Friday, 14 April 2017

[wanabidii] JOSEPHAT ISANGO UMENILIZA

JOSEPHAT ISANGO UMENILIZA

Na Happiness Katabazi

SAA MBILI asubuhi Leo niliingia Katika Group la Mtandao wa Whatsup la wafanyakazi ambao Tuliwahi kufanyakazi Katika Gazeti la Tanzania Daima na kukutana na taarifa Kuwa aliyewahi Kuwa Mwandishi wa Habari mwenzangu wa Gazeti Hilo ,Josephat Isango amefariki Dunia leo saa moja asubuhi katika Hospitali ya Malkia Ulimwengu ,Wilaya ya ikungi Mkoani Singida alikokuwa Amelazwa kwa wiki Moja kwaajili ya matibabu.

Sikuamini nikaamua kutuma ujumbe Kwenye Hilo group la Whatsup na Kuwauliza wanawazimu ?Kwanini wanamzushia "Mume wangu " Isango kifo?

Ndipo Mwandishi wa Gazeti Hilo la Tanzania Daima, Happiness Mnale " Wajina wangu" akanithibitishia Kuwa ni kweli Isango amefariki na akanitaka tuanze kutoa michango ya rambirambi ndipo nikaamini kweli Isango amefariki.

Chanzo cha Isango kuniita Mimi" Mke wake " na Mimi kumuita " My Husband " ni siku aliyekuwa Mhadhiri wa Sheria Mwandamizi nchini, Marehemu Dk.Sengondo Mvungi alipofariki Dunia nchini Afrika Kusini Novemba mwaka 2013alipokuwa akitibiwa majeraha aliyoyapata kutokana kavamiwa nyumbani kwake na wahalifu Kisha kumkatakata mapanga sehemu Mbali Mbali za mwili wake.

Dk.Mvungi Enzi za Uhai wake alipogombea urais Katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2005 Katika mzunguko wa pili wa kampeni nilikuwa Mwandishi wa Gazeti la Mtanzania ,aliyekuwa Mhariri wa Gazeti Hilo Gabriel Athuman alipangia Kazi ya kuzunguka nchi nzima na mgombea urais wa Chama cha NCCR - Mageuzi, Dk.Mvungi kwaajili ya kuripoti Habari zake .

Nilifanya Kazi hiyo kwa uaminifu mkubwa nakumbuka nilikuwa Mwandishi wa Habari mwanamke peke yangu Katika msafara huo ambao ulikuwa na jumla ya waandishi wanaume Saba.

Ndipo hapo waandishi wenzangu wakanipachika jina la First Lady wa Dk.Mvungi na wakimtuhumu Dk.Mvungi kumuibia Mke aliyekuwa Mgombea urais wa Chama cha TLP, Augustine Mrema ambaye ni rafiki yangu sana Kwani Katika mzunguko wa kwanza wa kampeni za 2005 ambao katikati ya mzunguko huo aliyekuwa mgombea mwenza wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) alifariki dunia hali iliyosababisha Tume ya Uchaguzi kusimamisha zoezi la kampeni na kusogeza mbele uchaguzi mkuu.

Nikiwa Mwandishi wa Gazeti la Mtanzania ,Mhariri alionipangia mzunguko wa Kwanza kuzunguka na Mrema nchi nzima ,nilizunguka naye na kuandika Habari zake Katika mazingira ya tabua na wasiwasi Kwani Katika mikutano ya Mrema Mara Kadhaa ilikuwa ikipata mushikeri kutoka kwa Polisi.

Sasa wakati wote huo niliyozunguka na Mrema nikapachikwa jina la utani na waandishi wa Habari " Mrs au First Lady wa Mrema" nilipohamishiwa Kwenye msafara wa kwa Dk.Mvungi nikapachikwa jina la " First Lady wa Dk.Mvungi".

Siku alipofariki Dk.Mvungi ,Isango ambaye tulikuwa tukifanya naye kazi ya uandishi wa Habari Katika Gazeti la Tanzania Daima, alisikitika sana akasema kuanzia siku hiyo amejitolea kunifariji Mimi mjane wa Dk.Mvungi hivyo yeye ndiyo Atakuwa mrithi wa Dk.Mvungi hivyo yeye nimempata mume wakuniliwaza yeye Isango.

Nilicheka sana licha nilikuwa na machungu ya kifo cha Dk.Mvungi.Na kweli tangu Mwaka 2013 hadi wiki iliyopita ambayo ni Mara ya mwisho Kuwasilisha na Isango ,Isango alikuwa akiniita Mimi Mkewe ,Tunapigia story Kwenye simu wee za siasa na umbea wa mtaani unasemaje ,tunacheka sana maana sote tunapenda kujadili Habari za siasa na umbea wa mtaani.

Isango ambaye ana elimu ngazi ya Shahada ,Licha ya Kuwa Mwandishi wa Habari ,Isango alikuwa Mwanachama wa Chadema na Mwaka 2010 aligombea Ubunge Jimbo la Singida mjini lakini alishindwa kufurukuta ambapo mgombea wa CCM,Mohamed Dewji ndiye Alishinda Ubunge.

Isango pia aliwahi Kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Singida lakini hakushinda.Lakini pamoja na kushindwa nafasi hizo ha kuacha kuipenda Chadema.

Isango alikuwa ni Mkatoriki Mzuri tu pamoja na madhaifu yake mengi ya kibinadamu.Isango alikuwa mcheshi na Mpenda utani sana.

Nilimpenda Isango hadi nimeamua kuacha kufanya shughuli zangu za kitaaluma Leo kukaa chini kuandika makala ya kifo Chake ili nimuenzi kwa kalamu yangu na niufahamishe umma Kuwa Isango alikuwa ni mtu wa aina gani kwa jinsi Mimi nilivyomfahamu ili umma Ufahamu.

Isango alikuwa ni mtu anayejiamini, asiyeogopa kuandika habari na makala licha alishawahi kupata misukosuko kutoka jeshi la polisi na mwenye Kupenda watu .

Kitu kikubwa kilichonifanya nimpende Isango ukiachilia Mbali mambo mengine, Isango alikuwa ni mtu au Mwandishi wa Habari mwenye akili ,moyo wa kipekee ambao baadhi ya waandishi wa Habari ambao wanaunga mkono Chadema ,CCM hawana .

Isango alikuwa Mwanachama Chadema,Mimi nilikuwa mwanadishi lakini Mwanachama wa CCM .Katika chumba cha Habari au tukikutana na Isango mitaani " Vibanda Hasara" tukianza kupiga story za kisiasa tunafanya chambuzi zetu vizuri tu na hata ukimkosoa kuhusu msimamo wake au Chama Chake Katika jambo Fulani alikuwa yupo Tayari kukubali kukosolewa na kujifunza ,wala hakuwekei kinyongo tofauti na waandishi wa Habari wengine ambao Hilo limewashinda.

Isango alikuwa na desturi ya kuwahi asubuhi Kazi ,kuna siku Polisi walimuweka mtego wa kumkamata kwasababu aliandika Habari ambayo walizani ni ya uchochezi.

Tulikaa naye saa Moja asubuhi Ofisi za Tanzania Daima ,Mtaa wa Mkwepu ,Askari wapelelezi wakiwa wamevalia kiraia walifika getini chini pale jengo la Bilicans wakajifanya wao wanataka kuonana na Mwandishi wa Habari yoyote ili wampe Habari hivyo Wakamuomba Mlinzi wa getini awatafutie Mwandishi .

Yule Mlinzi Anachukua simu pale chini akapiganie simu juu ghorofani ambapo ndipo chumba cha Habari kilipo ikapokelewa na Isango, Mlinzi akamweleza alichooelezwa na Askari wale wapelelezi Kuwa kuna Wanaitaji Mwandishi wa kuwatandika Habari ,Isango akamwambia Mlinzi awaruhusu watu wale bila kujua ni Askari wanaokuja kumkamata yeye waje Kwenye chumba cha Habari n a kwamba yeye ndiyo at awasikiliza na kuwatandika Habari Yao.

Askari wale kweli waliingia hadi chumba cha Habari na Kisha wakamgeuzia kibao Isango wakaondoka naye kwenda naye Kimya kimya Kituo cha Polisi Kati " Central" kwa mahojiano licha mwisho wa siku hawa kumshitaki.

Itakumbukwa Kuwa Septemba 14 Mwaka 2014 , Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrsia na Maendeleo ( CHADEMA) , Freeman Mbowe baada ya kushinda tena kwa Mara ya Tatu nafasi ya uenyekiti wa Taifa wa Chama hicho, Alitangaza maazimio Sita ya Mkutano Mkuu wa CHADEMA.

Moja ya azimio Hilo ambalo lilitangazwa na Mbowe ni ' Kwanza Chama kishirikishe umma kuaandaa migomo ya kila aina na maandamano isiyokuwa na kikomo ya nchi nzima na watu washirikishwe Katika zoezi hili ili kushinikiza Bunge Maalum la Katiba linaloendelea Dodoma lisitishwe'.

Baada ya Mbowe kutoa tamko Hilo Mimi binafsi nilitofautiana naye na niliandika makala iliyokuwa na kichwa cha Habari kisemacho : 'FREEMAN MBOWE , ' DOZEE DOZEEE'

Siku Chache baadaye Jeshi la Polisi lilimtaka Mbowe ajisalimishe Makao Mkuu ya Jeshi la Polisi kwaajili ya mahojiano Ambapo Mbowe Septemba 2014 alitii wito wa Jeshi la Polisi ambapo alifika makao Makuu ya Jeshi Hilo huku waandishi wa Habari na wafuasi wa Chadema wakiwa wamefurika wakitaka kuingia hadi ndani ya geti la Ofisi hiyo Hali iliyosababisha Polisi kuwazuia na Isango akajikuta akipigwa virungu na Polisi .

Siku hiyo alipopigwa virungu na Polisi Isango,nilimpigia simu na kumcheka na kumwambia simtaki tena mume gani anakubali kupigwa na anashindwa Kupambana ananitia aibu " Mkewe" Kwani Mimi "Mkewe " ni mtu wa mazoezi?

Isango alicheka sana ila akaniambia "mke wangu" sitarudi a tena kubishana na Polisi " Kwani amebaini Polisi wakiwa Kazini hawataki utani .

Mara Kadhaa Isango ambaye alikuwa aliongezeka uzito hivyo kufanya awe Mnene na kitambi kikubwa nilikuwa nikimshauri aanze kupunguza uzito kwa kufanya mazoezi Kwani amekuwa na uzito mkubwa ambao Una madhara makubwa katika afya yake na akakiri kabisa kuwa hata yeye uzito huo mkubwa umeanza kumsumbua na akakubaliana na ushauri wangu anakubaliana na ushauri wangu ila akasema Hilo la kufanya mazoezi limemshinda.

Isango nilikupenda sana rafiki ila Mungu amekupenda zaidi .Nitakosa mtu wa kupiga naye umbea wa "kisiasa'. Joseph Isango umeniliza.

Mungu aiweke roho yako Mahali panapo Stahili.

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
BLOGG: www.katabazihappy.blogspot.com
0716 774494
14/4/2017.










Sent from my iPad

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment