Thursday, 23 October 2014

[wanabidii] Rais Kikwete amteua Fella kuwa Katibu Mkuu Sekretarieti ya Kamati ya Kuzuia Biashara Haramu ya Binadamu

Rais Jakaya Kikwete amemteua Seperatus Fella kuwa Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Kamati ya Kuzuia Biashara Haramu ya Binadamu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Isaac Nantanga ilieleza kwamba uteuzi huo unaanzia Agosti ,mwaka huu.

Kabla ya uteuzi huo, Fella alikuwa Kaimu Katibu wa Kamati hiyo.
Taarifa hiyo ilisema Kamati hiyo ilianzishwa chini ya Sheria ya Kuzuia Biashara Haramu ya Binadamu ya mwaka 2008 na kazi yake kubwa ni kuzuia na kudhibiti biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu.

Aidha Nantanga alifafanua kwamba makosa yanayovunja sheria hiyo ni pamoja na kupanga, kupangisha au kutumia nyumba au jengo kwa ajili ya biashara hiyo na kughushi hati za Serikali kwa madhumuni ya kukuza biashara haramu.

Alisema makosa mengine ni kujipatia fedha kwa kuwatumikisha kwa nguvu watu wazima au watoto wa kike au kiume katika kufanya kazi za ndani au biashara nyingine haramu kama ngono na usafirishaji na usambazaji wa madawa ya kulevya, baada ya kuwalaghai au kuwachukua kwa nguvu kutoka katika makazi yao.

Aliongeza kuwa adhabu kwa wanaotiwa hatiani kwa kuvunja sheria hiyo ni kifungo kisichopungua mwaka mmoja(1) au kisichozidi miaka saba(7) au faini isiyopungua sh. milioni mbili au kuzidi sh. milioni 50 au vyote kwa pamoja.

Magreth Kinabo, Habari/MAELEZO

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment