Wednesday, 4 February 2015

Re: [wanabidii] NI PROFESSA LIPUMBA AU NI PROFESA LIPUMBAFU?

Picha ninayoipata kwa kuongozeka kwa matukio ya polisi kupiga na hata kuua raia hata wale ambao wameshawekwa chini ya ulinzi ni evidence of repression and fascism. Sioni kufanya hivyo kama sehemu ya kulinda sheria au amani. Kwa mtu anaye'justify' uovu wa aina hii ina maana naye ni sehemu ya huo uovu.

2015-02-04 14:47 GMT+03:00 Adam Mwambapa <adammwambapa@ymail.com>:
Huyo ndiye Mwandishi mahiri Happness Katabazi, aliyezawadiwa kazi huko Bagamoyo na walioona kama akili yake ipo timamu. Na sasa haya ndiyo mafanikio na mwonekano kwa waliomzawadia kuonesha kuwa amefuzu kile walimchomtuma kukisema, na hakika anasema na kutukana kwa anachojisikia inapolazimu kufanya hivyo wala hana wasiwasi mtoto wa kike.

Nasi kutokana na jinsi alivyoamua na kudhamiria kutukana, hatuna cha ziada kumlipa isipokuwa kumwombea kwa Mwenyezi Mungu ili kuumaliza ujana wake salama na kuukabiri uzee kama moja ya safari yetu muhimu na hatma ya mbio zetu za ujanani.


On Wednesday, February 4, 2015 9:56 AM, 'Happiness Katabazi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:


NI PROFESSA LIPUMBA AU NI PROFESA LIPUMBAFU?
Na Happiness Katabazi

JUMAPILI iliyopita Mwenyekiti wa Taifa wa Chama ya Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza  na waandishi wa Habari mambo  mengi likiwemo tukio la Polisi Kuzuia maandamano ya CUF Januari 27 na kuwapiga bila Sababu na kuwaibia baadhi ya vitu vyao.

Profesa Lipumba alisema pia anafanya jitihada ya kuonana  na Rais Jakaya Kikwete kumweleza tukio hilo na kwamba Serikali na CCM inakata kuvuruga amani na haihehimu  maridhiano yaliyofanyika  mwaka 2001, vinginevyo hali itakuwa  katika uchaguzi mkuu  mwaka huu.

Itakumbukwa Kuwa Januari 29 Mwaka huu, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe alitoa tamko la serikali kuhusu tukio la Januaria 27 Mwaka huu,ambapo pamoja na mambo mengine alimtaka mtu yoyote mwenye malalamiko kuhusu ukiukwaji wa Sheria za nchi, Nguvu nyingi na Polisi awasilishe malalamiko hayo Kwenye Dawati la uchunguzi na kwamba Dawati Hilo itayapokea na kuyafanyia kazi na kwamba Taasisi husika zitafanya uchunguzi Kama uenda Nguvu zaidi zilitumiwa na Polisi bila Sababu za Msingi.

Cha ajabu watu Wengi Wanaolaani tukio lile wameshindwa kufika Katika Dawati la uchunguzi kutoa malalamiko Yao likiwemo dai la jeshi la polosi limejivika  ukada wa CCM wameishia kutumia vyombo Vya Habari, katika mitandao ya kijamii Kulalamika na kutukana kitendo ambacho haisaidii kukomesha matukio Kama hayo wanayo dai Jeshi la Polisi linatumia Nguvu nyingi bila Sababu za Msingi.

Februali Mosi Mwaka huu, Professa Lipumba alipokuwa Akizungumza na waandishi    alisema anafanya jitihada za kumuona Rais Kikwete ili imfikishie kilio chao.

Kwa Madai hayo ya Lipumba ,Nimuulize Lipumba amesahau kuwa Kikwete Kuwa ni Mwenyekiti wa CCM Taifa na pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama na aliwahi Kuwa Ofisa wa Jeshi la Wananchi(JWTZ)?

Lipumba kadai Polisi imejivika  Joho la Ukada wa CCM.Sasa Lipumba yeye ni CUF haoni Kama akienda kumweleza Hilo Rais Kikwete ni sawa anafanyakazi ya 'kumvalisha Mbu miwani' au Kesi ya Nyani anampelekea Ngedere?

Halafu Lipumba anaenda kumweleza nini Rais Kikwete Kuwa yeye na wafuasi wake walijeruhiwa na Polisi ili iweje? Kwani Kikwete ni Daktari au nesi wa kuwatibia majeraha waliyoyapata kutokana na vipigo' Mpini ' wa Askari Polosi?

Tufanye Lipumba Hana Imani na Jeshi la Polisi kwa hiyo hata akienda kutoa malalamiko yake Katika Dawati la uchunguzi dhidi ya Polisi wale hayatafanyiwa  kazi.

Kwa nini Lipumba anashindwa Kufungua Kesi ya Madai ya fidia dhidi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya kuomba Mahakama itoe amri kwa wadaiwa Hao ili iwalipe fidia iliyotokana na madhara ya vipigo Vya Polisi?

Ibara 107 A(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, inasema Mahakama ni Chombo pekee cha kutoa haki na Ndio maana Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Biswalo Mganga, Januari 28 Mwaka huu, amemfungulia Lipumba Kesi ya jinai Na.25 / 2015, Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam.

Kwa nini Lipumba anashindwa kutumia haki hiyo ya Kikatiba kupata haki yake anayodhani anastahili kuipata? Vyombo Vya Habari, mikutano ya adhara ,kukutana na Kikwete haitakusaidia kupata hiyo haki yako ya Kikatiba ya kuandamana, kupewa fidia ya kujeruhiwa na Hasara iliyoupata CUF kwaajili ya kuandaa maandamano na mkutano wa adhara wa Januari 27 Mwaka huu.

Zaidi zaidi Mbele ya Jamii ya watu wenye akili timamu na waliotazama video ya Januari 27 Mwaka huu, ambao Katika video hiyo Ulipokuwa ukihojiwa  na polisi  wewe Mwenyewe (Lipumba) kwa Mdomo wako ulikiri Mbele ya Polisi wale na ulisema yafutatayo ;

' Barua  ya Jeshi la Polisi ya Kuzuia maandamano ya CUF mliipata  saa 12 Kabla  ya CUF kuanza maandamano na kwamba wewe na wafuasi wako siku hiyo ya Januari 27 mwaka huu, mlikuwa mkitembea kwa miguu huku mkiwa Wengi toka Ofisi za CUF- Temeke kwenda eneo la Mkutano ili Muende kuahirisha  mkutano ule.

Kwa maelezo hayo uliyoyatoa Lipumba wakati umezingirwa na Polisi na wafuasi wako wakichezea  'mpini wa Polisi' yaani kipigo huku ukionekana ni mpole sana,uliyekuwa ukitoa ushirikiano wa Hali ya juu kwa Polisi tena kwa heshima kubwa  na kujimaliza kwa maelezo yako ,niliishia kujiuliza msomi huyu ni Profesa Lipumba au ni Profesa Lipumbafu?

Yaani Lipumba Katika video ile amekiri kabisa Kuwa ni kweli saa 12 ,CUF ilipokea barua ya Jeshi la Polisi ya Kuzuia maandamano Yao lakini bado Lipumba siku hiyo ya Januari 27, akatoka nyumbani kwake akaenda hadi Ofisi ya CUF- Temeke, akiwaambia wafuasi wake watoke Katika Ofisi hiyo na waende kwa Wingi wao kwenda eneo la mkutano kwenda kuairisha mkutano ule wakati Tayari alikuwa anafahamu Kuwa Tayari Polisi ilishawakabidhi mapema barua ya Kuzuia maandamano hayo.

Kwa kitendo hiki cha msomi wa aina ya Lipumba kwa mdomo wake kupitia video ya tukio la Januari 27 Mwaka huu, ameonekana akikiri Mbele ya Polisi Kuwa Kabla ya kuanza maandamano Tayari CUF ilikuwa imeishapokea barua ya Polisi ya kukataza maandamano lakini yeye akawaongoza wafuasi wake kutembea kwa umoja wao kwenda kuarisha mkutano kinastahili kufanywa na msomi huyu?

Mzee wangu Lipumba naomba kukushauri jambo moja kwamba, kubali kuwa hadi sasa wewe ni mshitakiwa wa kesi ya jinai ambao polisi unaowakebehi ndiyo wachunguzi na mashahidi wa kesi yako.

Mwendesha Mashitaka ili ashinde Kesi yoyote ili  ya jinai , anategemea sana kazi iliyofanywa na wapelelezi wawe wa Takukuru au Jeshi la Polisi.

Hivyo nakushauri mzee wangu Lipumba kuanzia sasa acha kuendeleza  'ligi'  ya maneno na polisi, unaweza ukajikuta unaumia. Kumbuka msemo usemao mdomo uliponza kichwa.

Mahakama ipo kwaajili kutoa haki lakini siku zote Mahakama inatoa haki kutokana  na aina ya ushahidi ,hoja zilizowasilishwa Mbele yake na pande mbili zenye mgogoro.

Kumbuka katika Kesi yako mshitakiwa ni wewe peke yako na wala siyo viongozi wenzio wa UKAWA na baadhi ya wafuasi wako,vyombo vya habari ambavyo wewe unafikiri vinakusaidia kumbe vinazidi kukupalia makaa ya moto.

Walikuwepo watu wenye ushawishi mkubwa na wafuasi wengi kuliko wewe hapa nchini na waliokuwa mahiri sana Kubwabwaja kupitia vyombo Vya Habari kushinda wewe Lipumba , lakini Leo hii wamefyata Mkia huko Magerezani wa naangaika na Kesi zao.

Mfano Mzuri , Mwenyekiti wa chama cha TLP, Augustine Mrema, Sheikh Ponda Issa Ponda , Kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara  ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) Sheik Farid Hadi Ahmed (48) na wenzake, wanaoshitakiwa kwa kesi ya ugaidi Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam,na kuna siku Moja baadhi ya washitakiwa wenzake walilalamika mahakamani hapo Kuwa wamefanyiwa vitendo Vya kikatiri Magerezani  na Polisi ikiwemo kulawitiwa na Polisi Hali iliyosababisha waaribike vibaya sehemu za Siri.

Na kwa taarifa Yako, baadhi ya Wanajeshi nilioapata fursa ya kukutana nao Ana kwa Ana wamenieleza wamefurahishwa na kazi nzuri iliyofanywa na Jeshi la Polisi ya kuwashushua mkong'oto.

Na siku zote Askari wana umoja sana nawafahamu ni Baba  zangu wamenizaa na kunilea  na ukumbuke  pia Huyo Rais Kikwete aliwai Kuwa Mwanajeshi.

Kwa hiyo ukae ukijua ni wale wale, hawaangushanagi Hao na ukute akitazama ile video ya Januari 27 Mwaka huu, jinsi Lipumba ulivyokuwa  unatetemeka  Mbele ya Polisi Atakuwa anakucheka  sana na kukuona  Kumbe huna  ujanja Mbele ya Polisi wake ,ujanja wako upo Mbele ya Vyambo Vya Habari.

Nakushauri  usijiangaishe kwenda kwa Kikwete kumuona kumuelezea jinsi wewe na wafuasi wako mlivyotendwa na Polisi, Kwani naamini ukimpa Kisogo tu lazima ataangua kicheko na hata hivyo Kikwete Hana mamlaka ya kukusaidia ufutiwe Kesi yako Sasa unamfuata akusaidie nini?

Kweli Kuwa Profesa siyo kufahamu kila kitu na Lipumba amethibitisha Hilokupitia matamko yake mbalimbali .Mimtu mwenye huruma sana hivyo nakupa mbinu haramu ya ushindi wa Kesi ni hivi ;

Kamfuate DPP- Mganga au vijana wake kiaina muombe akufutie Kesi Kama unaweza maana DPP kwa mujibu wa Kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya Mwaka 2002 ,ndiyo hasa mwenye mamlaka ya Kufuta Kesi ya jinai, kamlilie Shida hiyo au nenda  kaliangukie Jeshi la Polisi kimya kimya  baadhi ya wapelelezi wa Kesi yako ili wakaaribu  mapema ushahidi  ili hata DPP akikataa kukufutia Kesi basi ushahidi kuishaaribiwa na Polisi na mashahidi mwisho wa siku Mahakama itatoa hukumu ya kukuachiria huru kwasababu ushahidi wa upande wa jamhuri utaonekana ni dhahifu.

Mbinu  hii inatumiwa  na watoto wa 'mujini' wanaokabiliwa na Kesi za jinai na wanafanikiwa kuchomoka ,wewe akili ya kutumia mbinu hii huna, Matokeo yake Kutwa unabwatabwata majukwaani na Kwenye vyombo Vya Habari.  Shauri yako 'watu watakula kichwa hicho' na huo Ubunge wa Temeke utausikia Redioni.

Kwa mujibu wa Gazeti la Habari Leo la Februali 2 Mwaka huu, lilihapisha Habari iliyomnukuu , Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo (Chadema) amefanya mkutano wake na waandishi wa Habarin,Februali Mosi Mwaka huu ambapo Ndesamburo  aliwataka viongozi wanaounda Umoja wa Katiba wa Wananchi (UKAWA), kuacha kulilalamikia Jeshi la Polisi kutokana na kazi wanazozifanya ikiwa ni kulinda Amani na Usalama wa nchi.

Aidha Ndesamburo alisema Haoni tatizo Kwa Jeshi la Polisi kutekeleza majukumu yake na wala Haoni sababu ya viongozi wa UKAWA Kulilalamikia Jeshi la Polisi kuhusu tukio lililotokea hivi karibuni na  anachoona Polisi inasaidia Vyama Vya upinzani ili wananchi  wavichague.

Ndesamburo pia ni UKAWA kama  alivyo Mwenyekiti wa Chama cha NCCR- Mageuzi, James Mbatia, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ambao Nyie wote wiki iliyopita msijitokeza ndani  na nje ya Bunge kulilalamikia Jeshi la Polisi Kuwa ni Jeshi linalotumika vibaya na limejivisha UKADA wa CCM na linawaonea wapinzani.

Itakumbukwa Kuwa Katika Mauji ya mkutano haramu wa Arusha mjini uliokuwa umeandaliwa na Chadema ,Ndesamburo, Mbowe,Dk,Slaa,Samson Mwigamba walipata Shuruba kutoka kwa Jeshi la Polisi Kwasababu waliokaidi amri ya Jeshi Hilo iliyokataza mkutano huo na wengine wakaambulia kufunguliwa Kesi mahakamani.

Kwa tamko Hilo la Ndesamburo ,Juzi ni wazi amekoma kukaidi amri za Jeshi la Polisi.Hongera sana Mzee Ndesamburo kwa kuliona hilo.Na wengine igeni mfano huo ukiwemo Lipumba ambaye hata kukimbia mbio huwezi na Tayari una Maradhi ya Shinikizo la Damu.

Mzee wangu Lipumba ni msomi wa ngazi wa Kimataifa,nakushauri Tenda matendo ya kisiasa yanayoendana na wasomi na umri wako wa kiutu uzima , utaheshimika.Kwani kwa baadhi  ya matukio unayoyafanya ikiwemo kuamasisha wafuasi wa CUF wasipige kura za maoni Katiba Pendekezwa na mambo mengi watu tumefika uamuzi wa kujiuliza huyu ni Profesa Lipumbafu?

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blogg: katabazihappy.blogspot.com
0716 774494
Februali 3 Mwaka 2015.







Sent from my iPad

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment