Monday 21 October 2013

[wanabidii] Kila Jambo analolianzisha ZITTO KABWE halifikii tamati

Naibu katibu mkuu wa Chadema na mbunge wa Kigoma Kaskazini mh Zitto Zuberi Kabwe ni miongoni mwa wa wabunge vijana kabisa wa kwanza kuonyesha kuwa vijana wanaweza haswa baada ya kujinyakulia sifa kedekede wakati wa bunge la 2005-2010 kwa kuwa ni mbunge mwenye kujenga hoja zinazokubalika na kuongea bila woga pale alipojuwa anatetea maslahi ya nchi.

Lakini baada ya Bunge la kumi 2010-2015 kuanza,mh Zitto amekuwa ni mtu asieleweka ndani ya bunge na hata ndani ya chama chake binafsi kwa hulka yake ambayo amejijengea sasa ya kukimbilia kuanzisha au kutangaza jambo ambalo either hana uhakika nalo au anajuwa haliwezi.

Zitto wa miaka hii ya 2013 sio Zitto yule wa miaka ya 2005 tuliomzoea.
Mwaka jana alianzisha sahihi kwa wabunge ili kumshinikiza waziri mkuu Pinda kujiuzulu lakini hadi leo sijui hata hizo sahihi ni ngapi zilipatikana na swala hilo liliishia wapi!!

Mwaka huu Zitto huyu huyu alitujia na habari nyingine kuwa atawataja viongozi wote walioficha pesa Uswis!!
Matokeo yake amekuwa kimya na majina yale hatujui yameishia wapi.

Wiki iliyopita Zitto huyu huyu tena akiwa km mwenyekiti wa PAC akaibuka na jipya lakini safari hii sio kwa viongozi wa Ccm pekee bali kwa vyama vyote vya siasa vinavyopata ruzuku kuwa eti havijaleta ripoti ya ukaguzi wa CAG kwa msajili wa vyama kwa zaidi ya miaka 5 na kuwataka makatibu wakuu wa vyama hivyo mara moja kuripoti kwake kuelezea sababu ya wao kushindwa kukaguliwa na CAG.

Lakini ajabu baada ya Sarakasi yote hiyo na vyama km CDM na CUF kutamka kuwa hawawezi kuripoti kwa Zitto kwa kuwa wana Makabrasha yanayoonyesha kukaguliwa kwao na kumtaka km anajuwa kuna Chama Zitto anakijua hakijakaguliwa basi akitaje,badala yake amekuwa kimya na kuachana na jambo hilo lililopamba kurasa za magazeti wiki iliyopita, leo anadai kuwa anaenda kufuatilia pesa zilizofichwa Uswis.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment