Thursday, 28 January 2016

Re: [wanabidii] Membe mwache Magufuli

Kubwa jinine alilolsema Membe ni kumtaka Rais ''awabembeleze'' wafanhya biasharia. nalo lijadiliwe. Tafsiri sahihi ya wafanya biashara ni wale ambao wanalipa kodi. Membe kutaka waliokwepa kodi wapewe miezi mitatu ni aina nyingine ya kutaka kuendeleza ufisadi. Membe alikusudia taifa liendeshweeje bila kodi? kama wafanyabiashara watabembelezwa KULIPA kodi na kwa hiyo siyo hiyari nchi iendelee kutegemea mama ntilie kulipa kodi kama miaka ya mateso ambayo watu wanatarajia mabadiliko? Maana yake Membe alipokuwa anagombea urais alikusudia kuendelea kuwabada wafaya biashara wadogo na kuwaachia uhuru wakibwa kuendelea kukwepa kodi?
N\ hilo linahitaji ahojiwe. Tuna tatizo la wsauliza maswali katika mijadala hii. nasema hivyo kama maswali yamnakuwa hayakupangwa na muulizwaji
--------------------------------------------
On Thu, 1/28/16, 'ananilea nkya' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] Membe mwache Magufuli
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Thursday, January 28, 2016, 1:35 PM


Fadhili,
Hii makala uliyoweka hapa nimeisoma. Ni nzuri. Ina ujumbe
mzuri kwa taifa. Nakubaliana na mwandishi Evarist Chachali
kwamba safari nyinyi za nje zilizofanywa na serikali
iliyopita, kwa kiwango kikubwa zilikuwa ni mkakati wa
kifisadi wa kunufaisha watawala wachache. Hivyo hatua ya
Rais Dr Magufuli ya kudhibiti ufisadi huo uliofanyika kwa
kisingizio cha ushirikiano wa kimataifa kukuza uchumi kumbe
ni biashara mahususi ya kuneemesha zaidi watawala wachache.
Namtia shime Rais Dr Magufuli asitetereke kwa hili la KUBANA
SAFARI UFISADI na wala asitiwe hofu na mwana CCM yoyote hai
au mfu maana umma mpana,uliofukarishwa ili hali watawala
wachache wakiwa matajiri kufuru kwa kunufaika kwa fedha na
rasilimali za nchi, uko nyuma yake. Mungu ibariki Tanzania

Ananilea Nkya
 E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com

--------------------------------------------
On Thu, 1/28/16, fadhil fadhil <fadhil.fadhil96@gmail.com>
wrote:

Subject: [wanabidii] Membe mwache Magufuli
To: "'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, January 28, 2016, 9:35 AM

Evarist Chachali



KATIKA tasnia ya ushushushu kuna kitu kinachoitwa Moscow
Rules (yaani
Kanuni za Moscow). Hizi ni kanuni za zama za Vita Baridi
ambazo majasusi
  waliopangiwa kazi nchini Urusi walipaswa
kuzizingatia, kwa
sababu nchi
hiyo ilikuwa nguli wa kukabiliana na majasusi. Moja ya
kanuni hizo
inasema; "Once is an accident. Twice is a coincidence.
Three times is an
  enemy action." Kwa tafsiri isiyo rasmi; kitu
kinachojiri
mara moja ni
ajali; kikijiri mara ya pili ulinganifu wa bahati mbaya,
sio
makusudi;
kikijiri mara ya tatu ni kitendo cha adui."



Nimeanza makala hii na angalizo hilo kwani ndio wazo
lililoniingia
kichwani mara baada ya kusoma kauli za aliyekuwa Waziri wa
Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa, katika Serikali ya Awamu ya
Nne, Bernard
Membe.



Wiki iliyopita, Membe alinukuliwa na vyombo vya habari
akimkosoa Rais
Dk. John Magufuli, angalau katika maeneo matatu. Kwanza,
Membe alidai
kuwa kiuhalisi, Dk. Magufuli hajapunguza idadi ya wizara
kama
alivyoahidi bali amepunguza idadi ya mifuko, na
kutanabaisha
kuwa Rais
hajabana matumizi yoyote kwa kupunguza ukubwa wa baraza la
mawaziri,
bali alichofanya ni kupunguza idadi ya mawaziri na sio
wizara.



"Alichofanya ni sawa na kuwa na mayai kumi halafu
ukaamua
kuyaweka
kwenye mifuko kumi, maana yake ni kwamba utakuwa na mifuko
kumi yenye
mayai," alisema waziri huyo wa zamani ambaye pia alikuwa
miongoni mwa
makada wa CCM waliowania kuteuliwa kugombea urais kwa
tiketi
ya chama
hicho tawala.



"Lakini unaweza kuwa na idadi hiyo hiyo ya mayai na
ukaamua kuyagawanya;
  mayai matatu unayaweka kwenye mfuko mmoja, mawili
kwenye
mfuko mwingine
  na yaliyobaki kwenye mfuko mmoja. Maana yake ni
kwamba
utaendelea kuwa
na mayai kumi lakini idadi ya mifuko imepungua. Hapa sasa
utakuwa
hujapunguza gharama za kuyatunza hayo mayai,"aliongeza
Membe.



Membe alidai kwamba Magufuli ameendeleza wizara zile zile
lakini kaamua
kuzikusanya pamoja, na kuona kuwa mfumo huo mpya wa wizara
unaweza
kuathiri uwasilishaji wa bajeti bungeni kwa vile mawaziri
sasa
watahitaji muda mwingi zaidi kuliko ilivyokuwa awali.



Hilo tutaliona kwenye Bajeti ya Serikali ya mwaka huu.
Tuone
kama bajeti
  itaongezeka au itapungua? Kwa sababu kama wizara
zimepungua
kama
tunavyoamini, lazima bajeti ipungue, sasa bajeti
ikiongezeka
au ikibaki
vile vile maana yake hakuna
kilichofanyika,"alitahadharisha.



Eneo la pili ambalo Membe alimkosoa Magufuli ni udhibiti
wa
safari za
nje, akidai kuwa Tanzania si kisiwa. Membe, aliyekuwa
mtetezi mkuu wa
safari mfululizo za Rais (mstaafu) Jakaya Kikwete nje ya
nchi, alisema
kuwa safari za nje zina manufaa kwa taifa, na kusisitiza
kuwa lazima
Rais Magufuli asafiri kwenda nje ya nchi.



"Tanzania si kisiwa, hata ukiwa tajiri namna gani lazima
utoke nje ya
nchi yako," alisema Membe, na kutahadharisha kuwa nchi
yetu inaweza kuwa
  kama Zimbabwe kwani ukijitenga, utatengwa.

Alisema nchi ina mabalozi 36 tu duniani kote kati ya nchi
194
zinazohitaji uwakilishi huo na kibaya zaidi, mabalozi
hawaruhusiwi
kuingia kwenye baadhi ya vikao, na hata wakiingia wakifika
kwenye hatua
ya uamuzi watazuiwa kushiriki.



Eneo la tatu ambalo japo hakumtaja Magufuli wala kukosoa
moja kwa moja
lakini linaloweza kutafsiriwa kama kuikosoa serikali kuhusu

wafanyabiashara, ambapo alitahadharisha serikali
kutowachezea.



Waziri huyo ambaye pia ni mbunge wa zamani wa Mtama (CCM)
alipongeza
kasi ya Magufuli katika vita dhidi ya ufisadi na kudhibiti
mianya ya
kukwepa kodi lakini akatahadharisha kuhusu haja ya kuwa
mwangalifu
katika kuwashughulikia wafanyabiashara. Alidai kuwa
wafanyabiashara wana
  masikitiko makubwa dhidi ya serikali, na anaona suala
hilo
litaibuka
kwa kishindo bungeni.



Licha ya maeneo hayo matatu, Membe alizungumzia kauli ya
aliyekuwa
mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa,
aliyedai
wafanyabiashara waliomuunga mkono wananyanyaswa. Alieleza
kuwa si dhambi
  kwa wafanyabiashara kufadhili vyama vya siasa wakati
wa
uchaguzi, na
kwamba serikali ya chama kilichoshinda uchaguzi inapaswa
kuwakusanya
wafanyabiashara wote na kufanya nao kazi na sio
kuwaburuza.



Kadhalika, mwanasiasa huyo alizungumzia kuhusu "timua
timua" ya watumishi wa umma wanaohusishwa na tuhuma za
ufisadi.



"Ni rahisi kumshughulikia mtu usiyemfahamu lakini siyo
rahisi
kumshughulikia mtu unayemfahamu," alidai Membe, na
kuongeza kuwa
haitokuwa shida kwa Magufuli kuwashughulikia watendaji
aliowakuta
serikalini ambao kimsingi hakuwateua, na hawafahamu.
Alihoji
iwapo Rais
ataweza kuwatimua aliowateua mwenyewe.



Kauli hizo za Membe zimezua mjadala mkubwa, hususan kwenye
mitandao ya
kijamii. Japo kabla yake, aliyekuwa Naibu wa Kazi, Ajira
na
Maendeleo ya
  Vijana, Makongoro Mahanga, alimkosoa Magufuli kuhusu
ukubwa
wa kabineti
  yake, ukweli kwamba Membe bado ni kiongozi wa juu wa
CCM
ilhali Mahanga
  alihamia upinzani, unaashiria mengi.



Lakini binafsi sikushangazwa na kauli hizo za Membe, hasa
kwa vile
awali, katika kitabu nilichokichapisha hivi karibuni
kuhusu
safari ya
urais wa Magufuli, mafanikio na changamoto katika urais
wake,
nilibainisha kuwa moja ya changamoto zinazoweza kumkabili
Rais huyo wa
Awamu ya Tano ni maadui wa ndani ya chama chake.

Kimsingi, hoja zote za Membe hazina mashiko. Kuhusu
anachoita ukubwa wa
baraza la mawaziri, la muhimu kwa Watanzania si ukubwa au
udogo bali
uchapakazi. Ni bora kuwa na mawaziri, manaibu na makatibu
wakuu hata
1,000 wachapakazi, kuliko kuwa na serikali ndogo
inayokumbatia mafisadi.



Pia Membe alipaswa kufahamu kuwa utendaji kazi wa viongozi
wa serikali
unategemea sana utendaji kazi na msimamo wa bosi wao,
yaani
Rais
aliyewateua. Ni dhahiri kuwa Membe anatambua kuwa Magufuli
si mtu wa
porojo, mtoa ahadi anazoshindwa kuzitekeleza mwenyewe
(rejea
kauli ya
"ninawajua wala rushwa kwa majina" ya Kikwete), na
kimsingi Watanzania
na dunia nzima wanafahamu kuwa kaulimbiu ya Hapa Kazi Tu
ya
Magufuli ni
tofauti na zama za nchi kujiendesha yenyewe (on
autopilot).



Kuhusu safari za nje, Membe amepotoka mno, pengine kwa
sababu kwa
wadhifa wake wakati huo, alikuwa mmoja wa wasafiri nje ya
nchi mara kwa
mara. Kwanza, Rais Magufuli hajawahi kutamka kuwa
hatosafiri. Kwa hiyo,
kauli ya Membe kuwa lazima atasafiri ni fyongo.



Pili, zuio la safari za nje sio 'blanket ban' bali ni
kwa safari zisizo
na tija. Lakini kwa nini tushangazwe na kauli hiyo ya
Membe
ilhali
tunafahamu misafara ya serikali iliyopita ilivyosheheni
wajumbe kwa
kutumia fedha za umma? Ni mtu mwenye matatizo tu anayeweza
kutetea
safari zenye manufaa zinazoligharimu taifa matrilioni ya
shilingi huku
faida tarajiwa zikiwa pungufu ya gharama husika.



Mwanadiplomasia msomi kama Membe alipaswa kuangalia hapo
jirani tu kwa
Rais Paul Kagame, kulinganisha idadi ya safari zake nje na
zile za
Kikwete kisha kuangalia hali ya uchumi kati ya nchi hizo
mbili.



Vilevile ni rahisi kwa Membe kuzungumzia mafanikio ya
safari
hizo kwa
vile ni Watanzania wachache wanaofahamu vituko
vilivyoambatana na safari
  hizo. Ni mara ngapi safari hizo za 'manufaa'
zilijumuisha shopping,
kuhudhuria birthday parties, na matukio mengine yasiyo na
tija kwa
serikali?



Kuhusu wafanyabiashara, ni upuuzi wa hali ya juu kuhisi tu
kuwa kuna
uonevu dhidi ya mfanyabiashara yeyote. Kama kuwabana
wafanyabiashara
wakwepa kodi ni uonevu basi Magufuli aongeze dozi, maana
hizi sio zama
za Tanzania kuwa shamba la bibi.



Membe anadai wafanyabiashara wana masikitiko na suala hilo
linaweza
kuibuka bungeni. Anamaanisha Bunge limejaa wafanyabiashara
au? Na kama
masikitiko yao ni kutokana na Serikali ya Awamu ya Tano
kuwabana ili
wasikwepe kodi na kwamba masikitiko hayo yanaweza
kusababisha kupoteza
wawekezaji, basi na waondoke hata kesho. Hatuhitaji
wakwepa
kodi nchini.
  Kimsingi, wanaolalamika wala hawastahili kuitwa
wafanyabiashara bali
wahujumu wa uchumi wetu.



Na hoja yake kuhusu 'timua timua' haishangazi kwani
moja
ya udhaifu wa
serikali ambayo Membe alikuwa waziri ilikuwa ni kuwaonea
aibu
wanaoboronga, na matokeo yake hali hiyo ilivutia
waborongaji
wapya kwani
  walishabaini kuwa hakuna wa kuwachukulia hatua. Hivi
Membe
anaweza
kutuambia lolote kuhusu ahadi ya Riais Kikwete aliyoitoa
Februari 2006
kwamba anawafahamu wala rushwa kwa majina na anawapa muda
wajirekebishe?
  Sawa,



Magufuli alipoingia Ikulu alikuta orodha hiyo ya wala
rushwa
aliowajua Kikwete na kuamua kuifanyia kazi?

Nimeeleza awali kuwa nimelizungumzia suala hilo kwa kirefu
kitabuni.
Sitaki kabisa kuamini kuwa kauli za Membe ni zake peke
yake.
Hisia
zinanituma kuamini kuwa huu ni moshi tu unaoashiria moto
unaowaka ndani
kwa ndani ya CCM kati ya makundi makuu mawili: la Hapa
Kazi
Tu la
Magufuli linalotaka kuiondoa Tanzania katika lindi la
ufisadi unaoifanya
  nchi yetu kuzidi kuwa masikini, na kundi la wanufaika
wa
ufisadi
linalomwona Magufuli kama mtu anayewaziba pumzi. Naam,
ufisadi ni
'lifeline' ya watu walioigeuza nchi yetu Shamba la
Bibi,
wakivuna
wasichopanda.



Nimalizie makala hii kwa kutoa wito kwa makada wa CCM,
ambao
wengi wao
wanaimba Hapa Kazi Tu, lakini wakisikia madhambi
yaliyofanywa na
mwana-CCM fulani wanakimbilia kuwanyooshea vidole
wapinzani.
Wapinzani
wakuu wa Magufuli hawapo Chadema au nje ya nchi bali wapo
ndani ya chama
  hicho tawala. Na njia pekee ya kupambana nao ni
kuweka
mbele maslahi ya
  taifa badala ya kutanguliza umoja na mshikamano wa
chama.
Kuna usemi
mchawi akimaliza kuroga mtaa hugeukia familia yake. Majipu
yaliyomo
ndani ya CCM yasipotumbuliwa mapema yatamkwaza Magufuli na
nchi yetu kwa
  ujumla.



Raia Mwema




--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and
hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to
the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment