Mbona Elisa unaegamia upande mmoja tu, yaani makosa unayaona kwa Nape tu. yaani huoni kabisa upande mwingine wa shilingi
2017-04-11 15:06 GMT+03:00 'Mohamed Mnzava' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
Makala yako ni tafsiri nzuri sana kuhusu kipindi kifupi cha safari ya kisiasa ya Nape.
Sent from my iPad--Elisa MuhingoKaka mkubwaMi mdogo wako napenda sana maandishi yako, ufikirisha na kuna wakati huwa nakuona kama mwalimu fulani ambaye huendesha somo lake kupitia vichokoo. Hii humsaidia mwalimu kuwaelewa wanafunzi wake upeo wao katika maeneo tofauti.Nape kupitwa na wakatiKama kuna kitu kimeiangusha Afrika na kule wananchi au jamii kumfanya kiongozi wao ni Mungu. Hagusiki, hakosolewi, ahambiwi tazama unakosea au mbele kuna hatari.Tazama viongozi wa dini, wa jadi, n.k. wapo kimya hata kama kiongozi akifanya mauaji. watayahita mauaji matakatifu.Nape anayeonekana kupitwa na wakati, ameonesha hataki, amekataa mfumo huo. Nape kama kijana mtu mkomavu kuelekea utu uzima, anaonyesha ukombozi kutoka katika fikra lala. Anavunja minyororo ya ukabila, ubaguzi, unyanyasaji na ubwana. Anaheshimu kwa dhati uongozi, lakini anakimbia unafiki wa kusifu sehemu chafu. Huyu ni wakisasa.Mama zetu wakiweza kuondokana na unyanyasaji bila kuogopa kuambiwa hawanaheshima na unyenyekevu, wanaume wote tutakuwa kama Nape, mtu wa kisasa.Nape, Kinana na MangulaWalikubali kuchafuka na ccm ( ilifika maali, mtu akiwa mwana ccm. mbele zatu alikuwa anaona haya) wakawa kama dhahabu katika tanuru, na wakaonekana wao wanafaha, na ccm ikafaha na mgombea akaonekana amefaha. Lazima ajisifu, ajigambe na aringie hilo.Moja ya sifa ya kupenda kwanza lazima ujipende. Njia ya kujiopenda ni kujisamehe ndipo utasamehe na wengine, utawatendea kiutu.Nape asipojisifu hata weza kusifu wengine, kujisifu huku ndiko kunampa nguvu ya kutambua uwepo wa wengine, sifa zitokanazo na matendo ya wengine na thamani ya sifa hizo.Asante mwalimuElisa Muhingo
From: 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
To: ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com>; wanabidii@googlegroups.com; prudence karugendo <prudencekarugendo@yahoo.com>
Cc: "stanley.nshange@nsn.com" <stanley.nshange@nsn.com>; "innokahwa@yahoo.com" <innokahwa@yahoo.com>; "akiobya@yahoo.com" <akiobya@yahoo.com>; "tkiobya@yahoo.com" <tkiobya@yahoo.com>; "hkahyoza@yahoo.com" <hkahyoza@yahoo.com>; "emmanuelelias2005@yahoo.com" <emmanuelelias2005@yahoo.com>; "repeatitagency@yahoo.com" <repeatitagency@yahoo.com>; "stanley.nshange@nokia.com" <stanley.nshange@nokia.com>; "uhalisi@yahoo.co.uk" <uhalisi@yahoo.co.uk>; "tundu.lissu@gmail.com" <tundu.lissu@gmail.com>; "pkarugendo@yahoo.com" <pkarugendo@yahoo.com>; "mbowe2008@gmail.com" <mbowe2008@gmail.com>; "bilhuda2006@yahoo.co.uk" <bilhuda2006@yahoo.co.uk>; "davidkafulila@yahoo.com" <davidkafulila@yahoo.com>; "muddy.kiobya@gmail.com" <muddy.kiobya@gmail.com>; "emmanuelelisa46@yahoo.com" <emmanuelelisa46@yahoo.com>; "wilfredlwakatare@gmail.com" <wilfredlwakatare@gmail.com>
Sent: Tuesday, April 11, 2017 1:09 PM
Subject: [wanabidii] NAPE: Kijana Anayepitwa na wakati kirahisi hivi?
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paulo Makonda alipofanya ziara yenye utata kituo cha matangazo cha Clouds, aliyekuwa waziri wa wizara husika Nape Nnauye alifanya makosa matatu kwa kupitia matamshi aliyoyatoa kulaani kitendo hicho.1) Kama kiongozi wa serikali alipaswa kutamka kwa tahadhali katika kuongelea kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar Es salaam kwa kuzingatia kuwa Makonda ni Mkuu wa Mkoa. Alipaswa kujihoji kama haiwezekani kuwa kitendo haramu cha Makonda kinaweza kuwa na manufaa Fulani kwa serikali anayoitumika.2) Kosa la pili ni kumhukumu Makonda halafu kuunda tume. Ilibidi atangulie kuunda tume ya kusikiliza pande zote kabla ya kuonyesha msimamo wake; au amlaani Makonda na aachie pale bila kuunda tume ya uchunguzi.3) Kwa kuzingatia kuwa Mkuu wa Mkoa anawajibika kwa waziri wa TAMISEMI, Nape angekuwa ametumia busara kuwasiliana na wizara husika ili washauriane na kushirikiana kumchunguza Makonda.Baada ya makosa hayo mwandishi mmoja alitoa makala iliyosema "Ningekuwa rais Nape angesikia mrithi wake radioni". Ndivyo ilivyotokea.Baada ya hapo Nape alifanya kosa jingine la msingi. Aliongea kwenye vyombo vya habari. Alifanya hivyo siku aliposikia kuwa sasa si waziri tena. Hizi ni tabia za ajabu. Haiwezekani zikawa za ajabu Nape asiwe mtu wa ajabu. Ukiiangalia tabia ya Nape unaweza kudhani nafasi pekee inayomfaa ni kuwa Rais. Chini ya hapo atakuwa anatumiwa na kutimuliwa.Sasa amekwenda jimboni kwake. Kafanya mikutano kadhaa. Mmoja akina mama walilala chini wakitaka atembee migongoni kwao. Wanampongeza. Ni shujaa. Sijui kwa kufanya nini? Nape kama mhamasishaji (Kama alivyokuwa Moses Nnauye) siwezi kushangaa mbwembwe hizo. Ila siwezi kupinga mtu akisema viliandaliwa viwe hivyo. Nimesoma maelezo fulani yakimnukuu Nape Nnauye katika moja ya mikutano yake. Anasema yeye ndiye alimuweka Magufuli madarakani. Kama ni kweli kasema sijui ina maana gani? Nakumbuka Rais Magufuli kuwahoji wafanya biashara kama kuna aliyemchangia japo shilingi aseme. Sijui kama Nape anataka kutwambia Rais angebadilisha kauli asiseme hela Nape angekuwa mmoja wao kunyosha mkono! Lakini tunajua wakati Nape akiwa Katibu wa CCM idara ya uenezi alifanya kazi kubwa iliyomletea ushindi Rais Magufuli katika kampeni za uchaguzi 2015. Watu wengi walifanya hivyo. Nami nikieleza nilichofanya kuna watakaoshangaa. Wote hao hakuna anayestahili kujiona ni yeye alileta ushindi labda awe wa ajabu. Wote walichangia ushindi huo.Nakumbuka wakati Nape, Adulrahman Kinana na Mzee Philip Mangula wanaitwa kuiongoza CCM, ilikuwa hoi na walikuja kujaribu kuifufua na kwa kweli walifanikiwa. Walifanikisha angalau katika mikutano yao (Hasa Mzee Kinana) kuongea lugha iliyokuwa ikitumiwa na wapinzani. Hii ilirudisha moyo wa watanzania wakaamini CCM inaweza kufufuka. Kinana anafahamika misimamo yake. Hata angebadilika hawezi kuupoteza kabisa uNyerere. Nawapongeza sana. Na Nape nampongeza pamoja na hao.Kipindi hicho CCM ilikumbatia watu fulani. Badala ya kumilikiwa na wanyonge ikawakumbatia matajiri na wanasiasa wengine waliojiona wao ni muhimu. Hata nyimbo kama "CCM ina wenyewe" ziliimbwa na kutafsiriwa 'vile'.Sasa CCM inafanya mabadiliko. Haitarajiwi siku za usoni kumuona mtu mmoja kuwa muhimu kuliko wengine. Inatarajiwa timu ikifanya kazi mafanikio yanakuwa yao wote. Kumkuta kiongozi leo hii anasema "mimi nilifanya hivi na vile" ni dalili ya kuelekea kupitwa na wakati na kutoiona CCM inakwenda wapi ili kwenda nayo. Hii ni hatari hasa kwa mtu anayeelekea kuamini kuwa siku moja 'atakumbukwa'. Anashindwa kuwaelewa watakaomkumbuka ni watu wa namna gani na kuwashawishi kwa mwenendo wake ili wamkumbuke kweli. Nape anapitwa na hilo bila kuliona. Inaposemwa CCM inafanya mabadiliko, inasemwa wakati Nape bado ni kiongozi wa CCM, na anaelekea kutoona mabadiliko na anaendelea ku-behave kiCCM ya zamani, anaelekea kupitwa na inaweza kuleteleza kutupwa.La pili linaloonyesha kuwa anaelekea kupitwa na wakati ni kusema " Kama rais hatachukua hatua kuhusiana na watu kutekwa basi 2020 anaweza kupoteza kura". Sitegemei mtu yeyote anayejua sheria na uendeshaji wa nchi aunganishe jinai hiyo na siasa za uchaguzi. Hili ni kosa la kuchukuliwa hatua za kisheria mara moja. Sasa yeye anasema mpaka 2020 wakati wa uchaguzi? Yaani kama si uchaguzi basi watu waachwe watekwe tu! Lakini jambo la ajabu katika matamshi haya ni kuwa utekaji huu sio kwanza unatokea hapa Tanzania. Dr. Ulimboka akiwa katikati ya kutetea maslahi ya Madaktari alitekwa na kusulubiwa na akatupwa na watekaji mahala atakapookotwa. Kiongozi wa CUF alipozolewa pale Posta na akapotea kwa siku kadhaa na kuja kuonekana mitaani baada ya siku. Dr. Mvungi akiwa kiongozi muhimu wa Tume ya katiba alivamiwa na kuumizwa vibaya sana na akafia Afrika ya Kusini. Kipindi hicho Nape alikuwa Mkuu wa idara ya uenezi ya CCM. Sikuwahi kumsikia akisema haya anayoyasema sasa baada ya matukio mawili ya utekani. Alinyamaza sheria "ichukue mkondo wake" (kama iliuchukua). Maneno haya kwa nini hakuyasema Dr. Ulimboka alipotekwa? Iweje anayasema leo wakati ametimuliwa kazi. Nape (Kwa kumbu kumbu zangu) ni kiongozi wa kwanza kutimuliwa kazi na akaitisha press conference siku hiyo hiyo. Kama angekuwa anasikiliza ushauri basi angezingatia ushauri huu: AKAE KIMYA. Mambo yatajipa huko mbele kama yalivyojipoa kwa wengine. Mwinyi anayemtolea mfano hakusikia baada ya kujiuzuru akiongea. Nape anasahau kuwa silent listeners ndio watakaoichagua CCM iliyobadilika na Magufuli wake aliyeibadilisha au mteule mwingine. Anafikiri wanaofikiwa na habari za kutekwa na kuyapa uzito wa kelele za siasa ni wengi sana mitandaoni na ndio wapiga kura pekee. Lakini ni wachache sana kwa ujumla wake. Bila kupiga hesabu hapo ataendelea kujihangaisha na anachoonekana kutafuta atakikosa kama watangulizi wake.Ninaamini kama alikuwa mshauri wa busara kwa nafasi aliyonayo ya uanachama wa CCM ushauri wake asingeutoa mitandaoni na hadharani kama wapinzani wa kisiasa. Kuna aliyefikiri kuwa kelele za Nape zilihesabiwa kumsaidia 'kuandaa atakapofikia' (akitimuliwa (maana alijua)). Kama ni hivyo aendelee maana ameishafika.Elisa Muhingo0767 187 507--Send Emails toKujiondoa TumaEmail kwendawanabidii+...@Utapata Email yakudhibitishaukishatumaDisclaimer:Everyoneposting to this Forumbearsthe soleresponsibilityfor any legalconsequences of his orher postings,andhencestatements andfacts must bepresentedresponsibly.Yourcontinuedmembership signifies thatyou agree tothisdisclaimer andpledge to abide byourRules andGuidelines.---You receivedthismessage because youare subscribedtotheGoogle Groups"Wanabidii"group.To unsubscribefrom this group andstop receivingemailsfromit, send an email towanabidii+...@For moreoptions, visitoptout.--Send Emails to wanabidii@googlegroups.comKujiondoa Tuma Emailkwendawanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email yakudhibitishaukishatumaDisclaimer:Everyoneposting to this Forumbears the soleresponsibilityfor any legalconsequencesof his or her postings,andhencestatements and factsmust be presentedresponsibly. Yourcontinuedmembershipsignifies that youagree to thisdisclaimer and pledgeto abide by our RulesandGuidelines.---You received thismessage because you aresubscribedtotheGoogle Groups"Wanabidii" group.To unsubscribe fromthis group and stopreceiving emailsfrom it, send anto wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com. For more options,visit--Send Emails to wanabidii@googlegroups.comKujiondoa Tuma Emailkwendawanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email yakudhibitisha ukishatumaDisclaimer:Everyone posting to thisForum bears the soleresponsibilityfor any legal consequencesof his or herpostings,andhencestatements and facts mustbe presentedresponsibly.Yourcontinued membershipsignifies that you agree tothisdisclaimer and pledge toabide by our Rules andGuidelines.---You received this messagebecause you aresubscribedtotheGoogle Groups "Wanabidii"group.To unsubscribe from thisgroup and stop receivingemailsfrom it, send an email towanabidii+unsubscribe@googlegroups.com. For more options, visit--Send Emails to wanabidii@googlegroups.comKujiondoa Tuma Email kwendawanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatumaDisclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.---You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com. For more options, visit https://groups.google.com/d/optout .
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com .
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout .
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com .
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout .
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment