Saturday, 11 October 2014

Re: [wanabidii] TAMKO LA WAKRISTO BUKOBA KUHUSIANA NA MAUAJI PAMOJA NA UCHOMAJI MAKANISA

Udini utalitesa taifa hili madhali hatuko tayari kuuongelea kwa uhuru. Tunatambua sana makemeo ya viongozi wetu wa siasa huku wakihisiwa kuushiriki, na hapa ndipo palipo na tatizo. Nimesikiliza kwa makini kusikia jina la mshukiwa. Nikahisi ni mwanzo mzuri kupita kandoni mwa tatizo.
Mazishi ya Mchungaji Kabuga yalihuzuliwa na Police wengi na habari juu ya mjahidina aliyejifanya kujiunga na kanisa lake na baadaye kumpa sumu tulifikiri zitafuatiliwa. Uamuzi wa familia na waumini kusamehe haikuwa sababu ya serikali kunyamaza. Ni makosa kuyafumbia macho matukio na badala yake kuwafuatilia wanaotoa maoni kama ninayoyatoa hapa na hili natamani kulisema tena
--------------------------------------------
On Sat, 10/11/14, Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com> wrote:

Subject: [wanabidii] TAMKO LA WAKRISTO BUKOBA KUHUSIANA NA MAUAJI PAMOJA NA UCHOMAJI MAKANISA
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Saturday, October 11, 2014, 9:32 PM

TAMKO LA WAKRISTO
BUKOBA KUHUSIANA NA MAUAJI PAMOJA NA UCHOMAJI MAKANISA
TAREHE 11/10/2014.

Baada ya tukio la kutisha
la kushambuliwa kwa washirika na
hatimaye kuuawa kwa mshirika na kujeruhiwa vibaya kwa
mwingine kanisani Kagemu
PAG; Wachungaji na viongozi wa kiroho wa Bukoba tumepokea
taarifa hizi kwa
mshtuko mkubwa. Tumekutana tarehe 10 Oct 2014 na kutafakari
hatima ya wakristo
katika eneo hili.

Matukio rejea
tuliyojikumbusha ni kama ifuatavyo:

1.      
Kanisa
la Living water pale Buyekera mlimani limechomwa moto mara
2

2.      
Kanisa
la Hofan ministries limechomwa moto pale Rugambwa.

3.      
Kanisa
la la International assemblies of God lilipo Magoti
lilichomwa moto na
kuteketea.

4.      
Kanisa
la TAG Kihwa lilichomwa moto na kuteketea

5.      
Makanisa
mengine maeneo ya vijijini kuchomwa moto nayo ni pamoja na
Ruhanga TAG, Kakindo
PAG na Kasharu EAGT.

6.      
Vitisho
na Kushambuliwa kwa mawe wakati ibada zikiendelea mara kwa
mara Kanisa la PAG
Buyekera.

7.      
Kanisa
la EAGT Kibeta kushambuliwa kwa mawe baada ya kundi la watu
kuvamia kanisani
miezi 3 iliyopita

8.      
Kanisa
la Harvest kushambuliwa kwa mawe usiku na kundi la watu.


9.      
Jaribio
la kuchomwa kisu Askofu Sesse Lazaro wakati akiwa
kanisani.

10.   Kifo
cha kutatanisha cha Mch Jackson Kabuga wa TAG Kashabo.

Mengi ya matukio haya
yameripotiwa
katika vyombo vya usalama ingawa hatujapata mrejesho wowote
toka vyombo hivi.

Kwa mtazamo wetu huu ni mpango
uliolasimishwa wa kujenga hofu na hatimaye kukomesha uhuru
wetu katika
kumwabudu Mungu. Matukio haya japo yanaonekana hayahusiani
lakini yamebeba
maudhui inayofanana na yanatekelezwa kwa mbinu zinazofanana
na inawezekana na
kundi moja lenye mtandao mpana.

Kwa tamko hili tunataka yafuatayo
yazingatiwe:

a.       Kwa
hali hii wakristo tutaweka mtandao unaojitegemea wa ki
ulinzi wa nyumba za
ibada, viongozi wa kiroho, na washirika wetu pamoja na hatua
nyingine zozote za
kiusalama tutakazoona zinafaa.

b.      Tunaitaka
serkali ifanye uchunguzi wa kina juu ya tukio hili na
mengine yaliyotangulia na
kutupatia taarifa ndani ya muda mfupi juu ya mafanikio au
kukwama kwa
uchunguzi. 

c.      
Kwa wakristo wote walioguswa na kuumizwa na
tukio hili maneno la Mungu toka Rumi 8:37-39 yawe faraja
yetu:

 "Lakini katika mambo hayo yote
tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. Kwa
maana nimekwisha
kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala
malaika, wala wenye
mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye
uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini,
wala kiumbe kinginecho
chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika
Kristo Yesu Bwana
wetu." Amen


 

Tamko
hili limetolewa na
wachungaji 35 waliokaa katika kikao cha dhararula PAG tarehe
10/10/2014 na
kutiwa sahihi kwa niaba yao na:-

 

Mch Crodward Edward.

Mwenyekiti wa Umoja wa wachungaji
Bukoba.



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment