Tanzania itakumbwa na balaa kubwa linalosababishwa na tofauti za kidini iwapo hali ilvyo sasa itaendelea kuwapo. Mijadala mikubwa katika ngazi zote na popote pale nchini yanahitajika sana ili kuepukane na balaa hilo. Watanzania wameishi kwa amani kwa miaka mingi sana. Hii ilisababishwa na kuwa na heshima ya dini zetu na mila zetu. Provocations za aina yeyote hazikuwapo. Cha msingi ilikuwa nchi na sio dini. Leo tunataka kuchukuwa ardhi au mali ya wafuasi fulani bila kujali reactions zitakazotokea. Kuchoma makanisa au miskiti , kujenga kwenye ardhi ya waumini fulani ikiwa ni pamoja na makaburi ni vitu vinavyo ongeza chuki kwenye jamii. Kwa nini tusiepuke hizo provocations? Dunia imebadilika sana. Leo tuna wasome wengi sana, sio wakristo tu kama ilivyokuwa hapo awali, bali pia waislaam ni wengi ambao wanaonyesha kuwa nao hawapo nyuma kwenye jumuia ambayo kwa miaka mingi walikuwa nyuma kielimu na hata kiuchumi. Inatosha vi masuala vidogovidogo kuzusha majanga. Nchi haiwezi kukaa kimya nakuona mabaya hayo yanaendelea. Sisi tulikuwa na mila zetu kabla ya dini hizo kuja. Leo wengi wetu ni waumini wa dini hizo na imekuwa ni part ya maisha yetu ya kawaida. Mababu zetu walizipokea dini hizo kwa upendo na sio kwa shari, na ndio maana waliweza kuishi kwa ujirani na hata kama walitofautiana kidini. Nawaomba ndugu wa-Tanzania na hasa wasomi msichoke kujadili suala hili kwa nia njema.
Mtanganyika
Od: "'Ngupula GW' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Do: "'ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>;
Wysłane: 23:11 Niedziela 2014-10-12
Temat: Re: [wanabidii] TAMKO LA WAKRISTO BUKOBA KUHUSIANA NA MAUAJI PAMOJA NA UCHOMAJI MAKANISA
> Tusipofika mahali tukajiuliza kwa nini vikundi vingi vya kigaidi vina base ya uislam na nini kifanyike katika nchii hii ili kukomesha kabisa mazingira yeyote ya kiugaidigaidi,tutegemee mvurugano wa amani kuendelea kukua nchini...na ndio maana tunasema tz ya sasa hatuhitaj msanii bali mtendaji na msimamiz wa mambo...ngupula
>
> 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii wrote:
>
> >N vibaya kunyamazia kama ilivyo vibaya kutamka lakini Hilder uhuru wa kuabudu nao utaleta sokomoko. Bukoba mjini kuna shule fulani ambayo kila mtu aliyeitembelea ana wasiwasi kwa mafunzo yanayotolewa pale (Nshambya). Eneo limegeuzwa 'Jangwa' au Uarabuni kwa kufugia pale kondoo. Hiyo si kitu lakini aina ya mafunzo yakiwemo ya'viungo' kila anayeona haelewi. Watu wanaishia kunong'ona kuwa huensa maandalizi ya IS yanaendelea pale. Ndio uhuru wa kuabudu uliomaanisha katika jibu lako hapo chini?
> >--------------------------------------------
> >On Sun, 10/12/14, 'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii wrote:
> >
> > Subject: Re: [wanabidii] TAMKO LA WAKRISTO BUKOBA KUHUSIANA NA MAUAJI PAMOJA NA UCHOMAJI MAKANISA
> > To: "wanabidii@googlegroups.com"
> > Date: Sunday, October 12, 2014, 12:27 PM
> >
> > Ubaguzi
> > wa dini haukuanza leo ni miaka mingi ila kwa sasa media ndio
> > ipo inauonyesha. Nikiwa umri mdogo nimeuona, kanisani
> > wakiingia wenzetu wasilamu na kufanya fujo; kujaribu kupokea
> > sakramenti na kupiga kelele yesu si Mungu. Ikafika siku za
> > sikukuu lazima kanisa liombe askari kwani walinzi wazee wa
> > kanisa hawakufaa kitu. Sanamu ya Bikira Maria ikiondolewa
> > pangoni na kukojolewa, kunyewa mavi, misalaba kuondolewa;
> > kanisa kuibiwa vikombe vyake na vitu vingine kwa sasa ni
> > kuajiri makampuni ya ulinzi. Bado tukitoka shule ya mzingi
> > ya mission kwenda ya serikali na nguo zetu ndefu na mwendo
> > wa kiumini tukitwa madukuo-kusukumwa kichwa, kupiga makwenzi
> > kichwani tukiitwa -makombo ya masista au Masea, wala nguruwe
> > na majina mengi. Ikifika siku-Maurid au kumepikwa ubwabwa
> > msikitini-about turn shuleni hapo ambapo ktk watoto 700 in
> > 1960s (shule kubwa ya serikali zile za awali sana) wakristu
> > walikuwa 15 tu. Tuliipata. Lakini, ikifika miradi ya kulea
> > na kutunza wakoma, watoto yatima na wale wanaookotwa,
> > albino, miradi ya maji, vibarua, kukwea minazi kuangua nazi
> > kanisa halikubagua ajira au needy person wa kumtunza katika
> > vituo vyake budi awe mkristu. Shule zake ilipokea dini zote
> > sisi tukisali kila mwalimu akiingia darasani wao hukaa
> > chini. Wakigawa unga wa uji wa purenda wakati wa njaa au
> > nguo za mitumba kwa masikini-hugawa bila kigezo cha dini
> > mradi tu mtu anatambuliwa ni masikini katika eneo. Wakoma
> > walitunzwa na pia wazee baadae serikali kuja kuvichukua
> > vituo hivyo na vimeishia. Shule zinazopeta za kidini wote
> > wakihudhuria isipokuwa ya masista au seminary ambapo budi
> > uwe mkristu. Kwa kifupi- huu ubaguzi wa sasa sio mpya ila
> > sasa unaongelewa kwa uwazi zaidi.
> > Bukoba au
> > Mkoa wa Kagera mtu hawezi kuamini kwamba yaliyotokea Uganda
> > wakati wa Kabaka Mutesa kuwachoma waitwao-'Mashahidi wa
> > Uganda' ndio yatakuwa yanaendelea sasa kwani huko dini
> > zote mbili ni strong sana na makardinari wakwanza wametoka
> > huko. Kinachotakiwa kwa sasa kila mtu awe na uhuru wake wa
> > kuabudu. Sali sana katika hekalu lako hata kama ikibidi
> > usali sana mpaka usijue kuwa nguo imekuvuka. Kuna uhuru wa
> > kuabudu-ugomvi wa nini mwenzako akisali wewe ukasirike? Kuna
> > siri gani hapo-anakuharibia nini mpaka uchukie? Mbona wewe
> > ukisali haji kukuharibia vyako au kukudhuru? Ni juzi tu
> > viongozi wa dini pande zote wamekaa kuungana na kuwa na
> > maamuzi ya bapoja ya kudumisha amani wanalipiga ball
> > kuonyesha upendo na ushirikiano. Kwa nini tena tuanze kurudi
> > nyuma? kuna nini hapa? Tujiangalie yasije kama yale
> > yatokeayo Jamuhuri ya kati ya wadini kuchinjana nyumba hadi
> > nyumba. Tumeoleana, tumechanganya dini na makabila-tujikanye
> > yasitukute hayo. Uhuru wa kuabudu upo kwa nini uchomee
> > wengine mahekalu yao na kuwaua? ISIS ndio imeshaingia? Mungu
> > atusaidie tuuone ukweli wa Uhuru sa Kuabudu tuliopewa na
> > Katiba ya Nchi.
> >
> >
> >
> > On Saturday, 11
> > October 2014, 23:23, 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii
> > wrote:
> >
> >
> >
> > Udini utalitesa taifa
> > hili madhali hatuko tayari kuuongelea kwa uhuru. Tunatambua
> > sana makemeo ya viongozi wetu wa siasa huku wakihisiwa
> > kuushiriki, na hapa ndipo palipo na tatizo. Nimesikiliza kwa
> > makini kusikia jina la mshukiwa. Nikahisi ni mwanzo mzuri
> > kupita kandoni mwa tatizo.
> > Mazishi ya
> > Mchungaji Kabuga yalihuzuliwa na Police wengi na habari juu
> > ya mjahidina aliyejifanya kujiunga na kanisa lake na baadaye
> > kumpa sumu tulifikiri zitafuatiliwa. Uamuzi wa familia na
> > waumini kusamehe haikuwa sababu ya serikali kunyamaza. Ni
> > makosa kuyafumbia macho matukio na badala yake kuwafuatilia
> > wanaotoa maoni kama ninayoyatoa hapa na hili natamani
> > kulisema tena
> > --------------------------------------------
> > On Sat, 10/11/14, Abdalah Hamis
> > wrote:
> >
> > Subject:
> > [wanabidii] TAMKO LA WAKRISTO BUKOBA KUHUSIANA NA MAUAJI
> > PAMOJA NA UCHOMAJI MAKANISA
> > To: wanabidii@googlegroups.com
> > Date: Saturday, October 11, 2014, 9:32 PM
> >
> > TAMKO LA WAKRISTO
> > BUKOBA KUHUSIANA NA MAUAJI PAMOJA NA UCHOMAJI
> > MAKANISA
> > TAREHE 11/10/2014.
> >
> > Baada ya tukio la kutisha
> > la kushambuliwa kwa washirika na
> > hatimaye kuuawa kwa ms
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
>
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment