Tuesday, 24 February 2015

Re: [wanabidii] WOSIA WA BABA WA TAIFA KUHUSU URAIS - Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya Mei 1, 1995

Urais haununuliwi bana kwan watanzania ni wehu hivo jamani wanaopiga kura si watanzania watampa mtu wanedhani atawaokoa na janga hili la ukosefu wa tumaini na ufukara uliokithiri....atakaeleta tumaini jipya



From: 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Saturday, February 21, 2015 10:12 AM
Subject: Re: [wanabidii] WOSIA WA BABA WA TAIFA KUHUSU URAIS - Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya Mei 1, 1995

Mawazo haypo yalizikwa eh?
Kwa hiyo sasa ni halali kununua urais? kitugani katika hayo hakifai?
--------------------------------------------
On Sat, 2/21/15, 'Fred Hans Kipamila' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] WOSIA WA BABA WA TAIFA KUHUSU URAIS - Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya Mei 1, 1995
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Saturday, February 21, 2015, 4:32 PM

Fakhi mawazo
hayo yalizikwa na Mwalimu October 1999 ni kama mavi ya
kale.
  
    From: Fakhi Karume
<fkarume@gmail.com>
  To:
wanabidii@googlegroups.com
  Sent: Saturday,
February 21, 2015 11:42 AM
  Subject: [wanabidii]
WOSIA WA BABA WA TAIFA KUHUSU URAIS - Uwanja wa Sokoine
mjini Mbeya Mei 1, 1995
   
Baba wa
Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alialikwa kuwa Mgeni Rasmi
kwenye kilele cha Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani
iliyofanyika kitaifa Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya Mei 1,
1995. Katika hotuba yake alieleza mengi, leo tunachukua
kipengele cha urais, alikuwa na haya ya
kusema:
"Naeleza
baadhi ya matatizo ambayo viongozi tutakaowachagua tuwe na
hakika iwapo wanayaona hivi kama sisi tunavyoyaona.
Yanawauma kama sisi yanavyotuuma na kwamba, watakapofika
hapo wanapopataka watusaidie kuyatatua.
"Wanayaona,
yanawakera na hata watakapofika hapo, hicho ndicho
kitakachowasukuma kutaka kuwa marais wetu na wabunge wetu.
"Marekani walikuwa na rais wao kijana mmoja mdogo anaitwa
John Kennedy. Walimpiga risasi. Marekani nao ni watu wa
ajabu sana! Vijana walilaani tukio hilo kwa kuwa walikuwa
wanadhani wamemchagua rais wa umri wa kama miaka arobaini na
mitatu au minne hivi.
"Sasa
huyo ni kijana, hata kwa hapa Tanzania leo ni kijana.
Alipochaguliwa na Marekani akawa rais wao. Katika hotuba
yake ya kwanza kabisa aliwambia wananchi wenzake, hasa
vijana "Usiulize Marekani itakufanyia nini, jiulize wewe
utaifanyia nini Marekani?"."Kila
anayetaka kuwa mgombea wa urais/ubunge ajiulize ataifanyia
nini nchi yake"Tunataka mtu anayetaka kuwa rais
wetu ajiulize anataka kuifanyia nini nchi yetu na sio nchi
yetu itamfanyia nini.
"Na
tunataka swali hilo ajiulize kila mtu anayetaka kuwa mgombea
wa chama cho chote kuwa mbunge/rais: "Kwa nini, kwa dhati
kabisa, anaumwa na umasikini wetu na umasikini huo ndiyo
unaomsukuma ashughulike na mambo haya ya siasa katika ngazi
hiyo ama ya ubunge ama ya urais". Kama sivyo,
hatufai!"Mtu hapakimbilii Ikulu: Hakuna
Biashara Ikulu. Mtu anayetaka kwenda ikulu kutaka faida yo
yote ikulu pale, hatufai hata kidogo. Wananchi, mimi nimekaa
pale Ikulu kwa muda mrefu zaidi kuliko mwingine ye yote,
wala sidhani kuna mtu mwingine anaweza kuzidi muda
huo.
"Tayari hapa
tumeweka sheria. Kwa mujibu wa sheria, mtu hawezi tena kukaa
Ikulu zaidi ya miaka kumi, kipindi ambacho hata hakijafikia
nusu ya kipindi nilichokaa. Mimi nimekaa miaka ishirini na
tatu!"Najua, kwa mtu halisi kabisa, Ikulu ni
mzigo! Hupakimbilii! Si mahali pa kupakimbilia hata kidogo;
huwezi kupakimbilia Ikulu. Unapakimbilia kwenda kutafuta
nini?"Ni mgogoro; ni mzigo mkubwa kabisa!
Ukipita barabarani, unakuta watu wana njaa, unaona ni mzigo
wako huo. Pazito pale! Huwezi kupakimbilia na watu safi
hawapakimbilii.
"Ukiona mtu anapakimbilia, na hasa
anapotumia tumia vipesa kwenda Ikulu, huyo ni mtu wa kuogopa
kama ukoma!"Mtu ye yote anayeonekana anapenda
sana kwenda Ikulu na hata yupo tayari kununua kura ili
kumwezesha kufika Ikulu ni wa kumkwepa kama ukoma. Kwanza,
hizo fedha kapata wapi.
"Mtanzania wa leo hawezi kununua
watu bila kwanza yeye kununuliwa.Na kama
kanunuliwa, atataka kuzilipaje? Kazipata wapi? Watanzania
wote ni masikini tu. Mtanzania anaomba urais wetu kwa hela!
Amezipata wapi? "Pili, kama hajanunuliwa, kazipata wapi?
Kama kakopa, atarudishaje? Ikulu pana biashara gani mtu
akope mamilioni halafu aende ayalipe kwa biashara ya Ikulu?
Ikulu mimi nimekaa kwa muda wa miaka ishrini na
mitatu.
"Ikulu ni
mahali pazito. Kuna biashara gani Ikulu?"Rushwa
na matumizi ya fedha bila utaratiba wakati wa chaguzi: Sisi
Waafrika ni watu wa ajabu sana. Unajua ni wadogo, lakini
nasema, ni udogo wa mawazo. Umaskini wa mawazo ni umasikini
mbaya kupita wote.
"Unaweza ukawa na almasi mfukoni,
akaja tapeli na kijiwe kimetengenezwa kama almasi akakuambia
"hebu tuone almasi yako. 
Bwana aa! Hii ya kwako sio almasi ni
chupa tu, almasi ni hii. Kwanza nipe bwana."
Mkabadilishana. Yeye akachukua almasi yako na akakuachia
kichupa na ukatoka hapo unashangilia kama
zuzu!"Sisi hapa Tanzania tulikuwa tumeanza
utaratibu ambao ukitumia fedha nje ya fedha za chama na
serikali na ukatumia fedha zako mwenywe katika uchaguzi,
tunakutoa. Hufai! Huo ndio ulikuwa utaratibu wetu. Tulikuwa
tunakuuliza: "hii nchi ya maskini, wewe mwenzetu una mali
umeipata wapi?""Mali, kwa wakati huo, kwetu
sisi ilikuwa ni sifa ya kukunyang'anya uwezo wa kugombea
uongozi Tanzania. Tulijua kwamba, kama una mali, utaficha.
Leo watu wanasema waziwazi: "Mwalimu uchaguzi wa mwaka huu
utapitishwaje?"
"Marekani wanatumia fedha nyingi
sana katika uchaguzi. Nyingi sana! Kama Marekani sasa hivi
wanazungumza watunge sheria inayofanana na ile mliyoitupa
ninyi mnadhani kwa sababu ni mawazo ya masikini, haina
maana. "Wakubwa wanayafikiria mawazo hayo sasa hivi.
Marekani wanafikiria uwezekano sasa wa kutunga sheria
itakayoweka utaratibu wa fedha za ugombeaji kutokana na
mfuko mmoja baada ya kugundua kwamba inapokuwa holela na
kila mtu akiachiwa lwake, inavuruga.
"Inaleta rushwa kubwa kabisa.
Unanunuliwa urais na unaweza kununuliwa na fedha za wauza
bangi na wauza baa. Wauza bangi wanaiona hatari hiyo, ninyi
haa!"Hapa tulikuwa na utaratibu mzuri kabisa tuliouanzisha
mlioutupa, mnafikiri, sisi mwaka huu fedha tu! Uchaguzi wa
fedha, mtazipata wapi? Mimi nimetoka juzi tu, mara
mmetajirika kiasi hiki!



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.






   

--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


0 comments:

Post a Comment