Barua ya wazi kwa wanyonge wenzangu!
Nimepata kuyasikia haya leo kuwa chama chetu cha ukombozi wa wanyonge Tanzania kwa taarifa zilizopo mtaani ni kuwa kimepata hati chafu ya matumizi mabovu ya fedha za serikali kinacho pewa kama (Ruzuku) kikatiba ili zitumike kuendesha chama hicho
kwetu sisi wonyenge hichi kidogo tunachopewa kinaweza kuonekana ulikuwa kama mtihani kwetu pindi tukipata kikubwa badae tutatumiaje?
Fedha za watanzania,fedha za wanyonge hao na walal hoi wanao tetewa,fedha zangu mimi na wewe
Ikiwa ni taarifa toka kwa mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali na mashirika ya umma CAG kama alivyo maliza ukaguzi wa vyama vya sasa mda usio mwingi
Mimi kama mnyonge nambari moja taarifa hizi zimenishutua sana,kuona kama sisi ambao ndo kama watetezi wa wanyonge hata hatukupaswa kudhaniwa vibaya achilia mbali kuwa tumefanya au kuhusika kushiriki kufanya ili kujenga taswira inayo fanana na malengo yetu mbele ya jamii
Mambo ambayo ni makusudio ya wanyonge walio wengi ilikuwa ni kuona sura safi na moyo safi unaoambatana na matendo ya viongozi wao kuelekea ukombozi unao lengwa
Kama wanyonge na mnyonge mimi,nimefadhaika sana,tunafadhaishwa sana na taarifa hii ni mbaya
Wanyonge wenzagu safari ya ukombozi kama ilivyo dhana yenyewe ni ndefu,ili tufike huko katika ukombozi unaokusudiwa isije kuwa kama Libya,Misri au kwingineko hatupaswi ku cover up(kufunika) mambo kama haya ambayo taswira yake inafedhehesha safari nzima na wafuasi wake....kama nilivyo wakumbusheni mara tu pale katiba ya chama mara ilipo vunjwa ni lazima sisi wanyonge ambao ndo tunawapa nguvu ya kusimama na kutusemea tuhoji wale wote wanao husika na hayo,bila kumuogopa papa au nyangumi wahusika wapewa adhabu na kulingana na fedheha hizi...tukifanya hivyo tutaonda matusi mengi yanayo tupata sisi ni chama chetu waliomo kwenye skendo hizo na wasio,tabia ya kufunika mambo na kuyatetea yalivyo au tumetenda sisi au wengine ni mbaya na ni kwa sababu itakapokuja dhoruba itawapeteni nyote waliomo na waiso kuwemo, ...kama kweli dhamira na malengo ni sawa na tuyasemayo siku zote basi tusifanyeni kama jirani au kwa kusema mbona jirani anafanya hivi nasi tufanye vile,,na mda ukifika wenye dhamira safi na waadilifu watangulizwe mbele kutetea wanyonge sisi
Msituone tuna sita sita kuwaamini wale wote wanao piga kelele za kuwa ni wakombozi wa wanyonge sisi,tunafanya hivyo na ni kwa sababu tunazo sababu,tunatambaua na tunapima na tumea na tunazo sababu....najua walio wachache hawewezi kutulewa kwa leo ila mda ukifika mtatuelewa au wengine kwa sababu ya mahaba mazito waliyo nayo wamalewa
Ni kweli tunauhitaji ukombozi lakini ni bora zaidi tukajikomboa kwa haya kabla ya kwenda huko mbali ambako nahisi tutakuwa tumechelewa
Mnyonge mimi nawatakieni asubuhi njema nikiwa nimefadhaishwa sana!
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment