Saturday, 14 November 2015

[wanabidii] Re: [Wanazuoni] Suala Si Tu Viongozi Kupenda Safari Za Nje, Bali Wanasafiri Vipi..? [1 Attachment]

Mwenye kigoda Maggid,

Hapa umelonga! Hata protocol za kulundikana uwanja wa ndege mtu akirudi Safari ya nje ya nchi!

Sent from my iPhone

On Nov 14, 2015, at 12:55 PM, Maggid Mjengwa mjengwamaggid@gmail.com [Wanazuoni] <Wanazuoni@yahoogroups.com> wrote:

 
[Attachment(s) from Maggid Mjengwa included below]


Ndugu,

Mwezi Juni 2011 nilipata kusafiri daraja moja na Balozi wa nchi ya Sweden ( Pichani) . Niliweka picha hiyo kwenye http://mjengwablog.com na kuzusha mjadala mkubwa. Niliandika kuwa ajabu ya mtoa misaada kusafiri Economy Class na Mpokea misaada kusafiri First Class, kwenye ndege moja. Na siku hiyo nakumbuka Balozi huyo wa Sweden, Lennart Hjalmaker aliingia wanakosafiria abiria akina sisi, hadi pale alipotokea mtu wa Serikali aliyetumwa kumwambia kuwa Mheshimiwa Balozi anatakiwa akapitie VIP, lakini bado ndani ya ndege tiketi yake ilikuwa ni ya kukaa Economy Class jirani na nilipokaa mimi na familia yangu.

Tumeona, kuwa Rais wa Awamu ya Tano, John Magufuli, ameonyeshwa kukerwa na tabia ya watendaji kupenda kusafiri nje ya nchi. Hivyo, Rais kaanzisha utaratibu mpya wa wahusika kuomba vibali.

Ni hatua njema na ya kuungwa mkono, maana , hiyo imepata kuwa moja ya mambo yenye kuukera umma kwa vile imehusisha matumizi makubwa ya fedha za umma.

Lakini, kuna mawili ya kuyaangalia; Mosi, hata wanapopata vibali, watendaji hao, hata ikiwa ni Mawaziri waache kutumia gharama kubwa kupanda First Class wakati hali yetu ya kiuchumi bado ni mbaya sana. Waache pia kuandamana na msururu wa watendaji wakati huko wanakokwenda mwakilishi mmoja au wawili wangetosha.

Pili, Rais John Magufuli aangalie pia kero ya misafara ya viongozi wanaongozana na wakubwa kwenye ziara ikiwamo ziara za Rais mikoani na wilayani. Katika nchi masikini inayopambana kutafuta mapato haiingii akilini na ni ulimbukeni unapoona msafara wa Rais au Waziri Mkuu kwenye ziara ya mkoani au wilayani una magari si chini ya 25! Hawa watu wote wanakwenda kufanya nini, na kama walihitajika, kwa nini wasikodiwe luxury bus likawemo kwenye msafara? Na wakati mwingine ajabu ni kuwa Waziri Mkuu anatembelea Wilaya, badala ya DC na watendaji kubaki huko wilayani kumsubiri Mkuu, nao watakwenda mkoani siku moja kabla na kuandamana na msafara wa Mheshimiwa kwenda kwenye maeneo yao ya kazi wilayani! Na hutokea pia kwa wakuu wa mikoa ya jirani nao hufunga safari kwenda kwenye mkoa ambao Waziri Mkuu au Rais anafanya ziara!

Naamini, ufatiti ukifanywa, tutaona pia, kuwa safari za ndani za watendaji nazo kuna ambazo zinatumiwa vibaya na kuongeza mzigo kwa wanyonge.

Maggid,
Nairobi.

__._,_.___

Attachment(s) from Maggid Mjengwa | View attachments on the web

1 of 1 Photo(s)


Posted by: Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com>
Reply via web post Reply to sender Reply to group Start a New Topic Messages in this topic (1)

Check out the automatic photo album with 1 photo(s) from this topic.
0.jpg


.

__,_._,___

0 comments:

Post a Comment