MAONI YANGU KWA KANISA.
1. Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake, Na moyoni mwake amemwacha BWANA. [Yeremia 17:5]
2. BWANA asipoulinda mji, Yeye aulindaye akesha bure. [Zaburi 127:1]
3. Nitayainua macho yangu niitazame milima; Msaada wangu utatoka wapi? Msaada wangu u katika BWANA, Aliyezifanya mbingu na nchi. Zaburi [121:1-2]
4. Na jamii ya watu wote pia wajue ya kwamba BWANA haokoi kwa upanga wala kwa mkuki; maana vita ni vya BWANA, naye atawatia ninyi mikononi mwetu. [1 Samweli 17:47]
[Unabii uliotolewa na Nabii Deborah James tarehe 19, Novemba, 2013].
"…..Sasa nasema siku ya leo unapotazama uovu, ubaya, uchafu, upatikanao nchini, nasema ni mimi Mungu aliye Hai ambaye anaweza kuyaondoa kabisa. Hiyo ni kwamba, kama wale wanaodai kuwa wangu watatubu kwa uhakika, na kunirejea mimi ndipo nasema kwamba mimi Mungu aliye Hai, nitarejesha tena haki. Kwa maana nasema naweza kufanya kile ambacho hakiwezekani kwa wanadamu, na nasema kwamba ni mimi Mungu aliye Hai ambaye naweza kutiisha na kuondoa majeshi ya adui.
Lakini nasema wakati wale wanaodai kuwa ni wangu, watakubaliana na ajenda za adui nasema hakuna tumaini linaloweza kupatikana. Kwa ajili hiyo nasema siku ya leo endelea kutubu kwa ajili ya dhambi, endelea kulia kwa ajili ya haki ili irejeshwe, kwa maana nasema kwamba ninawasikia wale ambao wamesimama vizuri na mimi.
Nasema kama utalia kwa uhakika kwa ajili ya watu kutubu, ni mimi Mungu aliye Hai ambaye anaweza kuwafanya hao wawe hivyo. Nasema vitu ambavyo wanadamu hawawezi kuvifanya, naweza kuvifanya! Kwa ajili hiyo nasema usiangalie mazingira, kana kwamba hayawezi kubadilishwa, lakini nasema niamini mimi. Nasema lia, lia, lia kwa ajili ya toba juu ya nchi, na mimi Mungu aliye Hai nitakusikia uliapo.
Nasema kwamba ni mimi Mungu aliye Hai ambaye kwa hakika nitakuwa ninawabariki watu wajitunzao wenyewe kwa ajili yangu. Hiyo ni wakati wale wanaodai kuwa wangu wakitembea kwa uhakika katika wakfu kwangu, ndipo nasema kwamba nitaleta amani katika nchi. Lakini nasema wakati wale wanaodai kuwa ni wangu, watanichepuka, wakienda katika njia za makahaba, wakijifanya wenyewe vitanda vya uasi, ndipo nasema kwamba nchi itateseka kwa ajili ya hayo yote…." Frank
On Saturday, October 11, 2014 9:32 PM, Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com> wrote:
TAMKO LA WAKRISTO BUKOBA KUHUSIANA NA MAUAJI PAMOJA NA UCHOMAJI MAKANISA TAREHE 11/10/2014.
Baada ya tukio la kutisha la kushambuliwa kwa washirika na hatimaye kuuawa kwa mshirika na kujeruhiwa vibaya kwa mwingine kanisani Kagemu PAG; Wachungaji na viongozi wa kiroho wa Bukoba tumepokea taarifa hizi kwa mshtuko mkubwa. Tumekutana tarehe 10 Oct 2014 na kutafakari hatima ya wakristo katika eneo hili.
Matukio rejea tuliyojikumbusha ni kama ifuatavyo:
1. Kanisa la Living water pale Buyekera mlimani limechomwa moto mara 2
2. Kanisa la Hofan ministries limechomwa moto pale Rugambwa.
3. Kanisa la la International assemblies of God lilipo Magoti lilichomwa moto na kuteketea.
4. Kanisa la TAG Kihwa lilichomwa moto na kuteketea
5. Makanisa mengine maeneo ya vijijini kuchomwa moto nayo ni pamoja na Ruhanga TAG, Kakindo PAG na Kasharu EAGT.
6. Vitisho na Kushambuliwa kwa mawe wakati ibada zikiendelea mara kwa mara Kanisa la PAG Buyekera.
7. Kanisa la EAGT Kibeta kushambuliwa kwa mawe baada ya kundi la watu kuvamia kanisani miezi 3 iliyopita
8. Kanisa la Harvest kushambuliwa kwa mawe usiku na kundi la watu.
9. Jaribio la kuchomwa kisu Askofu Sesse Lazaro wakati akiwa kanisani.
10. Kifo cha kutatanisha cha Mch Jackson Kabuga wa TAG Kashabo.
Mengi ya matukio haya yameripotiwa katika vyombo vya usalama ingawa hatujapata mrejesho wowote toka vyombo hivi.
Kwa mtazamo wetu huu ni mpango uliolasimishwa wa kujenga hofu na hatimaye kukomesha uhuru wetu katika kumwabudu Mungu. Matukio haya japo yanaonekana hayahusiani lakini yamebeba maudhui inayofanana na yanatekelezwa kwa mbinu zinazofanana na inawezekana na kundi moja lenye mtandao mpana.
Kwa tamko hili tunataka yafuatayo yazingatiwe:
a. Kwa hali hii wakristo tutaweka mtandao unaojitegemea wa ki ulinzi wa nyumba za ibada, viongozi wa kiroho, na washirika wetu pamoja na hatua nyingine zozote za kiusalama tutakazoona zinafaa.
b. Tunaitaka serkali ifanye uchunguzi wa kina juu ya tukio hili na mengine yaliyotangulia na kutupatia taarifa ndani ya muda mfupi juu ya mafanikio au kukwama kwa uchunguzi.
c. Kwa wakristo wote walioguswa na kuumizwa na tukio hili maneno la Mungu toka Rumi 8:37-39 yawe faraja yetu:
"Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu." Amen
Tamko hili limetolewa na wachungaji 35 waliokaa katika kikao cha dhararula PAG tarehe 10/10/2014 na kutiwa sahihi kwa niaba yao na:-
Mch Crodward Edward.
Mwenyekiti wa Umoja wa wachungaji Bukoba.
-- Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment