Wednesday, 22 October 2014

[wanabidii] MWALIKO WA UZINDUZI WA KITABU

Mwanazuoni Galacha wa Takwimu za Kibaolojia na Kitabibu na Mwanaakademia muhimu wa Sayansi, Profesa Karim F Hirji ameandika Kitabu Kipya cha Tawasufi, akiyaeleza kwa undani maisha yake ya sasa na ya zamani, akichambua kwa undani harakati za Kijamii, Matabaka ya Rangi na Kiuchumi, Ujamaa, Elimu na Sekta ya Afya katika miaka hii 50 ya nchi yetu Tanzania.

Jina la "Growing up with Tanzania - Memories, Musings and Maths", Kwa kuthamini nafasi ya Vijana kwa Ustawi wa Taifa, Profesa Karim Hirji alitoa Nakala tatu za Kitabu husika kwetu 'Kitabu Nilichosoma', na baada ya nakala husika kusomwa kwa mzunguko na Vijana kadhaa 'Kitabu Nilichosoma' kimeamua kuandaa 'Mduara wa Majadiliano' (Round-Table Discussion) juu ya Kitabu Husika ambao utafanyika siku ya Jumamosi, Tarehe 25, Oktoba 2014 kuanzia Saa 3:30 Asubuhi Mpaka saa 7:00 Mchana katika Mkahawa wa Vitabu wa Soma Book Cafe, Ulioko Mtaa wa Chato, Kinondoni Morocco Jijini Dar es salaam.

Kwa heshima na Taadhima naomba kuchukua nafasi kukualika kushiriki 'Mduara huu wa Majadiliano' kuhusu Kitabu hiki.

Kwa Mawasiliano
0717577517
Seif Abalhassan
Kitabu Nilichosoma

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment