Wednesday, 10 September 2014

Re: [wanabidii] HAMIS KIGWANGALLA KWA KUCOPY NA KUPASTE SPEECH YA OBAMA

Ndg wanajamvi,

Ninamshukuru mtoa hoja kwa kuanzisha mjadala huu mzuri kuhusu hotuba yangu. Na ninawashukuru nyote kwa kuchangia na zaidi kwa kusoma tamko la nia yangu. Hii inanidhihirishia jambo moja kwamba hotuba yangu imewagusa wengi kwa namna niliivyoiandika na kugusa maeneo mbalimbali jamii na nchi yetu. 

Mjadala huu ni mzuri maana unatanua wigo wa wasomaji wa hotuba yangu jambo ambalo sikulitarajia. Aliyelenga kuishusha hadhi hotuba yangu namsikitikia maana badala yake anaipandisha bila kujua. Nimeiweka hapo juu ili ambao hawajaisoma wairudie: hii ndiyo latest version ya hotuba ambayo niliisoma mbele ya hadhira waliokuwepo pale. Watakapoisoma watafakari ni maneno yapi nimeyatafsiri kama yalivyo, ili ku-warrant hotuba yangu kuwa ni a plagiarised piece. 

Kwa mtu aliyeenda shule na anayejua usomi na maana ya plagiarism, ama kuchukuwa kazi ya mwingine na kuifanya yako, atatakiwa kusema ni maneno yapi yaliyonukuliwa kama yalivyo? Ama yametafsiriwa lakini yamebaki na maana ile ile...kama ni yale ya ki-latin basi hata Obama naye atakuwa guilty of plagiarism, maana yale maneno E pluribus unum (mmoja baina ya wengi) yanapatikana kwenye nembo ya USA na wala si ya kutunga yeye...na hata yeye Obama alipoyatumia hakuweka source. 

Kama ni style, hiyo style ya kutoa mifano ni ya speakers wengi wazuri, Mwl. Nyerere, MLK Jr, Malcolm X, MK Ghandi n.k. Kama hiyo maana yake ni plagiarism, basi am guilty as charged. 

Hesabu maneno ya hotuba ya Obama inayotajwa hapa, yapo takriban 2300, hotuba yangu ina maneno 3400. Hotuba ya Obama ina video track record time ya dakika 18, ya kwangu ina dakika 39. Mimi naongelea wamachinga, mama ntilie, historia yangu ya umaskini, namnukuu Rais JK, n.k. Obama anaongelea mambo tofauti kabisa, yeye anamnadi Senator Kerry. Sasa nimeigaje?

Ninajua hotuba yangu ime-spark a lot of interest kwenye mbio za Urais na nafasi yangu, washindani wangu wameogopa, tulieni jamani, hii ndiyo kwanza saa 11 alfajir, hata asubuhi hakujacha. Nimesafiri kuja nje ya nchi kikazi, nimekuwa bize muda wote mpaka leo nilipoambiwa kuhusu hii thread na picha nyingine zenye maneno ya kejeli, kuna mengi ninayaona yakisemwa mitandaoni, ninaelewa kinachotokea. Fear of the coming in of a new kid in the block.

Nimeweka wazi nia yangu, basi acheni nipimwe na wanachama wenzangu wa CCM, na watanzania wenzangu, hilo ndiyo lengo langu. Acheni kuweweseka. 

Nimesoma digrii tatu kwenye vyuo vikuu vitatu tofauti na vyote ni reputable sana, na sasa nafanya Ph.D kwenye chuo reputable kabisa duniani (University of Cape Town), sijawahi kuwa accused kwa makosa ya kisomi kama hilo. Na pia ninaandika vitabu viwili, na kimoja kipo kwa editors wa awali, maprofesa wa vyuo vikubwa duniani, sijaambiwa kuhusu plagiarism hata mara moja. Ninaujua usomi na ninayajua vema makosa ya kisomi kuliko wanaojaribu kuishusha hadhi hotuba yangu, wakidhani wataichafua safari tuliyoanza. Wanasahau ule msemo kuwa kumpiga teke chura hakumuuwi bali kunamuongezea mwendo tu. Sasa nitaisambaza ichapwe kwenye magazeti ili watanzania wengi zaidi wapate kuisoma, wanitafakari, na mwisho wachukue hatua.

Ahsanteni kwa kunisoma,
HK.

2014-09-10 20:57 GMT+03:00 Emmanuel Muganda <emuganda@gmail.com>:

2014-09-10 13:55 GMT-04:00 Emmanuel Muganda <emuganda@gmail.com>:

Kumbe hata ile ya kubeba mke na watoto nayo amemwiga Obama!
em

2014-09-10 3:24 GMT-04:00 Magiri paul <kiganyi@gmail.com>:

Huo ni utaratibu wa kawaida wa Kigwangallah.

Dau dogo huambaa mwambao, kubwa huenda kwenye kilindi.

On Sep 10, 2014 9:31 AM, <mchunguzihuru@gmail.com> wrote:

HAMIS KIGWANGALLA KWA KUCOPY NA KUPASTE SPEECH YA OBAMA NA WEWE UNAUTAKA URAIS!!!

Ndugu zangu,Bob marley enzi za uhai wake aliwahi kusema, "You can fool some people for sometime but you cannot fool all the all the people all the time".Mchakato wa Urais wa nchi yetu umefikia pabaya,juzi Mbunge wa Nzega(CCM) Hamis Kigwangalla ambaye taaluma yake ni Daktari wa magonjwa ya binadamu naye alitangaza kuutaka Urais,sina ugomvi na nia yake.Bali nina ugomvi na uwezo wake mdogo wa kudhani anaweza kudanganya Taifa nzima mchana kweupe.Kigwangalla alitoa hotuba ambayo wengi waliisifia sana bila kujua,Ukweli ni kwamba Hotuba ya kigwangalla ni COPY and PASTE ya hotuba ya OBAMA aliyoitoa mwaka 2004,Boston katika mchakato wa kumtangaza mgombea urais wa marekani wa mwaka ule John kerry,Speech ile inafahamika sana kama OUT OF MANY ONE kwa kilatini E PLURI.BUS UNUM .Alichokifanya kigwangalla ni kuitafsiri tu ile hotuba kutoka kiingereza kuja kiswahili na kuisoma mbele ya wanahabari.Binafsi nina hazina kubwa ya Speech nyingi maarufu ulimwenguni nilipoisoma tu hotuba ya kigwangalla katika mtandao wa wanabidii forum nikaikumbuka OUT OF MANY ONE,ya OBAMA ktk DEMOCRATIC NATIONAL CONVENTION(DNC),2004.Wachambuzi wengi wa masuala ya hotuba wanadai hotuba ile ndiyo iliyomfanya OBAMA kupata Urais,kwani aliongea mambo mengi kumhusu yeye,chama chake cha Democrat na mstakabali wa Taifa akirajerea kitabu chake cha AUDACITY OF HOPE.Inamaana kingwangalla alifikiri naye kwa kucopy ile hotuba atapata Urais kwa kua tutamuona kichwa kwa kuwataja hadi wauza vitumbua km ishara ya kuonesha atakua Rais wa wote hahahahaha,Kigwangalla nafikiri tulia kwanza,ukirukaruka hata Ubunge hutapata kule nzega.kama mtu anashindwa kuandika Hotuba yenye kushawishi watanzania kumuamini atakua na uwezo wa kuongoza Taifa ??? Urais si lelemama......Tuwapime hawa wasaka Urais

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

"Vision is the ability to see the invisible!"
Hamisi A. Kigwangalla, MD, MPH, MBA
P.O.Box 22499,
Dar es salaam.
Tanzania.
Phone No: +255 754 636963
                +255 782 636963
website: www.peercorpstrust.org or www.hamisikigwangalla.com
Email: hamisi.kigwangalla@peercorpstrust.org or info@hamisikigwangalla.com
Skype ID: hkigwangalla
Blog: blog.hamisikigwangalla.com 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment