Tuesday 8 October 2013

Re: [wanabidii] Maoni ya Tundu Lissu baada ya hotuba ya Rais Kikwete ya mwisho wa Septemba 2013

Nina masahaka na haya ya lissu anasahau kwamba urais ni taasisi
chochote kinachotokea si rahisi mwenye nchi kutambua.

Nina swali moja kwa mhe. Lissu, ni kweli chadema wana nia ya dhati
kweli na wazanzibar, na kuyataka maoni yao, ikumbukwe Zanzibar
walipita katika kipindi kigumu ulipokuja muafa na serikali ya umoja wa
kitaifa chadema walipinga na kuwaita cuf kama "ccm b" na ikapelekea
kukataa kuunda serikali kivuli bungeni kwa kuwa ni "ccm b"

Je walitaka Zanzibar waendelee kugombana, wasizikane, kusalimiana na
kushugulika pamoja mambo ya kijamii kama hali ilivyokuwa miaka ya
nyuma, katika haya ni kweli wanania ya kweli kutaka maoni ya znz au
ndio kutafuta umaarufu znz?

Wakati huo huo maoni ya serikali 3 asilimia kubwa yametoka wapi kama
si Zanzibar na yalipatikane, naomba kufahamishwa juu hili.

pili napenda kuwatahadhlisha wale wanaobeza michango ya wenzao katika
majukwaa kama haya kwamba hii ndio demokrasi, usimshutumu mtu kwa
kutokuwa upande wako au kumkosoa kiongozi unayempenda au kumkubali.
Kumbukeni kuwa anayekukosoa anakupenda.

On 10/8/13, ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com> wrote:
> Tundu.
> Tunashukuru kwa maelezo haya. Lakini nashauri hivi. tafadhali fanya
> maandalizi ya viongozi wa vyama vitatu kukutana na Rais ku iron out mambo
> haya. Hili nawe unajua kuwa Rais (kama alivyoeleza) aliambiwa. Huko mtaongea
> nini? nafikiri haya ni sehemu yake. Watanzania tunataka kuona mswada wa
> sheria unarekebishwa na Rais anatia sahihi mswada unaokubalika ili tuone
> kama tutapata katiba tuitakayo.
> Mkiendelea kurumbana mwishowe hamtakipata kilichowatoa bungeni mkasusia
> mswaada na mkaungwa mkono na watanzania wengi na wema na Rais akiwemo.
> Ndugu yangu. naomba!!!!!!!!!!!!!
>
>
> ________________________________
> From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
> To: wanabidii@googlegroups.com
> Sent: Tuesday, October 8, 2013 1:45 PM
> Subject: [wanabidii] Maoni ya Tundu Lissu baada ya hotuba ya Rais Kikwete ya
> mwisho wa Septemba 2013
>
>
>
> Kwa hesabu zangu za haraka haraka, Rais Kikwete amenitaja mara nne katika
> hotuba yake:
>
> "... Mheshimiwa Tundu Lissu alitoa maoni yake."
>
> "Siyo tu kauli ya Mheshimiwa Tundu Lissu ni uzushi na uongo mtupu, bali pia
> ni ya unafiki, fitina na uzandiki wa hali ya juu."
>
> "... (K)wa Mheshimiwa Tundu Lissu kudai kuwa mapendekezo ya TEC na CCT
> hayakuheshimiwa ni uongo wa mchana
> usiokuwa na kichwa wala miguu."
>
> "Kama ni kwa sababu za Mheshimiwa Tundu Lissu nimeshasema hazina ukweli
> wowote."
>
> Na kwa hesabu zangu hizo hizo, Rais amesema 'ameambiwa', 'amefahamishwa' au
> 'ameelezwa' juu ya yaliyojiri kwenye Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala na
> baadaye Bungeni mara tisa!!! Katika hotuba yake, Rais hajaliambia Taifa ni
> nani hasa '(w)aliyemwambia' au 'kumfahamisha' au 'kumweleza' mambo hayo.
>
> Katika hali nadhani sitakosea kusema kwamba yote aliyoyasema Mheshimiwa Rais
> Dokta Jakaya Mrisho Kikwete ni mambo ya 'sikiasema' (au hearsay) kama
> wanavyosema wanasheria. Kisheria ushahidi wa sikiasema hauna thamani yoyote.
> Kwa maneno mengine, maneno ya JK hayana thamani yoyote kiushahidi, hata kwa
> ushahidi wa kipropaganda za kisiasa alizozifanya juzi.
>
> Lakini ni kauli zangu zipi ambazo zimezua mashambulizi haya makubwa from the
> First Citizen? Kwa wasiokumbuka, nilisema yafuatayo katika hotuba yangu ya
> Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni: "Katika kutekeleza majukumu yake ya
> kuuchambua Muswada huu, Kamati ... Ilikutana na wadau wengi mbali mbali.
> Hivyo, kwa mfano, Kamati ilipata maoni ya taasisi za kidini na za kiraia;
> taasisi za elimu ya juu na za kitaaluma; vyama vya siasa na asasi nyingine.
> Kwa sababu ambazo Kamati haikuelezwa vizuri na uongozi wa Bunge hili tukufu,
> mapendekezo ya Kamati kwenda Zanzibar kwa lengo la Kukusanya maoni ya wadau
> wa Zanzibar juu ya Muswada huu muhimu kwa mustakbala wa Jamhuri ya Muungano
> yalikataliwa."
>
> Nikaendelea kusema: "(Ni) muhimu Bunge lako tukufu lifahamu ukweli huu
> kwamba wadau pekee walioshirikishwa kutoa maoni yao juu ya Muswada ni
> Watanzania Bara tu. Wazanzibari hawakupatiwa fursa hiyo na hawakushirikishwa
> kabisa, licha ya Sheria yenyewe kuwa na mambo mengi yanayoihusu Zanzibar."
>
>
> Kuhusu uteuzi wa Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nilisema yafuatayo:
> "... Uteuzi wa Wajumbe wa Tume uliofanywa na Rais na ambao unatumiwa Kama
> mfano (wa kuteua Wajumbe 166 wa Bunge Maalum) wenyewe ulikuwa na walakini
> kubwa. Katika hili, kuna ushahidi wa Wawakilishi wa Baraza la Maaskofu
> Katoliki Tanzania (TEC), Baraza la Kikristo Tanzania (CCT) na asasi mbali
> mbali za kiraia zikiwemo za walemavu waliowasilisha maoni ya taasisi zao kwa
> Kamati juu ya Muswada huu. Wawakilishi hao waliiambia Kamati kwamba
> ijapokuwa waliandikiwa na Rais kuwasilisha majina ya Wajumbe wao kwa ajili
> ya kuteuliwa kwenye Tume, na walifanya hivyo, hakuna hata moja ya majina
> waliyopendekeza aliyeteuliwa na Rais kuwa Mjumbe wa Tume. Badala yake, Rais
> aliteua watu aliowaona yeye na washauri wake wanafaa. Kama taarifa za wadau
> hawa ni za kweli maana yake ni kwamba Rais na Mwenyekiti huyu wa CCM Taifa
> hawezi kuaminika tena kuteua Wajumbe halisi wa taasisi hizi katika Bunge
> Maalum...."
>
> To wind up, Kamati ilitengeneza orodha ya taasisi na watu binafsi wa
> Zanzibar ambao ilitaka kupata maoni yao. Hatukuonana na hata mmoja wa
> taasisi na watu binafsi hao kwa sababu Kamati haikuruhusiwa kwenda Zanzibar.
> Aidha, Kamati haikukutana na mwakilishi hata mmoja wa Serikali ya Mapinduzi
> Zanzibar. Pili, Wawakilishi wa TEC (Father Dr. Charles Kitima), CCT
> (Mchungaji Rohho) na wa SHIVYAWATA (nimemsahau jina) ndio walioiambia Kamati
> kwamba mapendekezo yao hayakuheshimiwa katika uteuzi wa Wajumbe wa Tume.
> Mimi sikuyatoa uchochoroni, yalisemwa hadharani mbele ya Kamati!
>
> Sasa kama ni uongo, fitina, uzandiki na mapambo ya aina hiyo aliyonipamba
> nayo Rais, basi ninakiri kuwa I'm guilty as charged!!!
>
> Tundu
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment