Sunday 27 October 2013

Re: [wanabidii] RAIS KIKWETE ANAWEZA KUONDOKA KABLA YA CCM 2015

Ngulupa humu kuna vipofu wengi.
Wako wasiotofautisha kati ya kuchangia na kuchangisha. Yaani mtu kila kukicha wakati anachangisha anachangia milioni ishirini, hqmsini, kumi. Ukiuliza TRA kama zimelipiwa kodi hukuti jibu sahihi. Watu waliotiwa upofu hawaoni hilo wanaona anachangisha tu Na hao ni vipofu ila sikujua kama ulimaanisha hao

From: "ngupula@yahoo.co.uk" <ngupula@yahoo.co.uk>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Sunday, October 27, 2013 7:17 PM
Subject: RE: [wanabidii] RAIS KIKWETE ANAWEZA KUONDOKA KABLA YA CCM 2015

Watanzania ni wepesi sana kujua unachoshindwa na wako tayari hata kupoteza miaka 5 kuzungumzia madhaifu yako..lakini kamwe hawawezi kujisumbua kuangalia unaweza nini na wafanyaje kukusaidia uwasaidie...leo hii mtu mwenye akili zake timamu analaumu waziwazi lowassa kusaidia kuchangisha fedha ili kusaidia kujenga nyumba za ibada na nk..eti anaita huko nako ni ufisadi..kimsingi mtu huyu ni mpofu wa kiroho na upeo wake kisiasa ni of single dimension..hajui dini zina sehemu gani ktk maisha ya mtanzania na mustakali wa taifa..haelewi pia changamoto za dini nyingi ni nini na  nini kifanyike ktk taifa hili ktk changamoto hizo... Haishangazi,hata Yesu alipokuwa anahubiri ufalme wa Mungu,wengine walimuona ni mkombozi,wengine walimuona hatari..mimi kauli yangu ni hii HAKUNA YEYOTE ATAYESHINDA KITI CHA URAIS TZ 2015 KWA KUJIFICHAFICHA. Tuliyafanya makosa hayo 2005 tukamchagua tuliyedhani tunamjua kumbe hatukumjua..the coming election,watz tuko tayari kuongozwa hata na mwizi kama ana uwezo wa kutusaidia..kuliko kumchagua tunayedhani ni mbwa kumbe ni simba au panya..ngupula
-----Original Message-----
From: ELISA MUHINGO
Sent:  27/10/2013, 12:20  pm
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] RAIS KIKWETE ANAWEZA KUONDOKA KABLA YA CCM 2015

Lakini Yona
Kikwete kama unavyosema Katabiri.
Kutabiri si kulaani. Kutabiri ni kusema kesho mvua itanyesha na ikinyesha si wewe uliileta. La. Uliona dalili. hapo haitegemewi kumpiga madongo aliyetabiri ila ni mwenye akili kushika mwavuli.
Kuanguka kwa CCM kunaelekea kufikia hatua ya kutoepukika na wala shida si Kikwete anayemaliza muda wake bali wanaotaka kuingia. Habari za wahuni kugawa rushwwa kwa Makatibu wa wilaya na mikoa hazijakanushwa na wala hakuzigawa JK. Kumshughulikia JK ni ujinga wa hali ya kuelekea upumbavu nmaana anaondoka kweli. Iwe 2015, 2014 au 1016 lakini anaondoka. Watanzania wanaweza kuvumilia madhaifu yake maana anamaliza muda na umebaki mfupi. Watanzania wanamuogopa huyo anayesambaza hela makanisani, misikitini, Jumuia za chama chake na sasa makatibu wa mikoa na wilaya. Huyo ni mmbaya zaidi na kama JK anawasaidia waTanzania kumuepuka tunamshukuru sana. Chama chetu kikimuangusha waTanzania tutamdaka na kumuweka chini asivunjike

________________________________
From: Yona Maro <oldmoshi@gmail.com>
To: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>; Wanazuoni <wanazuoni@yahoogroups.com>
Sent: Saturday, October 26, 2013 10:20 AM
Subject: [wanabidii] RAIS KIKWETE ANAWEZA KUONDOKA KABLA YA CCM 2015

Ndugu zangu 

Nimesoma habari kadhaa asubuhi ya leo vikikariri kauli ya rais kikwete ambaye ni mwenyekiti wa ccm kwamba ccm inaweza kuongoka mwaka 2015 .

Kauli hii nyepesi haiwezi kupita hivi hivi bila kuambiana ukweli .

Huyu raisi kikwete anayeitabiria CCM kuanguka mwaka 2015 anaweza kuanguka yeye mwenyewe aondolewe kwa kuondolewa kwenye nafasi ya mwenyekiti wa CCM taifa na rais wa Jamhuri kwa ujumla tena na wabunge wake wenyewe maana amechangia zao la CCM la sasa yeye kama mwenyekiti hata kama ameifanyia nini CCM na TAIFA kwa ujumla .

Tunakumbuka kuanzia mwaka 1995 alipokatazwa kugombea urais na wakubwa wa CCM alianza kutengeneza mtandao wa kumwingiza madarakani mwaka 2005 – Kwenye mbio hizi tunaona propaganda na ubaguzi uliotumika dhidi ya wana CCM wenzake haswa salim ahmed Salim aliyeitwa Majina ya kibaguzi baguzi .

Mwaka 2005 kuelekea 2010 rafiki yake kipenzi aliachia ngazi kama waziri mkuu kesi hiyo mpaka leo haijulikani iliishia wapi na hakuna mtu aliyefikishwa mahakamani au hata kusikia ameshinda au kushinda kesi .

Mwaka 2010 makundi ambayo yaliasisiwa na kikwete mwenyewe yanaendelea kimpango wao , baadhi yao walienda kuanzisha chama cha CCJ lakini wakaacha baada ya kupewa uwaziri na nafasi nyingine ndani ya CCM ,ubaguzi ule ulioanza miaka hiyo unaendelea kutafuna ndani ya CCM na Taifa kwa ujumla .

Mwalimu JK – Bila CCM imara nchi itayumba 

Na ndio sasa tunaona CCM Si imara kama ilivyokuwepo miaka kadhaa iliyopita sasa hivi nchi inayumba kuanzia ubaguzi wa kidini , mkoa , ukabila , uchama na rangi yote haya yamekuwa ni fahari kwa baadhi ya makundi ya watanzania kuongelea na kusifiana .

MCHAKATO WA KATIBA 

Mara kadhaa rais kikwete amekutana na viongozi wa vyama vya upinzani ikulu kwake yeye na kwa wenzake wanaomshauri vibaya anaona Sifa na ni democrasia kitu ambacho sio kwamba amekubali kusaliti CCM yake kwa vyama vya Upinzani huko Ukulu .

Hivi vyama vya upinzani viliondoka vyenyewe bungeni kwa kususa na waliobaki walipiga kura kwa kukubaliana sasa iweje rais ambaye ni mweyekiti wa chama kilichopigia kura rasimu bungeni awaite na wabadilishe mambo ina maana hakubaliani na ule wingi wa wabunge wake ?

MWISHO .
Nasema na nasisitiza kwamba kabla ya mwaka 2015 rais kikwete anaweza kungoka yeye mwenyewe kwa kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye na wabunge wake mwenyewe ndani ya bunge kama akiendelea na hizi tabia tabia zake .

Tunashukuru kwa yale aliyoyatendea taifa hili lakini kwa hali ilivyosasa hivi yeye ashike nafasi yake la sivyo yeye ndio ataondoka ikulu kwa aibu 

--

Find Jobs in Africa Jobs in Africa
International Job Opportunities International Job Opportunities
Jobs in Kenya Jobs in Kenya
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment