Thursday, 4 September 2014

Re: [wanabidii] TAARIFA YA WAWAKILISHI WA TAASISI ZA DINI BMK KUHUSU MWENEND WA BUNGE MAALUM LA KATIBA

Nimeishiwa maneno...

Sent from Yahoo Mail on Android



From: 'godfred mbanyi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>;
To: <wanabidii@googlegroups.com>; oldmoshi@gmail.com <oldmoshi@gmail.com>;
Subject: Re: [wanabidii] TAARIFA YA WAWAKILISHI WA TAASISI ZA DINI BMK KUHUSU MWENEND WA BUNGE MAALUM LA KATIBA
Sent: Thu, Sep 4, 2014 11:29:39 AM


Mmmh! Very interesting Utopian tale!

--------------------------------------------
On Wed, 9/3/14, 'Hamisi Nkuluzi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] TAARIFA YA WAWAKILISHI WA TAASISI ZA DINI BMK KUHUSU MWENEND WA BUNGE MAALUM LA KATIBA
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>, "oldmoshi@gmail.com" <oldmoshi@gmail.com>
Date: Wednesday, September 3, 2014, 10:05 PM

Ukweli ni aibu kwa
viongozi wetu wa  madhehebu wala hawana maana kabisa , wapo
kwa masilahi yao , kama walifuatilia midahalo kabla ya
kuanza BMK wala hawangekuwa wanaendelea kuhudhuria. Pili
hawa wanaojiita wakristo hivi wanapewa mamlaka na kutoka
biblia ipi maana hawaruhusiwi kuapa lakini kwa kuogopa
kaisari walikula kiapo ,wamesahau Daniel na wenzake
walivyokuwa watii kwa sheria ya Mungu wa Israel hata kufa.
Suala la kuapa halipo kuanzia kitabu cha mwanzo hadi ufunuo
huwezi kulisoma. Wanisaidie hawa viongozi wa Dini ya
Kikristo.kwa nini isiendelee tu katiba ya zamani kwani hata
ingekuwa Tanganyika bado inahitaji viongozi waaminifu na
waadilifu siku hizi waliopo madarakani ndio matajiri.
Nadhani kama viongozi wanamuogopa Mungu aliyehai wangeacha
kuendelea kula hela ya
  wanyonge
 


    On Wednesday,
September 3, 2014 9:46 PM, 'Jovi kamuntu' via
Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
   

  Ni aibu kuweka liwaya
kama hii hapa. Soma mwisho
BAKWATA KIKRISTO
maana yake nini. Kutumiwa kubaya
sana. Jovin
Bifabusha



DIRECTOR

KWFF LTD

P. O. Box 313

Skype: jovin.bifabusha

Karagwe, Tanzania

+255 784 709200

 
    On Wednesday, September 3, 2014 9:26
PM, Yona Fares Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:
   

  TAARIFA YA WAWAKILISHI WA
TAASISI ZA DINI WA BUNGE MAALUM LA KATIBA TOKA WAJUMBE 201
KUHUSU MWENENDO WA SHUGHULI ZA BUNGE MAALUM LA KATIBA

Sisi Wawakilishi wa Jumuiya
na Taasisi za Dini, tuliopendekezwa na Taasisi zetu na
baadaye kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, baada ya kushauriana na Rais wa Zanzibar kuwa
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, na kula kiapo cha
utekelezaji wa jukumu hili kubwa.
Tukiamini kuandaa Katiba Mpya
kwa maridhiano ya Kitaifa kwa wananchi
  wote, tulipokea jukumu hili kama wajibu wetu Kitaifa. Aidha
tunaamini kwamba katika kupata maridhiano ya Kitaifa ni
muhimu kuheshimu kila wazo na fikra inayotolewa na
kuunganisha fikra hizo kwa usahihi, kwa njia ya kidemokrasia
kwa kupiga kura na kukubaliana na matokeo ya wengi.

Kama ilivyoelezwa hapo awali,
kabla ya kuanza shughuli za Bunge Maalum, kila mjumbe
alikula kiapo cha kuwa mwaminifu na mtiifu kwa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na kwa kadiri ya uwezo wake na ufahamu
wake, kufanya kazi zinazomhusu, bila upendeleo na kumuomba
Mwenyezi Mungu amsaidie.

Tumeshangazwa na kusikitishwa
sana kuona kwamba mchakato wa kutayarisha Katiba
itakayopendekezwa na Bunge hili kwa wananchi, unachafuliwa
taswira yake. Bunge Maalum la Katiba linachafuliwa na,
shughuli zake kuingiliwa na kupotoshwa na wajumbe wenzetu
walio nje ya Bunge, Makundi, Taasisi na Vyombo mbali mbali
vya habari, uhalali na ukweli wa shughuli za BungeMaalum la
Katiba unapotoshwa. Wananchi wanaaminishwa yasiyo na
ukweli.

Upotoshwaji huu umezua
mijadala mbali mbali katika jamii ya Watanzania na bado
linaendelezwa kama ifuatavyo:

1. Kwamba Bunge Maalum la
Katiba halina uhalali kwa kuwa hao wajumbe wenzetu
walioondoka wameliondolea uhalali wake kwa vile hwapo,
wakiwepo Bungeni basi uhalalai wake utakuwepo -
utapatikana;
2. Inadaiwa kwamba Kanuni za
Bunge Maalum la Katiba zinavunjwa ovyo ovyo;
3. Inadaiwa pia, kwamba kinachojadiliwa sasa
katika
  Bunge hili ni Waraka mwingine na si Rasimu iliyotayarishwa
na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, iliyowasilishwa rasmi
Bungeni na kuanza kujadiliwa na wajumbe;
4.
Inadaiwa na watu na Taasisi mbali mbali, kwamba viongozi wa
dini, wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, na wajumbe wa Kundi
la 201, wanapewa rushwa. Isitoshe Vyombo vya habari
vimeandika tuhuma kama hizi.
5. Inadaiwa pia
kwamba wajumbe waliomo katika Bunge hili ni wachache,
ukilinganisha na hao walioko nje ya Bunge hilo; 
6. Bunge hili, kwa tuhuma hizo, lazima
lisitishwe au livunjwe na Mhe. Rais.

Kabla ya kuanza kuusahihisha
  upotoshwaji huo, sisi Wawakilishi wa Taasisi za Dini mbali
mbali na Wajumbe wa Kundi la 201 katika Bunge Maalum la
Katiba, tunapenda kufahamisha umma wa Tanzania mchakato wa
kutayarisha Katiba Mpya ulivyo kisheria.

Tunapenda kuwafahamisha
Watanzania wenzetu kwamba mchakato huu una hatua tatu kwa
mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Mpaka hivi sasa ni
hatua moja imekamilika. Hatua ya pili ndiyo inayoendelea, na
hatua ya tatu bado haijaanza.

Hatua ya kwanza ni ile ya
uandaaji wa Rasimu. Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya
83 iliunda Tume ya Mabadiliko ya Katiba, chini ya kifungu
cha tano cha sheria hiyo. Tume hii ilipewa jukumu la
kuratibu na kukusanya maoni ya wananchi juu ya Katiba,
kuanisha na kuchambua maoni ya wananchi na kisha kuandaa
rasimu ya Katiba. Kazi hiyo ilifanyika kwa kipindi cha
takriban miaka miwili na hatimaye Rasimu ya Katiba
ilikamilika.

Hatua ya pili ilikuwa ni
kuipeleka Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalum la Katiba,
ambalo liliundwa kwa shughuli maalum ya kuandika Katiba
inayopendekezwa, ili ifikishwe kwa wananchi ambao wataamua
waikubali au waikatae kwa kuwa wao ndio wenye maamuzi ya
mwisho. Hawa ni Watanzania wote wenye uwezo wa kupiga kura
kwa kutoa maoni yao. Hoja ya Mamlaka ya Bunge hili
hatujazungumzia kwa vile imefikishwa Mahakama Kuu ya
Tanzania ili kupata tafsiri sahihi ya mamlaka ya Bunge hili.
Tunachoweza kusema ni kwamba jukumu kuu la Bunge hili ni
kutengeneza Katiba inayopendekezwa na Bunge ili ifikishwe
kwa wananchi waipigie kura ya maoni. Hatua hii ya pili bado
inaendelea.

Hatua ya tatu ni pale Bunge
Maalum la Katiba tutamkabidhi Mhe. Rais Katiba
inayopendekezwa ambayo itafikishwa kwa wananchi ili
waikubali kama wataridhika nayo au kuikataa kama haikidhi
matarajio yao.

Hatua hii ni ya mwisho
wananchi wakiikubali tunapata Katiba Mpya wakiikataa,
tunaendelea na Katiba tuliyonayo.

Kilichotokea ni kwamba,
wajumbe wenzetu walio nje ya Bunge hili wameamua kuukiuka
utaratibu uliowekwa kisheria. Badala yake wamepeleka Rasimu
ya Katiba kwa wananchi wakati mchakato wa kutayarisha Katiba
inayopendekezwa bado haujakamilika.

Sisi Wawakilishi wa Taasisi
za Dini, ambao kuuhubiri, kuutangaza na kuusimamia ukweli ni
moja ya majukumu yetu katika jamii, tumesikitishwa sana na
taarifa potofu zinazosambazwa kwa
  makusudi na makundi, taasisi na vyombo vya habari mbali
mbali na tukiwa wajumbe wa Bunge hili ambao tunafahamu kwa
kina na tunaridhika na kila hatua ya mchakato huu. Tuna
wajibu wa kusahihisha upotofu huu, unaoendeshwa kwa makusudi
na hivi kuwaeleza Watanzania ukweli na hali halisi inayojiri
hapa Bungeni. Watanzania msifadhaishwe na wala msibabaishwe.
Hali ni shwari. Mchakato unaendelea kwa amani na utulivu.

Katika kusahihisha upotofu
unaozungumzwa kupitia mijadala na midahalo mbali mbali
katika jamii, tunaomba kufafanua hali ilivyo kama
ifuatavyo:-

TUHUMA KWAMBA BUNGE MAALUM
LA KATIBA KUKOSA UHALALI
Jambo hili si
kweli hata kidogo kwani kuna wajumbe wa aina tatu Bungeni
ambao wamewekwa na kutambuliwa kisheria. Hawa ni kama
wafuatao:
1. Wabunge
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
2. Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi
Zanzibar.
3. Wajumbe 201 walioteuliwa na
Mhe. Rais, baada ya kupendekezwa na Taasisi, Mashirika na
makundi mbali mbali nchini,
Uhalali wa Bunge unakuwapo
wakati wajumbe kutoka makundi hayo matatu wapo Bungeni, na
si Vyama vya Siasa pekee. Iwapo kwa mfano wajumbe wa 201
wakiamua kutoshiriki katika shughuli za Bunge, basi sehemu
moja muhimu ya Bunge haitakuwapo na uhalali wa Bunge
hautakuwepo.
Hata hivyo, Kanuni za Bunge
Maalum la Katiba zimeweka idadi ya akidi ambayo ni nusu ya
wajumbe wote wa Bunge Maalum. Akidi hii ikifikiwa Bunge
huendelea na shughuli zake. Akidi hii hufikiwa kila wakati
BungeMaalum linapokutana. Hii inamaanisha kwamba Bunge
Maalum la Katiba linaendesha shughuli zake kwa misingi ya
sheria na taratibu zilizojiwekea. Bunge lina uhalali wa
kufanya shughuli zake kwa mujibu wa sheria.


TUHUMA KWAMBA KANUNI ZA
BUNGE MAALUM LA KATIBA ZINAVUNJWA
Suala
hilo halijawahi kutokea. Kanuni za Bunge Maalum la Katiba
zilipitishwa na wajumbe wote kwa mujibu
  wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Sheria Namba 83. Vile
vile uendeshaji wote wa shughuli za Bunge zinafanywa kwa
mujibu wa Kanuni za Bunge Maalum. Kanuni hizo zinatoa fursa
ya Bunge Maalum kuzirekebisha pindi inapobainika ipo haja ya
kufanya hivyo kwa mujibu wa kanuni Namba 87.


WARAKA MWINGINE
UNAJADILIWA NA SI RASIMU YA TUME 
Hili
nalo si kweli. Tunawahakikishia Watanzania wote kwamba sisi
kama Wawakilishi wa Taasisi za Dini miongoni mwa wajumbe wa
Kundi la 201, kwa ujumla tunasema hii si kweli. Ni
upotoshaji wa makusudi. Tunaijadili Rasimu ya Tume ya
Mabadiliko ya Katiba ibara
  kwa ibara. Ibara nyingi zimeachwa kama zilivyo. Kuna ibara
ambazo zimeboreshwa au kurekebishwa, kuna ambazo
zimeondolewa na kuna nyingine mpya ambazo zimewekwa ili
kuweka mambo ya msingi ambayo Rasimu haikuyazingatia au
haikuyaona.


WAWAKILISHI WA TAASISI ZA
DINI, WAJUMBE WA KUNDI LA 201 WA BUNGE LA KATIBA KUPEWA AU
KUPOKEA RUSHWA
Sisi Wawakilishi wa
Taasisi za Dini na Wajumbe wa Kundi la 201 wa Bunge hili
tumesikitishwa sana na taarifa hii iliyosambazwa na baadhi
ya watu, na kukaririwa na baadhi ya vyombo vya habari aidha
kupitia kwenye mijadala, midahalo na makongamano mbali
mbali.
  Baadhi yetu sisi Viongozi wa Kiroho tumeapishwa viapo vya
uadilifu katika uongozi wetu wa kiroho na tuko mstari wa
mbele kuongoza waumini wetu kuepuka dhambi ya tamaa ya
fedha, na kusema uongo. Taarifa kama hizo hazionyeshi
heshima kwa dini au nafasi zetu za kipekee katika uongozi wa
kiroho. Taarifa hizi zinatangazwa kwa makusudi na watu mbali
mbali kupita vyombo vya habari kwa malengo ya kisiasa na
kutudhalilisha sisi Viongozi wa kiroho mbele ya umma.
Tunaomba tabia hii ikomeshwe.


TUHUMA KWAMBA BUNGE KUWA
NA WAJUMBE WACHACHE
Hili nalo si kweli.
Wajumbe wanaohudhuria Bunge wanakidhi
  akidi inayohitajika kwa mujibu wa kanuni.


HOJA YA KUSITISHWA AU
KUVUNJWA KWA BUNGE MAALUM
Hii ni hoja
inayozungumzwa katika mijadala mbali mbali katika jamii.
Msingi wa hoja hiyo ni kutokuueleza umma ukweli ulioko
Bungeni kwa kupeleka taarifa potofu kwa wananchi kwamba
Bunge Maalum limekosa mwelekeo. Hatuoni sababu za hoja hii
kutiliwa maanani kwa kuwa hakuna sababu za msingi na za
kisheria za kufanya hivyo.

HITIMISHO
Kumekuwa na taarifa mbali mbali zenye malengo
ya ama kuingilia shughuli za Bunge hili au kutudhalilisha
sisi wajumbe ambao si Wabunge au Wawakilishi. Wajumbe 201,
ambao mchango wao katika mijadala ya Kamati mbali mbali
umekuwa na uzito wa pekee, hautambuliki katika taarifa hizo
ambazo zimejaa malengo ya kisiasa zaidi kuliko ukamilishaji
wa shughuli za Bunge Maalum.
Kuna taarifa nyingine
zimesambazwa zikiwa na upotoshaji mkubwa, licha ya kwamba
Taasisi zinazosambaza taarifa hizo zina wajumbe wake katika
Bunge Maalum. Wajumbe hao wangeweza kuzielimisha Taasisi zao
ukweli ulipo hapa Bungeni, na hivyo kuwafikishia wasomaji
wao taarifa zilizo za kweli na ili kulijengea Bunge hili
heshima machoni pa umma wa Tanzania na Kimataifa.
Udhalilishaji kama huu unatuumiza hata sisi wajumbe ambao
kwa hiari yetu tuliamua kubaki Bungeni na kuyatimiza hayo
ambayo tulitumwa tuje tuyakamilishe.
Kama tulivyosema hapo awali
ni
  wajibu wetu
  kama Viongozi wa Dini na Wajumbe wa Bunge hili kuutaarifu
umma hali halisi katika shughuli za Bunge Maalum na kuwasihi
wapotoshaji kwamba wauheshimu ukweli na wawaheshimu
watanzania kwa kuwaeleza ukweli.
Ahsanteni
sana.
…………………….
  …………………………
SHEIKH HAMID
MASOUD JONGO ASKOFU AMOS JOSEPH MUHAGACHI 
BAKWATA KIKRISTO
TAREHE 3 SEPTEMBA,
2014




--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


 
   



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


 
   

--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment