Kwanini wabunge hawapendi kuonekana live majimboni badala yake wanapenda kuonekana live luningani?
Tangu jana kumekuwa na mjadala katika mitandao ya kijamii na juu ya wabunge wetu kupingana na serikali juu ya usitishaji wa kurusha bunge live na badala yake bunge kuwa recorded kwa lengo la kubana matumizi kama ilivyotangzwa jana bungeni na waziri wa habari Nape Nauye.
Swali langu la msingi ikiwa tulishangilia Rais Magufuli Kufuta shererhe za uhuru kwa ajili ya kubana matumizi ambazo zingegharimu takribani bilioni nne na pesa hizo zikatumiwa katika ujenzi wa barabara sasa kuna tabu gani ikiwa pesa za kurusha bunge live ambazo nazo ni bilioni 4 ikiwa nazo zitatumika katika shughuli za maendeleo haswa tukaletewa vijijini ambapo wananchi hawana maji, umeme na huduma duni za afya?
Swali langu la lingine kwa muda mrefu wabunge wetu wa vyama vyote wamekuwa na desturi ya kutoonekana majimboni hadi kipindi cha uchaguzi au ziara ya waziri mkuu, makamu wa rais na rais, sasa inakuwaje leo wanapenda kuoinekana live bungeni wakati hatuwaoni live majimboni?
Wadau naomba nieleweke vyema sipingi bunge kutoonyeshwa lakini ikiwa wahandisahi wa habari wanaendelea kuwepo na bunge kurekodiwa na kuonyeshwa baadaye sidhani kama ni tatizo ikiwa tutaokoa hizo bilioni nne na kuzipeleka katika umeme kuliko kuonyesha live wakati mwananchi mwenyewe unayetaka akuone hana umeme
0 comments:
Post a Comment