Friday, 6 November 2015

Re: [wanabidii] URAIS WA DR. MAGUFULI, NI FUNZO TOSHA KWA WENGINE

Katika chaguzi hizi za vyama vingi tuna mambo mengi ya kujifunza kutokana na chaguzi hizi, wapo viongozi wanaopatikana kwa kuwekwa na magenge ya watu wenye maslahi binafsi na wapo viongozi wanaopambwa na porojo za majukwaani, tumeona matumizi ya picha za uongo, matangazo mfululizo kama tunauza vocha za tigo na mihemuko ya kutengeneza.

Lakini tatizo kubwa ninaloliona sijui kama na wengine wanaliona ni ukosefu wa mtizamo mpana wa kisera. Ukitizama uchaguzi wa 1995 2005 na 2015 chama kile kile kina maono tofauti kabisa si chama tawala wala chama pinzani.

Ipo haja ya kutizama upya namna tunavyoendesha siasa zetu, tunaendesha siasa kana kwamba tunagombania utajiri. jana nilikuwa naangalia documentary ya fisi na simba yanagombania mzoga wa nyati. Fisi anautaka na simba anautaka ni makelele vitisho na majigambo kwa kwenda mbele.

Kusema utaondoa umasikini wa watanzania kwa miaka mitano ni uongo wa mchana kweupe hata kumi nako nikuwadanganya watu, mwaka 2010 chadema wajigamba kufuta ufisadi na nyumba za tembe na kuuza mfuko wa saruji elfu tano leo hawazungumzi hilo tena wamekuja na mambo mengine kabisa ya elimu bure na kufuta ufukara.

mwaka 2010 ccm walikuja na sera ya kufuta umasikini, leo hawazungumzi tena habari ya kufuta umasikini wanakuja na sera ya kufunga mafisadi kuna jamaa aliniambia ile kofia ya caw boy nje imeandikwa "hapa ni kazi tu" ndani imeandikwa "jitegemee" sasa tufuate maandishi ya ndani au nje? je nimafisadi yaleyale ya slaa 2010 au nimengine tena yameibuka?

Ipo haja ya kukaa chini na kuweka sera za nchi za muda mfupi na muda mrefu ili tujue vipa umbele vyetu hasa ni nini, ili wakati wa kampeni tuwashindanishe wagombea kwa namna gani tutafikia malengo tuliyojiwekea na sio ukiwakuta mama lishe unawambia utawapa steel wire za kusugulia masufuria, ukiwakuta machinga unawambia siwafukuzi barabarani, ukiwakuta bodaboda unawambia hakuna kuvaa helmet bora wakushangilie tu. hapana hatuwezi kujenga nchi kwa mtindo huo.

Katika uchaguzi uliopita nilitegemea wanasiasa watueleze ni kwa mna gani tutatoka hapa tulipo na kufikia uchumi wa kati ambao tumebakiza per capital ya us$ 15 tu. Magufuli alisema masikini nchi hii ni 28% ya watanzania lakini je nani aliyesema kuwa kufikia 2020 watakuwa wamebaki 12% angalau

2015-11-06 16:27 GMT+03:00 fadhil fadhil <fadhil.fadhil96@gmail.com>:

Urais wa Dr Magufuli, ni funzo tosha kwa watu wengine

Miezi kama minne iliyopita ni watu wachache sana waliokuwa wakiamini kwamba Dr Magufuli atakuja kuwa Rais wa nchi yetu, Hii ilitokana na mfumo uliokuwepo huko nyuma wa kuchagua mgombea ku-base zaidi kwenye makundi ndani ya Chama na umaarufu wa mgombea.

Kilichomwibua Dr Magufuli ni record yake ya uchapakazi, uadilifu, kutoyumbishwa hovyo hovyo kwa sababu ya kusimamia kile anachokiamini kwa manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla, Hiyo imejidhihirisha zaidi katika wizara zote alizowahi kuziongoza mfano Ujenzi na Miundombinu pamoja na Kilimo na ufugaji.

Fundisho tunalopata hapa ni kwamba usingoje mpaka upewe nafasi kubwa ya utumishi ndio uanze kuonyesha namna ya kuwatumikia wananchi. Piga kazi tu hata kama huna cheo chochote, usingoje mpaka uwe Waziri, Mbunge, M /"kiti serikali ya mtaa, nk*

WASIPOKUONA BINADAMU MUNGU ATAKUONA NA KUKUINUA TU

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment