Mashaka Makama,
Nakukushukuru sana kwa kusoma andiko langu:
Hata hivyo ili niweze kukujibu swali uliloniuliza endapo mimi ni mwanaharakati au mwanasiasa nahitaji kwanza unieleze kwa mtazamo wako:
1) Mwanaharakati ni nani?
2) Mwanasiasa ni nani?
3) Uchochezi ni nini?
4) Je andiko langu lina uchochezi gani?
5) Je ni kosa la jinai (uchochezi) sisi wananchi wa Tanzania kuandika uchambuzi kususu siasa za nchi yetu?
6) Je siasa za Tanzania ni mali binafsi ya watu maalum kama wewe tu na wananchi wengine wakijihusisha wanakuwa wanafanya kosa la jinai?
Ananilea Nkya
E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com
--------------------------------------------
On Fri, 11/6/15, 'Mashaka Makana' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: Re: [wanabidii] HONGERA UKAWA MPEIPA NCHI SOMO
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Friday, November 6, 2015, 3:16 PM
Mama Nkya unanichanganya! Wewe ni mwanaharakati
au mwanasiasa?
Sent
from Yahoo Mail on Android From:"'ananilea
nkya' via Wanabidii"
<wanabidii@googlegroups.com>
Date:Fri, Nov 6, 2015 at 17:00
Subject:[wanabidii] HONGERA UKAWA MPEIPA
NCHI SOMO
HONGERA UKAWA MPEIPA NCHI
SOMO
Na Ananilea Nkya
Baada ya uchaguzi mkuu
kukamilika, Watanzania wote wanaopigania mabadiliko
ili kila baada ya uchaguzi nchi yetu ipate uongozi
uongozi
utakaowezesha mamilioni ya Watanzania wanaoteseka kwa
umaskini kuondokana na umaskini wao, bila shaka
watavipongeza vyama vinanyounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi UKAWA.
UKAWA
wametoa somo kubwa kwa nchi yetu kuhusu changamoto kuu
zinazokabili nchi yetu kufikia uchaguzi huru na wa haki kama
nitakavyoeleza katika makala hii.
Aidha wanachama na viongozi wa CCM ambao
waliamua kuchukua maamuzi magumu kuondoka katika chama
hicho na kuungana na UKAWA katika kupigania mabadiliko nao
wanastahili pongezi kubwa.
Miongoni viongozi hao ni Edward Lowassa
aliyekuwa mgombea Urais CHADEMA –UKAWA ---ambaye
ushawishi wake wa kisiasa umeacha historia ya aina yake
katika uchaguzi wa vyama vingi Tanzania.
Wengine Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, Waziri
Mkuu mstaafu Mheshimiwa Fredrick Sumaye na Waziri wa Mambo
ya Ndani mstaafu Lawrence Macha.
Viongozi
hawa wamejitoa mhanga kukubali kujishusha na kuwa sehemu
ya harakati za wananchi kutafuta mabadiliko ya
kunufaisha walio wengi.
Tena wamejitoa bila kujali kudhalilishwa
kwa matusi na kunyanyaswa na vyombo vya dola kama
wanavyonyanyaswa wananchi wa kawaida.
Ninaamini ni watu wasioitakia mema Tanzania
na wasiojali maslahi ya Watanzania wengi ndio pekee
watawabeza viongozi hawa kutokana na uamuzi wao wa
kuungana na wana mabadiliko.
Lakini Watanzania wanaoelewa vema mchango
wa uongozi katika harakati za ukombozi watawapongeza na
kuwatia moyo viongozi hawa waliojitoa mhanga na kuthamini
mchango wao katika kupigania maslahi ya Watanzania walio
wengi maana bila viongozi kujitolea ili kuleta
mabadiliko, mabadiliko hayawezi kupatikana.
Zaidi ya yote vyama
vinavyounda UKAWA ambavyo ni
NLD, NCCR-Mageuzi, CHADEMA Nna CUF vinastahili pongezi
kubwa kwa sababu umoja wao katika uchaguzi wa mwaka huu
umetoa somo jipya katika siasa za vyama vingi Tanzania.
Jambo moja kubwa ambalo
UKAWA wamewathibitishia Watanzania ni kwamba vyama vya
upinzani vikishirikiana kwa dhati na kujiandaa vema
kupata viongozi makini na wenye dhamira ya kweli ya
kuleta mabadiliko kweli ya kunufaisha mamilioni ya
Watanzania maskini, wanashinda uchaguzi kwa kura
nyingi.
Jambo muhimu zaidi
sana ambalo UKAWA wametoa somo kwa Watanzania katika
uchaguzi huu ni kwamba nchi yetu bado ina safari ndefu
kufikia uchaguzi HURU NA WA HAKI unaowesha mshindi
kutangazwa mshindi na si vinginevyo. Je amani inaweza
kutamalaki kwenye jamii yetu kama uhuru na haki kwenye
uchaguzi vitaendelea kuchezewa kwenye uchaguzi?
Swali
hili msingi wake ni mgogoro ulipo sasa kuhusu
kutotangazwa kwa matokeo ya mshindi katika uchaguzi wa
Urais Zanzibar na UKAWA kutokukubali matokeo ya
Urais.
UKAWA katika
uchaguzi huu wametoa somo kwamba kuna matatizo makubwa
matatu yanayokwamisha uchaguzi huru na wa haki
Tanzania. Mambo hayo ni haya:
1)
Walioko madarakani kutokuwa na dhamira ya dhati (political
willingness) kuona mfumo wa siasa za vyama vingi
ukistawi na kuleta manufaa kwa mamilioni ya Watanzania
wanaoteseka kwa umaskini nchini. Dhamira inakosekana
kutokana walioko madarakani kunufaika na kuwepo kwao
madarakani.
2) Mifumo ya kisheria
na kitaasisi iliyokuwa inatumika kutawala wakati wa mfumo wa
chama kimoja cha siasa kuendelea kutumika katika mfumo wa
vyama vingi hivyo kunufaisha chama kilikuwa madarakani.
3)
Vyombo vya dola kutumika kisiasa kunyanyasa wananchi
wanapodai haki ya uchaguzi huru na wa haki.
Hivyo matatizo haya
yasipotafutiwa ufumbuzi wa kikatiba kabla ya uchaguzi
mwingine 2020 tbila shaka idadi ya wapiga kura
ikapungua sana uchaguzi ujao kutokana na wanachi kukata
tamaa kwamba uchaguzi hauna manufaa yoyote kw amaisha
yao.
Lakini kibaya zaidi
tusishangae umaskini ukiongezeka mara dufu
miongoni mwa mamilioni ya Watanzania tuendako maana
hata kama serikali ya Rais John Magufuli itafanya kazi
kubwa na kuweza kukuza uchumi kutoka asilimia saba (7%)
ilivyo sasa na kufikia asilimia kumi na tatu (13%) huenda
uchumi huo usiwanufaishe Watanzania wengi wanaoteseka kwa
umaskini.
Hii ni kutokana
Katiba na mifumo ya kiutawala iliyopo nchini hivi sasa
kutoa mwanya kwa watawala
kujitajirisha zaidi wao wenyewe kwa fedha na mali za
za nchi huku mamilioni ya Watanzania wakibaki maskini
wa kutupa.
Kwa hiyo kazi
kubwa aliyonayo Rais Dr John Magufuli, UKAWA, vyama
vingine vyote vya siasa na Watanzania wote ni kutafakari
hatma ya mamilioni ya Watanzania wanaoteseka kwa umaskini
kwa kuzingatia hayo matatizo matatu niliyoyaainisha hapo
juu. Mungu Ibariki Tanzania.
Note: Ninaridhia anayetaka kuchapisha andiko
hili afanya hivyo lengo likiwa ni kujifunza tuijenge nchi
yetu nzuri Tanzania.
Ananilea Nkya
E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata
Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to
this Forum bears the sole responsibility for any legal
consequences of his or her postings, and hence statements
and facts must be presented responsibly. Your continued
membership signifies that you agree to this disclaimer and
pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message
because you are subscribed to the Google Groups
"Wanabidii" group.
To unsubscribe
from this group and stop receiving emails from it, send an
email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment