Monday, 13 October 2014

Re: [wanabidii] Jaji Warioba: Tusidanganyane, kutaka Serikali tatu ni kuvunja Muungano



On Monday, October 13, 2014, 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
> Hapana. Kiii si kubombea madaraka. Kiini ni mwelekeo wa kuuvunja Muungano kwa kuiongezea nguvu Serikali ya Zanzibar ikaelekea kuwa Nchi badala ya ilivyokuwa toka mwanzo wakati wa uasisi wake. kwa kupima mambo. na kuona ugumu wa kuirekebisha serikali ya zanzibar kurudi mahala pake zikiwa mbili tu, mazingira ambayo yamemfanya rais wa Zanzibar amuone wa Muungano kama 'mwenzake ikapendekezwa ziundwe tatu ili mbili kwa kadri tunavyosonga mbele itafikia mahala itagundua mwenzao ni Tnganyika. Ukweli ni kuwa ni hatari sana kuendelea kuimarisha nguvu ya Zanzibar huku Tanganyika unainyamazia. Vijana wa Tanganyika watakapokuja hawatakuja kudai kurekebisha muungano ila Tanganyika yao. Njia pekee salama ya kulinda muungano ni Serikali tatu ambazo zitaharakisha kuingia serikali moja. na itakuwa hivi: Wazanzibari wana mambo mengi wanayafaidi ndani ya mfumo wa serikali mbili. ambayo kwa ukubwa wake Watanganyika hawajai (sasa wameanza kujali) Siku wakiyakosa kwa sababu
>  ya kuwepo Tang\anyika haiweekani wakaamua kuuvunja muungano ila watarufi kujadiliana na tanganyika ndani ya Mfumo ulio katika Rasimu ya pili ya Tume ya warioba. Wanaweza kuja kwa kuomba zirudishwe serikali mbili na wakaambiwa hapana. Ama Tatu ama moja. hawawezi kupinga labda kama hawaoni udogo wa visiwa vyao
> Hekima hiyo inawezekana ndani ya mfumo wa serikali tatu (maana katikaq huu wa mbili imeshindikana.
>
> Ieleweke muungano umekuwa dhaifu sasa.
> 1964 Rais wa Jamhuri ya Muungano aliweza kuchanganya udongo wa Zanzibar na tanganyika peke yake huku wa Zanzibar akiwa anaangalia. Ilikuwa hivyo kwa sababu yeye alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano akiwawakilisha wazanzibari na watanganyika.
> Jumatano iliyopita tumemkosa mtu mmoja kupokea katiba pendekezwa mpaka Shein akaipokea kwa niaba ya waZanzibari na Kikwete sijui alipokea kwa niaba ya nani maana bila kuwawaqkilisha wazanzibari hata watanganyika hawawakilishi. Ni jambo dogo sana kijuu juu lakini lipimeni muone linaashiria nini
> --------------------------------------------
> On Mon, 10/13/14, Telesphor Magobe <tmagobe@gmail.com> wrote:
>
>  Subject: Re: [wanabidii] Jaji Warioba: Tusidanganyane, kutaka Serikali tatu ni kuvunja Muungano
>  To: wanabidii@googlegroups.com
>  Date: Monday, October 13, 2014, 6:10 AM
>
>  "...kuna watu
>  wanafikiri kuimarisha Muungano ni kuwa na serikali tatu,
>  unaimarishaje? Sasa
>   hivi kiini ni ugomvi wa madaraka kati ya Serikali ya
>  Muungano na
>  Serikali ya Zanzibar. Hivi ukileta serikali tatu, ugomvi huu
>
>  hautakuwapo? Ukileta Serikali ya Tanganyika yenyewe haitadai
>  madaraka?
>  Mwisho wataomba madaraka hadi Serikali ya Muungano isiwe na
>  chochote. Hivi
>   Serikali ya Tanganyika kwa mfano ikawapo, ikataka iwe na
>  wimbo wake wa
>  Taifa, bendera yake, nembo yake, kisha inadai ifanye
>  biashara ya nje,
>  unafikiri tutakuwa tumefika wapi? Ni kwamba tutakuwa
>  tunaondoa Muungano na kurudisha Tanganyika na Zanzibar.
>  Lakini kama wananchi wanataka hivyo, sawa. Lakini
>   tukivunja Muungano madhara yake ni makubwa sana kwa pande
>  zote mbili.
>  Mimi naamini wale wanaotaka serikali tatu wanajua nia yao ni
>  kuvunja
>  Muungano na huu ndio ukweli. Ukianzisha serikali tatu, maana
>  yake
>  unavunja Muungano." Haya maneno yananipa shida. Si hivi
>  ambavyo huwa tunamsikia Warioba akielezea kwa nini tume
>  iliweka muungano wa serikali tatu kama ilivyoelezwa kwenye
>  rasimu na bango kitita. Huenda mwandishi amefanya tafsiri
>  yake. Ninasema hivi kwa sababu muundo wa serikali tatu
>  unaonekana kwenye uhalisia wenyewe wa utendaji wa serikali.
>  Mfano tu, ni muundo wa mahakama. 1) Kuna Mahakama Kuu ya
>  Tanzania (ambayo haina mamlaka Zanzibar). 2) Kuna Mahakama
>  Kuu ya Zanzibar (ambayo haina mamlaka Tanzania Bara) 3) Kuna
>  Mahakama ya Rufaa (ambayo ina mamlaka Tanzania Bara na
>  Zanzibar). Muundo huu upo na haujavunja muungano. Pia kuna
>  mifano mingine, ambayo kiutendaji inaonyesha wazi kwamba
>  tuna serikali tatu ingawa kinadharia zinasemwa mbili. Kwamba
>  nchi mbili zinapounga ni ama zinaunda serikali moja (siyo
>  mbili), ama zinaunda serikali tatu za shirikisho. Hivyo,
>  tuwe makini sana tusiwapotoshe wananchi as if hatujamsikia
>  Warioba akizungumzia serikali 2 na 3 na kwamba haya
>  mahojiano ndiyo tu yameibua kile ambacho Warioba anakiamini.
>
>
>  2014-10-12 20:02
>  GMT+03:00 Jane Mwakalukwa <mwakalukwa@gmail.com>:
>  Raia
>  Mwema: Unazungumziaje suala la Katiba mpya?Jaji
>  Warioba: Sina hakika kama viongozi wetu wanaelewa
>  ni kitu gani kilicho muhimu. Nadhani tunaingia katika tatizo
>  hili la kila mmoja anatazama manufaa yake.Katiba
>  hii msingi wake ulikuwa ni chama kimoja. Tumefanya
>  mabadiliko kuna mambo ambayo yametokana na chama kimoja
>  lakini ni ya msingi katika kuendesha nchi. Ni muhimu
>  tuyatazame na kati ya hayo ni Tanzania ya aina gani
>  tunayotaka kuijenga.Moja
>  ambalo limetokana na mfumo wa chama kimoja ni kwamba TANU,
>  ASP na CCM vilikuwa na itikadi ambayo ilikuwa inafafanua
>  tunataka Tanzania ya aina gani na wananchi wakaielewa.Bila
>  kujali ulikuwa unakubaliana na Ujamaa na Kujitegemea ulijua
>  huu ndio mwelekeo wetu tunataka Tanzania ya Ujamaa na
>  Kujitegemea. Ni Ujamaa na Kujitegemea na miiko yake ilikuwa
>  inaeleweka nchi nzima. Wananchi walikuwa wanatoa uamuzi
>  kulingana na itikadi.Sasa
>  hakuna. Hatujui ni Tanzania gani tunayotaka kuijenga na hapo
>  nadhani tunapokwenda kwa wananchi tutarajie hilo kwamba
>  kubwa tunalotaka kutoka kwa wanannchi ni Tanzania gani
>  wanataka tuijenge.Tusiende
>  kwamba kulazimisha kuyazungumza haya tunayoona ni makubwa
>  kwa sababu watazungumza kwa jinsi wanavyoona mambo yao.
>  Unaweza kwenda sehemu ukakuta tatizo lao ni ardhi. Wengine
>  wanaweza kuzungumzia madini. Tuyasikilize yote haya na
>  kutokana na hayo utaona Watanzania wanataka Tanzania ya aina
>  gani.Katika
>  kile kifungu cha malengo muhimu ya Taifa haya yaelezwe ndani
>  ya Katiba kwamba Watanzania malengo waliyonayo ni
>  haya.Kwa
>  hiyo, kwangu hili ni muhimu la sivyo tutabaki katika yale
>  yale ya kujidanganya kwamba Tanzania ni nchi ya Ujamaa na
>  Kujitegemea wakati ile misingi haipo. Lazima tujipange
>  kuhakikisha tunajenga Tanzania tunayotaka. Katiba ni
>  wananchi na wananchi waachwe waamue mambo yao muhimu.Tusipofafanua
>  Tanzania tunayoitaka bado tutakuwa na mgogoro kwa sababu
>  hapatakuwa na yard stick ya kuwapima viongozi na
>  Tanzania tunayotaka kuijenga.Kuna
>  suala la msingi kuwa wananchi ndiyo wenye madaraka. Lazima
>  tueleze ni madaraka gani yako kwa wananchi, kwamba wana
>  uwezo upi wa kukataa viongozi.Saa
>  hivi kuna kujichanganya, unakuta tunasema madaraka yako kwa
>  wananchi lakini tumeyahamisha kwa kiwango kikubwa kwenda
>  kwenye dola au kwenye vyama vya siasa.Serikali
>  utakuta imepewa madaraka makubwa lakini wanasema ni kwa
>  niaba ya wananchi. Vyama vya siasa navyo ni hivyo, vimepewa
>  madaraka makubwa nao wanasema ni kwa manufaa ya
>  wananchi.Sasa
>  hivi pamoja na Katiba kusema kwamba msingi wa madaraka ni
>  wananchi kwa hiyo wanachagua wawakilishi lakini bado msingi
>  huo unabanwa kwamba unawaambia kama unataka mwakilishi
>  lazima ufuate taratibu hizi. Kama wewe si mwanachama wa
>  chama cha siasa basi huna nafasi hiyo.Kwamba
>  watu wanaweza kumchagua mwakilishi lakini chama cha siasa
>  kinaweza kumfukuza huyu mwakilishi. Wanakorofishana ndani ya
>  chama wanamfukuza na anapoteza mandate ya
>  wananchi kama vile mwakilishi huyo alichaguliwa na chama.
>  Lazima mipaka iwekwe ndani ya Katiba.Baada
>  ya hapo tuangalie zile taasisi muhimu, Bunge, Serikali na
>  Mahakama tuangalie upya mgawanyo wa madaraka haya,
>  ile separation of powers iwepo lakini pia lazima
>  kuwapo checks and balances. 
>
>  Sasa hivi nadhani itabidi
>  tuimarishe Mahakama. Iwe na uhuru wa kifedha, wasitegemee
>  hisani ya Katibu Mkuu wa Hazina.Kama
>  tumefika mahali unasema Bunge litapata bajeti kiwango fulani
>  na vyama vya siasa vinapata bajeti fulani, Mahakama nayo
>  lazima tuseme wanapata asilimia fulani.Tuingie
>  kwenye utendaji, tuangalie mgawanyo wa madaraka kati ya Rais
>  na taasisi za utendaji. Najua Rais lazima atakuwa na
>  madaraka lakini kuna mahali pengine ama madaraka haya
>  yanaweza kwenda kwenye taasisi au utendaji wake Rais lazima
>  ashauriwe.Inawezekana
>  tukaamua, je, kuna umuhimu wa kumpa Rais madaraka ya kuteua
>  mawaziri lakini wawe wanathibitishwa mahali? Ateue majaji
>  lakini wathibitishwe mahali.Sasa
>  hivi naona kuna watu hawataki Rais awe na madaraka makubwa
>  lakini mimi nafikiri Rais lazima awe na madaraka isipokuwa
>  tuangalie yale mengine awe nayo lakini kwa kushauriwa.
>  Lazima katika Taifa kuwe na mtu mnasema lazima awe na
>  madaraka haya, isipokuwa ni kutengeneza utaratibu.Hata
>  kama tunataka Rais wa kikatiba tu ingawa sioni hilo kama ni
>  zuri katika nchi, kama tunataka awe waziri mkuu sawa. Lakini
>  suala la madaraka ni muhimu.Katika
>  mabadiliko ya mwaka 1984 nia ilikuwa kupunguza madaraka ya
>  Rais, Waziri Mkuu asimamie zaidi utendaji lakini sasa hivi
>  unaona kama Waziri Mkuu hana madaraka ya kusimamia
>  utendaji.Imejitokeza
>  Rais anasimamia utendaji, anakwenda wizara kwa wizara,
>  anatoa maagizo ya utendaji, Katiba haijamzuia lakini
>  imemuwekea mtu wa kumsaidia, nimeona kwenye Bunge Waziri
>  Mkuu anaulizwa maswali ya papo kwa papo anazumgumzia sera.
>  Sera si ya kwake, iko chini ya Rais.Kwa
>  hiyo tutakapozungumza Katiba ni lazima hapa tufafanue nini
>  kazi za waziri mkuu au kama kuna sababu ya kuwa na waziri
>  mkuu. Tuzungumze, je, mawaziri wawe kama walivyo kutokana na
>  Bunge?Bunge
>  nalo liangaliwe, madaraka yake yafafanuliwe. Unajua wakati
>  mwingine Bunge limeingilia mambo ya utendaji, lazima sasa
>  iwepo mipaka kati ya Serikali na Bunge na tujue nani
>  anastahili kuchaguliwa kwenda bungeni, tujue utaratibu wa
>  kupiga kura.Sasa
>  hivi wanazungumzia sana Tume ya Uchaguzi. Tuzungumzie hili.
>  Kuna watu wanafikiri lazima iwakilishe makundi fulani
>  fulani. Zanzibar wanazungumzia uwakilishi wa vyama.
>  Kwingine, Afrika Kusini wanaye kamishna. Ghana wanayo tume
>  ambayo mwenyekiti ni yule yule, amekuwapo kwa muda kwa
>  sababu yuko huru.Naamini
>  Tume yetu ikiwa na wajumbe kutoka vyama vya siasa haitakuwa
>  huru. Nadhani utaratibu wa Katiba mpya utuwezeshe kupata
>  maoni ya wananchi.Ninachokiona
>  sasa ni kila kundi kwa maslahi yake linatumia hoja ya
>  wananchi kuwa wanataka utaratibu fulani. Vivyo hivyo,
>  Serikali nayo inataka kuweka mipaka fulani kwa maslahi ya
>  wananchi.Tusiweke
>  mipaka. Wananchi watoe mawazo yao. Kuna vyama vya siasa
>  vinasema kwa manufaa ya wananchi tuwe na Bunge la Katiba
>  ambalo litachagua Tume na kutoa hadidu za rejea na kusimamia
>  mchakato na baada ya kupitisha watakwenda kwa
>  wananchi.Sikubaliani
>  na hilo. Wananchi waachwe wazungumze yote wanayotaka, Katiba
>  yao iweje. Wakishakuzungumza, hiyo tume itengeneze muswada
>  wa katiba urudi kwa wananchi. Wazungumze, kusiwe na kikundi
>  hapa katikati kinasema kwa manufaa ya wananchi.
>  Hapana.Wananchi
>  wazungumze muswada na chombo cha kupitisha kipitishe
>  baadaye. Wasilete vikao hapa katikati huku wanajitafutia
>  nafasi. Mchakato huu uende moja kwa moja kwa wananchi.
>  Tusiwawekee mawazo.Kuna
>  wanaharakati wanataka kuleta mambo ya kuwajaza wananchi.
>  Nina hakika wananchi wakiachiwa uhuru, watasema na wataalamu
>  watapanga vizuri. Nasisitiza la msingi ni kuwaacha wananchi
>  waseme wanataka nchi ya namna gani.Suala
>  la Muungano pia liwe katika Katiba. Tusipokuwa makini kwa
>  maneno yanayozungumswa sasa tutavunja Muungano.Muungano
>  huu una misingi yake na upo kwa manufaa ya wananchi.
>  Tufafanue manufaa hayo ni nini kwa mwananchi wa
>  kawaida.Wakati
>  wote kwa mwananchi wa kawaida, kumekuwa hakuna matatizo ya
>  Muungano. Matatizo yanatoka kwenye midomo ya viongozi.Shughuli
>  za wananchi wa kawaida haziangalii orodha ya mambo ya
>  Muungano, bali haki yao kama raia. Wanajiona ni raia katika
>  shughuli zao za kibiashara au nyingine. Mwananchi wa kawaida
>  anaona anayo haki ya kufanya biashara mahali popote.
>  Wananchi wamezoa hivyo. Msiwafikishe mahali wakajiona kuwa
>  kwenda Zanzibar au kuja Bara inabidi wafuate taratibu za
>  kwenda Kenya au Uganda.Tunayo
>  matatizo ya madaraka, kwamba unazo Serikali mbili kwa hiyo
>  yale yaliyomo kwenye orodha ya Muungano ni kuonyesha
>  Serikali hii ina madaraka gani. Wanagombania madaraka.Kama
>  suala ni mafuta au mengine tuzungumze. Inategemea
>  mnavyokubaliana, tusije kuongeza au kupunguza kwenye orodha
>  mambo ambayo yatakuja kuwatenganisha wananchi. Kama kwa
>  mfano, kuna watu wanafikiri kuimarisha Muungano ni kuwa na
>  serikali tatu, unaimarishaje?Sasa
>  hivi kiini ni ugomvi wa madaraka kati ya Serikali ya
>  Muungano na Serikali ya Zanzibar. Hivi ukileta serikali
>  tatu, ugomvi huu hautakuwapo? Ukileta Serikali ya Tanganyika
>  yenyewe haitadai madaraka? Mwisho wataomba madaraka hadi
>  Serikali ya Muungano isiwe na chochote.Hivi
>  Serikali ya Tanganyika kwa mfano ikawapo, ikataka iwe na
>  wimbo wake wa Taifa, bendera yake, nembo yake, kisha inadai
>  ifanye biashara ya nje, unafikiri tutakuwa tumefika
>  wapi?Ni
>  kwamba tutakuwa tunaondoa Muungano na kurudisha Tanganyika
>  na Zanzibar. Lakini kama wananchi wanataka hivyo,
>  sawa.Lakini
>  tukivunja Muungano madhara yake ni makubwa sana kwa pande
>  zote mbili. Mimi naamini wale wanaotaka serikali tatu
>  wanajua nia yao ni kuvunja Muungano na huu ndio ukweli.
>  Ukianzisha serikali tatu, maana yake unavunja
>  Muungano.-
>  See more at: http://www.raiamwema.co.tz/jaji-warioba-tusidanganyane-kutaka-serikali-tatu-ni-kuvunja-muungano#sthash.pzEssMWC.EFRLlLub.dpuf
>
>
>
>
>  --
>
>  Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
>   
>
>  Kujiondoa Tuma Email kwenda
>
>  wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
>   Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
>   
>
>  Disclaimer:
>
>  Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
>  for any legal consequences of his or her postings, and hence
>  statements and facts must be presented responsibly. Your
>  continued membership signifies that you agree to this
>  disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>  ---
>
>  You received this message because you are subscribed to the
>  Google Groups "Wanabidii" group.
>
>  To unsubscribe from this group and stop receiving emails
>  from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>
>  For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
>
>
>
>
>
>
>  --
>
>  Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
>   
>
>  Kujiondoa Tuma Email kwenda
>
>  wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya
>  kudhibitisha ukishatuma
>
>   
>
>  Disclaimer:
>
>  Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
>  for any legal consequences of his or her postings, and hence
>  statements and facts must be presented responsibly. Your
>  continued membership signifies that you agree to this
>  disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>  ---
>
>  You received this message because you are subscribed to the
>  Google Groups "Wanabidii" group.
>
>  To unsubscribe from this group and stop receiving emails
>  from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>
>  For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
>
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
>

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment