message-----
From: Telesphor Magobe <tmagobe@gmail.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Wed, 27 Mar 2013 13:29:16
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Reply-To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Dk. Slaa atajwa kumtuma Saanane kummaliza Zitto Kabwe

Jambo hili ni la jinai na Mtanzania na wale waliokubali kuwa kulikuwa
na kitu kama "unga unga" (sumu na naamini huyo alieyepewa na kukubali
kwenda kumdhuru Zitto na yule aliyempa - wote ni watuhumiwa wa kutaka
kumdhuru Zitto). Kama kweli serikali yetu ina vyombo vya usalama
makini jambo hili lingechunguzwa na wataobainika wachukuliwe hatua. Na
kama si kweli, basi serikali ichukue hatua kali kwa gazeti husika kwa
kuzusha mambo ambayo yanaleta uhasama, chuki na kulipiza kisasi katika
jamii. Kama siyo kweli, hii inaonesha tu uwezo na namna ya habari
vyombo vyetu vya habari vinaweza kuandika maana "nyoka huuma
afikiapo!"

On 3/27/13, rwechungura_nestory@yahoo.com <rwechungura_nestory@yahoo.com> wrote:
> Ndugu zangu haya yamezoeleka. Tukio limepitisha mwaka na ni la hatari. Iweje
> litolewe sasa na watu ambao tayari wamefukuzwa kwenye chama na kuhamia chama
> adui. Swali kwa nini sasa hivi na sio wakati hule? Na taarifa zinaonekana
> kuchukuliwa kimzaamzaa. Nitakuwa mgumu kuamini habari hizi ukitilia maanani
> chanzo chake. Naendelea kulijenga taifa langu.
> Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Airtel Tanzania.
>
> -----Original Message-----
> From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
> Sender: wanabidii@googlegroups.com
> Date: Tue, 26 Mar 2013 23:52:35
> To: Wanabidii<wanabidii@googlegroups.com>
> Reply-To: wanabidii@googlegroups.com
> Subject: [wanabidii] Dk. Slaa atajwa kumtuma Saanane kummaliza Zitto Kabwe
>
> *Yadaiwa ilipangwa anyweshwe sumu hotelini
> *Dk. Slaa atajwa kumtuma Saanane kummaliza
> *Mwenyewe akanusha, asema ni siasa chafu
>
> TISHIO la kuuawa kwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na
> Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe, sasa limechukua sura mpya, baada ya
> kuibuika kwa madai mapya kuwa Bosi wake, Dk. Willbrod Slaa, alipanga
> njama za kumuangamiza, MTANZANIA Jumatano linaripoti.
>
> Duru za habari zinaeleza kuwa Zitto, ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma
> Kaskazini na Naibu Kiongozi wa Upinzani bungeni, anadaiwa alitaka
> kuuawa kwa sumu na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Slaa, ambaye
> alimtumia kada na Mjumbe wa Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA), Ben
> Saanane, kutekeleza mpango huo.
>
> Habari zinadai kuwa tukio hilo lilipangwa kutekelezwa Mei mwaka jana,
> katika Hoteli ya Lunch Time, iliyoko Mabibo External, jijini Dar es
> Salaam.
>
> Kwamba Zitto alilengwa kuuawa kwa kuwekewa sumu kwenye kinywaji chake
> wakati akiwa kwenye mazungumzo na baadhi ya makada vijana wa chama
> hicho katika Hoteli ya Lunch Time.
>
> Mmoja wa watu waliokuwa katika tukio hilo amelieleza MTANZANIA
> Jumatano kuwa Zitto alinusurika baada ya aliyetumwa kumuwekea sumu
> hiyo kuidondosha na hivyo kuonekana kwa watu waliokuwa eneo hilo.
>
> Anamtaja mtu aliyetumwa kumuua Zitto kuwa ni Ben Saanane, ambaye
> aliangusha karatasi ya nailoni iliyokuwa na ungaunga unaosadikiwa kuwa
> sumu na kuonekana kwa watu waliokuwa eneo hilo, akiwemo Zitto mwenyewe
> pamoja na aliyekuwa Naibu Mwenyekiti wa Bavicha, Juliana Shonza na
> Mtela Mwampamba.
>
> Akizungumza na MTANZANIA Jumatano, Shonza alikiri kutokea kwa tukio
> hilo kwa kueleza kuwa yeye na Mwampamba walihoji kilichokuwa ndani ya
> nailoni ile, ambacho kilionekana wazi kuwa ni unga unga ni nini,
> ambapo Saanane alikiri kuwa ilikuwa sumu ambayo alipewa na Dk. Slaa,
> ili amuwekee Zitto.
>
> Shonza alidai kuwa siku ya tukio, yeye na Zitto walikuwa wamekaa meza
> moja na Saanane ambaye mkono wake wa kushoto ulikuwa umefungwa bandeji
> aliyowaeleza kuwa aliifunga kutokana na maumivu ya mkono.
>
> Alisema wakiwa katika maongezi, huku Saanane akionyesha kuzidiwa na
> kilevi alichokuwa amekunywa, alitoa bahasha ya kaki yenye fedha ili
> alipie gharama za vinywaji vya wote ambayo ilidondoka na ndani yake
> ikatoka karatasi ndogo ya nailoni ikiwa na unga mwekundu.
>
> Kwa mujibu wa Shonza, Saanane alipobanwa aeleze unga ule ulikuwa nini,
> awali alidai ni kilevi aina ya kuberi, huku akiwataka wasiifungue
> nailoni hiyo, jambo ambalo Mwampamba alilikataa na kulazimisha
> ifunguliwe pale pale.
>
> "Kwa hasira Ben alitaka arudishiwe ile karatasi, lakini, Mwampamba
> aliondoka nayo, usiku huo huo Saanane alimtafuta Mwampamba hadi
> nyumbani kwake akidai apewe mzigo wake.
>
> "Mwampamba alimwambia atampa mzigo wake kwa sharti moja tu la kusema
> ukweli kuhusu kilichomo ndani ya nailoni hiyo na hapo ndipo Ben
> alipokiri kuwa alipewa mzigo huo ambao una unga unga wenye sumu na Dk.
> Slaa, ili amuwekee Zitto kwa sababu amekuwa akimsakama ndani ya vikao
> vya chama.
>
> "Huo ndiyo ukweli ambao nitausema popote, sasa kama Ben alitudanganya
> kwa kumsingizia Dk. Slaa hiyo ni juu yao wenyewe," alisema Shonza.
>
> Shonza alisema hali hiyo iliwaogofya na kuanza kuwa makini katika
> mapito yao na kuongeza kuwa Zitto bado yuko Chadema kwa sababu ana
> roho ngumu, mvumilivu na mkomavu wa kisiasa, anayeweza kukabiliana na
> mambo ya hatari.
>
> Dk. Slaa alipoulizwa na MTANZANIA Jumatano kuhusu madai hayo, alisema
> hilo ni kosa la jinai, ambalo kama anatuhumiwa kulifanya anapaswa
> kushtakiwa kwenye vyombo vya dola badala ya tarifa hizo kupelekwa
> katika vyombo vya habari.
>
> "Usipende kutumiwa na watu, lakini aliyekutuma anajua amekutuma kwa
> sababu gani. Sasa nitakujibu, hivi suala la kuua si ni jinai? Sasa
> suala la jinai linapelekwa kwenye vyombo vya dola au kwenye vyombo vya
> habari? Huyo aliyesema yuko Chadema au yuko wapi? Aliyesema hakwenda
> polisi? Aliyetaka kuuawa hakwenda pia? Sasa ninyi media mmekuwa nani?
>
> "Wa kumuuliza suala hili ni Saanane mwenyewe au Shonza, wangekuwa na
> nia njema wangekwenda polisi au Zitto mwenyewe angekwenda polisi
> kushitaki kwa kutaka kuuawa," alisema Dk. Slaa.
>
> Naye Saanane ambaye amefanya mahojiano na MTANZANIA Jumatano kuhusiana
> na mambo mbalimbali mabaya ambayo yamekuwa yakielekezwa kwake,
> akizungumzia madai hayo alisema madai hayo hayana ukweli wowote, bali
> yanaibuliwa sasa na mahasimu wake kisiasa kwa lengo la kutaka
> kumshusha baada ya majaribio mengi dhidi yake kushindwa.
>
> "Kwanza siku ambayo wanasema tulikuwa wote mimi sikuwa huko, nashangaa
> na haiingii akilini kwamba mimi niende hadi Temeke (kwa Mwampamba)
> tena usiku wa manane kwa ajili ya kufuata sumu ya kuulia panya.
>
> "Hizi ndizo siasa halisi za maji taka, kuliko nipange njama za kuua
> mtu kwa malengo ya kisiasa, ni bora niache siasa. Ni mwendawazimu
> pekee atakayeweza kuamini tetesi hizi za ovyo kabisa zinazofanywa na
> vijana walioshindwa kujenga hoja za maana kwenye majukwaa," alisema
> Saanane.
>
> Aliwaonya watu wanaohasimiana naye kisiasa kuacha kumchafua Dk. Slaa
> kwa kutumia jina lake katika mambo wanayomtuhumu, kwa kile alichoeleza
> kuwa ni dhambi kubwa kutunga uongo na kuusambaza ili kutafuta huruma
> ya umma wa Watanzania.
>
> "Nadhani lengo lao hapa ni kumchafua Dk. Slaa kwa tuhuma hizi za uongo
> zilizotolewa kwa mara ya kwanza na vijana waliotimuliwa Chadema kwa
> kukisaliti chama na baadaye kuhongwa na makada na viongozi wa CCM
> ambao wamejiunga nao sasa.
>
> "Sasa kwa tuhuma hizo, kwa nini wasiripoti polisi, inaingiaje akilini
> mtu kupanga njama kubwa kiasi hicho halafu ukae kimya tu," alisema
> Saanane.
>
> http://mtanzania.co.tz/index.php?option=com_content&view=article&id=6419:siri-ya-kuuawa-zitto-yafichuka&catid=25:siasa&Itemid=41
>
> --
> Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
> International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
>
> --
> Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
> International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
>
>

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment