Thursday, 23 October 2014

Re: [wanabidii] JK: Mfumo wa Rais kung'atuka madarakani ni mzuri

angeshauri na ubunge na wenyeviti wa vyama ingefaa sana. haingii
akilini mwalimu anapofikisha miaka 60 anastaafishwa kwa nguvu lakini
urais wengine wanakaribia miaka sabini wanautaka.

On 10/23/14, Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com> wrote:
>
>
> JK: Mfumo wa Rais kung'atuka madarakani ni mzuri
>
> • Unatoa nafasi kwa nchi kupata mawazo na fikra mpya
> • Anaamini Tanzania itapata Rais bora zaidi wa kumrithi yeye
> • Atamani muda wake umalizike akalee wajukuu
>
> Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
> amesema kuwa mfumo wa Tanzania ambako Rais anatumikia nafasi ya uongozi kwa
>
> muhula wa miaka mitano na siyo zaidi ya miaka 10 ni mfumo mzuri na
> unaovutia kwa sababu unaiwezesha nchi kupata fikra na mawazo mapya.
>
> Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa anaamini kuwa Tanzania itapata Rais bora
> zaidi kuliko yeye, Rais ambaye ataiwezesha Tanzania kusonga mbele kwa kasi
> kubwa zaidi.
>
> Rais Kikwete pia amesema kuwa anayo hamu kubwa ya kumaliza muda wake wa
> uongozi, ili arudi kijijini kushughulika na wajuu wake na mifugo yake.
>
> Rais Kikwete ametoa kauli hiyo leo, Jumatano, Oktoba 22, 2014, mjini
> Beijing, China, wakati akizungumza na mabalozi wa Afrika wanaoziwakilisha
> nchi zao katika China.
>
> Mkutano huo uliofanyika kwenye Nyumba ya Kufikia Wageni wa Serikali ya
> China ya Diaoyutai, ulikuwa shughuli ya kwanza ya Rais Kikwete katika ziara
>
> yake rasmi ya siku sita ya Jamhuri ya Watu wa China ambako amealikwa na
> Rais Xi Jinping.
>
> Wakati wa maswali na majibu, Mheshimiwa Balozi Sola Onadipe, Naibu Balozi
> wa Nigeria katika China, alishangazwa na kauli ya Rais Kikwete kuwa
> anatamani amalize muda wake wa uongozi, ili astaafu na kusema kuwa
> lingekuwa jambo la maana kwa Afrika kama viongozi wengine wangekuwa na
> mawazo ya namna hiyo ya kuheshimu Katiba za nchi zao na kung'atuka kwenye
> uongozi muda wao unapowadia.
>
> Rais Kikwete amemwambia Balozi huyo: " Ni kweli naona kama muda hauendi kwa
>
> kasi ya kutosha, ili niweze kuwa raia wa kawaida na nipate muda wa kuchunga
>
> ng'ombe na mbuzi wangu na nilime mananasi yangu kwa nafasi ya kutosha.
> Lakini Mheshimiwa Balozi usishangazwe na utayari wangu kuondoka katika
> uongozi."
>
> "Kwanza utaratibu huu wa miaka mitano ama miaka 10 ni utaratibu wa
> Kikatiba, ni jambo lililoko katika Katiba yetu na hatuna kishawishi cha
> kulibadilisha. Pili, kazi hii ya Urais ni kazi ngumu sana. Kwa hakika,
> binafsi nawaonea gele sana wenye nguvu na ubavu wa kutaka kubakia kwenye
> kazi hii kwa miaka mingi. Pengine wana nguvu zaidi kuliko mimi," amesema
> Rais Kikwete na kuongeza:
>
> " Lakini pia kuna uzuri katika mfumo huu wa kwetu kwa sababu kila baada ya
> miaka mitano na hata kama ni baada ya kila miaka kumi, anaingia mtu
> mwingine madarakani akiwa na fikra mpya na mawazo mapya."
> " Mfumo huu ni mfumo unaoniridhisha sana na wala hakuna kinachonishawishi
> nibakie katika madaraka zaidi ya muda wangu kikatiba. Nina hakika, nchi
> yetu itapata kiongozi mwingine, bora kuliko hata mimi, kuongoza vizuri nchi
>
> yetu."
>
> Rais Kikwete pia amesema kuwa siyo busara pia kwa kiongozi kuwasikiliza
> wale wanaoshauri wakisema kuwa akiondoka madarakani nchi itavurugika.
> "Kwa hakika, hawa wanatetea maslahi yao tu wakisema kuwa ukiondoka wewe
> madarakani, wao hawatakuwa tena mabalozi ama mawaziri ama nafasi nyingine
> yoyote."
>
> Imetolewa na:
> Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
> Ikulu,
> DAR ES SALAAM.
>
> 22 Oktoba, 2014
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
>

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment