Tuesday, 24 February 2015

[wanabidii] EDWARD LOWASSA MCHAPAKAZI, MWANASIASA, MFANYABIASHARA NA MUUAJI ANAYETABASAMU

EDWARD LOWASSA MCHAPAKAZI, MWANASIASA, MFANYABIASHARA NA MUUAJI WA ANAYETABASAMU.

Edward Ngoyayi Lowassa ni mwanasiasa na mjasiliasiasa nchini Tanzania, mfanyabiashara wa anga za ukanda huu wa kusini mwa Jangwa la Sahara, Mume wa Bibi Regina na Baba wa Familia huru. Safari ya maisha ya Lowassa ni safari ndefu yenye milima na vilima vingi vyenye kusukuma hadi utosi wa unywele zake mweupe. Maisha ya Edward Lowassa yanaanzia katika vilindi vya upwa wa Monduli kunako Mkoa wa Arusha chini ya vipaji na mapaji ya Mzee Ngoyayi siku ya Alhamisi ya saa nne za asubuhi kwa majira Afrika Mashariki katika Boma la mzee Ngoyayi katika tarehe 26 ya mwezi 8, mwaka 1953

Edward Ngoyayi Lowassa alianza masomo ya shule ya msingi katika vilima na vilindi vya upwa wa Monduli tarehe sita ya mwezi kwanza kwa mwaka 1961 na kuhitimu masomo hayo ya msingi mwaka 1967. Tarifa za maendeleo yake shuleni zinamuweka kwenye sehemu ya wanafunzi waliotoka kundi la wafugaji wenye uwezo mzuri darasani hali iliyomfanya afaulu kujiunga na Shule ya sekondari ya Arusha mwaka 1968, Bado Lowassa aliendele kudhihirisha uwezo wake darasani ambapo mwaka 1971 alihitimu vizuri na kufanikiwa kujiunga na masomo ya kidato cha sita mwaka 1972 katika shule ya vipaji maalumu ya Tabora na kuhitimu mwaka 1973.

Uwezo wa Edward Lowassa ulikuwa mzuri zaidi darasani ambapo mwaka 1974 alijiunga na Chuo kikuu Dar es Salaam akichukua shahada ya kwanza katika taaluma ya MAZINGAOMBWE, ambapo mwaka 1977 alihitimu akiwa ni muigizaji mzuri wa mazingaombwe na tamthiria aliyepikwa kitaalamu kabisa, Edward Lowassa alijaribu kwa miaka sita akisota kusaka ajira ama kujiajiri kupitia taaluma yake lakini kwa bahati mbaya soko la filamu na mazingaombwe lilikuwa duni nchini, hivyo mwaka 1983 aliamua kurudi masomoni kusaka fani nyingine ambapo mwaka 1984 alipata shahada ya pili katika sayansi ya maendeleo ya jamii kwenye Chuo Kikuu cha Hull nchini Uingereza.

Baada ya kuhitimu shahada ya pili, Lowassa alifanikiwa kupata kazi serikali akihudumu nafasi ya Waziri mdogo wa haki na mambo ya bunge katika ofisi ya Makamu wa Rais (1990-1993) na
Mkurugenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (1989 - 1990) na mwisho akahudumu
Waziri mdogo wa mazingira na mapambano dhidi ya umasini katika ofisi ya Makamu wa Rais (1988-2000)
Mwaka 1990 uchaguzi wa mwisho wa chama kimoja Lowasa alichaguliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano akichukua nafasi ya Luteni Lepilal Ole Molomeit Baada Ya Jimbo La Uchaguzi La Longido Kuanzishwa Na kumshinda Dr Toure Katika Kinyanyang'anyiro Cha Ubunge

KISIASA.

Siasa za Lowassa ni siasa za mrengo wa kulia zinazoishi na kuamini katika uwezo wa fedha na shibe, Lowassa ni muumini mzuri wa Ubepari ijapokuwa anahudumu katika chama kinachojinasibisha katika mrengo wa kushoto. Ndani ya CCM Lowasa anasifika kwakuwa mwanamitanda (makundi) na hili ameliishi tangu alipoingia kwenye siasa rasmi mwaka 1990. Kisiasa Lowasa anakabiliwa na tatizo la kubuni, kuibua, kujenga hoja na kuisimami hiyo mpaka mwisho. Kwamjibu kwa kumbukumbu za Bunge hakuna mahali panapoonyesha Lowasa aliwahi kupeleka hoja Bungeni na kuisimamia tangu alipoingia Bungeni 1990. Lowasa anakabiliwa na tatizo lingine la uwezo wake mdogo/kutojua kabisa kutoa hotuba thabiti za kisiasa ama za kijamini. Kwaujumla Lowassa sio mwanasiasa bali ni mjasiliasiasa mahiri nchini kwakuwa ameitumia vema siasa na fursa zake na kuwa mkwasi mkubwa katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

UADILIFU WA LOWASSA.

Katika nyanja hizi tunamuona katika sura mbili, kwenye masuala yake ya ndani Lowassa ni Baba wa familia mwaminifu kwa mkewe kipenzi Regina, Lakini sura nyingi ni mbaya kwake na inamuondolea sifa za kiongozi bora kwasababu ya mapito na makandokando yake, 
Kashifa ya kwanza ambayo haijawahi kukanushwa na Lowasa mwenyewe ama yeyote yule sababu iliyoitwa na inayoaminika mpaka sasa kuwa "Lowassa ana utajiri mkubwa usio na ufafanuzi alikoupata kwa mda mfupi tu na ulianza alipokuwa yu mkurugenzi wa AICC"

Ikumbukwe mwaka 1995 ikiwa ni miaka mitano tu tangu aingie katika siasa na kuwa Mbunge alichukua fomu ya kuwania Urais sambamba na rafiki yake wa karibu Jakaya Kikwete, huu ulikuwa uamuzi mkubwa na uliolazimu idara kumchunguza japo tayari walikuwa na taarifa zake, hoja hii ilisimamiwa Mwalimu Nyerere na ilikuja baada ya Lowassa na wapambe wake kukodi ndege binafsi kutoka Arusha kwenda Dodoma kuhudhuria vikao vya uteuzi wa urais mwaka 1995, kitendo hiki kilimfedhehesha sana Mwalimu na wazalendo wengine na hata kufikia kushinikiza kuliondoa jina la mwanasiasa huyu nguli wa Tanzania,
Uadilifu wa Lowassa unatiliwa shaka kwakuwa mpaka leo Mamlaka ya mapato Tanzania haijaweza kututhibitishia uhalali wa utajiri aliona Edward Lowassa kupiti kodi anayotakiwa kulipa mtu huyu. Tangu astaafu kama wafuasi wake wanavyopenda kusikia na kuona ama afukuzwe uwaziri mkuu mwaka 2007 taarifa za kuaminika kutoka vyanzo muhimu ndani ya ofisi zake za Political Entrepreneurshipp iliyopo Msasani mkabala na Ubalozi wa USA, Team Lowasa iliyopo Upanga na Umoja wa Wabunge wa CCM iliyopo Dodoma nikuwa Lowassa alitenga Tsh 35 bilioni kwa ajili ya kujitakasa, ambapo mpaka leo hii ameshatumia Tsh18 bilioni,
Kuna maswali mengi sana yanazaliwa kutokana na mwenendo wake kisiasa, Je pesa hii ameipata wapi? Imelipiwa kodi kiasi gani? Atairudishaje?
Labda niwaelekeze watafiti na wadadisi wenzangu wa siasa hebu watafute jalada la Edward Lowassa la enzi za TANU pale Lumumba. Mzee Paul Sozigwa suala hili analifahamu fika.

Ndiyo, Mwl. Nyerere alichukizwa na tabia ya Lowasa ya kujitajirisha kwa kuiba mali ya umma. Lowasa, licha ya tuhuma za wizi enzi akiwa AICC, kujimilikiaha majumba ya Masajili wa Majumba wakati akiwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mijini, Mwl. Nyerere alikuwa akifahamu wizi wa Lowasa tangu enzi za TANU. Kati ya mwaka 1974 na 1977 Lowasa aliiba pesa za TANU alizopewa kusimamia ujenzi wa ofisi ya TANU vijana Arusha akiwa Katibu na msomi toka UDSM

Badala ya kujenga ofisi ya TANU Lowasa alinunua kiwanja na kujenga nyumba yake binafsi. Jambo hilo lilipogundulika mwaka 1982, lilimkasirisha sana Mwl hivyo kuamuru afukuzwe kwenye chama. Wazee walipiga magoti kumuombea msamaha kuwa kijana atajirekebisha, Ni marehemu Edward Moringe Sokoine ndiye alimwombea msamaha zaidi kwa Mwl. mpaka abadilishiwa adhabu. 
Edward Lowasa alipewa adhabu mbadala; kuhudhuria Ofisi Ndogo ya Chama Mtaa wa Lumumba Dar es Salaam kila siku bila kukosa, kuwa kazini masaa 8 bila kutoka lakini bila kupangiwa kazi yoyote hadi Chama kingeona ametubu na kujutia na hatimaye apangiwe kazi nuingine. Lowasa alitumikia adhabu yake hadi Sokoine alipofariki.

Hiyo ndio sababu kuu ya Mwl. Nyerere kumkatalia Lowasa kugombea urais. Kikwete, Mkuchika, Twaha Khalifan, Kinana, Bagenda na Msekwa wanajua ukweli wote kuhusiana na jambo hili. Ila maadamu kwa sasa hakuna tena maadili ya uongozi wa kisiasa nchini Tanzania, Lowassa anaweza kuachiwa awatawale wezi, wala rushwa na mediocre wa nchi hii.

Jambo kubwa zaidi kwa Lowassa na ambalo litamtesa zaidi ni tuhuma hizihttps://wikileaks01.wordpress.com/2011/10/ zinazosema kuwa alihusika katika mauaji ya Mwalimu Julius Kamparage Nyerere, taarifa hizo ziliibuliwa na mtandao wa Wikileaks 2011 na mpaka leo Lowassa hajakanusha.

UTENDAJI WA LOWASSA.

Lowa ni mchapakazi mzuri anayefanya kazi kwakutarajia makofi ya shukrani, katika eneo hili Lowasa ni mmoja ya Watanzania wengi wachapakazi vizuri hii ni kwakuangalia matokeo ya utumishi wake huko nyuma hasa kisiasa zaidi. Tatizo kuu la Lowasa nikuwa hana fikra mpya ama wazo jipya katika utendaji, huamini uasili wa jambo/kitu bila kubuni na kukipa sura mpya kizae matoke chanya, hilo ni tatizo kuu na la hatari kwa nchi yenye ndoto za kusonga mbele. Pia hathamini utalamu ama taaluma bali huamini pesa inaweza yote.
Lowassa amehudumu katika serika na chama kwenye nafasi za Waziri wa ardhi na makazi mwaka 1993 - 1995, Waziri wa Maji na Mifugo mwaka 2000 - 2005 na Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2005 - 2008.
Sehemu amehudumu kwa ufanisi japo kumbukumbu zinazoonyesha kuwa aliwahi kukuibua hoja iwe binafsi au ya kiwizara na ikazaa matunda, kuna hoja inayoimbwa mitaani kuwa Lowasa ndie aliyebuni na kuanzisha ujenzi huo, lakuni ukweli suala hili ni zao la aliyewahi kuwa waziri mwandamizi Makweta, yeye ndie alilibuni na kulifikisha serikalini na Lowasa alipoingia akiwa Waziri Mkuu ilikuwa ni Utekelezaji tu.

Mtazamo wangu kwa aina ya mwanasiasa kama huyu hata vizazi vyetu vitakuja kuyatandika mboko makaburi yetu ikiwa tutahongwa hela Watanzania wote nakisha tukampeleka Ikulu. Kazi yake ya kwanza itakuwa ni kurudisha pesa yake.

Ikulu sio pango la WALANGUZI


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment