Monday 29 September 2014

Re: [wanabidii] WARAKA WA WARIOBA DHIDI YA WASIRA

Kwa nini Warioba kutumia muda wake kumjibu Wasira? Hana mengine ya kufanya hadi kujibizana naye? Nafikiri angenyamaza na kuwaachia wanaostahili kumjibu kama wapo
--------------------------------------------
On Sat, 9/27/14, Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com> wrote:

Subject: [wanabidii] WARAKA WA WARIOBA DHIDI YA WASIRA
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Saturday, September 27, 2014, 7:05 AM

Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba
ameandika waraka kumjibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
(Uhusiano na Uratibu), Stephen Wasira kwa kauli yake kuwa
ndiye aliyemkimbiza CCM kwenda upinzani mwaka
1995.
Katika waraka wa maandishi alioutuma kwa gazeti
hili, Jaji Warioba alisema maelezo ya Wasira dhidi yake
katika mahojiano maalumu na gazeti hili hayakuwa sahihi na
hivyo akamtaka ajifunze kusema ukweli kwa kuwa mambo
anayosema yanaweza kumrudia baadaye.
Waraka wenyewe huu hapa:
Tarehe 22 Septemba 2014, Gazeti la Mwananchi
lilitoa taarifa ya mahojiano kati yake na Mheshimiwa Steven
Wasira. Katika mahojiano hayo, Mheshimiwa Wasira alisema
mimi ndiye niliyemkimbiza CCM.
Tangu mchakato wa Katiba Mpya kuanza nilikuwa
napata taarifa kwamba Mheshimiwa Wasira alikuwa amenifanya
mtaji wake katika kutetea msimamo wake. Wakati mmoja kuna
kiongozi mwenzake aliniuliza kama nina ugomvi binafsi na
Mheshimiwa Wasira kwa sababu kila akipata nafasi kwenye
vikao vyao ananishambulia. Wakati wa mabaraza ya Katiba
nilipata taarifa za aina hiyo. Nilichofanya ni kuwaarifu
viongozi wake wa CCM.
Mengi aliyosema Mheshimiwa Wasira siyo ya kweli.
Napenda nitoe ufafanuzi kwa machache yafuatayo:-
Niligombea mara mbili na Mheshimiwa Wasira.
Baada ya Uchaguzi wa 1990 ambao nilishinda kwa kura nyingi
sana, uchaguzi huo ilitenguliwa kwa sababu nilifanya kampeni
kwa kutumia gari la Waziri Mkuu.
Uchaguzi ulirudiwa mwaka 1992. Niliunda timu ya
kampeni, Mheshimiwa Wasira akiwa kiongozi. Aliniomba
atangulie jimboni kuandaa mazingira. Alipofika huko akaanza
kampeni dhidi yangu na kutangaza kwamba anagombea. Wakati
huo kura za maoni zilikuwa zinapigwa na wajumbe wa
halmashauri kuu ya wilaya. Wajumbe walikuwa kama 600.
Nilipata kura 400 na Mheshimiwa Wasira alipata kura chache
akiwa mtu wa tatu au nne. Baada ya matokeo akatangaza
anajitoa kwenye mchakato na jina lake lisipelekwe NEC.
Alikataliwa kwa sababu kufuatana na kanuni, muda wa mtu
kujitoa ulikuwa umepita.
Mwaka 1995, kura za maoni zilikuwa zinapigwa
kwenye kata. Tulianza na Kata ya Sarama ambayo iko upande wa
mashariki, siku ya tatu tulifika Nyamuswa ambacho ndicho
kijiji ninachotoka. Nyamuswa ilikuwa kituo cha tano kati ya
vituo 12.
Baada ya hapo tulielekea magharibi ya jimbo
anakotoka Mheshimiwa Wasira. Baada ya kura kupigwa katika
Kata ya Guta, Mheshimiwa Wasira alijitoa kwa sababu aliona
hawezi kunishinda hata kama angepata kura zote za kata mbili
zilizobaki. Siyo kweli kwamba Nyamuswa ilikuwa ya mwisho
kupiga kura na siyo kweli wananchi wa kata nzima walipiga
kura. Kumbukumbu zote zinaweza kupatikana wilayani na makao
makuu ya CCM.
Mheshimiwa Wasira anasema kwamba nilikuwa Jaji
na kesi iliyopelekwa mahakamani ni kama kesi ya tumbili
kupelekwa kwa nyani, kwa maana kwamba majaji walinipendelea.
Kumbukumbu za kesi hiyo zipo. Wakati huo sikuwa jaji.
Isitoshe huko nyuma uchaguzi nilioshinda 1992 ulitenguliwa.
Kwa nini wakati huo sikupendelewa? Kumbukumbu za kesi
zinaeleza kwa nini Mheshimiwa Wasira alifungiwa kugombea kwa
kipindi.
Mheshimiwa Wasira ni kiongozi wa Taifa kwa
kipindi kirefu. Ni mbunge wangu na namtambua hivyo. Tunaweza
kuwa na mtazamo tofauti katika baadhi ya mambo lakini hiyo
si sababu ya kusema mambo yasiyo ya kweli kwa nia ya
kujijenga kisiasa.
Yeye ni Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu
ya CCM. Yeye ni Waziri mwandamizi. Yeye anafikiria kugombea
urais. Ni vizuri basi akajifunza kusema kweli (ambayo ni
ahadi mojawapo ya WanaCCM). Akumbuke anayosema yanaweza
kumrudia mbele ya safari.
J.S. Warioba
24-09-2014




--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment