Mimi nadhani jukumu la kwanza la kulinda amani ni nchi husika, ambazo ziko kwenye mgogoro wa kivita. Ni kama familia, ambayo mume na mke mara kwa mara wanagombana na kupigana, huwezi kulaumu wasuluhishi kwa ugomvi wa hao wanandoa. Ila ni kweli pia, wasuluhishi kuingilia kati na kutoa ushauri. Hata hivyo, bado ni wanandoa wenyewe wanaoweza kusahihisha makosa yao na kuanza kuishi kwa amani. Umoja wa Mataifa ni umoja ambao nchi wanachama wamejiunga kwa hiari yao na hauna jeshi. Kuna mambo mengi, ambayo umoja huu kwa kuwepo kwake umesaidia sana. In fact, it's better kuwa na Umoja wa Mataifa kuliko kutokuwa nao kabisa maana mambo yangekuwa balaa! Hivyo, hata kama tunatoa critical assessment tuwe tunajaribu kuwa fair. Jukumu la kulinda amani ni la nchi zenyewe na watu wake. Nchi haziwezi tu kuanzisha migogoro halafu mambo yakienda out of control watu waanze kulaumu Umoja wa Mataifa as if ndio ulioanzisha hiyo migogoro na machafuko. Hata hapa kwetu Tanzania, mara nyingi maoni/vilio vya wananchi havisikilizwi na viongozi wetu wanatumia ubabe kunyamazisha vilio hivi visisikike na kutafutiwa ufumbuzi. Matatizo yakitokea wa kulaumiwa wa kwanza ni viongozi wenyewe na siyo wasuluhishi au wanaosaidia kutuliza machafuko yasiendelee kwani nao wanatoka katika nchi pengine zinazohitaji msaada fulani. Tujifunze kuwa wapenda amani na tusiwe wepesi wa kuanzisha shari halafu tuwasubiri wengine waje watusaidiea kukabiliana nayo. Ndiyo maana ni lazima tuanze kujenga utamaduni wa uadilifu, uwazi na uwajibikaji katika viongozi wetu na pia kwa raia wenyewe kwa ujumla.
On Fri, Oct 24, 2014 at 10:13 AM, Novatus Kambota <novakambota@gmail.com> wrote:
--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CABkmAOL763WWVXoZqpw39AP2KHPE3YR-ENqMUTFmm6_v1R8rDw%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment