Thursday, 28 January 2016

Re: [wanabidii] Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete akabidhi ripoti ya jopo lake kwa Ban Ki Moon

Ukiangalia wa uangalifu unaweza kuona jinsi UN inavyojitahidi kuDistabilize taifa letu. Kazi hiyo JK alipewa na wastaafu wangapi? mara zote kazi hizi hufanywa na viongozi wastaafu. mtafute Tonny Brsire. Joachim Chisano etc lakini nakumbuka kumbambikiza Mkapa kazi hizi ambazo walimbambikiza JK. Tusipokuwa waangalifu hatutaona ninachokisema.
--------------------------------------------
On Tue, 1/26/16, 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete akabidhi ripoti ya jopo lake kwa Ban Ki Moon
To: "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Tuesday, January 26, 2016, 2:23 PM


Mwenyekiti
wa Jopo la Ngazi ya Juu kuhusu Mwitikio wa Kimataifa wa
Majanga ya
Kiafya, Rais Mstaafu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi
Katibu Mkuu
wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon Ripoti ya Jopo lake katika
hafla fupi
iliyofanyika Jumatatu Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Kushoto ni Bw.
Rajav Shah (USA) na Bw. Marty Natalegawa ( Indonesia) ambao
ni sehemu ya
wajumbe wa Jopo hilo.

Na
Mwandishi Maalum, New York

Mwenyekiti
wa Jopo la Ngazi ya juu kuhusu Mwitikio wa Kimataifa wa
Majanga ya Kiafya, Rais Mstaafu, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete,
jana
Jumatatu, amemkabidhi Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki
Moon,
Ripoti ya Jopo lake.

Mhe.
Jakaya Kikwete aliteuliwa na Ban Ki Moon, kuongoza Jopo
lililokuwa na wajumbe watano mwezi Aprili 2015. kwa mujibu
wa hadidu za
rejea Jopo hili lilitakiwa kutekeleza majukumu yake kuanzia
mwezi Mei
hadi Desemba 2015.

Akipokea
ripoti hiyo, katika hafla fupi iliyofanyika Ofisini kwa
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa . Ban Ki Moon, pamoja na
kumshukuru
Mwenyekiti wa Jopo Mhe. Jakaya Kikwete pamoja na timu yake,
amesisitiza
kwamba, mapendezo yaliyotolewa na Jopo hilo yatazingatiwa na
kufanyiwa
kazi.

"
Ninatoa shukrani zangu za pekee na za dhati kwako wewe kama
Mwenyekiti kwa uongozi wako , na pia kuwashukuru wajumbe
uliofanya nao
kazi. Ripoti hii ambayo imesheheni mapendekezo na ushauri
itazingatiwa
na kufanyiwa kazi". Amesema Ban Ki Moon.

Akabanisha
kwamba, mapendekeo na ushauri uliomo ndani ya Ripoti ya Jopo
atauwasilisha pia kwa Shirika la Afya Duniani ( WHO).

Katibu
Mkuu pia amesema Ripoti hiyo itasaidia sana katika kutoa
mwongozo kwa Jumuiya ya Kimataifa juu ya namna ya kuimarisha
na
kuboresha miundombinu ya afya ili iweze kukabiliana na
magonjwa ya
milipuko.

Vile vile
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amemhakikishia Mwenyekiti
wa Jopo Mhe. Jakaya Kikwete na wajumbe wake kwamba, Ripoti
hiyo itawekwa
hadharani mapema iwezekanavyo ili Nchi wanachama wa Umoja
wa Mataifa na
makundi mbalimbali ya jamii waweze kuisoma.

Kwa upande
wake, Mwenyekiti wa Jopo, Rais Mstaafu Mhe. Jakaya Mrisho
Kikwete, amemshukuru Katibu Mkuu Ban Ki Moon, kwa kumpatia
heshima ya
kuongoza Jopo hilo, jopo ambalo amesema walifanya kazi kwa
ushirikiano
wa hali ya juu.

Wajumbe
wengine wa Jopo hilo walikuwa ni Bw. Celso Amorim ( Brazil),
Micheline Calmy ( Switzerland), Marty Natalegawa (
Indonesia) Joy
Phumapi ( Botswana) na Rajav Shah ( USA).

Jukumu
kubwa ya jopo hilo kwa mujibu wa hadidu za rejea, pamoja na
mambo mengine, lilikuwa ni kutoa mapendekezo ya namna ya
kuimarisha
mifumo ya kitaifa na kimataifa katika kuzuia na kukabiliana
na majanga
ya kiafya yakiwamo magonjwa ya mlipuko, ikiwa ni pamoja na
kujifunza
kuhusu mwitikio wa Jumuiya ya Kimataifa kufuatia kuibuka kwa
janga la
ugonjwa wa Ebola.

Katika
utekelezaji wa majukumu yake Jopo lilikutana na kufanya
majadiliano ya kina na makundi mbalimbali yakiwamo ya
wataalamu,
wawakilishi wa nchi tatu ambazo ziliathirika sana na ugonjwa
wa Ebola (
Liberia, Siera Leone na Guinea),Mashirika ya Kimataifa na
Kikanda ,
Taasisi za Fedha za kimataifa, wahudumu wa Afya, Wasomi ,
Watafiti,
Sekta Binafsi na wataalam wa fani na kada
mbalimbali.​
 








--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment