Tuesday 8 October 2013

Re: [wanabidii] Maoni ya Tundu Lissu baada ya hotuba ya Rais Kikwete ya mwisho wa Septemba 2013

Just let it go Mgonge.

mngonge <mngonge@gmail.com> wrote:

>makubwa hayo, madogo yana wenyewe.
>Kwa leo mimi napita tu. Hivi Lissu kama Lissu alitinga Ikulu na hayo madai
>ya JK au kuna sehemu nyingine walikutana akwamwambia hayo? nimeshindwa
>kuelewa premises alizozitumia Jk kuanzisha hoja ya kumtuhumu Lissu kama
>Lissu. Kama kuyasikia ni wapi aliyasikia? Baada ya kuvilaumu vyama vya
>upinzani kwa ujumla wake why Lissu as Lissu? Ebu nisadieni waungwana
>
>
>2013/10/8 Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
>
>> Kwa hesabu zangu za haraka haraka, Rais Kikwete amenitaja mara nne katika
>> hotuba yake:
>>
>> "... Mheshimiwa Tundu Lissu alitoa maoni yake."
>>
>> "Siyo tu kauli ya Mheshimiwa Tundu Lissu ni uzushi na uongo mtupu, bali
>> pia ni ya unafiki, fitina na uzandiki wa hali ya juu."
>>
>> "... (K)wa Mheshimiwa Tundu Lissu kudai kuwa mapendekezo ya TEC na CCT
>> hayakuheshimiwa ni uongo wa mchana
>> usiokuwa na kichwa wala miguu."
>>
>> "Kama ni kwa sababu za Mheshimiwa Tundu Lissu nimeshasema hazina ukweli
>> wowote."
>>
>> Na kwa hesabu zangu hizo hizo, Rais amesema 'ameambiwa', 'amefahamishwa'
>> au 'ameelezwa' juu ya yaliyojiri kwenye Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala
>> na baadaye Bungeni mara tisa!!! Katika hotuba yake, Rais hajaliambia Taifa
>> ni nani hasa '(w)aliyemwambia' au 'kumfahamisha' au 'kumweleza' mambo hayo.
>>
>> Katika hali nadhani sitakosea kusema kwamba yote aliyoyasema Mheshimiwa
>> Rais Dokta Jakaya Mrisho Kikwete ni mambo ya 'sikiasema' (au hearsay) kama
>> wanavyosema wanasheria. Kisheria ushahidi wa sikiasema hauna thamani
>> yoyote. Kwa maneno mengine, maneno ya JK hayana thamani yoyote kiushahidi,
>> hata kwa ushahidi wa kipropaganda za kisiasa alizozifanya juzi.
>>
>> Lakini ni kauli zangu zipi ambazo zimezua mashambulizi haya makubwa from
>> the First Citizen? Kwa wasiokumbuka, nilisema yafuatayo katika hotuba yangu
>> ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni: "Katika kutekeleza majukumu yake ya
>> kuuchambua Muswada huu, Kamati ... Ilikutana na wadau wengi mbali mbali.
>> Hivyo, kwa mfano, Kamati ilipata maoni ya taasisi za kidini na za kiraia;
>> taasisi za elimu ya juu na za kitaaluma; vyama vya siasa na asasi nyingine.
>> Kwa sababu ambazo Kamati haikuelezwa vizuri na uongozi wa Bunge hili
>> tukufu, mapendekezo ya Kamati kwenda Zanzibar kwa lengo la Kukusanya maoni
>> ya wadau wa Zanzibar juu ya Muswada huu muhimu kwa mustakbala wa Jamhuri ya
>> Muungano yalikataliwa."
>>
>> Nikaendelea kusema: "(Ni) muhimu Bunge lako tukufu lifahamu ukweli huu
>> kwamba wadau pekee walioshirikishwa kutoa maoni yao juu ya Muswada ni
>> Watanzania Bara tu. Wazanzibari hawakupatiwa fursa hiyo na
>> hawakushirikishwa kabisa, licha ya Sheria yenyewe kuwa na mambo mengi
>> yanayoihusu Zanzibar."
>>
>>
>> Kuhusu uteuzi wa Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nilisema
>> yafuatayo: "... Uteuzi wa Wajumbe wa Tume uliofanywa na Rais na ambao
>> unatumiwa Kama mfano (wa kuteua Wajumbe 166 wa Bunge Maalum) wenyewe
>> ulikuwa na walakini kubwa. Katika hili, kuna ushahidi wa Wawakilishi wa
>> Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Baraza la Kikristo Tanzania
>> (CCT) na asasi mbali mbali za kiraia zikiwemo za walemavu waliowasilisha
>> maoni ya taasisi zao kwa Kamati juu ya Muswada huu. Wawakilishi hao
>> waliiambia Kamati kwamba ijapokuwa waliandikiwa na Rais kuwasilisha majina
>> ya Wajumbe wao kwa ajili ya kuteuliwa kwenye Tume, na walifanya hivyo,
>> hakuna hata moja ya majina waliyopendekeza aliyeteuliwa na Rais kuwa Mjumbe
>> wa Tume. Badala yake, Rais aliteua watu aliowaona yeye na washauri wake
>> wanafaa. Kama taarifa za wadau hawa ni za kweli maana yake ni kwamba Rais
>> na Mwenyekiti huyu wa CCM Taifa hawezi kuaminika tena kuteua Wajumbe halisi
>> wa taasisi hizi katika Bunge Maalum...."
>>
>> To wind up, Kamati ilitengeneza orodha ya taasisi na watu binafsi wa
>> Zanzibar ambao ilitaka kupata maoni yao. Hatukuonana na hata mmoja wa
>> taasisi na watu binafsi hao kwa sababu Kamati haikuruhusiwa kwenda
>> Zanzibar. Aidha, Kamati haikukutana na mwakilishi hata mmoja wa Serikali ya
>> Mapinduzi Zanzibar. Pili, Wawakilishi wa TEC (Father Dr. Charles Kitima),
>> CCT (Mchungaji Rohho) na wa SHIVYAWATA (nimemsahau jina) ndio walioiambia
>> Kamati kwamba mapendekezo yao hayakuheshimiwa katika uteuzi wa Wajumbe wa
>> Tume. Mimi sikuyatoa uchochoroni, yalisemwa hadharani mbele ya Kamati!
>>
>> Sasa kama ni uongo, fitina, uzandiki na mapambo ya aina hiyo aliyonipamba
>> nayo Rais, basi ninakiri kuwa I'm guilty as charged!!!
>>
>> Tundu
>>
>>
>> --
>> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>> ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
>> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
>> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree
>> to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>> ---
>> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
>> "Wanabidii" group.
>> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
>> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>>
>
>--
>Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
>Kujiondoa Tuma Email kwenda
>wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
>Disclaimer:
>Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>---
>You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
>To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment