On Sat, Feb 13, 2016 at 18:52, Telesphor Magobe<tmagobe@gmail.com> wrote:Asane dada Ananilea Nkya! Kuogopa kukosolewa ni kasoro kubwa mno kwenye uongozi wa nchi. Kama nilivyosema kwenye mchango wangu wa kwanza ni kwamba hata kama mtu anafanya vizuri akikosolewa na kukubali kukosolewa atafanya vizuri zaidi. Kama angeridhika tu na hali yake asingeweza kufanya vizuri zaidi! Hivyo, kumkosoa rais si kumkatisha tamaa wala kutomtendea haki kwa vile bado ana muda mrefu mbele yake! Bali ni kumsaidia afanye vizuri zaidi na akishafanya vizuri zaidi, akikosolewa tena ata'sustain' hiyo hali ili asirudi nyuma. Hali hii ndiyo huwa inaleta maendeleo. Huwa wakati mwingine nachangia kitu kilichotokea kwangu. Huwa nasema kuwa nilipoanza maisha nilikuwa sina kitanda, meza ya chakula, TV, kabati la vyombo na pia nilikuwa na pair moja tu ya viatu etc. House help wangu akawa amepeleka habari kwa neighbours. Hivyo, baadhi ya akina mama wakaanza kusema: "mtu mwenyewe analala chini, hana meza ya chakula, ana viatu pair moja tu, hana TV...etc." Mwanzoni iliniumiza, lakini nikaona walichokuwa wanakisema siyo uwongo. Nilichofanya ni kuorodhesha walivyosema sina, kisha kila nikipata hela nilikuwa nanunua kimoja baada ya kingine na hatimaye wale waliokuwa wakinicheka walijikuta nimewaacha nyuma kimaendeleo. Ningekasirika na kuanza kujibizana nao leo hii nisingekuwa na vitu nilivyoweza kununua baada ya kutafakari kuwa sina na navihitaji pia. Hivyo, kwa kunisema, neighours wangu walinisaidia/challenge na nilivyokubali nikapiga hatua. Lakini ni kwa sababu mimi mwenyewe nilikubali kuwa waliyosema kuhusu mimi yalikuwa kweli. Kujitambua ni hatua muhimu sana katika maendeleo.--2016-02-13 17:34 GMT+03:00 'ananilea nkya' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:Magobe umetuweka sawa. Nakubaliana nawe asiyekubali kukosolewa pia asikubali kusifiwa. Kwa maoni yangu kukosoa na kusifia vyote vina mchango kwenye maendeleo. Lakini kiongozi wa umma anayeweza kuleta maendeleo makubwa ni yule ambaye kwanza yeye mwenyewe anafiriki sana (ana original ideas zake siyo siyo za kukopa) na yuko tayari kukosolewa na wengine wanaofikiri tofauti naye---maana bila kukosoana tena kikweli kweli bila unafiki--maendeleo ya kweli yawe ni ya mtu binafsi ama ya taifa hayawezi kupatikana. Binafsi huwa nawapenda sana wakosoaji makini wenye moyo wa uzalendo maana hao ndio wamekuwa wajenzi wakubwa wa taifa letu. Wasifiaji mara nyingi ni walinda maslahi binafsi na wamepungukiwa kitu kimoja muhimu katika uongozi unaoweza kunufaisha walio wengi--ujasiri.
Ananilea Nkya
E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com
--------------------------------------------
On Sat, 2/13/16, Telesphor Magobe <tmagobe@gmail.com> wrote:
Subject: Re: [wanabidii] Kina nani wanaompinga Magufuli?
