Tuesday 30 September 2014

Re: [wanabidii] Re: Kinachoendelea BMK kinatia kichefuchefu



Kaka, endelea kuongea yale unayoyaamini. Ukifika wakati mabadiliko huwa yanakuja. Hata hao unaowaita wa pembezoni, kuna siku watashtuka na wataukataa ukandamizaji wa kimfumo wanaofanyiwa bila wenyewe kujua.






2014-09-30 14:00 GMT+03:00 Selemani Rehani <srehani@hotmail.com>:
Nimetoka katika hotel moja kupata chakula cha mchana. TBC wanaonyesha live zoezi la kupiga kura rasimu ya katiba. Wajumbe wengi wa CCM wanapopewa nafasi wanapiga kura ya wazi. Kabla ya kusema "ndio" wanatanguliza mbwembwe nyingi na lugha za kujigamba na mwisho wake wanasema "ndio" kana kwamba wanamkomoa mtu fulani au chama fulani. Hivi kweli katiba inastahili kufanyiwa hivyo? wanatoa lugha za ajabu sana, kwa mfano, mtu anasimama na anasema anapiga kura kwa niaba ya vijana, kwa niaba ya wanawake, kwa niaba ya wananchi wa Kishapu, wananchi wa Bunda, Watanzania wote, eti wamenituma niseme "ndio" Jamani huu si utani huu? ni wapi na ni lini aliwa-consult wananchi au vijana au wanawake?
 
Lakini, kilichonistajabisha pale, ni kuwa karibu sehemu kubwa ya watu katika hotel hiyo ambao wanapata chakula cha mchana, wanakerwa, wanachefuka, wanaona kinyaa kwa yale wanayoyasikia! Sasa swali langu, kama watu hawaridhiki na kinachoendelea, iweje bado hawa CCM wanaweza kuendelea kutuburuza? iweje kuwa hatuwezi kuchukua hatua, kupaza sauti zetu kwa nguvu na kuzuia wizi huu? Na je CCM hawalijui hili? kama wanalijua ujasiri wa kutupuuza kiasi hiki wanautoa wapi? Nini hicho kinachowapa jeuri hii? wanategemea nini?
 
Nadhani wanapopiga mahesabu yao wanategemea nguvu ya wale ambao walioko pembezoni, ambao ndio wengi, kama sikosei ni 70% ya watanzania ambao wanaishi maisha ya shurba, shida na umaskini uliokithiri, hawana access ya information, wanapigania mlo mmoja kwa siku, hivyo ni rahisi sana kuwahadaa kwa vizawadi na vipesa kidogo. HAPA NDIPO NGUVU YAO IPO. Pia nguvu yao ip katika hii Tume mbovu ya uchaguzi ambayo ndio itasimamia zoezo zima la kura ya maoni.
 
Wataumia vitisha, hila, ghilba na kila aina ya hadi tamutamu kuwarubuni wananchi ambao ni waoga, hawajishughulishi kutafuta ukweli wa mambo ili waiunge mkono katiba yao ya CCM.
 
Hawajali kabisa hii resistance ya 30% ambayo ndio sisi tunaopiga kelele.
 
Ku- transform hii nchi ni kazi kubwa kweli. Nadhani ilikuwa rahisi kumuondoa mkoloni lakini si rahisi kuleta transformation katika nchi hii. Kama tungeweza kufanikiwa ku-transform nchi hii, basi hatua ya kwanza ilikuwa ni kupitisha rasimu ya katiba kama ilivyopendekezwa na Warioba. Hiyo ilikuwa hatua ya kwanza ya ku-transform nchii, kwa kuwa hilo limeshindikana, basi sina matumaini kabisa ya kuweza ku- transform nchi hii. Nchi hii itaendelea kukosa uwajibikaji, itaendelea kuwa maskini na wengi wataendelea kuogelea katika lindi la umaskini. Hata hiyo gesi haitaweza kufanya lolote. Wataendelea kulindana kama wanavyofanya katika IPTL, Richmond, EPA, Meremeta, n.k.  Wachache wataendelea kugawana raslimali na kutumia ufukara wa wengi kuendelea kukaa madarakani, wao na watoto wao, wajukuu zao na vitukuu vyao.
 
Inasikitisha,
 
Sele

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.




--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment