Sunday, 12 October 2014

Re: [wanabidii] TAMKO LA WAKRISTO BUKOBA KUHUSIANA NA MAUAJI PAMOJA NA UCHOMAJI MAKANISA


Ipo shule Makuyuni Monduli Umasaini imeanzishwa pamoja na msikiti na wamasai wameingia dini maana dini zilizotangulia umasaini ni za kilokole sasa wanavaa kanzu na watoto wasomao hapo hijabu. Lakini yaliyokwisha kutokea hapo ni maovu ambayo sitoyataja hapa.

Lakini hakuna kiongozi nchini aliyekwenda kusema kuwa hao Maasai wasiingizwe dini ya kikristu au kiislamu kwani toka zama hizo waliosoma waliingia na waliobali remote areas wana dini zao za mila- traditionalists hao na wengineo wanan uhuru wao. Kuwa walokole au waislamu ni juu yao.

Na ukristu ulioingia Umasaini umekuwa tofauti na maeneo mengine. wameruhusu Mzee wa kimasai abaki na wake zake alionao ila asiongeze wapya (adaptation). sasa nikajiuliza-ni bible ipi tena inaruhusu haya.Isipokuwa, ukimwambia awaache-wakale wapi, utatesa mama na watoto bwerere wasio na hatia. Basi waruhuru Padri wa RC aoe maana ni binadamu na ndoa ikivunjika kisheria waoe badala ya kuwa na michepuke ambayo ni hatarishi. Sister kama muumini naye aolewe (adaptation). kumcha Mungu si lazima uwe peke budi uwe ndani ya mfumo wa kibinadamu ili umche vizuri zaidi bila ya kumkosea Mungu kimafichoni-huruhusiwi lakini wewe umezaa mafichoni.

Kuna haja ya kupiga msasa jamii sio wa kisiasa tu bali wa kidini kuwa una uhuru wako kusali kivyako mradi tu usikewr wengine na kuvunja sheria. nani ana haki ktk jinsi ya kusali? Kwa nini utake mwingine asali kama wewe. labda kuna jipya au siri hapa kisiasa.Kwani hata huko wanakopigana ISIS na wengineo si suala la dini-ni ubinafsi kukata vichwa watu, kubomoa majumba etc. wanamtegemea Marekani na nchi za Ulaya kupeleka majeshi kuwasaidia (hawa ulaya, USA ni wakristu, bendera zao zina misalaba, katiba zao zina utambua ukristu wao); huko ndio boti za wahamiaji wanakimbikia na wapandao ndege, lori, train, kudandia lori na kukaa uvunguni avuke tunnel channel (spain, austria, australia, Germany, France, UK,  USA). Hapa hakuna udini na akihojiwa anasema-anataka akasome, afanye kazi kwa amani etc-ana malengo. Muislamu, amekimbia mapambano ya dini. Na anayetoka ulaya kwenda kujiunga na ISIS anaficha uso asijulikane na akihojiwa anataka uso ufichwe-anaogopa kufa lakini yeye aliua au anaua. Akirudi ulaya-USA anarudi kwa kificho na hati za kupika-Why mtu wa dini na wa Mungu usionyeshe uso kwa ujasiri wa kumkiri Mungu uonae wa kweli na utaingia peponi kwa kukata vichwa watu? Hapa pana dini kweli au ubinafsi?

Tusiingize TZ huko kwa akina ISIS. Kila mtu kwa upande wa dini yake akazanie elimu, maendeleo kiuchumi; somesha watoto usioze vichanga; tumia hela za sadaka kuboresha mashule na vyuo, huduma za afya za shirika lako la dini uingie kwenye ushindani kiuchumi na kiajira Wale wenye kabila za mila kinyume na maendeleo za kuoza vichanga nao waache watumie raslimali kuleta maendeleo yao katika jamii yao. Mbunge na Diwani nao wapimwe jinsi kati wanahamasisha maendeleo majimboni/kata sao kio kulewa choya kutwa na kutafuta Kura kwa rushwa. Maendeleo ni kwa kushindana kwa juhudi sio kubweteka kisha uone unaonewa na kumharibia mwenzako.

Tuhubiri upendo na ushirikiano wa kweli.Tumechanganyika vibaya, tuulinde mchanganyo wetu na amani yetu. Tuepuke na hizo vurugu za katiba ambazo wengine wameshatuna mifuko fedha ili watupeleke pabaya. Tujadili badala ya maandamano na kupigana virungu. Mungu ibariki TZ.



On Monday, 13 October 2014, 0:10, 'Ngupula GW' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:


Tusipofika mahali tukajiuliza kwa nini vikundi vingi vya kigaidi vina base ya uislam na nini kifanyike katika nchii hii ili kukomesha kabisa mazingira yeyote ya kiugaidigaidi,tutegemee mvurugano wa amani kuendelea kukua nchini...na ndio maana tunasema tz ya sasa hatuhitaj msanii bali mtendaji na msimamiz wa mambo...ngupula

'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

>N vibaya kunyamazia kama ilivyo vibaya kutamka lakini Hilder uhuru wa kuabudu nao utaleta sokomoko. Bukoba mjini kuna shule fulani ambayo kila mtu aliyeitembelea ana wasiwasi kwa mafunzo yanayotolewa pale (Nshambya). Eneo limegeuzwa 'Jangwa' au Uarabuni kwa kufugia pale kondoo. Hiyo si kitu lakini aina ya mafunzo yakiwemo ya'viungo' kila anayeona haelewi. Watu wanaishia kunong'ona kuwa huensa maandalizi ya IS yanaendelea pale. Ndio uhuru wa kuabudu uliomaanisha katika jibu lako hapo chini?
>--------------------------------------------
>On Sun, 10/12/14, 'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
>
> Subject: Re: [wanabidii] TAMKO LA WAKRISTO BUKOBA KUHUSIANA NA MAUAJI PAMOJA NA UCHOMAJI MAKANISA
> To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
> Date: Sunday, October 12, 2014, 12:27 PM
>
>  Ubaguzi
> wa dini haukuanza leo ni miaka mingi ila kwa sasa media ndio
> ipo inauonyesha. Nikiwa umri mdogo nimeuona, kanisani
> wakiingia wenzetu wasilamu na kufanya fujo; kujaribu kupokea
> sakramenti na kupiga kelele yesu si Mungu. Ikafika siku za
> sikukuu lazima kanisa liombe askari kwani walinzi wazee wa
> kanisa hawakufaa kitu. Sanamu ya Bikira Maria ikiondolewa
> pangoni na kukojolewa, kunyewa mavi, misalaba kuondolewa;
> kanisa kuibiwa vikombe vyake na vitu vingine kwa sasa ni
> kuajiri makampuni ya ulinzi. Bado tukitoka shule ya mzingi
> ya mission kwenda ya serikali na nguo zetu ndefu na mwendo
> wa kiumini tukitwa madukuo-kusukumwa kichwa, kupiga makwenzi
> kichwani tukiitwa -makombo ya masista au Masea, wala nguruwe
> na majina mengi. Ikifika siku-Maurid au kumepikwa ubwabwa
> msikitini-about turn shuleni hapo ambapo ktk watoto 700 in
> 1960s (shule kubwa ya serikali zile za awali sana) wakristu
> walikuwa 15 tu. Tuliipata. Lakini, ikifika miradi ya kulea
> na kutunza wakoma, watoto yatima na wale wanaookotwa,
> albino, miradi ya maji, vibarua, kukwea minazi kuangua nazi
> kanisa halikubagua ajira au needy person wa kumtunza katika
> vituo vyake budi awe mkristu. Shule zake ilipokea dini zote
> sisi tukisali kila mwalimu akiingia darasani wao hukaa
> chini. Wakigawa unga wa uji wa purenda wakati wa njaa au
> nguo za mitumba kwa masikini-hugawa bila kigezo cha dini
> mradi tu mtu anatambuliwa ni masikini katika eneo. Wakoma
> walitunzwa na pia wazee baadae serikali kuja kuvichukua
> vituo hivyo na vimeishia. Shule zinazopeta za kidini wote
> wakihudhuria  isipokuwa ya masista au seminary ambapo budi
> uwe mkristu. Kwa kifupi- huu ubaguzi wa sasa sio mpya ila
> sasa unaongelewa kwa uwazi zaidi.
> Bukoba au
> Mkoa wa Kagera mtu hawezi kuamini kwamba yaliyotokea Uganda
> wakati wa Kabaka Mutesa kuwachoma waitwao-'Mashahidi wa
> Uganda' ndio yatakuwa yanaendelea sasa kwani huko dini
> zote mbili ni strong sana na makardinari wakwanza wametoka
> huko. Kinachotakiwa kwa sasa kila mtu awe na uhuru wake wa
> kuabudu. Sali sana katika hekalu lako hata kama ikibidi
> usali sana mpaka usijue kuwa nguo imekuvuka. Kuna uhuru wa
> kuabudu-ugomvi wa nini mwenzako akisali wewe ukasirike? Kuna
> siri gani hapo-anakuharibia nini mpaka uchukie? Mbona wewe
> ukisali haji kukuharibia vyako au kukudhuru? Ni juzi tu
> viongozi wa dini pande zote wamekaa kuungana na kuwa na
> maamuzi ya bapoja ya kudumisha amani wanalipiga ball
> kuonyesha upendo na ushirikiano. Kwa nini tena tuanze kurudi
> nyuma? kuna nini hapa? Tujiangalie yasije kama yale
> yatokeayo Jamuhuri ya kati ya wadini kuchinjana nyumba hadi
> nyumba. Tumeoleana, tumechanganya dini na makabila-tujikanye
> yasitukute hayo. Uhuru wa kuabudu upo kwa nini uchomee
> wengine mahekalu yao na kuwaua? ISIS ndio imeshaingia? Mungu
> atusaidie tuuone ukweli wa Uhuru sa Kuabudu tuliopewa na
> Katiba ya Nchi.


>
>      On Saturday, 11
> October 2014, 23:23, 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii
> <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
>
>   
>
>  Udini utalitesa taifa
> hili madhali hatuko tayari kuuongelea kwa uhuru. Tunatambua
> sana makemeo ya viongozi wetu wa siasa huku wakihisiwa
> kuushiriki, na hapa ndipo palipo na tatizo. Nimesikiliza kwa
> makini kusikia jina la mshukiwa. Nikahisi ni mwanzo mzuri
> kupita kandoni mwa tatizo.
> Mazishi ya
> Mchungaji Kabuga yalihuzuliwa na Police wengi na habari juu
> ya mjahidina aliyejifanya kujiunga na kanisa lake na baadaye
> kumpa sumu tulifikiri zitafuatiliwa. Uamuzi wa familia na
> waumini kusamehe haikuwa sababu ya serikali kunyamaza. Ni
> makosa kuyafumbia macho matukio na badala yake kuwafuatilia
> wanaotoa maoni kama ninayoyatoa hapa na hili natamani
> kulisema tena
> --------------------------------------------
> On Sat, 10/11/14, Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
> wrote:
>
>  Subject:
> [wanabidii] TAMKO LA WAKRISTO BUKOBA KUHUSIANA NA MAUAJI
> PAMOJA NA UCHOMAJI MAKANISA
>  To: wanabidii@googlegroups.com
>  Date: Saturday, October 11, 2014, 9:32 PM

>  TAMKO LA WAKRISTO
>  BUKOBA KUHUSIANA NA MAUAJI PAMOJA NA UCHOMAJI
> MAKANISA
>  TAREHE 11/10/2014.

>  Baada ya tukio la kutisha
>  la kushambuliwa kwa washirika na
>  hatimaye kuuawa kwa ms

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment