Saturday, 13 February 2016

Re: [wanabidii] Kina nani wanaompinga Magufuli?

Asane dada Ananilea Nkya! Kuogopa kukosolewa ni kasoro kubwa mno kwenye uongozi wa nchi. Kama nilivyosema kwenye mchango wangu wa kwanza ni kwamba hata kama mtu anafanya vizuri akikosolewa na kukubali kukosolewa atafanya vizuri zaidi. Kama angeridhika tu na hali yake asingeweza kufanya vizuri zaidi! Hivyo, kumkosoa rais si kumkatisha tamaa wala kutomtendea haki kwa vile bado ana muda mrefu mbele yake! Bali ni kumsaidia afanye vizuri zaidi na akishafanya vizuri zaidi, akikosolewa tena ata'sustain' hiyo hali ili asirudi nyuma. Hali hii ndiyo huwa inaleta maendeleo. Huwa wakati mwingine nachangia kitu kilichotokea kwangu. Huwa nasema kuwa nilipoanza maisha nilikuwa sina kitanda, meza ya chakula, TV, kabati la vyombo na pia nilikuwa na pair moja tu ya viatu etc. House help wangu akawa amepeleka habari kwa neighbours. Hivyo, baadhi ya akina mama wakaanza kusema: "mtu mwenyewe analala chini, hana meza ya chakula, ana viatu pair moja tu, hana TV...etc." Mwanzoni iliniumiza, lakini nikaona walichokuwa wanakisema siyo uwongo. Nilichofanya ni kuorodhesha walivyosema sina, kisha kila nikipata hela nilikuwa nanunua kimoja baada ya kingine na hatimaye wale waliokuwa wakinicheka walijikuta nimewaacha nyuma kimaendeleo. Ningekasirika na kuanza kujibizana nao leo hii nisingekuwa na vitu nilivyoweza kununua baada ya kutafakari kuwa sina na navihitaji pia. Hivyo, kwa kunisema, neighours wangu walinisaidia/challenge na nilivyokubali nikapiga hatua. Lakini ni kwa sababu mimi mwenyewe nilikubali kuwa waliyosema kuhusu mimi yalikuwa kweli. Kujitambua ni hatua muhimu sana katika maendeleo.

2016-02-13 17:34 GMT+03:00 'ananilea nkya' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
Magobe umetuweka sawa. Nakubaliana nawe asiyekubali kukosolewa pia asikubali kusifiwa. Kwa maoni yangu kukosoa na kusifia vyote vina mchango kwenye maendeleo. Lakini kiongozi wa umma anayeweza kuleta maendeleo makubwa ni yule ambaye kwanza yeye mwenyewe  anafiriki sana (ana original ideas zake siyo siyo za kukopa) na yuko tayari kukosolewa na wengine wanaofikiri tofauti naye---maana bila kukosoana tena kikweli kweli bila unafiki--maendeleo ya kweli yawe ni ya mtu binafsi ama ya taifa hayawezi kupatikana. Binafsi huwa nawapenda sana wakosoaji makini wenye moyo wa uzalendo  maana hao ndio wamekuwa wajenzi wakubwa wa taifa letu. Wasifiaji mara nyingi ni walinda maslahi binafsi na wamepungukiwa kitu kimoja muhimu katika uongozi unaoweza kunufaisha walio wengi--ujasiri.

Ananilea Nkya
 E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com

--------------------------------------------
On Sat, 2/13/16, Telesphor Magobe <tmagobe@gmail.com> wrote:

 Subject: Re: [wanabidii] Kina nani wanaompinga Magufuli?
 To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
 Date: Saturday, February 13, 2016, 7:58 AM

 Hakuna
 anayempinga! Kuna wanaomkosowa. Kupinga na kukosowa hakuna
 maana sawa. Kukosowa ni kusema namna kitu kichenye matokeo
 mabaya kingeweza kufanywa kwa namna tofauti na kuleta
 mafanikio chanya, au kitu kizuri kingeweza kufanywa kwa
 namna nyingine na kuwa kizuri kuliko au kitu kizuri kuliko
 kingeweza kufanywa kwa namna ambayo kingekuwa kizuri zaidi
 ya vyote. Kama kuna watu wanaoweza kumsifia rais kwa yale
 anayofanya, kuna watu wanaweza pia kumkosowa kwa yale
 anayofanya. Kama kumkosowa rais si sahihi kwa vile ameanza
 kazi muda si mrefu na bado ana miaka kadhaa ya kumpima, basi
 hata kumsifia si sahihi kwa mantiki hiyohiyo. Kwa upande
 mwingine, kupinga ni kuonyesha kuchukizwa na kitu
 kinachofanyika na kutaka kisifanyike. 

 2016-02-12 13:58 GMT+03:00
 'lang'itomoni lokomoi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:





 NI wazi kuwa
 siyo watu wote ni mashabiki wa uongozi na aina ya uongozi wa
 Rais Magufuli. Ni
 wazi siyo wote walifurahia kuchaguliwa kwake na kwa hakika
 si wote wanafurahia
 kile ambacho kinajulikana kama Operesheni Tumbua
 Majipu.
  Ni kufanya
 makosa
 kudhania kuwa watu wote wanafurahia au wanapaswa kufurahia
 operesheni hii au
 kuchaguliwa kwa Magufuli. Wapo wenye kumpinga, na wengine
 wameshajitokeza wazi
 kumpinga. Hili kwa kweli siyo la kushangaza na lenyewe tu
 siyo habari.


 Swali kubwa
 ambalo linaweza kuwa habari ni kuwa hawa wenye kumpinga ni
 kina nani na ni kwa
 nini. Je wote wenye kumpinga wanampinga kwa sababu wanataka
 kitu kingine au
 wanampinga kwa sababu wanaona hawana jinsi isipokuwa
 kumpinga?

 Je, wenye kubeza
 serikali hii na uongozi wa Magufuli wanafanya hivyo kwa
 sababu wanafurahia au
 wanatamani ule uongozi uliopita au wanatamani uongozi
 mwingine ambao haupo na
 haujawahi kuwepo bado?

 Kwa maoni
 yangu, wenye kumpinga Magufuli wako kwenye makundi
 mbalimbali, makundi ambayo
 ama yanaunganishwa na baadhi ya mambo.


 Kundi la
 wapinga mabadiliko haya si yale

 Kundi hili
 naweza kusema ndio kundi lenye watu wengi wenye kumpinga
 Magufuli na ambao
 watajitokeza wengi wakijionesha wanafanya kwa nia njema.
 Hawa ni wale ambao
 mgombea wao alishindwa na Magufuli na ahadi zile za
 mabadiliko ya mtu mmoja
 yakakataliwa ndiyo yanasumbua kwa sababu bado hawaamini kuwa
 mtu wao (siyo
 mabadiliko yao tu) alikataliwa.
  Kundi hili,
 haliwezi na halitakuwa na sababu ya
 kushabikia mambo yanayofanywa na Magufuli hata akifanya
 nini.

 Hawa mara
 nyingi ni watu ambao hawachelewi kuhamisha magoli.

 "Kama kweli
 Magufuli
 anatumbua si tuone kama atatumbua Bandari" wanasema.
 Bandari wanatumbuliwa na
 wao wanarudi "ah ile mbona rahisi sana kama kweli anataka
 kutumbua Bandari si
 atumbue Uhamiaji tuone"; uhamiaji kunatumbuliwa na hawa
 (hawakiri kuona
 kilichotokea bandari wala uhamiaji) wanarudi na goli
 jingine; "ah mbona yule
 kaonewa kama kweli ye mwanamme si aiguse Takukuru";
 Takukuru inaguswa mwisho
 wanakuja na kusema "Vipi escrow". Na itakapoguswa
 hawatakubali bado watatafuta
 goli jingine na jingine. Hawa ni wa mabadiliko yale;
 mabadiliko ya kuzungurusha
 mikono na hawako tayari kuacha kuzungurusha
 mikono.


 Tukumbuke
 neon kubwa la hawa wakati wa kampeni lilikuwa "CCM iondoke
 kwanza mengine
 baadaye". Tatizo ni kuwa yale mengine yameanza kutokea
 sasa wakati CCM iko
 madarakani na hili ni gumu sana kulipatanisha.
 Walijiaminisha kuwa yale
 "mengine" hayawezi kutokea CCM ikiwa madarakani na
 kwamba yanayotokea ni
 kinyume (antithesis) cha fikra zao zote na ndoto zao. Hawa
 hawawezi kumuunga
 mkono Magufuli wala kushabikia mabadiliko haya.


 Kundi la
 wakosoaji hawa

 Lipo kundi
 jingine la wakosoaji 'hawa'. Hawa ni wakosoaji wa
 serikali. Hawa ni watu ambao
 kwao serikali ni ya kushukiwa wakati wote. Ni kundi zuri
 sana kwenye utawala wa
 kidemokrasia kwani kundi hili halipendi geresha na
 mazingaombwe; ni kundi
 ambalo linawaangalia wanasiasa kama viongozi wa ngoma;
 wanajua wanafanya
 burudani na kuhakikisha watu wanapokea kwa kiitikio na
 manyanga. Wakosoaji
 "hawa" wao
 wanaweza kufurahia mabadiliko lakini wakati huo huo
 wanayashuku
 mabadiliko hayo; hawaamini nia za wanaotaka kuleta
 mabadiliko na hawachelewi
 kutafuta kasoro ili waweze kusema "aha si unaona amefanya
 hivi tena".


 Kundi hili
 nalo kama kundi lile la mwanzo halitakoma; litaendelea
 kumshuku Magufuli,
 litaendelea kuhoji ukweli wake na malengo yake na
 halitochelewa kulia "kavunja
 katiba" "kaingilia Bunge" "kaingilia Mahakama"
 "dikteta n.k". Ni kundi ambalo
 lipo kama mwiba wa lazima ili serikali isije kufikiri au
 kuishi bila
 kuangaliwa.


 Kundi la
 waathirika wa haya

 Kuna kundi
 na ninaamini litazidi kuwa kubwa zaidi kwa siku
 zinavyokwenda; hili ni kundi la
 waathirika wa mabadiliko haya. Wale watu wanaopoteza nafasi
 zao na watu ambao
 wanaaanza kuguswa na mabadiliko haya hawawezi kamwe kuwa
 mashabiki wa yule
 ambaye amesababisha jamaa, ndugu, mabodi au marafiki zao
 kuanza kuwa na maisha
 magumu.

 Kwa kadiri kwamba
 Magufuli anaanza kulazimisha uchumi wetu
 kujirekebisha ndivyo ambavyo wapo watu wengi ambao walikuwa
 wamezoea kuishi
 maisha fulani na sasa maisha hayo hayapo tena; na kama
 baadhi ya mishahara na
 posho zitakavyofutwa – kama inavyotarajiwa – kwenye
 Bunge la bajeti ni wazi
 kuwa Magufuli atapoteza mashabiki na marafiki wengi; na kwa
 vile hawa wanaweza
 kuwa wengi, kundi hili litazidi kumpinga na linaweza kuwa na
 watu wengi ndani
 ya serikali na ndani ya chama tawala.


 Makundi haya
 matatu naamini ndio makubwa na yataendelea kuwepo kwa kadiri
 ya kwamba Magufuli
 anaendelea na ajenda yake ya kusafisha utumishi serikalini,
 kubana matumizi
 yasiyo ya lazima na kurejesha nidhamu na heshima kwa
 Watanzania.
  Siyo wote
 watafurahia na si wote watasimama na kuunga mkono. Nina
 uhakika hata wale ambao
 walipiga makofi kushangilia kutumbua majipu wanaweza leo hii
 wasiwe tena wa
 kwanza kushangilia hasa baada ya wao wenyewe kutumbuliwa.
 Bado kazi kubwa
 inakuja na ngumu zaidi lakini kama alivyosema Rais –
 "hakuna namna nyingine".


 Nina uhakika
 pamoja na watu wengi wenye kumpinga bado wapo wengine wengi
 ambao nao
 wataendelea kuunga mkono na kumtia shime kwa sababu tunajua
 kushindwa kwake ni
 hasara kwa taifa na vizazi vijavyo.


 Hili tusiliruhusu
 litokee. -





 --

 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

  

 Kujiondoa Tuma Email kwenda

 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

  

 Disclaimer:

 Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
 for any legal consequences of his or her postings, and hence
 statements and facts must be presented responsibly. Your
 continued membership signifies that you agree to this
 disclaimer and pledge to abide by our Rules and
 Guidelines.

 ---

 You received this message because you are subscribed to the
 Google Groups "Wanabidii" group.

 To unsubscribe from this group and stop receiving emails
 from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

 For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.






 --

 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

  

 Kujiondoa Tuma Email kwenda

 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya
 kudhibitisha ukishatuma

  

 Disclaimer:

 Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
 for any legal consequences of his or her postings, and hence
 statements and facts must be presented responsibly. Your
 continued membership signifies that you agree to this
 disclaimer and pledge to abide by our Rules and
 Guidelines.

 ---

 You received this message because you are subscribed to the
 Google Groups "Wanabidii" group.

 To unsubscribe from this group and stop receiving emails
 from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

 For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment