Tuesday, 24 February 2015

Re: [wanabidii] SIO KASHFA NI SWALI TU. MBONA UKIRISTO MWEPESI HIVI?

Swali lililoulizwa na Bw.Juma ni zuri na linapaswa kujibiwa kwa ufasaha maana lina mantiki na pengine anataka kufahamu ukristo maana yake nini. Naomba nitoe maelezo kwa ufupi maana suala hili ni pana sana.
Kwanza ukristo ni maisha wala sio dini. Tatizo ni kuwa kutokana na kuwepo kwa madhehebu mengi  ya kikristo na namna kila dhehebu linavyofanya kazi wakati mwingine  inawachanganya wale wasio wakristo kufahamu ukweli. Biblia ndio mwongozo wa ukristo na hivyo yeyote anayeishi kwa muongozo wa Biblia ndiye mkristo wa kweli. Kwa mkristo wa kweli, imani yake ipo katika kumtegemea Yesu Kristo katika kila jambo. Hivyo, siku ya kusali haina  mchango mkubwa katika kumfanya mkristo kumepndeza Mungu bali muda wote anatakiwa kuwa connected na huyo Yesu ndivyo ataweza kushinda dhambi. Kama maandiko yasemavyo, Yesu alisema Kaeni Ndani yangu nami Ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika anyi, msipokaa ndani yangu. Yohana 15:4. hIvyo,  Msingi wa ukristo ni Kristo mwenyewe kuwa ndani ya watu wake. Na suala hili linamhusu  kila binadamu. Yesu alikuja duniani kwa ajili ya kuokoa watu, na alikufa kwa ajili ya dhambi za wanadamu wote. Kila atakayemwamini anapata uzima wa milele bila kujali dini ya mtu, rangi jinsia au kabila. Ukristo ni maisha mapya yenye mtazamo mpya na sio dini bali ni uzima wa Mungu ndani ya watu na uzima huo unaanza hapa hapa duniani. Yaani mtu unaunganishwa ktk mtandao wa Mungu na anakuwa na ushirika na Mungu masaa yote. Suala la kanisani lengo lake ni mkusanyiko wa pamoja kwa ajili ya kumwabudu huyo Mungu wa kweli ambaye kila mwamini anatakiwa kuwa naye moyoni. Sasa kuhusu pepo, sisi wakristo hatuiti pepo bali ni uzima wa milele ambao yeyote anayemwamini Yesu anaupata tangu anapoamua kumpa Yesu maisha na atakapokufa huo uzima alioupokea unampeleka mbinguni kwa baba. Ndio maana kwa wakristo wa kweli, mtu akishakufa haiwezekani kumwombea maana tayari anakuwa ameshakwenda alipopachagua alipokuwa hai. Kwa mkristo wa kweli hakuna kustrugle kimwili bali kinachotakiwa na kuimarisha yale mahusiano na ushirika na Mungu kwa njia ya Kristo Yesu. Na kwakweli amri kuu ni UPENDO ambao umegawanyika sehemu 2 Kumpenda Mungu na kumpenda Jirani. Lakini kamwe mtu hawezi kumpenda jirani kama hajaanza kumpenda Mungu kwanza  maana Mungu ndiye anatuwezesha kwa kila jambo likiwemo la kumpenda Jirani. Ukimpenda jirani huwezi kumfanyia jambo baya. Kwa msingi huo mtu anayetimiza amri hiyo ya Upendo anakuwa ametimiza amri zote za Mungu automatically. Tofauti ya Ukristo na dini ni kuwa kwenye dini watu wanajitahidi kutimiza sheria zilizowekwa na dini husika lakini kwa ukristo wa kweli mtu anajitahidi kuimarisha uhusiano na Mungu  kwa njia ya kusoma Biblia na kufanya maombi ikwa ni pamoja na kusikiliza mahubiri. Kwa njia hii mkristo wa kweli anapata muongozo wa kuishi na kushinda Dhambi na shetani. Changamoto iliyopo kwa wakristo wengi ni kutokuwa na ufahamu huu na pia kuishi kwa mazoea tu na desturi. Matokeo yake watu wanajikuta wanaishi kwa sheria za madhehebu yao bila kufahamu ukristo ni nini. Matokeo yake watu wanajikuta wakijivunia dini kwa kuwa tu wamefanya jambo fulani la kidini bila kufanya maamuzi ya kumpa Yesu maisha. Hayo ndiyo yanawachanganya watu wa dini nyingine maana bila mkristo kuwa na yYesu ndani ya maisha yake hawezi kushinda dhambi wala kumshinda shetani ambaye ni mjaribu. Ndipo hapo tunawakuta watu wanajiita wakristo lakini wakifanya maovu kama watu wengine. Maandiko yanasema ''Mkiongozwa na Roho hampo chini ya Sheria'' na tena wale wanaoongozwa na ''Roho wa Mungu hao ndio wana wa Mungu'' Kwa hiyo mkristop wa kweli ni yule aliye na Roho wa Mungu ndani yake na anaongozwa na Roho huyo na hawezi kutenda dhambi na hata ikitokea akatenda bila kujua huyo Roho atamjulisha na atatubu. Kwa kuongozwa na Roho wa Mungu mtu anakuwa yupo connected na Mungu kiroho na hivyo anafahamu mapenzi ya Mungu na kuyafuata na hapo haihitaji kwekewa sheria mbalimbali maana mtu wa namna hiyo automatically anatimiza sheria zote nzuri zilizowekwa na Serikali au na dhehebu lake. Na pia maandiko yanasema Na kila mfanyalo , kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye Wakolosai 3; 17.


On Tuesday, February 24, 2015 8:38 PM, 'Reuben Mwandumbya' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:


Ngupula;
Naomba nami niweke kamchango ka imani yangu.
Kwamba Ukristo ni maisha halisi zaidi ya kushinda kanisani.
Kongoro pepo ni zaidi ya ulivyouliza swali,kanisa ni nyumba ya jumuiko la jumla la waumini,lkn pepo inaanzia maisha ya nyumbani kwako na hasa upendo wako kwa jirani yako.
Sio rahisi km unavyoamini nyie,ingekua hivyo binafsi ningehamia kanisani.

Reuben

Sent from Huawei Mobile

'ngupula' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Ndugu Juma, ukristo ni mgumu kuliko dini yeyote ile.....hebu chungulia haya mambo machache tu....ukristo unasema.....ukimwangalia mwanamke kwa kumtamani tu....umekwisha zini naye...ni dhambi .. ukitaka kutoa sadaka yenye dhawabu basi ni lazima iwe siri hata mkono wako wa kushoto usijue ulichokifanya. ..katika ukristo hakuna mizani ya mema na mabaya....bali ukikosea moja umekosea yote.. ...haturuhusiwi visasi sis....bali aliyekutendea mabaya bas we mtendee mema.....raha ya ukristo ni. msamaha....ukikosea unafuta....dhambi zetu zinaandikwa kwa pensil.. Ngupula.

mngonge franco <mngonge@gmail.com> wrote:

Juma
Binafsi ninaamini zaidi utekelezaji wa tunachokiamini kuliko kwenda mara nyingi kwenye nyumba za ibada. Wakristu wanayo amri kuu ambayo ni upendo, ukiwa na upendo huwezi kumfanyia mwenziyo baya. Kusali/kuswali mara nyingi sawa, kufunga funga sawa lakini swali la msingi ni je unawatendea mambo mema binadamu wenziyo? Kesha unaswali/unasali, funga ramadhani/kwaresima milele yote kama kufunga au kuswali kwako hakuendani na matendo mema ni bure.

2015-02-24 17:28 GMT+03:00 Juma Kongoro <jumakongoro@gmail.com>:
SIO KASHFA NI SWALI TU. MBONA UKIRISTO MWEPESI HIVI?
Mimi ninavyojua ili upate kitu lazima ujitume sana tu.
Kwa mfano ili ufaulu mtihani wa shule lazima usome sana, uhudhurie vipindi na usitegee vyenginevyo utafeli. Vyuo vikuu watu wanakessha madarasani, wanakesha matheater au vyumbani kutafuta first class au pass
Ili upate mazao. lazima ulime kwa bidii.watu wanahamia mashambani, wengine wanaliwa na simba ili kupata mazao mengi na bora
Ili upate uongozi kama ubunge lazima upige kampeni kwa sana tena bila ya kulala.ujitume sana.
Kwa upande wa dini waislam wao wanaswali mara 5 kwa siku bila ya kukosa, hata ukiwa mgonjwa lazima usali, wanafunga, wanatoa zaka na kila wakati unatakiwa usome quran. yaani ujitume kwa sana ili uingie peponi.kwa mwanamke lazima uvae hijab wakati wa baridi au Joto hio ni lazima,yaani muislam dunia imekuwa kwake kama jela. hii yote ni kufaulu maisha ya dunia ili kuipata pepo
Lkn kwa upande wa pili wa dini naona wao wanasali j2 hadi j2 tena atakae.
Sioni kwenda makanisani kila wakati wala majumbani siwaoni kusoma biblia, yaani sioni jitihada hasa kutafuta PEPO. kidogo wanaona walokole. Jee kweli biblia ndio inavyosema hivi kama pepo ni rahisi rahisi?
JEE NI KWELI PEPO RAHISI RAHISI HIVI?
hili sio kashfa ni swali tu
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


0 comments:

Post a Comment