Sunday 19 February 2017

Re: [wanabidii] Re: [Wanazuoni] Je ni kweli? Tanzanian Farmers Are Facing Heavy Prison Sentences If They Continue Their Traditional Seed Exchange

Mpita Njia-----Sote twapita tu hapa duniani. Ni mapito tu lakini kuna mateso. Na sasa huu ukamataji wa biashara haram, kipato cha kukaribisha wahamiaji haram, kuwabeba na kuwapitisha kwenda nchi jirani; ulimaji bangi kubanwa na mimea kuteketezwa na mbinu nyingine za kipato cha rahisi rahisi kubanwa; uhamiaji nchi za jirani na ulaya kuwa mgumu na ukiulazimisha unaishiwa kutendewa maovu ukiomba ubalozi ukuokoe-hiyo hakuna-kufa au nyongwa ulijitakia! Trump nae hatutaki tuache tupigane tuuane tutakuja kujijua na kushika adabu zetu-sote hatuna kudumu hapa duniani!

Kama Kawa ninachangia tena kusisitiza:
Vyuo vya kilimo vina vijiji vya mashamba ya mifano. Ukienda Mikumi kwa mfano nikijiji cha Msimba nikimojawapo. Juu milimani kijiji cha Vidunda na vinginevyo Kidodi ward ukielekea Ruaha-Kilombero Morogoro. Panda juu Vidunda milimani kuna mbuzi wakubwa toka Finland wa kutoa lita 3. Kuna nguruwe (haram) ambao wote hulishwa mashuduna vyakula walivyofundishwa kutengeneza. Ni Hivyo Msimba village unapoelekea Iringa kabla hujafika Ruaha Mbuyuni. Msimba wana kilimo cha mbegu za kisasa na kuzalisha mbegu za kuuza za hybrid na traditional irrigation system yao imeboreshwa. Wamefundishwa kubebesha miti ya matuna na kuwa na vitaru vya miti rafiki na mazingira miti ya kuuza kupata pesa.

Mbegu za muda mfupi za mahindi, mihogo zipo hata nami nimezijaribu DSM. Utaalamu wa grafting, budding miembe na miti mingine ya matunda upo na utaona miche hiyo mitaani vijana wanauza mfano miembe na ina kamba za kubebeshea na viandiko. Mingine huitoa vyuo vya kilimo na misitu hapa hapa bongoland wakaileta DSM kuuza kwa bei mbaya. Mtu ananunua mapaka mche wa maua kwa shs 50,000/=. Huyu atashindwa kumsaidia mzazi wake apate mbegu za kisasa za muda mfupi zinazoendana na mabadiliko ya hali ya hewa? Au amnunulie agro-chemicals na kumuelekeza matumizi yake. Wanapopewa dawa za kuoiga na kuelekezwa-bado matumizi ni mabaya vijijini walimako korosho, pamba, kahawa. Cancer zinaongezeka kutokana na kudharau maagizo ya matumizi ya dawa. Hata umuelekeze ubaya wa mercury-bado ataitumia mikono wazi badala ya kuvaa gloves na atatumia pia dawa use dilution ndogo kuvulia samaki au kuweka katika pombe ya gongo ili iwe kali wateja waifurahie!

Ukienda maduka ya mbegu utauliza ya muda mfupi ya mahindi au mpunga kwa majina kibao-Katumani, TMVI etc utanunua na atakupa maelekezo ipi inakufaa. Wacha wale opportunists wauzao hovyo mbegu na madawa vijijini bila ufahamu, yapo maduka unapewa maelekezo. Ila utapeli wa wauzaji kudanganya watu ili apate pesa upo. Ukimwambia unataka mwembe bolibo au dodo wa muda mfupi atakwambia huu hapa, ukimcheki tena umwambvie ninataka aina hii utaona anakuonyesha pale pale. Wauza mbegu nao hununua zilizopita muda kwa bei poa kuibia wenzao au raia.

Katika masoko ya nchi hii hata DSm pia utakuta na utapata mtama wa kienyeji na mtama wa kisasa wa muda mfupi na utaona ulivyo unapishana sura. Kuna ngano, soya, maharage ya kisasa na ya zamani yana mwonekano tofauti. Tatizo katika mazao sasa pamoja na miti ya matunda ni ugonjwa wa ukungu na matumizi mabaya ya agro-chemicals ambazo nazo wauzaji huuzia wakulima zilizo expire. tatizo kuu ni la wakulima wetu kukataa kubadilika. Ila kikiwa kwako kimemea vizuri waje kuiba au kuomba au kununua kwa gharama. Unaweza ukakuta mtu ana eneo kubwa la kilimo au la anapoishi lakini kutwa yupo amekaa barazani hafanyi lolote na kila alacho inabidi anunue. Nyumba yake wazi haina hata mti wa matunda lakini daili anakula embe, pera, zambarau na kokwa anatupa jalalani. Akiona maembe kwa jirani-ni kuomba tu au kuiba! hawa unawafanya nini? Lazimisha kila nyumba iwe na miti ya kuni na ya matunda na kagua kuwa anayo ili tupunguze Unyumbu, afya duni na umasikini, mazingira kuwa mabaya!

Panda miembe ya muda mfupi kama utaila labda uwe na ukuta kuzuguka shamba. Maembe haya utayaona hata vijana wanakouza miche ya miti ya maua, matunda yameiva yana rangi mbalimbali. watakuja kuchuma shamba zima usikute kitu. Kama upo DSM na una miti hiyo watapita mpaka chini ya kalveti kuingia ndani ya ukuta kuiba kama hakuna mbwa wa kuwakimbiza. Tatizo ni kujitambua na kuzingatia kilimo cha kisasa kulingana na hali ya hewa na mazingira. Unapanda mahindi ya miezi 6 hupati kitu kila msimu kisha unalia njaa.

Wafugaji walikuwa wakinunua mahindi kwa kuuza mifugo. Baadae wakaona mifugo inakuwsha kwani boma huweza kutumia gunia moja la mahindi kwa wiki kwa kupika uji kunywa (na siku hizi wanapika ugali) kutokana na wingi wa watu. Kwa sasa wanalima wenyewe mahindi, maarage (gwara), mbaazi na mazao mengine. Danida funded NGOs zimesaidia kilimo ndani ya maeneo yao ya Loliondo, NCAA. Fika uone mashamba yalivyo Loliondo, Monduli, babati, Kiteto, Manyara-Terrat, Loiborsirret, Naberera etc. Kwa hiyo ulimbikizaji mifugo na kilimo cha plau na trekta na wenginge ndani ya NCAA wameweka wasukuma kama vibarua wa kuwalimia haviendani na wildlife conservation. Mahindi yanauzwa ktk magulio yao na pastoral council hutoa hela za mahindi wafugaji wauziwe kwa bei rahisi. Wahusika hununua mabovu kiufisadi. Hivyo wafugaji wafanya biashara wa kupeleka mahindi ndani ya vijiji ktk wildlife conservation areas wapo na wanaolima extensively ili wasiuze mifugo yao wapo. Kama mfugo mmoja ni laki 5 mpaka 8 ni gunia ngapi za mahindi? Mbuzi huuzwa zaidi kuliko ng'ombe. Kufuga kisasa inakuwa utata wafugaji ambao walikuwa hawalimi zamani sasa wanalima hivyo kuweka mifugo mingi pamoja na degradation iliyopo ndio tija na sifa kimila kwa socio-cultural status yako. Sasa tuwaache kulimbikiza na kuharibu ardhi na kunyima wanyamapori na livestock majani ya kula au tulazimishe usugaji endelevu kama sheria? Tuwape chakula cha bure cha msaada waendelee kulimbikiza mifugo na kuharibu ardhi na vyanzo vya maji au waachwe wafe ili wajifunze kuuza mifugo wanunue chakula au anayekufa njaa na mifugo anayo achukuliwe hatua? Kipi kinafaa-land use planning na sheria ukilima na kufuga sustainably au kuacha uholela na mapigano na land degradation na njaa.

Kama Mpare anaweza kulazimisha kilimo na ufugaji endelevu kwa kulazimisha na kurnganisha maeneo ya kilimo na ufugaji na mifugo michache ya nyumbani kwa maziwa; kulinda misitu ya miti ya kuhifadhi ardhi na maji; kulazimisha kilimo cha hybrid crops wakati wa kiangazi ambapo umwagiliaji maji hutumika; kulazimisha mixed cropping kwa kulinda ardhi na kulazimisha kama ardhi ikizeeka-uiache ifanye regeneration mpaka indicator plants ziote ndio kamati ya mila ya kilimo ikuruhusu ulime mazao; kulamizima ukate majani shambani upelekee mifugo nyumbani sio uingize mifugo shamba ni kwako. Ingiza ng'ombe shambani kwako ulipe ng'ombe! Kwa nini kiserikali tushindwe kulazimisha kilimo cha smaet agriculture na mabadiliko ya tabia nchi tunayaona. Mpare analazimisha mazao ya kuchanganya yaweje (ona picha ya mchanganyo Ndugu Irrigated farming area na picha ya ukaguzi wa indicator plants Kisiwani Barazani village mzee akionyesha kuwa sasa shamba tayari linaweza kulimwa uoto wa indicator plants za regenation tayari poa)-extension staff wa kilimo wanashindwa nini kushirikiana na kamati za mazingira, kilimo na ufugaji kulazimisha wananchi kuzingatia ulinzi wa mazingira, kilimo na ufugaji endelevu for food security and poverty alleviation?

watafiti wa kilimo na mifugo wamechoka kuelimisha watu wanafanya yao. Ukienda utawakuta wanapanda miche ya matunda wanauza, wanafuga ng'ombe kisasa wanauza maziwa. Wanafanya tafiti za mimea mpaka za madawa na baadhi kuanza kuuza dawa kutibu maradhi ya mifugo na binadamu. kila mmoja nje ya nyumba yake ya serikali aishipo ana banda la mifugo ya kisasa na analima anapata chakula cha kutosha, anatumia mbolea ya mifugo. Ukimwambia unamuhamisha atoke Ngerengere aende Naliendele Mtwara au Uyole Mbeya-atakuambia ninaacha kazi! Kwa sababu-alipopangiwa aliona anaonewa kuondoka Dar aende LMU Ngerengere. amefika hapo ahame tena na uchumi huo-NO way! Pia walimu wa shule za Msingi na Medical Doctors. Unamtoa Mjini Morogoro aende Kisanga Tarafa ya Mikumi ni mbali sana sana na mji ila kuna irrigation system. Huko utamkuta analima, kununua mazao ya wengine na kujaza lorry ndogo na kupeleka Mikumi Mjini, Morogoro, Chalinze account imejaa hela hategemei mshahara kiduchu wa halmashauri. Mwambie ahame-atakuambia anaavcha kazi tena bila mafao au ataomba kustaafu mapema kuliko kuhama.

Hakuna cha kufunga mtu hapa maneno tu bali waache wafe njaa! Ila tatizo la kuacha kutumia sheria watauza visichana viwe malaya kudandia malori, kujiuza siku ya gulio ili wapate hela (na ukimwi) kulisha familia na vibibi vinavyowalea! Wafugaji wataoza vichanga kupata mifugo zaidi badala ya kuiuza ili ng'ombe moja wa Parakuyo Maasai huko Chalinze au Ngerengere ampe gunia 13 za mahindi ambapo gunia moja ni 60,000/= ng'ombe ni laki 8. Atakula mahindi yake ya ng'ombe mmoja kwa miezi mitatu na kwa mwaka atauza ng'ombe 4 ili kuishi badala ya kuachia 500 kati ya elfu moja wafe kutokana na ukame bila ya kupata faida. Hivyo itabidi utumie mbinu ya sheria Mkulima apande kinachostahili kupandwa kwa faida yake mwenyewe na mfugaji atumie wise use of mifugo yake kwa maendeleo yake na atumie kinyesi shambani anakolima/kulimisha.

Ni kama unavyokamata mla madawa ya kulevya kwa faida yake na taifa! Zuia kilimo na ufugaji haribifu-kwa kutumia sheria. Lele mama na visingizio vya kijinga viishe. TZ kuna kila kitu na hakuna ambacho hakijafanyika kwa elimu na vitendo. tatizo ni continuity and sustainability and institutional memory which is lacking. Kila siku tunarudia yale yale na tulikotoka bila ya kukubali kujifunza kutoka makosa yetu. Tunajali tumboni street to, sifa, siasa za kujipinga daima ili kujikomoa na ubinafsi ambao ni donda sugu.

Tulalamike lakini tutakuja kuuona ukweli. Ni kama ilivyokuwa UDSM kilimo na mifugo kibao na ukataji miti watu wakitoka mbali kukata miti. Sasa angalia kilimo na uharibifu mazingira ulipopigwa marufuku-msitu umekua na kuna matangazo ya simba, chui kuonekana. pamoja na utata huu na ule vibaka kujificha-mazingira yameboreka. Na bado kama construction na environmental engineers watatumia wanafunzi wao kufanya mazoezi ya kuboresha miundo mbinu kwa kukarabati mifereji wazi na ngazi za zege zilizoporomoka; kuchimba boreholes za kupeleka maji juu ya majengo marefu na kusimamia upandaji wa miti ya matunda ya muda mfupi kwa kuwatumia Sokoine University-sio Chui tu wataongezeka, afya bora kwa watoto wa wafanyakazi kupata matunda, nyuki kupata chavua ya asali na kuboresha miti na vibaka kupata matunda ya kuiba kuongeza kipato. Sasa haoa Kazi tu. Asiyetaka kubadilika-Mwache Afe!!

Kama Kawa

--------------------------------------------
On Sun, 19/2/17, Mpita Njia <akihaule@gmai.com> wrote:

Subject: [wanabidii] Re: [Wanazuoni] Je ni kweli? Tanzanian Farmers Are Facing Heavy Prison Sentences If They Continue Their Traditional Seed Exchange
To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Cc: Wanazuoni@yahoogroups.com, khildegarda@yahoo.co.uk
Date: Sunday, 19 February, 2017, 23:29

Mbona hii
inatisha sana! Ni sheria ipi inayolitamka hilo? Watafiti
tusaidieni.   Hivi tunahitaji mbegu zenye masharti hayo?
Mchango wa vyuo vyetu vikuu vya kilimo katika hili upoje?
 Waliombwa ushauri ?
Tulipata maoni ya taasisi binafsi
zinazohusika na kutetea maslahi ya wakulima? Au nazo
ziliwekwa mifukoni ili kufunika kombe?

 
On Sunday, 19 February 2017 12:29:53
UTC+1, Hildegarda Kiwasila wrote:Wangechukuliwa hatua wakulima na
wafugaji-ningefurahi sana sana.

Namna fulani ya kukomesha  matumizi mabaya
ya ardhi, kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi
pamoja na njaa na maradhi  ifanyike kwa kutekeleza bylaws
za sheria kuu.



Unafika unaona milima na mitelemko lakini
mkulima analima milimani bila ya makinga maji. Matokeo
udongo huporomoka na mto kujaa mchanga maji kukauka.



Vyanzo vya maji kwa mifugo, binadamu na
wanyama pori kukosekana kutokana na kilimo hatarishi na
ufugaji kiholela usiozingatia ulinzi wa mazingira
yanayotegemewa na mifugo na binadamu. Kuweka SIASA mbele
nauroho wa hongo/rushwa badala ya kuzingatia misingi ya
maishana ya sekta husika ni tatizo kuu.  Tumetoka kwenye
conventional extension services tukaingia katika community
participation system ya Training and visit system katika
kilimo na ufugajikuwa na mpaka volunteers katika kilimo na
mifugo na sheria ndogondogo. Tukaja Shamba Darasa and big
results now. Mashamba na makundi ya shamba darasa kuanzia
jinsi ya kupanda, kutambua mbegu bora mpaka kuvuna. Kisha
kila linalofanywa ktk shamba darasa mtu anatakiwa afanye
kwake na anakaguliwa. wakiachiwa waendelee baada ya shamba
darasa na ukaguzi-wanarudia kule kule walikotoka. Community
forestry, Community-based natural resource management
systems, WMA kwenye wanyamapori with  benefit sharing
systems etc yote haya bure tu! Mijini nako mifumo shirikiki
ya SUDPF na  sasa CIUP yote bure tuu! Uchafu mitaa hiyo
ikishwa kuboreshwa kama kawa!



Agroforestry imefundishwa kuanzia enzi za
baba wa taifa-kilimo ni kazi, kazi ni uhai, mtu ni kazi,
panda mti kata mti! You name it. NGOs kama TCRS, CONCERN
wamesaidia masuala hayo ya kilemi endelevu na ufugaji kisasa
mbuzi, ng'ombe. Ikaanzishwa mpaka IPI- hapo UDSM
kutengeneza mashine ndogondogo za kutumika kukamulia mafuta
ya alizeti, matofari ya interlocking etc; Miradi donor
supported ya kutunza mazingira na catchment areas Danida
Iringa-Njombe -Makete na multi-donors Rukwa (RUDEP) pamoja
na kusaidia kilimo kwa lishe bora kupanda soya, maharage,
mahindi dwarf; TIRDEP-Tanga (GTZ) integrated projects.
Iringa Catchment office ilihusika ili kulinda Kihansi Dam,
Ruhudji, Wetlands za Kilombero kwa ajiri ya Rufiji River. Na
sasa ni River Basin Authorities zinahusika na kwa Project
yoyote EIA ni lazima. Vitaru vya miti vya kata na Katibu
Tarafa alipewa alipewa pikipiki kuhamasisha kilimo endelevu
na upandaji miti.

Milima ya Lushoto pamoja na huko Lushoto
toka zama hizo ni muhimu kwa kulisha nyanya, kabichi Dar na
misitu ilikuwepo toka ukoloni wa ujerumani kwa ajiri ya
mbao-utaona kilimo milimani bila ya makinga maji. Makinga
maji ni lazima milima ya Upare na wanapanga mpaka mawe na
kulima endelevu kimila ni lazima. ukipanda mazao
mchanganyiko wa mahindi na kunde ni must kilimo cha
mabondeni. Ukilima mahindi au mpunga wa miezi sita (6)
wakati wa kiangazi kilimo cha umwagiliaji-kamati ya mila
itang'oa!! unatakiwa upande ya muda mfuipi usimalize
maji. Ingiza mifugo shambani kwako ulipe mfugo! ina maana
unaharibu mazingira. kata mti usioruhusiwa kukatwa
upambuliwe kufidia uharibifu. Watachukua cha thamani kiuzwe
wagharimie mazingira. Kama mila inaweza kwa nini serikali
isiweze? inaachia wanalima ndani ya forest protected areas,
wanahamahama na mifugo kwenda watatako na kutia gharama
wengine. watu kulala nje mashambani kulinda yasiliwe na
mifugo!



Pumba tumbu-kiongozi na msomi unaporuhusu
maelfu ya mifugo eti hameni Mbeya nendeni Mkuranga, Kilwa,
Tunduru! Wakati maeneo yao watokako-wanalima, wanauza mazao
na kununua mifugo zaidi. Mmeshaharibu Mbeya hamieni
mkaharibu Mkuranga, Lindi na Tunduru! Mifugo hadi Bunju
kibao mashambani-Kulikoni? Anayeruhusu masuala haya
atumbuliwe! Vita ya wenyewe kwa wenyewe inakuja TZ
itakayosababisha na lack of land use planning vijijini na
kuzuia wakulima na wafugaji kuhama na kulima kokote watakako
na hasa wafugaji kuvamia na kulishia mazao ya wengine mifugo
yao. Wanatakiwa walime mahindi waweke gharani ili walishie
mifugo yao wakati wa ukame sio wanalima Loliondo, Monduli,
Mwanza  etc wanauza mpaka nchi jirani. USA wanalima mahindi
ya njano kwa mifugo wanakuja kutulisha sisi huku na
wakimbizi nchi za jirani na makambini nchini kwetu walipo.
Mfugaji alime mahindi ya kulishia mifugo yake na apande
nyasi za lishe zipo kibao au mifugo yake ipunguzwe kwa
lazima iuzwe kama vile mkulima anayelima isivyotakiwa
atakavyoadhibiwa ili kuondoa food insecurity. Ifike pia
kuwaambia wananchi na kuwapa muda wa kuboresha nyumba
zao-kwa amri! Nyumba ya miti inaweza kuwa bora sio ile isiyo
madirisha, choo na ina matundu wazi kibao nyoka anaweza
kuingia. House design za makabila mbalimbali zilizoboreshwa
za kienyeji zilisha kufanyiwa kazi na Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Makazi zipo Building Research Agency Mwenge.



Semi-arid area ng'ombe mmoja square
acre tano akiwa katika mazingira ya kienyeji. leo mtu anao
elfu 5+ hata 10 na analima hapo ktk maeneo ya kuchungia.
Wakipewa maeneo ya nyongeza na GVt-wanaongeza mifugo na
wengine toka mikoa mingine na nchi jirani kuhamia. Nchi
inakua jangwa. Mtu ana mifugo elfu 5 lakini hana nyumba
bnora, hasomeshi watoto ndio kwanza anaoza vichanga apate
mifugo zaidi. tupo tunawaangalia. Anaowakaribisha
kinyemela-wanamlipa ng'ombe-anaongeza mzigo wa
degradation. Pamoja na mifugo mingi-hawawezi kuchangia
kujenga huduma za maji yao na mifugo bali kuvamia vyanzo vya
maji ktk misitu ya hifadhi maji na ya wanyama pori.
Kisingizio ukame wakati tunausababisha. Hivyo basi-kamata
mifugo iliyoingia mtoni na misitu ya hifadhi-uza, mpe
zilizobaki baada ya kukata za uharibifu. Tulazimishe
sustainable farming and livestock keeping ili kuepuka
climate change effects na umasikini wa kujitakia.



Zama hizo Chalinze wakilima mtama na mihogo
ambayo ikichukua miezi 6 -mtama na mihogo 6+ kwa assa kuna
mtama dwarf na unajaa vizuri umejaza. Vile vile uwele na
ulezi ambayo Dodoma, Singida wanapanda pia na wanavuna
kichizi. Unakuta eti kwa sababu hapati pumba za kutengeneza
pombe na pure za kande akitwanga mahindi ya hybrid hayati
hizo yanasagika yote hivyo anapanda mahindi ya miezi 6 na
hapati kitu hata kutokana na ukame. Ujenzi wa nyumba mpaka
mabondeni walikokuwa wanalima zamani hivyo kwa assa wanalima
milimani au maeneo ya miinuko na bila uhifadhi ardhi na
hapati kitu. Kwa nini asilime mahindi ya muda mfupi?
Walifundishwa Singida na TCRS kilimo endelevu cha agro
forestry na mazao mchanganyiko na kupewa mashine za
kukamulia alizeti kupata mafuta na kuuza. makapi walishie
mifugo. daima tunaanza upya kila siku yale yale tunarudi
tulikotoka. Hata mihogo ya muda mfupi ipo na michungwa,
minazi. wao wanataka ya kienyeji kama mnazi wageme na Tembo
walewe kutwa. wakipewa mimea kama Choya kulima kuongeza damu
kama chakula, juice wao wanatumia Choya kupika gongo. Pamoja
na mbinu za shirikishi ktk sekta ya misitu, wanyamapori,
kilimo, maji na ulinzi wa miradi na mfumo wa maji kupitia
water User Associations, Uboreshaji na usimamizi wa
Mitaa/Vijiji kupitia decentralized systems-bado utata
unaendelea. Hata ukusanyaji na uzoaji takataka upo
decentralized-hela hufisadiwa. VICOBA, SACOSS-akaunt
hufungwa-ufisadi wa viongozi! Mtanzania umfanye nini?
Ukienda fisheries WWF na wengineo wamefitahidi misity na
bahari community participation na kuwahusisha ktk ulinzi wa
misitu, mikoko, mazalia ya samaki na misaada kibao na
vikundi vya ushirika vya wavuvi, ulinzi wa mazingira na
alternative income generation activities mpanga fish ponds
za mikokoni kando ya bahari-wanatiliana sumu kuuliana samaki
au hawaangalii fish ponds zao vizuri wanavua kiharam mpaka
ndani ya Marine Park. Kisha-tunaonewa! Ndani ya National
Park mifugo kibao! umetoka Monduli, manyara-Terrat na Mwanza
umejaza mifugo ndani ya Mashamba na National Park Mikumi.
Kule hata siku moja hulishii mifugo yako shambani. bibi wa
watu akifuguka mifugo isile-unamchapa, unambaka kumkomesha!



Kama unalima mazao ya muda mrefu na bila
kuzingatiwa kilimo cha hifadhi-ushughulikiwe. Extesion staff
muhusika asipozingatia watu wake katika kata, wilaya
wanazingatia kilimo na ufugaji endelevu-watumbuliwe. Kama
Maofisa ugani wakilazimishwa kwa sasa kwa sekta zote kuona
kuwa sera, mikakati, sheria za sekta zote
zinazingatiwa-Tanzania itaepuka athari mbaya za Mabadiliko
ya Tabia Nchi na Tutapeta kiuchumi, kijamii na kimazingira.
Haiwezekani tuachie watu walime na kufuga watakavyo. Hivi
sasa  mapigano yanayozuka nchini kwa kuruhusu watu kuzurura
na mifugo eti ukame; kukata misitu eti wanaganga njaa;
 pumba za kutoa leseni za kukata miti kuuza mbao na mkaa
bila ya mtu kuwa na shamba lake la miti; kuwaacha watu
wanalima kando ya mito na katika ktk vyanzo vya maji-waache
wapiga kura wetu; kuvamia na kulima ndani ya misitu
hifadhii; kupima viwanja vya nyumba ktk wetland; kuwapa
maeneo ya kulima au kuchunga wao wanajenga nyumba, lodges na
vilabu vya pombe ni kosa na Kansa ya kuleta umasikini na
maradhi makubwa. Kansa zinaongezeka kwa maji kuingia madawa
ya kilimo na ya mifugo iingiayo vyanzo vya maji. Njaa
inaongezeka na kuleta madhara kutokana na food insecurity
mtu analima mazao kila msitu ambayo yanachukua muda mrefu na
kuna mvua chache. ana mbolea kinyesi kinaleta
trachoma-hatumii kinyesi  kurutubisha shamba bali analima
hivyo hivyo na akipewa mbolea anaitumia kulima bangi. Pesa
apatazo kutoka bangi-hazionyeshi mabadiliko ya maisha
kijijini bali ni pombe, kuoa, zinaa-ukimwi!



Tupoje sisi-kufanya mazoezi kupunguza
mwili, kisukari na vitambi-Mpaka mh Kingagwala na Ummy
waseme na Mzee Mwinyi atangulie mbele kuonyesha mfano!
Kufagia na kuzoa taka-mpaka Rais Aseme na aongoze kufagia na
kuzoa takataka ndio wajumbe, madiwani, mbunge naye atokezee
kufagia. Haya assa ni kulima mazao yanayostahimili ukame
-Smart agriculture and sustainable livestock keeping iwe kwa
bakora. Easy Come Easy Go itakwisha lini kutegemea tupewe
,isaada na tuifisadi pia. Basi uza ng'ombe watatu upate
debe moja la mahindi au iache ife nawe ufe. Ukiingia kuuza
madawa ukikamatwa nchi za nje-Nyongwa unastahili! Hakuna
hela za ubalozi toka TZ za kukusaidia!! Wale wanaovamia
nyumba za viongozi vijijini na vituo vya polisi kutokana na
kushitakiwa au kutajwa wamefanya makosa wakikamatwa-nyonga!
Hakuna kuwalisha bure jela na akiwa jela afanyekazi za
kuzalisha mali sio kula kulala.



Ni hivyo katika ufugaji-vituo vya mifugo
kikanda. Unapeleka mfugo kupandikizwa mbegu bora au unawaita
kuja kwako kukupigia sindano na kupandikiza mbegu ya aina ya
mfugo utakayo. Majani ya lishe bora ya mifugo, ufugaji bora
wa kuku wa kienyeji na wakisasa. Mbuzi wakubwa wa kisasa wa
kutoa maziwa lita tano na jinsi ya kutengeneza chakula chao
wanafundishwa na ukitaka Livestock management unit inakuja
kwako kukufundisha uwe mfano kwa wengine-wewe hutaki. Kuwe
na Land Use Planning na iwe marufuku kuhamahama kwenda ardhi
si yako ama sivyo utatumbuliwa na kufirisiwa. Vita itazuka
kama tutaachia uvamizi wa ardhi na matumizi mabaya ya ardhi
yaendelee. Mipango matumizi ardhi izingatiwe. Hakuna
kubadili matumizi ardhi yaliyopangwa bila kibali. Huwezi
ukapewa eneo la kiwanda ukajenga lodges; eneo la kilimo
ukaweka yard ya magari na vilabu vya pombe la kufuga na
malisho ya mifugo unapewa former sisal estate land au
national park inakuwa de-gazetted ukaweka tented camps za
utalii. TUMBUA! BOMOA!!



Vyuo vya kilimo na ufugaji navyo
vitumbuliwe pale ambapo vipo lakini wananchi vijiji na mitaa
iliyozunguka chuo hiko wanalima na kufuga kizamani-kienyeji.
unaona jirani na chuo cha kilimo wananchi wanalima bila ya
makinga maji, hakuna nyasi za kuzuia mmomonyoko wala matuta
na miti hakuna. Nyumba jirani na chuo zipo uchi kabisa hata
miti ya kivuri hakuna lakini chuo kina miti mingi mizuri na
tree nurseries. Aibu! Kuwaje hata jirani na chuo kinachotoa
mainjinia wa mazingira mitaa na vijiji jirani na mito imejaa
taka ngumu, maji ya kinyesi kinachotiririshwa mtoni? wapi
tunafanyia practical training ya wanafunzi kama hata mita
100 kutoka chuo unaingia mtaani kwa wananchi uchafu
umezagaa. Una ranch ya mifugo ya kisasa lakii Kata hiyo
wafugaji wote wanafuga kizamani! Hivi tupoje sisi
watanzania? Halafu-eti serikali ndio haijali wananchi!
Lakini kulima bangi, kuuza na kuratibu usafirishaji wa
madawa ya kulevya tunaongoza na tukikamatwa-tunalalamika
pia! Tuna malengo gani hasa-kulalamika imekuwa culture.
Culture ya visasi nayo inapunguza  ari ya utekelezaji
sheria kwani muhusika anahofia usalama wake. Na ndio unakuta
hata extesion staff wanakaa mijini badala ya Katani na
vijijini kwa kuhofia kupigwa, kuchonwa, kubakwa na wavunja
sheria ambao hasa wanastahili kutumbuliwa. Tutafika? Ndio
maana mkoloni alitutandika bakora. Juhudi za baba wa taifa
nyingi sana na waliofuata hadi leo tupo pale pale. Hata ile
liberalization of the economy  local investors  wameitumia
vibaya kimagahamu kushika uchumi  imekuwa ndoto-wanauza
madawa na wakulima wadogo wanapanda bangi! What a mess!
Tubadilike- kubali kurekebishwa na  tukajirekebisha



Kama Kawa

Nipo-nimerudi

0755308198



------------------------------
--------------

On Sat, 18/2/17, Emmanuel Sulle esul...@gmail.com
[Wanazuoni] <Wana...@yahoogroups.com> wrote:



 Subject: [Wanazuoni] Je ni kweli?
Tanzanian Farmers Are Facing Heavy Prison Sentences If They
Continue Their Traditional Seed Exchange

 To: "Wanazuoni" <Wana...@yahoogroups.com>

 Date: Saturday, 18 February, 2017, 21:48

 

 

  

 

 

 

   

 

 

     

       

       

       Wakubwa nimesoma hii habari ni

 kama sijaamini vile! Naombeni mnisaidie.
Kama ni kweli basi

 akina yule Mkuu si hii ndiyo hoja ya
msingi kutengua hii

 sheria ya kikoloni jamani? Someni wenyewe

 Je ni kweli? Tanzanian Farmers Are

 Facing Heavy Prison Sentences If They
Continue Their

 Traditional Seed Exchange

 

 https://www.organicconsumers.
org/news/tanzanian-farmers- are-facing-heavy-prison-
sentences-if-they-continue- their-traditional-seed

 

 

 

     

     

 

     

     __._,_.___

 

           

   

 

 

     

     

 

     

         

         Posted by: Emmanuel Sulle
<esul...@gmail.com>

       

     

     

 

     

                         
 Reply

 via web post

                       •

             

                Reply to sender  
         

           •

             

               Reply to group    
       

           •

             Start a New

 Topic

           •

                           
 Messages in this

 topic

                 (1)

                       

 

         

 

             

         

             

         

             

             

                 Have you tried
the highest rated

 email app?

                 With 4.5 stars in
iTunes, the Yahoo Mail app is the

 highest rated email app on the market.
What are you waiting

 for? Now you can access all your inboxes
(Gmail, Outlook,

 AOL and more) in one place. Never delete
an email again with

 1000GB of free cloud storage.

             

         

               

     

     

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

     Visit Your Group

 

     

   

 

 

 

   

    • Privacy • Unsubscribe • Terms
of Use

 

 

 

 

 

 

   

 

 

   

   

   

 

 

 

     

 

 

 

 

     

 

   .

 

 

   

 

 

 

 

 __,_._,___

 

 

 

 #yiv3372610449 #yiv3372610449 --

   #yiv3372610449ygrp-mkp {

 border:1px solid
#d8d8d8;font-family:Arial; margin:10px

 0;padding:0 10px;}

 

 #yiv3372610449 #yiv3372610449ygrp-mkp hr
{

 border:1px solid #d8d8d8;}

 

 #yiv3372610449 #yiv3372610449ygrp-mkp
#yiv3372610449hd {

 color:#628c2a;font-size:85%;
font-weight:700;line-height: 122%;margin:10px

 0;}

 

 #yiv3372610449 #yiv3372610449ygrp-mkp
#yiv3372610449ads {

 margin-bottom:10px;}

 

 #yiv3372610449 #yiv3372610449ygrp-mkp
.yiv3372610449ad {

 padding:0 0;}

 

 #yiv3372610449 #yiv3372610449ygrp-mkp
.yiv3372610449ad p {

 margin:0;}

 

 #yiv3372610449 #yiv3372610449ygrp-mkp
.yiv3372610449ad a {

 color:#0000ff;text- decoration:none;}

 #yiv3372610449 #yiv3372610449ygrp-sponsor

 #yiv3372610449ygrp-lc {

 font-family:Arial;}

 

 #yiv3372610449 #yiv3372610449ygrp-sponsor

 #yiv3372610449ygrp-lc #yiv3372610449hd {

 margin:10px

 0px;font-weight:700;font-
size:78%;line-height:122%;}

 

 #yiv3372610449 #yiv3372610449ygrp-sponsor

 #yiv3372610449ygrp-lc .yiv3372610449ad {

 margin-bottom:10px;padding:0 0;}

 

 #yiv3372610449 #yiv3372610449actions {

 font-family:Verdana;font-
size:11px;padding:10px 0;}

 

 #yiv3372610449 #yiv3372610449activity {

 background-color:#e0ecee;
float:left;font-family: Verdana;font-size:10px;
padding:10px;}

 

 #yiv3372610449 #yiv3372610449activity
span {

 font-weight:700;}

 

 #yiv3372610449 #yiv3372610449activity
span:first-child {

 text-transform:uppercase;}

 

 #yiv3372610449 #yiv3372610449activity
span a {

 color:#5085b6;text- decoration:none;}

 

 #yiv3372610449 #yiv3372610449activity
span span {

 color:#ff7900;}

 

 #yiv3372610449 #yiv3372610449activity
span

 .yiv3372610449underline {

 text-decoration:underline;}

 

 #yiv3372610449 .yiv3372610449attach {

 clear:both;display:table;
font-family:Arial;font-size: 12px;padding:10px

 0;width:400px;}

 

 #yiv3372610449 .yiv3372610449attach div a
{

 text-decoration:none;}

 

 #yiv3372610449 .yiv3372610449attach img {

 border:none;padding-right: 5px;}

 

 #yiv3372610449 .yiv3372610449attach label
{

 display:block;margin-bottom: 5px;}

 

 #yiv3372610449 .yiv3372610449attach label
a {

 text-decoration:none;}

 

 #yiv3372610449 blockquote {

 margin:0 0 0 4px;}

 

 #yiv3372610449 .yiv3372610449bold {

 font-family:Arial;font-size:
13px;font-weight:700;}

 

 #yiv3372610449 .yiv3372610449bold a {

 text-decoration:none;}

 

 #yiv3372610449 dd.yiv3372610449last p a {

 font-family:Verdana;font- weight:700;}

 

 #yiv3372610449 dd.yiv3372610449last p
span {

 margin-right:10px;font-
family:Verdana;font-weight: 700;}

 

 #yiv3372610449 dd.yiv3372610449last p

 span.yiv3372610449yshortcuts {

 margin-right:0;}

 

 #yiv3372610449
div.yiv3372610449attach-table div div a {

 text-decoration:none;}

 

 #yiv3372610449
div.yiv3372610449attach-table {

 width:400px;}

 

 #yiv3372610449
div.yiv3372610449file-title a, #yiv3372610449

 div.yiv3372610449file-title a:active,
#yiv3372610449

 div.yiv3372610449file-title a:hover,
#yiv3372610449

 div.yiv3372610449file-title a:visited {

 text-decoration:none;}

 

 #yiv3372610449
div.yiv3372610449photo-title a,

 #yiv3372610449
div.yiv3372610449photo-title a:active,

 #yiv3372610449
div.yiv3372610449photo-title a:hover,

 #yiv3372610449
div.yiv3372610449photo-title a:visited {

 text-decoration:none;}

 

 #yiv3372610449
div#yiv3372610449ygrp-mlmsg

 #yiv3372610449ygrp-msg p a
span.yiv3372610449yshortcuts {

 font-family:Verdana;font-
size:10px;font-weight:normal;}

 

 #yiv3372610449 .yiv3372610449green {

 color:#628c2a;}

 

 #yiv3372610449 .yiv3372610449MsoNormal {

 margin:0 0 0 0;}

 

 #yiv3372610449 o {

 font-size:0;}

 

 #yiv3372610449 #yiv3372610449photos div {

 float:left;width:72px;}

 

 #yiv3372610449 #yiv3372610449photos div
div {

 border:1px solid

 #666666;height:62px;overflow:
hidden;width:62px;}

 

 #yiv3372610449 #yiv3372610449photos div
label {

 color:#666666;font-size:10px;
overflow:hidden;text-align: center;white-space:nowrap;
width:64px;}

 

 #yiv3372610449
#yiv3372610449reco-category {

 font-size:77%;}

 

 #yiv3372610449 #yiv3372610449reco-desc {

 font-size:77%;}

 

 #yiv3372610449 .yiv3372610449replbq {

 margin:4px;}

 

 #yiv3372610449 #yiv3372610449ygrp-actbar
div a:first-child {

 margin-right:2px;padding- right:5px;}

 

 #yiv3372610449 #yiv3372610449ygrp-mlmsg {

 font-size:13px;font-family: Arial,
helvetica, clean,

 sans-serif;}

 

 #yiv3372610449 #yiv3372610449ygrp-mlmsg
table {

 font-size:inherit;font:100%;}

 

 #yiv3372610449 #yiv3372610449ygrp-mlmsg
select,

 #yiv3372610449 input, #yiv3372610449
textarea {

 font:99% Arial, Helvetica, clean,
sans-serif;}

 

 #yiv3372610449 #yiv3372610449ygrp-mlmsg
pre, #yiv3372610449

 code {

 font:115% monospace;}

 

 #yiv3372610449 #yiv3372610449ygrp-mlmsg *
{

 line-height:1.22em;}

 

 #yiv3372610449 #yiv3372610449ygrp-mlmsg
#yiv3372610449logo {

 padding-bottom:10px;}

 

 

 #yiv3372610449 #yiv3372610449ygrp-msg p a
{

 font-family:Verdana;}

 

 #yiv3372610449 #yiv3372610449ygrp-msg

 p#yiv3372610449attach-count span {

 color:#1E66AE;font-weight: 700;}

 

 #yiv3372610449 #yiv3372610449ygrp-reco

 #yiv3372610449reco-head {

 color:#ff7900;font-weight: 700;}

 

 #yiv3372610449
#yiv3372610449ygrp-reco {

 margin-bottom:20px;padding: 0px;}

 

 #yiv3372610449 #yiv3372610449ygrp-sponsor
#yiv3372610449ov

 li a {

 font-size:130%;text- decoration:none;}

 

 #yiv3372610449 #yiv3372610449ygrp-sponsor
#yiv3372610449ov

 li {

 font-size:77%;list-style-
type:square;padding:6px 0;}

 

 #yiv3372610449 #yiv3372610449ygrp-sponsor
#yiv3372610449ov

 ul {

 margin:0;padding:0 0 0 8px;}

 

 #yiv3372610449 #yiv3372610449ygrp-text {

 font-family:Georgia;}

 

 #yiv3372610449 #yiv3372610449ygrp-text p
{

 margin:0 0 1em 0;}

 

 #yiv3372610449 #yiv3372610449ygrp-text tt
{

 font-size:120%;}

 

 #yiv3372610449 #yiv3372610449ygrp-vital
ul li:last-child {

 border-right:none !important;

 }

 #yiv3372610449

 





--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment