Wandugu nimesoma hii hadithi ndefu sana aliyoiandika huyo anayejiita Katabazi.
Nahisi kama vile Ana visa binafsi na Halima Mdee. Maneno na lugha aliyotumia haina tofauti na maneno watumiao mijimama mashangingi wa mjini. Halafu naambiwa anasomea fani ya sheria na ni mwandishi wa habari.
This is shame to her!
Sikutegemea mtu msomi kama huyu angeweza kuthubutu kutumia lugha isiyo na staha kama hii. Waalimu wake kama mmo katika janvi hili hili hebu tusaidie kumuelimisha jamani. Sina hakiki CHADEMA watakapo ingia ikulu 2015 na hakuna akashika wizara ya habari na utangazaji Katabazi atakuwa na lipi la kusema, Au anafikiria CCM wataendelea kutawala nchi hii milele! Haiwezekani.
Katabazi badirika, acha ushabiki usiokuwa na tija!
Nahisi kama vile Ana visa binafsi na Halima Mdee. Maneno na lugha aliyotumia haina tofauti na maneno watumiao mijimama mashangingi wa mjini. Halafu naambiwa anasomea fani ya sheria na ni mwandishi wa habari.
This is shame to her!
Sikutegemea mtu msomi kama huyu angeweza kuthubutu kutumia lugha isiyo na staha kama hii. Waalimu wake kama mmo katika janvi hili hili hebu tusaidie kumuelimisha jamani. Sina hakiki CHADEMA watakapo ingia ikulu 2015 na hakuna akashika wizara ya habari na utangazaji Katabazi atakuwa na lipi la kusema, Au anafikiria CCM wataendelea kutawala nchi hii milele! Haiwezekani.
Katabazi badirika, acha ushabiki usiokuwa na tija!
From: 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii
Sent: 10/9/2014 18:39
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] HALIMA MDEE,TULIA UZAE
Angemshauri na Nelson Mandela asibishane na sheria za kikaburu maana nazo zilikuwa halali
Ni hatari kuwa na watu kama hawa katika jamii. Ni wabaya kuliko mabwaza zao
--------------------------------------------
On Thu, 10/9/14, Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com> wrote:
Subject: [wanabidii] HALIMA MDEE,TULIA UZAE
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Thursday, October 9, 2014, 11:07 AM
HALIMA
MDEE,TULIA UZAE
Na Happiness Katabazi
MAKUNGWI na wanawake waliotuzidi umri upenda Kuwaasa watoto
wa kike hususani wale walitimiza umri halali wa kuingia
Kwenye mahusiano hususani Kwenye ndoa Kuwa :'
Mwanamke yeyote aliyekamilika kuitwa mwanamke na aliyefundwa
anapaswa kufanya vurugu, utundu chumbani wakati akiwa na
mumewe au Mpenzi wake wakifanya tendo la ndoa '.Nimelazimika
kutumia Msemo huo wa Makungwi kwasababu , kwa zaidi ya wiki
Moja sasa tumeshuhudia Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake
(BAVICHA) Halima Mdee (35) akifanya vurugu na kupingana na
amri halali za Jeshi la Polisi Mkoa Kanda Maalum ya Dar es
Salaam.Kamanda
wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alitangaza
kuyapiga marufuku maandamano yaliyokuwa yameandaliwa na Mdee
lakini Mdee na wenzake waliipuuza amri hiyo ya Kova na
mwisho wa siku Oktoba 4 Mwaka huu, Mdee na wanawake wachache
wa Chama hicho walijaribu kuandamana wakaishia
kusambaratishwa na Polisi na Kukamatwa kupelekwa Katika
Kituo Cha Polisi OysterbayOktoba
6 Mwaka huu, Mdee na wenzake wakafunguliwa Kesi ya jinai
mbele ya Hakimu Janeth Kaluyenda, Wakili wa Serikali Mkuu,
Bernard Kongola alidai Mbali na Mdee washitakiwa wengine ni
Rose Moshi (45), Renina Peter 'Lufyagila', Anna
Linjewile (48), Mwanne Kassim (32), Sophia Angel (28),
Edward Julius (25), Martha Mtiko (27) na Beatu Mmari
(35).Kongola
alidai kuwa washtakiwa hao Oktoba 4, 2014, wakiwa Mtaa wa
Ufipa, walikiuka amri halali ya kutawanyika iliyotolewa na
Mrakibu wa Polisi (SP), Emmanuel Tillf kwa niaba ya Jeshi la
Polisi kitendo ambacho ni kinyume na Kifungu cha 124 cha
Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 iliyofanyiwa
marekebisho mwaka 2002.Katika
shtaka la pili, siku hiyo ya tukio katika eneo hilo,
washtakiwa hao wanadaiwa wote kwa pamoja , walifanya
mkusanyiko usio halali kwa lengo la kutembea kwenda kwenye
Ofisi ya Rais Ikulu .Alidai kuwa kosa hilo ni kinyume na
Kifungu cha 74 na 75 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya
16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.Na
washitakiwa Hao walikana Mashitaka ila Masharti ya dhamana
walishindwa kutimiza,Mahakama ikaamuru wapelekwe gerezani
hadi Jana walipopata dhamana.Kesi
hiyo ikaairishwa hadi Oktoba 21 Mwaka huu,itakapokuja
kwaajili ya washitakiwa hao kusomewa maelezo ya awali
kwasababu upelelezi wa Kesi hiyo umekamilika.Mdee
ni msomi wa Sheria na nimiongoni mwa wanasiasa wachache
vijana wenye ujasiri wa kujitokeza hadharani kukataa jambo
ambalo yeye anafikiri jambo Hilo halina maana.Mimi
Nampongeza kwa kipaji hicho tu Cha uthubutu wa kujitokeza
hadharani Mara kwa Mara kupinga licha Mimi binafsi wakati
mwingine uwa sikubalini Sababu zake nyingine anazotumia
kupinga jambo Fulani.Lakini
nitajisikia vibaya Kama sitampongeza Mdee ambaye ki umri
tupo sawa ,kwa kuweza kuchaguliwa Kuwa Mwenyekiti wa
BAWACHA.Hakika
ameandika historia ya kijana mwenye umri Kama wake kuaminiwa
na Chama Chake kupewa nafasi hiyo ambayo a anaongoza
wanawake ambao ni wanachama wa CHADEMA ambao wengine
wamezidi yeye na mama yake umri.Hongera Mdee kwa ushindi
huo.Maana
matendo mengine anayoyatenda ya kuamasisha vurugu, uzushi ni
wazi kabisa anaonekana ni mwali 'msungo'. Yaani ni
mwanamke ambaye hajafundwa Mafundo ya kike au kama alifunda
basi anayapuuza.Anachokifahamu
yeye ni Mafunzo ya darasani na siasa chafu za ugovi ambazo
zikazidi kumshushia heshima yake Kwa Wapiga kura wake wa
jimbo la Kawe, Jamii ya wapenda ustaharabu, Amani na Utawala
wa Sheria na wasomi.Kinachonikera
kwa Mdee hii tabia yake ya kufanya 'Usela Mavi'
wakati amelelewa Katika familia ya wasomi Kwani baba yake ni
msomi na Mdee Mwenyewe amepata fursa ya kusoma shule lakini
tunamshangaa a ataenda matendo ambayo hawapaswi kutendewa na
mtu Kama yeye.Mdee
ni msomi wa Sheria na msomi yoyote wa Sheria, Mwaka wa
kwanza wa shahada ya kwanza ni lazima ufundishwe somo la
Criminal Law ambalo somo Hilo mwalimu pamoja na mambo
mengine anatumia Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16 ya
Mwaka 2002 ( Penal Code).Na
hiyo Sheria inaweka wazi makosa mbalimbali kwa Kifungu kwa
Kifungu Mdee amelisoma na kufaulu somo Hilo na anafahamu
Kuwa ndani ya Sheria Hilo Kuwa kuna kosa la kukaidi amri ya
Jeshi la Polisi, kufanya mkusanyiko haramu Adhabu zake ni
zipi.Lakini
Mdee ambaye amekuwa akijitapa eti yeye ni Mwanasheria mzuri
ndiyo amekuwa miongoni mwa wasomi wa Sheria ambao
ameshitakiwa Kutenda matendo ya kuvunja Sheria wazi wazi kwa
kukaidi amri ya Jeshi la Polisi iliyokuwa ikimtaka
asiandamane kwa Kigezo eti Rais Jakaya Kikwete ameamualia
Ikulu.Nimuulize
Halima hivi Rais Kikwete ni Hawara yako,ndigu yako hadi
mkutane sehemu huyo Kikwete akupe mualiko uende Ikulu ,wewe
na hao wafuasi wako bila Katibu wa Rais kujua mualiko
huo?Rais
ni Taasisi kwa wale tunaofahamu, hivyo huwezi kujikurupukia
tu ukaamka Leo ukachukua kundi la wahuni wenzio na mabango
juu ukasema unaenda Kumuona Rais Ikulu eti Rais Kikwete
amekupa Mwaliko?Kama
siyo kumsingizia Rais na kumchonganisha Rais Kikwete na
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ni kitu gani?
Maana Kama Rais Kikwete alikualika kweli.Si haraka sana Rais
angetengua amri ya Kamanda Kova ya kuwazuia msiende kumuona
Ikulu?Unafikiri
ni kwanini amri ya Kova iliendelea kubaki Kama ilivyo? Jibu
ni Jepesi tu ,Halima ni muongo, Mzushi na aliyekuwa anataka
kujipatia umaarufu wa kijinga Kuwa eti Mwaliko wa Rais
Kikwete amemwalika Ikulu.Alichokuwa
akikitafuta Halima ni kutaka kujionyesha yeye ndiyo
Mwenyekiti Mpya wa BAWACHA na kwamba ni ngangari kweli kweli
kuliko Mwenyekiti aliyepita Suzan Lyimo na hivyo
anaushawishi mkubwa wa kuweza kuwashawishi wanachama
wanawake wa Chama hicho waweze kuandamana mwisho wa siku
sifa anapata Halima Kuwa ni mwanamke Shujaa na aliogopi
jeshi la polisi, Kumbe ni Ujinga mtupu.Kama
Mdee kweli wewe uliogopi Jeshi la Polisi kwanini ile Oktoba
4 Mwaka huu, mlivyo andamana ,Polisi ilivyo watawanya
,kwanini wewe uliogopa ksago utakimbia Kwenda kujificha ili
kukwepa kipondo Cha Polisi?Kama
wewe ni Shujaa kweli kwanini Oktoba 7 Mwaka huu,
ulipofikishwa Katika Mahakama ya Kisutu kwanini uliyakana
hayo Mashitaka?Maana
Kabla hujafikishwa mahakamani ulikuwa ukijigamba kupitia
vyombo Vya Habari Kuwa kuandamana ni Haki yako na hutakiwi
kuomba Kibali?Kama wewe ni Shujaa kwanini ulikubali kupewa
dhamana?Shujaa
au kamanda gani anaogopa kukaa gerezani kweli licha ni kweli
dhamana ni Haki yako ?Ningekuona Wewe ni Shujaa kweli
usingeomba dhamana ungesema upo Tayari kwenda kukaa gerezani
ili ukiwa gerezani pia huweze kutoa hoja zako kwa mahabusu
wa kike zinazohusu msimamo wako na Chama Chako Cha kuipinga
Katiba iliyopendekezwa Bunge na kujua matatizo
yanayowakabili.Kamanda
gani akiona kilungu Cha Polisi na Gari za Maji ya
kuwasha'Kikojozi' Ana kimbia?Unatakiwa ukae upambane
na Polisi Kwani ulijigamba licha Polisi imekataza maandamano
yenu ,wewe na wanachama wako mtaandamana.Halima
Tanzania hii unayoiona hivi sasa watu wanaishi kwa amani
tofauti na nchi za wenzetu , Elewa Kuwa Kuwa watu walipoteza
Uhai wao,Jasho Lao wakaijenga nchi hadi Leo hii wewe
umeikuta,ukasoma, umepata madaraka ambayo ya kulevya hadi
unaanza jeuri ya kukaidi amri ya Jeshi la Polisi na kuwa Ana
aliwataka wanachama wenzako wafanya vitendo Vya kuvunja
Sheria.Mamlaka
husika hazitakuacha ufanye huo uhuni wako ambao mwanamke
yeyote mwenye haiba ya kike hawezi kufanya .Na
Mbaya zaidi ulichokuwa ukikipigania Cha kutaka Rais Kikwete
asipokee Katiba iliyopendekezwa na Bunge hujafanikiwa Kwani
Jana jioni Kikwete na Rais wa Zanzibar Dk.Mohamed Shein
wameipokea Katiba kutoka kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge
Maalum la Katiba, Samuel Sitta na tumemshuhudia Rais
alishindwa kuficha hisia zake na akajikuta akitamka zaidi ya
Mara mbili kwamba anayofuraha sana sana kuona tendo Hilo la
Kihistoria ilifanyika chini ya uongozi wa serikali yake na
akasema kabisa Katika ile ni nzuri sana na awashawishi
Watanzania waipigie kura ya ndiyo.Ila
Kwa mwanamke ambaye Hana haiba ya kike na Mwanamke ambaye
hajithamini na atambui mambo yapi mwanamke afanye na mengine
asifanye ,atayafanya Kama wewe Halima ambaye tunakuhesabu ni
msomi,kiongozi lakini unashiriki adharani Kutenda matendo ya
kuvunja Sheria.Kiongozi
yoyote mzuri anatakiwa awe ni mfano wa kuwaongoza wafuasi
wake wafikie malengo waliyoyakusudia, sasa Mdee ambaye ni
kiongozi lakini unawaongoza wafuasi wako waende njia isiyo
sahihi kwa kishiriki vitendo vya uvunjifu wa sheria na
matokeo yake mmeishia kushitakiwa na kulala Gerezani na
kujitia nuski.Halima
tambua kuwa hata kama mwanamke awe na fedha ,mali ,madaraka
kiasi gani bado mwanamke anatakiwa hajiheshimu na afanye
matendo ambayo mwanamke anatakiwa atende .Siyo
mwanamke asimame hadharani atende matendo ya kihuni huni
ambayo tumezoea kuona yanatendwa wanaume wahuni wahuni au
wanawake wahuni wahuni tu ,Kama wewe ulivyotenda.Labda
ni mwambie Mdee vitendo hivyo vya ukahidi na Kauli ambazo
hazikawii kutolewa kwenye kinywa Cha mwanamke mwenye haiba
ya kike,Hupaswi kujifanya.Wanaopaswa
kufanya matendo Kama hayo ni baadhi ya wanawake kama Asha
Ngedere, na wanawake wengine ambao kufanya vitendo vya
kihuni, kusutana na wengine hadi wameunda vikundi
vinavyokodisha kwaajili ya kuchamba watu, ambao wanawake hao
wanaofanya vitendo hivyo vya kihuni wanapatikana sana huko
uswahili mitaa ya Mburahati Madoto, Kigogo Luhanga,
Mburahati kwa Binti Kahenga ,vurugu ndiyo sifa zao tena
wanaona fahari kuona watoto wao wanafuata nyayo za mama zao
za kufanya vitendo Vya kihuni na kishenzi.Halima
Hupaswi kufanya vitendo vya uvunjifu wa sheria na vya kihuni
huni, waachie wakina Asha Ngedere , wewe unapaswa hivi sasa
ukae katika ofisi mpya ya Bawacha , ubuni mipango yako
yakuwaletea wanachama wako na taifa maendeleo kwa njia
amani.Una
mambo mengi ya kufanya siyo kuanzisha maandamano haramu
.Hivi kweli unashindwa kuketi kitako ukaanzisha hata taasisi
yako binafsi ,Ukaanda harambee za kuchangia kutokomeza mimba
za utotoni, au kufanya utafiti wa nini kwanini wanawake
wengi wanashambuliwa na ugonjwa wa UTI na mambo
mengine,ukaalika watu wenye Fedha zao wakashiriki harambee
wakachangia Fedha utapata za kuendesha Programu hizo?Lakini
umeama kujigeuza Kituko Mbele ya Jamii ya wanawake
wastaarabu ya kushiriki kushinikiza kufanya maandamano
haramu. Kama Fedha, madaraka unayo.Tatizo Lako nini Mdee
hadi unaamua kushiriki vitendo hivyo Vya kihayawani ambayo
bins kushushia heshima?Umri
ndiyo huo una unazidi kukutupa mkono na ukae ukijua hivyo
vitendo vya 'Usela Mavi' unavyofanya mwina mwisho
wake.Ebu
Mdee achana na usela Mavi , anza kuweka fikra na matamanio
ya siku Moja na wewe uitwe mama wa Fulani.Mshirikishe
Mungu Katika matamanio hayo ,Mungu atakupa mtoto na
ukishampata mtoto ni wazi utakuwa busy sana na kuangaika na
mambo ya mtoto na familia yako kwa ujumla na utajikuta
unaoendokana na vitendo hivyo Vya kihuni ambavyo mwanamke
mkorofi akisha bahatika kupata mtoto wake anaachana navyo
Kwani anaona aliendelea anavyo anakuwa kama anamdhalilisha
mtoto wake.Achana
na wazimu huu unaoufanya wa kujifanya wewe ni jike dume,
umesababisha watu kuanza kuhoji Kuwa Mdee ni mwanamke
kweli?Anaujua uchungu wa Mwana?Na je Halima amebahatika
kupata mtoto?Na
Wengi wanahoji hivyo kwasababu wanasema wanashangaa na
kujiuliza kuwa hivi Mdee alishawahi kubeba mimba na akalea
mtoto na kuitwa mama hawezi kufanya hayo anayoyafanya?Wanajiuliza
Mdee ni mwanamke wa aina gani ambaye hana uchungu hadi
anaamasisha wanawake wa Chadema waandamane Katika maandamano
haramu ambayo wanaenda kupigwa ma Polisi na kufunguliwa Kesi
mahakamani na hadi wakalala gerezani siku Moja?Na
wengine wa nadiriki Kusema Mdee pamoja na usomi wake na
madaraka aliyonayo ,anaitaji kutafutiwa Makungwi kama Bibi
Hindu, Bibi Chau wamfunde ili ajue mwanamke anatakiwa aweje
,avae mavazi gani, na vitendo gani afanye Mbele za watu na
vipi afanye.Maana
licha ya madaraka na usomi aliyonayo,wakati mwingine
tunamshuhudia akitenda na kuongea mambo ambayo mwanamke
aliyefundwa kuwa mwamke na kuwa kiongozi , hapaswi kuyatenda
Kama ya kupayuka payuka ovyo ovyo tena wakati mwingine kwa
hoja zisizo na mashiko.Kuna
wanawake wako Tanzania mashughuli dini Kama Dk.Asha Rose
Migiro, Profesa Anna Tibaijuka na wengine Wengi, huwezi
kuwasikia wakifanya vitendo Vya kihuni huni na vya
kuamasisha watu Wavunje Sheria.Wao ubishina Kwa hoja,
ustaarabu.Bado
namkumbuka aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake ya
Chama cha Tanzania Labour(TLP), Getrude Pwila Enzi zile Mkuu
wa Jeshi la Polisi, IGP- Omar Mahita.Kwa
mama huyu alikuwa ni rafiki yangu nalilikuwa naandika Habari
za Chama Cha TLP kinachoongozwa na 'mume wangu wa
zamani', Agustine Mrema.Pwila
alikuwa ni mwanamke machachari sana kila uchao alikuwa
akiwaamasisha wanawake wa TLP waandamane Katika maandamano
haramu hadi Wizara ya Mambo ya Ndani huku wakiwa wamevua
Fulana wamebaki na Sidiria tu na walikuwa wakiaa nje ya ya
Wizara ya mambo ya ndani tangu asubuhi hadi jioni wakitoa
maneno ya kulikashfu Jeshi la Polisi, Rais aliyekuwa
madarakani, Benjamin Mkapa na aliyekuwa Msajili wa Vyama Vya
Siasa, Mahundi.Na zoezi Lao la kubaki NA Sidiria walijifanya
zaidi ya Mara tano Kipindi kile Cha Miaka 2002- 2004.Mimi
,Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi, Jocye Mmasi tulikuwa ni
miongoni mwa waandishi tuliokuwa tukishiriki maandamano hayo
na kuandika Habari.Leo hii Pwila amepotea Katika ulingoni wa
siasa, hasikiki tena na ukizungumza naye anajutia kitendo
kile alichokuwa akijifanya cha kuongoza wanawake wa TLP
kuvua nguo na kubaki na Sidiria pale nje ya Makao makuu ya
Jeshi la Polisi na Wizara ya Mambo ya Ndani.Sasa
na wewe Mdee ukae ukijua wewe ni Kama una beep tu, hata
hujamfikia Pwila Kwani Pwila alikuwa anaushawishi mkubwa kwa
wafuasi wake walishapigwagwa sana Polisi lakini mwisho wa
siku walipokuja kutambua uhuni ule waliokuwa wakiufanya
kwanza ulikuwa ukiwadhalilisha wao wenyewe binafsi.Walikuja
kubaini wao kama wanawake wa TLP walichokuwa wakikipigania
kwa njia ya maandamano haramu eti jeshi la Polisi lina
mnyanyasa Mrema ni batiri .Waliachana
na vitendo hivyo na ndiyo ikawa Chanzo Cha umoja wa wanawake
TLP kusambaratika na wanawake Wengi kaumua kuiama TLP
kwasababu ya kubaini Pwila alikuwa alikuwa alikuwa
akiwaongoza Kutenda vitendo Vya Uvunjifu wa Sheria ambavyo
mwisho wa siku walikuwa wakaishia kupigwa virungu na Polisi
,kufunguliwa Kesi mahakamani na kupelekwa gerezani.Sasa
wanawake wenye akili timamu ambao mnaoamini Katika Utii wa
Sheria bila shuruti wa Bawacha ,mfano huo Hao juu wa Pwila
msiuupuze Kwani sote ni mashahidi Enzi za mtangulize wa
Halima, Suzan Lyimo akiwa Mwenyekiti wa Bawacha,
hakutukiwahi kumshuhudia Lyimo akiwaamasisha wanawake
washiriki vitendo Kama hivyo Vya kuvunja Sheria Kama
afanyavyo Mwenyekiti Mpya wa Bawacha ,Mdee ambaye hata Ofisi
mpya ya Bawacha ajaikaa vizuri, ajaeleza kwa vitendo
vipaumbele vyake ni nini.Pwila
hakuwa na elimu kama Mdee ila alikuwa na ushawishi na Tayari
alikuwa ni Mzima , Mdee ni kijana na bado ana Muda mrefu
Mungu akimjalia wa kulitumikia taifa hili na kujiandalia
rekodi safi.Sasa
kwa mtindo huu wa Mdee tena mtoto wa kike kutaka Kupambana
na Polisi kwa jeuri ya kijinga na Mbaya zaidi anawaamasisha
wanawake wachama Chake washiriki vitendo hivyo
,vitamsababishia kumporomosha au kumpotea Kwenye Medani za
siasa nchini Kwani Watanzania ni watu wasiyopenda ni wapenda
Amani na utulivu.Tambua
Mdee wewe ni kiongozi kijana ,unapofanya mambo mazuri au
Mabaya sifa hizo unazipata wewe na vijana wenzako kwa
ujumla.Hujachelewa
unaweza kubadilika licha Tayari umeishaingia Kwenye rekodi
Mbaya ya Watanzania Kuwa Mdee ni kiongozi ambaye
analazimisha maandamano ambayo yamekatazwa na Polisi hivyo
wewe ni Mpenda Vurugu.Na
Kwa taarifa yako Mdee ,siasa hizo unazotaka kuzileta hapa
Tanzania, haziwezekani,ndiyo maana wewe na Chama Chako kila
mlipokuwa mkijaribu kufulukuta kuhusu kutaka kufanya
maandamano yenu mliyosema mtaandamana nchi nchi,
hamjafanikiwa kwasababu Watanzania na vyombo Vya dola
havitaki aina ya siasa mnavyotaka kulileta hapa nchini
.Kwasababu
mbinu yenu ya kufanya siasa ilikuwa haina kheri zaidi ya
kutuletea vurugu na mbinu yenu ya kufanya maandamano
imeshadoda sijui mnabuni mbinu gani nyingine ili iwarejeshee
umaarufu kwasababu Tayari Chama chenu kinashuka Kwa kasi
Umaarufu kwasababu mmoja tu ya kulazimisha matendo
yanayovunja Sheria Kama maandamano haramu.Mdee
tambua hapa Tanzania kuna wanawake wameshika nyadhifa kubwa
na nyeti nchini,lakini wanaojiheshimu na niwatiifu wa Sheria
za nchi Yao, watiifu na Kamwe hutawaona wafanya vioja Kama
unavyofanya wewe Vya kushiriki vitendo Vya Uvunjifu wa Amani
kwa makusudi.Wanawake
Hao wengine wapo Kwenye majeshi yetu ,serikalini na taasisi
mbalimbali za kiraia wametulia tulia.Na wanauwezo wa
kusaliti nchi,au kuanzia virugu na wanaushawishi na mvuto
mkubwa sana kuliko wewe lakini wametulia wanaipenda nchi Yao
na wanatii Sheria za nchi bila shuruti.Iweje
wewe Mdee ambaye umedhiirisha wazi Huna Nguvu wala karama ya
kushawishi wanawake wote wa Chadema wakatii agizo Lako la
kuwataka wanawake wa Chadema waandamane kupinga Katiba
iliyopendekezwa na Bunge Kwani ndani tulishuhudia siku ulipo
jaribio kuandamana ukashughulikiwa.Ni
idadi ndogo sana ya wanawake wa Chadema waliitikia agizo
Lako na wanawake wengine wa Chadema ambao tuna wafahamu
ambao tupo nao mitaani, wasomi na wamama watu wazima wenye
akili timamu na wenye utashi walikata kushiriki wanasema
hawawezi kukubali kuingizwa kwenye matatizo na Mdee,
kwasababu wanamfahamu Mdee ni mtu wa aina gani na mwisho wa
siku watakuja kuonekana wao ni mahayawani Kwani wasingekuwa
mahayawani wasingeitikia wito haramu wa Mdee wa kwenda
kushiriki maandamano haramu na kweli hawakwenda.Ona
sasa ukahidi wako kwa Jeshi la Polisi umekufanya wewe na
wafuasi nane muingie Kwenye orodha ya washitakiwa Katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kwasabu hiyo Tayari
mmeishakuwa ni Kama watumwa wa Mahakama hiyo ambao mtatakiwa
mfike tarehe itakayopangwa wakati ulikuwa na uwezo kabisa wa
kujizua usitende makosa unayoshitakiwa nayo.Sasa
utajikuta badala ya kwenda kutimiza majukumu mengine
,unakwenda kushinda Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
kufuatilia hatima ya Kesi yako.Muulize
Mzee Mabere Marando,Agustine Mrema ,Samson Mwigamba na
wengine wanafahamu vizuri madhara ya kushitakiwa kesi za
aina hiyo uliyoshitakiwa nayo hadi leo wamekoma kushiriki
vitendo kama hivyo ulivyoshitakiwa nayo.Mimi
napenda sana kukaa nyuma ya wanasiasa wa vyama vyote na
kufualitia matamko wanayoyatoa NA uchapaji Kazi wao.Ila
nachukizwa mwanasiasa yoyote ambaye anaamasisha wafuasi wake
watende matendo ya kuvunja Sheria za nchi na kuhatarisha
Amani ya nchi kwa makusudi.Hii
tabia sipendi Kwani mwisho wa siku wanatumia ni wafuasi siyo
viongozi Hao wakuu na hata wanapopelekwaga gerezani
wanasiasa wenye vyeo Vya juu magezera uwaweka viongozi Hao
Kwenye vyumba vyenye hadhi wale wafuasi wa kiongozi Huyo
uwekwa Kwenye selo ya 'Kajambanani'.Mdee
Jana Oktoba 8 Mwaka huu, wakati unaondoka Katika Mahakama ya
Kisutu ulitamka baadhi ya maneno Kuwa ulivyolala gerezani
Juzi wala hawajakukomoa.Hivi kwani kuna mamlaka ilikuwa
imepanga kukukomoa ulalae gerezani kwa makusudi?Kwani
ulivyokuwa gerezani ' ulikula Bata'.Huo
uongo wadanganye watu ambao Hawajawahi kutembelea magezera
na kupata Habari za Magereza wanay
[The entire original message is not included.]
0 comments:
Post a Comment