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Saturday, February 13, 2016, 7:58 AM
Hakuna
anayempinga! Kuna wanaomkosowa. Kupinga na kukosowa hakuna
maana sawa. Kukosowa ni kusema namna kitu kichenye matokeo
mabaya kingeweza kufanywa kwa namna tofauti na kuleta
mafanikio chanya, au kitu kizuri kingeweza kufanywa kwa
namna nyingine na kuwa kizuri kuliko au kitu kizuri kuliko
kingeweza kufanywa kwa namna ambayo kingekuwa kizuri zaidi
ya vyote. Kama kuna watu wanaoweza kumsifia rais kwa yale
anayofanya, kuna watu wanaweza pia kumkosowa kwa yale
anayofanya. Kama kumkosowa rais si sahihi kwa vile ameanza
kazi muda si mrefu na bado ana miaka kadhaa ya kumpima, basi
hata kumsifia si sahihi kwa mantiki hiyohiyo. Kwa upande
mwingine, kupinga ni kuonyesha kuchukizwa na kitu
kinachofanyika na kutaka kisifanyike.
2016-02-12 13:58 GMT+03:00
'lang'itomoni lokomoi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
NI wazi kuwa
siyo watu wote ni mashabiki wa uongozi na aina ya uongozi wa
Rais Magufuli. Ni
wazi siyo wote walifurahia kuchaguliwa kwake na kwa hakika
si wote wanafurahia
kile ambacho kinajulikana kama Operesheni Tumbua
Majipu.
Ni kufanya
makosa
kudhania kuwa watu wote wanafurahia au wanapaswa kufurahia
operesheni hii au
kuchaguliwa kwa Magufuli. Wapo wenye kumpinga, na wengine
wameshajitokeza wazi
kumpinga. Hili kwa kweli siyo la kushangaza na lenyewe tu
siyo habari.
Swali kubwa
ambalo linaweza kuwa habari ni kuwa hawa wenye kumpinga ni
kina nani na ni kwa
nini. Je wote wenye kumpinga wanampinga kwa sababu wanataka
kitu kingine au
wanampinga kwa sababu wanaona hawana jinsi isipokuwa
kumpinga?
Je, wenye kubeza
serikali hii na uongozi wa Magufuli wanafanya hivyo kwa
sababu wanafurahia au
wanatamani ule uongozi uliopita au wanatamani uongozi
mwingine ambao haupo na
haujawahi kuwepo bado?
Kwa maoni
yangu, wenye kumpinga Magufuli wako kwenye makundi
mbalimbali, makundi ambayo
ama yanaunganishwa na baadhi ya mambo.
Kundi la
wapinga mabadiliko haya si yale
Kundi hili
naweza kusema ndio kundi lenye watu wengi wenye kumpinga
Magufuli na ambao
watajitokeza wengi wakijionesha wanafanya kwa nia njema.
Hawa ni wale ambao
mgombea wao alishindwa na Magufuli na ahadi zile za
mabadiliko ya mtu mmoja
yakakataliwa ndiyo yanasumbua kwa sababu bado hawaamini kuwa
mtu wao (siyo
mabadiliko yao tu) alikataliwa.
Kundi hili,
haliwezi na halitakuwa na sababu ya
kushabikia mambo yanayofanywa na Magufuli hata akifanya
nini.
Hawa mara
nyingi ni watu ambao hawachelewi kuhamisha magoli.
"Kama kweli
Magufuli
anatumbua si tuone kama atatumbua Bandari" wanasema.
Bandari wanatumbuliwa na
wao wanarudi "ah ile mbona rahisi sana kama kweli anataka
kutumbua Bandari si
atumbue Uhamiaji tuone"; uhamiaji kunatumbuliwa na hawa
(hawakiri kuona
kilichotokea bandari wala uhamiaji) wanarudi na goli
jingine; "ah mbona yule
kaonewa kama kweli ye mwanamme si aiguse Takukuru";
Takukuru inaguswa mwisho
wanakuja na kusema "Vipi escrow". Na itakapoguswa
hawatakubali bado watatafuta
goli jingine na jingine. Hawa ni wa mabadiliko yale;
mabadiliko ya kuzungurusha
mikono na hawako tayari kuacha kuzungurusha
mikono.
Tukumbuke
neon kubwa la hawa wakati wa kampeni lilikuwa "CCM iondoke
kwanza mengine
baadaye". Tatizo ni kuwa yale mengine yameanza kutokea
sasa wakati CCM iko
madarakani na hili ni gumu sana kulipatanisha.
Walijiaminisha kuwa yale
"mengine" hayawezi kutokea CCM ikiwa madarakani na
kwamba yanayotokea ni
kinyume (antithesis) cha fikra zao zote na ndoto zao. Hawa
hawawezi kumuunga
mkono Magufuli wala kushabikia mabadiliko haya.
Kundi la
wakosoaji hawa
Lipo kundi
jingine la wakosoaji 'hawa'. Hawa ni wakosoaji wa
serikali. Hawa ni watu ambao
kwao serikali ni ya kushukiwa wakati wote. Ni kundi zuri
sana kwenye utawala wa
kidemokrasia kwani kundi hili halipendi geresha na
mazingaombwe; ni kundi
ambalo linawaangalia wanasiasa kama viongozi wa ngoma;
wanajua wanafanya
burudani na kuhakikisha watu wanapokea kwa kiitikio na
manyanga. Wakosoaji
"hawa" wao
wanaweza kufurahia mabadiliko lakini wakati huo huo
wanayashuku
mabadiliko hayo; hawaamini nia za wanaotaka kuleta
mabadiliko na hawachelewi
kutafuta kasoro ili waweze kusema "aha si unaona amefanya
hivi tena".
Kundi hili
nalo kama kundi lile la mwanzo halitakoma; litaendelea
kumshuku Magufuli,
litaendelea kuhoji ukweli wake na malengo yake na
halitochelewa kulia "kavunja
katiba" "kaingilia Bunge" "kaingilia Mahakama"
"dikteta n.k". Ni kundi ambalo
lipo kama mwiba wa lazima ili serikali isije kufikiri au
kuishi bila
kuangaliwa.
Kundi la
waathirika wa haya
Kuna kundi
na ninaamini litazidi kuwa kubwa zaidi kwa siku
zinavyokwenda; hili ni kundi la
waathirika wa mabadiliko haya. Wale watu wanaopoteza nafasi
zao na watu ambao
wanaaanza kuguswa na mabadiliko haya hawawezi kamwe kuwa
mashabiki wa yule
ambaye amesababisha jamaa, ndugu, mabodi au marafiki zao
kuanza kuwa na maisha
magumu.
Kwa kadiri kwamba
Magufuli anaanza kulazimisha uchumi wetu
kujirekebisha ndivyo ambavyo wapo watu wengi ambao walikuwa
wamezoea kuishi
maisha fulani na sasa maisha hayo hayapo tena; na kama
baadhi ya mishahara na
posho zitakavyofutwa – kama inavyotarajiwa – kwenye
Bunge la bajeti ni wazi
kuwa Magufuli atapoteza mashabiki na marafiki wengi; na kwa
vile hawa wanaweza
kuwa wengi, kundi hili litazidi kumpinga na linaweza kuwa na
watu wengi ndani
ya serikali na ndani ya chama tawala.
Makundi haya
matatu naamini ndio makubwa na yataendelea kuwepo kwa kadiri
ya kwamba Magufuli
anaendelea na ajenda yake ya kusafisha utumishi serikalini,
kubana matumizi
yasiyo ya lazima na kurejesha nidhamu na heshima kwa
Watanzania.
Siyo wote
watafurahia na si wote watasimama na kuunga mkono. Nina
uhakika hata wale ambao
walipiga makofi kushangilia kutumbua majipu wanaweza leo hii
wasiwe tena wa
kwanza kushangilia hasa baada ya wao wenyewe kutumbuliwa.
Bado kazi kubwa
inakuja na ngumu zaidi lakini kama alivyosema Rais –
"hakuna namna nyingine".
Nina uhakika
pamoja na watu wengi wenye kumpinga bado wapo wengine wengi
ambao nao
wataendelea kuunga mkono na kumtia shime kwa sababu tunajua
kushindwa kwake ni
hasara kwa taifa na vizazi vijavyo.
Hili tusiliruhusu
litokee. -
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

0 comments:
Post a Comment