Thursday 17 October 2013

Re: [wanabidii] Sheria ya Mabadiliko ya Katiba: Kuna Mgongano wa Kimaslahi ama ni Maslahi ya Umma Yanalindwa?

Nakushukuru sana ndugu Victor kwa maoni yako. Nimesoma mahala fulani jana kuwa Rais aliusaini mswada huo tarehe 10 October. naamini rais alisaini mswada huo na kukaa na wapinzani kwa lengo la kuepusha shari kama usahuri wa makala ya Dr Kigwangala katika makala anayoizungumzia.
Kuna mambo nilifikiri Dr atakuwa jasiri wa kuyaongelea katika makala hii ya sasa.
Rais anasaini msada huu unaohitaji marekebiso kwa mara ya pili. katika mara zote wabunge wa U[pinzani wanakuwa wameona kitu ambacho wabunge wa chama Tawala wanakuwa hawakukiona na wapinzani wanaposema wabunge hao (wa CCM) hawakioni mpaka inalazimika kususia kikao, na kwa mshangao Rais anakwenda kukiona walichokosa kukiona swabunge wa chama chake.
Mimi nilitegemea Dr Kigwangala angelionelea hilo kuwa wabunge wa CCM wana mpango gani Bungdeni kuwasikiliza wapinzani ili Rais asilazimike3 kuwa anasaini miswada inayorekebishwa hapohapo. Ni jambo la kushangaza kusema eti huwezi kuwa "perfe3ct" kastikas mambo yote. Yaani watu wazima mnaona mtu anasema 1x10=50. Mwingine anasema tusahihishe hapo. Wengine mnasema tupige kura. Na tunajua mko wengi na hamna aibu. Unawalazimisha watu wennye akili kujadili hesabu hiyo. Wakikisusia kikao unawalaumu?
Rais kaokoa jahazui. Wabunge wetu wa Chama tawala watusaidie kujua kuko mbele itakuswaje kuepuka msada wa Tatu kusainiwa kama hii miwili
Elisa
--------------------------------------------
On Wed, 10/16/13, Victor Mwita <victormwita@gmail.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] Sheria ya Mabadiliko ya Katiba: Kuna Mgongano wa Kimaslahi ama ni Maslahi ya Umma Yanalindwa?
To: wanabidii@googlegroups.com
Cc: afya-club@googlegroups.com, mabadilikotanzania@googlegroups.com
Date: Wednesday, October 16, 2013, 8:35 AM

Mh. Dr. Hamis suala la Katiba ni letu
sote, unfortunately wote nyie wabunge tuliowaamini
kutuwakilisha mnalipeleka kivyama. Ningefurahi mantiki tu
ndio ingewaongoza na sio itikadi. Kwangu mm wote (majority
na minority) mliongozwa na itikadi katika kujadili na
kupitisha hii sheria. Namshukuru Mh. Rais kwa kuona kuwa
Tanzania ni kubwa kuliko nyie mnaoona kila kitu kisiasa.


Kila nchi ina mambo ya kitaifa yanayovuka itikadi za vyama.
Hapa kwenu bungeni hakuna kitu kama hicho?

Ww ni msomi na mtaalam pia but niliona mchango wako
haukureflect upeo mkubwa ambao najua unao.

Naamini Mh. Rais atatumia busara zile zile alizotumia na
kuweka maslahi mapana ya Taifa katika kuusaini au kutousaini
muswada maana Katiba inampa mamlaka ya kufanya moja kati ya
hayo.
On Oct 16, 2013 5:51
PM, "Dr. Hamisi A. Kigwangalla" <hkigwangalla@gmail.com>
wrote:





Sheria ya Mabadiliko ya Katiba: Kuna Mgongano wa
Kimaslahi
ama ni Maslahi ya Umma Yanalindwa?



Na Dkt. Hamisi
Kigwangalla, MB.

Wiki iliyopita niliandika makala iliyokuwa inachambua ni
nini iwe njia ya kupita kufikia kukamilisha mchakato wa
kukamilisha 'sheria ya
marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya Katiba ya mwaka
2013' kwa muafaka wa
kitaifa. Kufuatia nia safi ya Mhe. Rais Jakaya Kikwete,
kupitia hotuba yake
adhimu kwa Taifa ya mwezi uliopita, wengi tulibaki
tukijiuliza ni nini kifuate?

Mhe. Rais anataka muafaka wa kitaifa na anataka
kutuunganisha watanzania wote ili tufike salama kwenye
kukamilisha mchakato wa
kuandika katiba mpya. Hili, narudia tena, kwa yeyote yule
mwenye akili timamu
na mwenye kulitakia mema Taifa letu atalikubali, na kwenye
hili asirudi nyuma
kamwe. Akijaribu kurudi nyuma kwa hakika nafsi yake itamsuta
na kwa Mungu
atapaswa kujibu. Mzigo wa Taifa hili uko mikononi mwake.
Hautui mpaka dhamana
tuliyompa imuondoke.

Sisi kazi yetu ni kumshauri na kuonesha tunachokitamani,
na
yeye atapima na kuamua.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano, Ibara ya 62
na
63, Bunge lina sehemu mbili, Rais wa Jamhuri na wabunge, na
kwa maana hiyo
sheria ama jambo lolote lile haliwezi kuwa limekamilishwa
bila kupitia moja ya
sehemu hizi. Sheria tunayoizungumzia hapa imepitia hatua ya
kwanza ya
kupitishwa na wabunge, inasubiri uamuzi wa sehemu ya pili
sasa, Rais wa
Jamhuri. Anaweza kuamua lolote kwa mamlaka aliyopewa na
Katiba ya Jamhuri wa
muungano, kusaini ama kutokusaini. 

Katika makala ile nilijaribu kuchambua kwa ufupi sana,
nini
kitatokea kama angechukua njia ipi. Binafsi, nilijitahidi
sana kuepuka kuonesha
msimamo wangu mkali kwenye jambo hili, kwa kuheshimu mamlaka
ya Rais na kuepuka
kuonekana najaribu 'kumteka nyara' fikra zake.

Ukweli utabaki kuwa ukweli tu kwamba, niliegemea zaidi
kwenye njia ya muafaka wa kitaifa na ambayo itatuacha
wabunge wote na
watanzania 'washindi'. Staili hii ni ya kimarekani.
Inaitwa 'win – win
situation'. Sikuweka msimamo wa chama changu ila nilisema
ukweli tupu.

Nimepata maoni na maswali mengi sana kutoka kwa wasomaji,
nikaamua
nijibu baadhi ya hoja hapa. Kwanza, nisisitize kuwa mchakato
wa kupitishwa kwa
sheria ile bungeni ulikamilika ipasavyo na hakukuwa na
mapungufu yoyote yale
kwa mujibu wa Katiba, Sheria, Kanuni na tamaduni zilizopo.
Wengi wanataka
kuaminishwa ama wanajilazimisha kuamini kuwa sheria haiwezi
kutungwa na
kupitishwa na Bunge bila kupelekwa kwa 'wadau'. Si
kweli, maana si lazima. Hili
ni jambo la busara tu ndani ya kamati husika kuamua
kukusanya 'maoni' na 'ushauri'
wa watu ambao wanaaminika kuwa ni 'wadau' ama walengwa
wa sheria inayotungwa. Napigia
mstari tena, kuwa ni 'busara' tu na hivyo si hitaji la
lazima la Katiba, Sheria
ama Kanuni.

Vyombo vyenye kazi ya kutunga sheria ni Rais kwa upande
mmoja na Wabunge kwa upande wa pili. Wabunge
walikwishamaliza kazi yao, bado
tunasubiria Rais naye afanye ya kwake.

Lakini nikiri pia kuwa kuna vipengele vya sheria ile
iliyopitishwa na Bunge vinaweza kuwa na mapungufu; hili si
kitu sana, kwa maana
hakuna sheria iliyowahi kutungwa na ikategemewa kuwa kamili
("perfect") kama
msahafu wa quran ama biblia. Na ndiyo maana ikawepo fursa ya
kufanya
marekebisho kwenye sheria. Na labda niseme tu hapa kwamba,
huu ni moja ya
msingi wa ushauri wangu kwa Mhe. Rais kwenye makala yangu
iliyopita. Kwamba akikamilisha
mchakato wa kutungwa na kupitishwa kwa sheria hii kwa
kusaini na kisha kuelekeza
serikali kupeleka bungeni mapendekezo ya marekebisho kwa
njia ya 'hati ya dharura'
atakuwa ameliokoa Taifa na kila kitu kitaenda kwa ratiba
kama ilivyo.

Kilichotokea Bungeni ni kwamba, wapinzani walisusia
mchakato
wa kutunga sheria ile ilhali wakijua fika kuwa hakuna
kilichoenda mrama zaidi
ya kuwa na mapendekezo yao ambayo walishindwa kuyapenyeza
kwa njia ya 'ushauri
na ushawishi' (Consultation and consensus building) katika
hatua za awali na walijua
kuwa kwa kuwa wao ni wachache wasingefanikiwa kuyapitisha
bungeni. Wakaamua kutengeneza
hoja za maksudi za kususia mchakato ili hapo baadaye wapewe
fursa ya
kusikilizwa na Rais ili washinikize yapite ama sivyo
'wataliteka nyara' Taifa
kwa vitisho vya kuhamasisha uasi wa wananchi dhidi ya
serikali.

Kuna wasomaji waliniandikia wakisema kuwa ni heri ya wale
wabunge waliotoka nje ya bunge kuliko ya wale waliobaki
ndani ya bunge 'wakitukana!'
Kutukana ndani ya bunge ni jambo linalokatazwa. Hivyo hakuna
aliyebaki na
kuanza kutukana.

Lakini, tabia ya kususia kikao cha bunge si ya kiuongozi
na
ni kosa la kikatiba. Kwa mujibu wa ibara ya 63 ya Katiba ya
Jamhuri ya
Muungano, wabunge ni wawakilishi wa wananchi kwenye
kuisimamia na kuishauri
serikali, na kwenye kutunga sheria. Kuwepo ndani ya Bunge ni
kutekeleza jukumu
la kwanza la msingi la Mbunge yeyote yule la kikatiba la
'uwakilishi'. Kusema lolote
ama kutosema ni mambo ya upili. Kuwa na hoja ya msingi ama
'pumba' ni mambo ya
nafasi ya tatu kabisa kwa umuhimu, ukizungumzia demokrasia
ya uwakilishi
bungeni.

Kwa maoni yangu, mchakato wa mashauriano na maridhiano
ungepaswa
uwe unafanyika mwanzoni kabla hatujaingia bungeni kujadili
sheria na hatimaye
kuingia kwenye tofauti kubwa namna hii. Niwashauri wenzetu
wa upinzani na hata
wa CCM bungeni kuitumia vizuri nafasi ya Waziri Mkuu pale
Bungeni, maana yeye
ni msimamizi mkuu wa shughuli za serikali Bungeni.
Mashauriano, maridhiano na
mapatano yataleta utangamano na mshikamano wa kitaifa,
tuyakumbatie. Hili Taifa
ni letu sote, hatuna sababu ya kuhitilafiana kiasi hiki kama
kweli kuna hoja za
msingi.

Kwa namna mchakato ulivyoenda na kwa kuzingatia hapa
tulipofikia, njia pekee iliyopo si ya kuonesha namna gani
wabunge walio wengi
waliupitisha muswada huu bungeni bila umakini. Siwaoni
wabunge wa CCM wakifurahishwa
na wakiridhia mtazamo ama uamuzi wenye msingi huu.

Namna pekee ya busara itakayotoa ushindi kwa kila kundi
ni
kutambua kazi ya wabunge walio wengi walioupitisha muswada
ule na pia kutambua
mapungufu yaliyopo – mfano lile la kuiua tume ya
mabadiliko ya katiba kabla ya
mchakato kufikia mwisho. Hili kiukweli lina mantiki ndani
yake; tukiwa kwenye
bunge la katiba hakutokuwa na serikali, sasa ni nani
atakayejibu na kuweka sawa
hoja za wabunge? Hili kwa kweli wabunge tuliopitisha muswada
ule hatukuliona
vizuri. Hivyo basi,  jambo hili na
mengine ya namna hiyo yasipuuzwe, yapelekwe bungeni kama
marekebisho.

Kama Rais akiamua kuchukua njia ya kutoisaini sheria hiyo
na
hivyo kuirudisha bungeni ikiwa na maoni yake itakuwa fedheha
kubwa kwa wabunge
wa CCM, chama tawala anachotokea,  na
wale wachache wa upinzani walioshiriki kuupitisha muswada
huu. Siwezi kuamini
kama anaweza kuwafedhehesha wabunge wake kiasi hicho. Najua
kuna wasomaji
wataguna kwenye hili, lakini haiondoi ukweli kwamba hili
halina sura nzuri
kwenye siasa na uongozi wa Taifa letu. Hata kama tunamtaka
Rais wetu asimame kitaifa
namna gani, lakini si kwa gharama ya kuwafedhehesha wabunge
wake. Ni busara
kutafuta njia ya kuyaunganisha mapendekezo ya wapinzani
kwenye sheria hii
kimkakati bila kuleta 'stalemate'.

Rai yangu kwa watanzania wenzangu ni kuwa, kuweni makini
sana
na sisi wanasiasa, kuna nyakati baadhi yetu huyageuza maoni
na malengo yao ya
kisiasa kuwa ya umma. Mitazamo ya kisiasa ya kundi moja la
kisiasa si lazima
iwe sahihi zaidi ya kundi jingine. Tusishabikie bila kujua
ukweli wa mambo
maana tutaliangamiza Taifa kisha tuje kujuta wakati maji
yalikwisha mwagika. Na
sisi wanasiasa tuwajibike ipasavyo (tuwe 'responsible')
kwa Taifa hili maana
yakiharibika hapa wanaopoteza zaidi ni wananchi! Hii ni
dhamana yetu, tuitendee
haki.

Dkt. Hamisi
Kigwangalla ni Mbunge wa Jimbo la Nzega na Mwenyekiti wa
Kamati ya Bunge ya
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
 Anapatikana kwa simu na +255782636963 na
Email: hkigwangalla@gmail.com



"Vision is the ability to see the invisible!"
Hamisi A. Kigwangalla, MD, MPH, MBA
P.O.Box 22499,
Dar es salaam.
Tanzania.
Phone No: +255 754 636963

                +255 782
636963
website: www.peercorpstrust.org
or www.hamisikigwangalla.com


Email: hamisi.kigwangalla@peercorpstrust.org
or info@hamisikigwangalla.com
Skype ID: hkigwangalla


Blog: blog.hamisikigwangalla.com 






--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.


---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.





--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.



--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment