Monday, 9 November 2015

Re: [wanabidii] KIKWETE KAULI HATARI UCHAGUZI

Hii ndo nchi ya demokrasia? nina makengeza
 
God created men in LOVE ,let us live with LOVE



On Saturday, October 17, 2015 4:50 PM, 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:


Ni haki kwa watanzania kubaki vituoni kusubiri matokeo. Lengo ni kujua matokeo na kujua kiongozi wako ngazi fulani na kujua mwelekeo wa kiongozi ambaye kura zake zinahitaji jumba toka sehemu nyingine.
Huko nyuma tumeshuhudia hayo. mara kadha nimekuwa nawapigia vijana wangu waliolala vituoni kutaka kujua nani kashinda.
Siku hizo makundi yote yalisimama na kusubiri matokeo. Aliposhinda wa chama fulani wote na wa chama kingine waliungana kushngilia.
Mwaka huu ni tofauti.
Kuna vyama vimetamka wazi kuwa hsi kwamba wanaenda kusubiri matokeo bali wanakwenda kulinda kura. Wanasema kama matokeo yataonesha chama chao kimeshindwa basi kura zao zimeibiwa. Hapa ndio Rais anasema hakuna kulinda kura. Maana yake kuna chama kikitangazwa kushindwa wakati wananchama walioshinda wamesimama pembeni basi hapo ngumi na mateke vinaanza. Wote tunajua kuwa rais anaendesha nchi kwa vyombo vya dola. Ni uelewa gani tena kuwa rais anatishiwa kushitakiwa ICC kwa sababu ya kutumia vyombo vyake vya dola. Kuna kila dalili kuwa kuna watanzania hawathamini tena nchi yao; uongozi wa nchi kwa kudhani kuwa watakwenda kulalamika ICC. WATU HAO WAMECHELEWA. hakuna kugombana. Hakuna kupigana. Wala hakuna kwenda ICC. Kama mtu anafikiri atawapiga mawe Polisi na wasifanywe lolote. HUU NAO NI UPUMBAVU MPYA.
--------------------------------------------
On Fri, 10/16/15, 'ananilea nkya' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] KIKWETE KAULI HATARI UCHAGUZI
To: mabadilikotanzania@googlegroups.com, "WANA BIDII" <wanabidii@googlegroups.com>
Cc: "Wanazuoni - Informal Network of Tanzanian Intellectuals" <wanazuoni@yahoogroups.com>
Date: Friday, October 16, 2015, 11:42 AM

RAIS KIKWETE WANANCHI KULINDA KURA
UTAEPUKA KUSHTAKIWA
 
Na Ananilea Nkya

Uchaguzi mkuu utakaofanyika Jumapili tarehe 25 Oktoba mwaka
huu 2015 huenda vyombo vya dola vikatumika kifisadi kupora
mamlaka ya wananchi   kuchagua kiongozi
wanayemtaka katika ngazi ya Urais, ubunge na udiwani.

Hii ni kwa sababu Rais Kikwete   siku
alipozima mwenge wa Uhuru huko Dodoma alitoa kauli 
hatari kwamba   vyombo vya dola
vitawashughulikia wananchi ambao watakuwa wako karibu na
vituo vya  kura  kulinda kura zao na kushuhudia
kuwa atakayeshinda  atakuwa  ameshinda kihalali na
siyo kwa  'goli la mkono' (wizi).

Kinachoshangaza  Rais Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)   ametoa 
kauli hii  huku akijua wazi kuwa  sheria ya
uchaguzi  inawaruhusu wananchi kukaa mita 200 kutoka
kituo cha kupigia kura kwa lengo la kushuhudia upigaji
kura,  kuhesabu kura na kutanga matokeo.
 
Vyama vya upinzani  vikiwepo  vinavyounda Umoja wa
Katiba ya Wananchi (UKAWA) –CHADEMA, CUF, NCCR-
Mageuzi  na NLD  ambavyo  vimeamua
kusimamisha mgombea mmoja mmoja kwenye nafasi ya urais,
ubunge na  udiwani   vimekuwa 
vikiwahimiza  wananchi  kulinda kura.

Kufuatia kauli hiyo ya Rais Kikwete wananchi
wanauliza:  Rais ambaye anapaswa kuwa mlinzi namba moja
wa sheria za nchi inakuwaje ametoa kauli inayoashiria kuwa
anakusudia   kuvunja sheria ya uchaguzi?

Wananchi wanauliza swali hili kwa sababu  Rais
kutumia  vyombo  vya umma vinavyopaswa
kulinda  usalama  wa wananchi  kama 
vile  jeshi la  polisi au 
jeshi   la wananchi kunyanyasa wananchi 
siku ya kupiga kura  kinyume na sheria  ya
uchaguzi  ni  sawa na  kufanya ufisadi katika
mchakato wa   kupata viongozi wa  nchi.

Kufanya ufisadi huo   siyo tu
ni   kuvuruga amani na  demokrasia ya
uchaguzi unaohusisha vyama vingi vya
siasa   bali pia  ni  kukwamisha
juhudi za kukomesha umaskini unaowatafuna wananchi wengi
kutokana ambao chanzo chake  ni ufisadi.

Rais Kikwete  kutumia vibaya  nguvu ya
kimamlaka   aliyopewa na
umma   kwa 
kuagiza   vyombo vya 
dola   kunyima wananchi kulinda kura
zao   ni kutaka    viongozi 
wan chi yetu wapatikane kwa njia za ufisadi na wizi wa kura
na hivyo wakiingia  madarakani  wataendelea
ufisadi huo huo  katika  chaguzi zijazo.

Hii ni hatari kubwa kwa taifa kwa sababu madhara yake 
ni makubwa  kwa  maendeleo ya  nchi
yetu  kudumu kwa  amani  ya kweli inayotokana
na haki  kutendeka kwenye uchaguzi.

Ndiyo sababu wananchi  wanauliza   lengo
la Rais Kikwete  lilikuwa ni nini  kutaka
kuvunja  sheria ya uchaguzi kama siyo  anafanya
hivyo  kuandaa mazingira ya kutekeleza  azma
ya   chama chake ---Chama cha Mapinduzi 
(CCM)  kutumia 'goli la mkono' kupata ushindi 
kwa gharama yoyote kama wanavyozungumza kwenye majukwaa ya
kampeni?
 
Maswali haya ya wananchi  yanatokana na ukweli
kwamba   kauli  ya Rais 
Kikwete  kuzuia wananchi  kuwa  karibu na
vituo vya kupiga kura kinyume na sheria ya
uchaguzi   ilianza kutolewa  kwa
msisitizo  na  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) Jaji  mstaafu Damian Lubuva.

Lubuva alinukuliwa akihoji:  "Tume inashangaa kwa
nini vyama vinang'ang'ania kubaki katika vituo vya
kupigia kura''.

Kadhalika, jambo linaloshangaza wananchi ni
kwamba   hata Msajili wa vyama vya siasa ,
Jaji Francis Mutungi naye ameunga mkono uvunjaji huo wa
sheria ya uchaguzi  kwa sababu  badala ya
kumshauri Rais  kufuta kauli yake hiyo , ameuunga
mkono.

Jaji Mutungu amenukuliwa akisema ''ni kweli sheria
imeruhusu wananchi kubaki katika kituo cha kupiga kura kwa
umbali wa mita 200, lakini sheria hiyo ina upungufu ambao
wameuona ndio maana Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetoa
kauli hiyo ya kuwezesha uchaguzi kufanyika katika mazingira
ya amani''

Wananchi wanauliza kama  sheria ya uchaguzi 
ilikuwa na mapungufu ni kwa nini serikali haikuipeleka
Bungeni iweze kufanyiwa marekebisho kabla ya uchaguzi 
wakati uchaguzi  halikuwa  jambo  ghafla?

Kadhalika  wananchi wanauliza:  Rais Kikwete 
pamoja na Jaji Lubuva na Jaji Mutungi  wamepatwa na
nini gafla  kiasi kwamba  wameamua 
kushabikia uvunjifu wa Katiba ya nchi na  sheria ya
uchaguzi  kunakoweka  rehani amani, usalama na
heshima kubwa ambayo Tanzania imejijengea mbele ya mataifa?
 
Pengine kinachowafanya  wananchi kuamini kuwa 
huenda   Rais 
Kikwete   na na CCM yake  wanakusudia
kutumia  'goli la mkono'  kupata viongozi wa
nchi yetu kwa kutumia ufisadi wa kura  ni kwamba 
Jaji  Lubuva na  Jaji Mutungi  wote ni 
mwanasheria   waliobobea na kwa nyadhifa
zao  wanapaswa  kuitiii Jamhuri ya Muungano 
kama  walivyoapa siku walipoteuliwa  kushika
nyadhifa hizo na siyo vinginevyo.

Kutii  Jamhuri maana yake  siyo  kusema ndiyo
kwa kila analosema, kuagiza au analotaka Rais wa Jamhuri
yetu,  bali  ni kutumia  busara  na
kuheshimu  kiapo cha utii  kwa Jamhuri 
kumshauri  Rais  kuepuka  kutoa 
kauli  au  kupanga  mambo maovu
yanayoweza  kufanya uchaguzi kultumbukiza nchi yetu
kwenye machafuko.

Hebu jiulize ni wanawake wangapi, watoto wangapi, wazee
wangapi na vijana wangapi wataathirika ikitokea hii kauli
hatari ya Rais Kikwete ikitekelezwa na nchi yetu ikakumbwa
na machafuko kwenye uchaguzi mwaka huu?

Rais Kikwete ajue kwamba kwa kauli alioyoitoa  kama
atatekeleza hiyo azma yake ni lazima katika uchaguzi wa
mwaka huu kutokee umwagaji mkubwa wa damu kwa sababu kauli
yake  imewafanya wananchi kuamini kuwa haki yao ya
kulinda kura inapokonywa na Rais kwa kuamua kuivunja sheria
ya uchaguzi.

Muhimu, wananchi  hasa katika  wakati huu 
nchi inaelekea kwenye siku ya uchaguzi mkuu  tarehe
25,  wanategemea   Jaji Lubuva kuonyesha
hekima, busara na ujasiri wa hali ya kuu kuhakikisha NEC
inasimamia na kutenda    ili  wananchi 
waridhike kwa dhati kabisa kwamba haki imetendeka kwenye
uchaguzi maana bila haki kutendeka hakuna amani ya kweli nay
a kudumu Tanzania.
 
Aidha  wananchi  wanatarajia pia  kuwa 
wadau  wakubwa wa amani vikiwepo vyombo vya habari na
hususan wahariri ,  viongozi wa dini zote,  wakuu
wa vyombo vya  usalama  hususana jeshi la polisi
na jeshi la wananchi,  viongozi wa vyama vya siasa,
mashirika ya kiraia NGOs mfano TAMWA, TGNP na LHRC 
wasomi,  wahanahakati na kila mtu mwenye nia njema na
Tanzania anachukua hatua bila 
woga   kumtahadharisha Rais  Kikwete
kwamba  kuvunja sheria ya uchaguzi kwa kuwazuia
wananchi kulinda kura zao ni ufisadi  mbaya
utakaoigharimu nchi yetu .

Bila  kumtaadharisha Rais Kikwete,  ikitokea
vyombo vya dola vikapambana na wananchi walioamua kutumia
haki yao ya kisheria  kulinda kura,  Jaji 
Lubuva na  Mutungi hawatakwepa  mkono wa sheria za
kimataifa  kwa  kushiriki  jinai 
ya  kufisadi uchaguzi  wa mwaka huu 
kwa  kuamua  kuwasaidia  watawala  wa
CCM wanaotaka chama chao  kung'ang'ania madaraka
kwa gharama yoyote  hata kama kitakuwa
kimekataliwa  na wananchi.

Tukumbuke kuwa kauli ya kwamba CCM itashinda kwa gharama
yoyote imekuwa ikitolewa na viongozi mbali mbali waandamizi
wa CCM akiwepo Katibu Mkuu wao, Abrahamani Kinana.

Hivi sasa  baada ya  Jaji Lubuva na Jaji
Mutungi  kuungana na Rais Kikwete kutaka 
kuvunja  Katiba ya  nchi yetu na
kukiuka   sheria ya uchaguzi  ili
kuwanyima  wananchi haki ya  kukaa karibu na 
vituo vyao vya kura  hadi  mwisho kujua hatma ya
kura yao   kumewafanya wananchi kuuliza :

Hivi Tanzania  imebinafsishwa
lini   na  lini   na
kugeuzwa kuwa   mali binafsi ya 
Rais  Kikwete   na watawala wachache wa
CCM  kiasi  kwamba wanaweza  kufanya lolote
na Watanzania wengine wote hawana  tena mamlaka juu ya
nchi yao?

Hivi Tanzania  imebinafsishwa   kwa
hivyo hivi sasa   nchi hii  ni
mali   binafsi ya  Rais KIkwete na
watawala wachache wa  CCM kwa hivyo wanaweza 
kufanya watakavyo na wananchi hawana  tena mamlaka juu
ya nchi yao?

Wananchi  wanauliza  kama  Tanzania
haijabinafsishwa kifisadi  Rais Kikwete, Jaji Lubuva na
Jaji Mutungi  wanapata  wapi  kile 
Dakta Harrison  Mwakyembe alichokiita 'jeuri ya
kifisadi'  ya kutaka kuvunja  sheria za
uchaguzi  kuruhusu vyombo vya dola  kunyanyasa
wananchi siku ya uchaguzi ili sauti ya umma inayotaka
mabadiliko ya uongozi  isisikike kupitia sanduku huru
la kura?

Wananchi wanauliza maswali haya kwa sababu wanaona kauli
iliyotolewa na Rais Kikwete kwamba ataamuru  vyombo vya
dola kushughulikia wananchi watakaokuwa karibu na vituo vya
kupigia kura na kisha kauli hiyo kushabikiwa na Jaji Lubuva
na Jaji Mutungi  kunaashiria  wanataka Tanzania
iingie kwenye balaa zililozikumba 
nchi   kadhaa  za Afrika ikiwepo nchi
jirani ya Burundi.

Kwa Rais Kikwete kutaka kuivunja  sheria ya uchaguzi
juu ya haki ya wananchi, tafsiri yake ni
kwamba   anataka kuweka historia mbaya 
ya  kuingiza Tanzania kwenye  machafuko  kwa
kulaka kulazimisha  CCM kubaki madarakani  kwa
'goli la mkono'  ambalo  ni sawa  ni sawa
na uhaini.

Je  kwa  Rais Kikwete  kwa kutaka 
kuvunja sheria ya uchaguzi inayoruhusu wananchi  kukaa
mita  200  kutoka kituo cha uchaguzi  anataka
kuwaambia Watanzania kuwa   tarehe 25 Oktoba
2015  amejiandaa   kutumia  vyombo
vya dola  kuwapora wananchi Watanzania  mamlaka ya
kuamua  nani awe kiongozi wao?

Kama Kikwete ndivyo anataka ni vema ajiandae kushtakiwa
kwenye mahakama ya Kimataifa   ya makosa ya
jinai.

Akiamua kutekeleza jinai hiyo  siyo tu atakuwa
amejidhalilisha mwenyewe na CCM yake bali pia Wanzania
wote  na  Tanzania ambayo  inaheshimika
duniani kote kutokana na  misingi ya haki na 
kuheshimu  wananchi kulikojengwa na muasisi wa taifa
hili Juliua Nyerere.

Lakini zaidi itakuwa ni aibu kwa CCM ambayo imeongoza
nchi  hii  miongo mitano  kuonekana kuwa
serikali yake  haikuanzisha vyama vingi  kwa nia
ya dhali kuleta ushindani wa kisiasa kukomesha umaskini
unaotafuna mamilioni  ya Watanzania.
   
Hii ni kwa sababu Rais wa serikali  ya CCM kujaribu
kuvunja sheria  ya  uchaguzi  kulazimisha
CCM  kubaki madarakani ni kukataa mfumo wa vyama vingi
usifanye kazi   kuondoa umaskini.

Huku ni kukataa mabadiliko wakati  mmoja wa 
waasisi mashuhuri wa CCM, Mzee   Kingunge
Ngombale Mwiru  ambaye  ameamua kuondoka CCM kwa
tuhuma za kukiukwa kwa  Kanuni na Katiba ya chama hicho
wakati wa mchakato wa kumpata mgombea urais, amekiri
hatadhani kuwa chama hicho sasa kimechoka, kimekosa
pumzi,  uchumi wa  nchi umekwama, kinakodisha
mavuvuzela kutukana watu , hivyo  madadiliko ni 
lazima mwaka huu 2015.

Lakini zaidi Rais Kikwete  asipoacha kutekeleza kauli
yake  atakuwa  ameuthibitishia ulimwengu 
kwamba Tanzania  ni miongoni mwa  nchi
ambazo  wanazuoni Daron Acemoglu and James Robinson
kwenye kitabu chao ''Why Nations Fail '' 
  wanadai kwamba   chanzo  kundi
kubwa la wananchi kubaki maskini na kikundi kidogo cha
watawala kujajirika kufuru ni  chama kinapokuwa
madarakani serikali  kukataa mabadiliko ya
uongozi   hivyo kutumia  vibaya vyombo
vya dola  kung'ang'ania madaraka.
 
Hii itakuwa ni aibu kwa CCM iliyoongoza  Tanzania 
miongo mitano  kuonekana kuwa serikali yake 
haikuanzisha vyama vingi   vya siasa 
kwa nia ya dhati  ya kuleta ushindani wa kisiasa
kukomesha umaskini unaotafuna mamilioni  ya Watanzania.
Mungu ibariki Tanzania.
 
Note: Nimeridhia yeyote anayetaka kuchapisha au kusambaza
andiko hili afanye hivyo.  Tuwasiliane: ananilea_nkya@yahoo.com

Ananilea Nkya
 E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


0 comments:

Post a Comment