Wote hao uliowataja ni altenatives in a different order. Lakini hata ndani ya CCM kuna wengine wanaofaa. Huyu wa kwenu sio kuwa anafaa ila amewekeza sana. Mfano ni hoja hii jinsi mambo yalivyofinyangwa kwenye magazeti. Tunaweza kusema zaidi lakini yafaa kukomea hapo. Adha za mitandao kutupatia rais inapaswa kuwa mara ya mwisho. Mitandao inapamba usaha inauita supu.
--------------------------------------------
On Tue, 2/10/15, 'lesian mollel' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: Re: [wanabidii] Lowassa anadanganywa na wabunge wanaonyemelea mamilioni aliyonayo
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Tuesday, February 10, 2015, 3:08 PM
mzeeemhigo mlete
mnaedhan kuingia ikulu badala ya lowasa tujue give us
altenative president to be ambaye ni msafi msiwe mnaongea
utopianism jamani.........mleteni, mtajeni mwenye sifa zenu,
clean and smart ambaye watanzania watamkubalia kuongoza
nchi kwa kura nyingi au lipumba, sema kama unamtaka dk
slaaa, ama kaka yetu Mbatia....semeni
From: 'ELISA
MUHINGO' via Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com>
To:
wanabidii@googlegroups.com
Sent: Tuesday, February
10, 2015 2:57 PM
Subject: Re:
[wanabidii] Lowassa anadanganywa na wabunge wanaonyemelea
mamilioni aliyonayo
Huu ndio ubovu wa kutumia mitandao kuusaka
urais. Mtandao huu sasa uunakosa watu makini kama
waliokuwemo ndani ya mtandao wa 2005.
Mambo
kama haya yalikuwepo 2005 lakini umakini wa waliotumiwa sasa
haupo.
najua sasa kuwa huenda taifa hili
lisipokuwa makini tutampata mhuni kuingia ikulu.
Mungu apishe mbali
--------------------------------------------
On Tue, 2/10/15, Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com>
wrote:
Subject:
[wanabidii] Lowassa anadanganywa na wabunge wanaonyemelea
mamilioni aliyonayo
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Tuesday, February 10, 2015, 1:10 PM
Lowassa
anadanganywa na wabunge wanaonyemelea mamilioni
aliyonayoNa
Mwandishi
MaalumMAGAZETI
kadhaa yatolewayo kila siku
nchini, Jumatatu Februari 9,
2015,
yaliongozwa na habari kuu kuhusu
Mbunge wa
Monduli, Edward Lowassa kwamba 'anang'ara
katika mbio za urais'.Katika habari hiyo,
magazeti hayo
yote yalinukuu kauli za
wabunge saba wa CCM wanazodaiwa kuwa
walizitoa katika hafla iliyotajwa kuwa "ya aina yake"
ya
chakula cha jioni, Jumamosi
iliyopita.Lakini katika hali isiyokuwa ya
kawaida, hafla hiyo kamwe haikutaja ilikofanyika zaidi ya
kuelezwa tu kuwa "nyumbani kwa kigogo mmoja
wa CCM",
Kilimani mjini Dodoma.Kwa
nini kigogo huyo alifichwa utadhani hafla hiyo
ilikuwa
haramu au kwamba iliambatana na
vitendo vya kihalifu?Wabunge waliotajwa na kunukuliwa
wakizungumza ni Deogratius Ntukamazina
(Ngara), Diana
Chilolo (Viti Maalum –
Singida), Stephen Ngonyani au
'Profesa
Maji Marefu' (Korogwe Vijijini) na Mary
Chatanda ambaye pia wa Viti Maalum (Tanga) na Katibu wa
CCM
wa Mkoa wa Singida.Wengine ni
Kapteni John Komba (Mbinga Magharibi), Mussa
Azzan Zungu
(Ilala) na Yahya Kassim Issa
ambaye ni mbunge wa Chwaka,
Zanzibar.Wote
walinukuliwa
wakimwelezea Lowassa ambaye
pia ni Waziri Mkuu wa zamani
kwamba "ni
kiongozi bora, kiongozi makini, chaguo la
Watanzania" na kadhalika.Ntukamazina kwa mfano alisema:
"Kule kwangu Ngara wananiuliza yule waziri
mkuu aliyeleta
hizi shule za kata yuko
wapi? Mimi nawajibu atarudi na kila
mtu
mitaani anataja jina lako, kwa hiyo sauti ya wengi ni
sauti ya Mungu".Wasiwasi
kuhusu habari hiyo
Kila gazeti, licha ya
habari hiyo kuandikiwa ukumbini na
isiyokuwa ya uchunguzi, yote hayakutaja jina la mwandishi
kwa kusema ni "Mwandishi Wetu, Dodoma",
halafu zote
zinafanana kwa kila kitu katika
mambo yafuatayo:
(i) Kutotaja jina la
kigogo wa CCM aliyeandaa hafla hiyo
kuwa ni
nani;(ii) Idadi ya
wabunge waliohudhuria
hafla hiyo imetajwa na kila gazeti
kuwa 150
utadhani kila mwandishi aliwahesabu au walihesabiwa
mlangoni, kisha hesabu yao ikatangazwa
hadharani;(iii) Wabunge waliotajwa kwenye
magazeti hayo kuwa waliongea ni walewale; na(iv) Wabunge hao
pia wametajwa kwa
mtiririko uleule, nukuu
zilezile, namna ileile huku kila
kitu
kikiwa kinafanana kama barua iliyopigwa photocopy na
kusambazwa huko kote;Katika
hali hiyo, yapo mambo kadhaa ya kutilia wasiwasi kwa
wasomaji makini ambayo ni pamoja na haya
yafuatayo:
(i) Kuna kila mwelekeo wa kuwa
hafla hiyo iliandaliwa kwa
agizo au kwa
gharama za Lowassa mwenyewe;(ii) Kuna kila mwelekeo wa
kuwa
hafla hiyo iliandaliwa maalum kwa
ajili ya kampeni za urais
za Lowassa,
lakini ukakosekana umakini wa kutosha ili
kufanikisha siri iliyolenga kuwadanganya Watanzania;(iii)
Wabunge waliozungumza
inaelekea kwamba
waliandaliwa maalum, halafu inawezekana
kuwa maneno waliyozungumza walipewa au walielekezwa na
Lowassa mwenyewe ama na washauri wake; na(iv)
Habari hiyo imeandikwa na
mwandishi mmoja,
kisha ikasambazwa katika magazeti hayo yote
kwa gharama za mwanasiasa na mbunge huyo ikiwa ni sehemu
ya
kampeni zake za urais.Ili
kuthibitisha vinginevyo, magazeti hayo inabidi
yajibu
maswali makubwa yafuatayo kwa
wasomaji wake ambao ni pamoja
na mimi
kwamba ilikuwaje habari hiyo ifanane kwa zaidi ya
asilimia 75 kuhusu:(i)
Mpangilio wa wabunge walivyozungumza katika hafla
hiyo?(ii) Ilikuwaje idadi ya
wabunge waliozungumza na kunukuliwa na magazeti hayo yote
iwe ileile?(iii) Ilikuwaje
mtiririko wa habari hiyo ufanane kiasi hicho kwa magazeti
yote na kuonekana kuwa imeandikwa na mwandishi
mmoja kama
kweli ni tofauti?(iv) Kama
habari hiyo iliandikwa na waandishi tofauti,
wapi
walikokutana, kisha wakakubaliana kuwa
nukuu zao zote ziwe
ni zilezile?(v) Wapi
waandishi hao walikokutana na kukubaliana kuwa
vilevile
mtiririko wa nukuu zote hizo
ufanane kama mayai?Mfano ninaomaanisha ni kama pale
Mbunge wa Ngara, Deogratius Ntukamazina
aliponukuliwa na
magazeti hayo yote
akisema:"…Oktoba tutakuwa na uchaguzi
mkuu wa kumchagua kiongozi atakayesukuma mbele nchi
yetu."Sote tunafahamu chama
chetu bado hakijatangaza utaratibu, lakini sisi wabunge
marafiki zako tunakuomba muda ukifika uchukue
fomu kwa
sababu unatosha".Nukuu hiyo
ya neno kwa neno ipo katika kila gazeti,
halafu imeandikwa
kwa staili ileile na kwa
aya zinazofanana utadhani ilipigwa
'photocopy' na kusambazwa huko kote.Mbali na hapo,
habari hiyo pia
inafanana kwa kila kitu
katika magazeti hayo yote ambapo,
pale
palipoandikwa bila ya kunukuu neno kwa neno inakuwa
hivyo kwa kila gazeti, na pia kila
paliponukuliwa (quoted)
napo panakuwa
vilevile utadhani pamefanyiwa
'scanning'.Aidha,
magazeti hayo yote
yamemwandika Chilolo kwa aya moja yenye
maneno 22 tu kama ifuatavyo:"Kwa upande wake, Mbunge wa
Viti
Maalum, Diana Chilolo (CCM) aliunga
mkono kauli ya
Ntukamazina kwa kusema
Lowassa ni chaguo la wengi".Wasomaji wote makini
walioisoma
habari hiyo ndani ya magazeti
hayo au baadhi yake hakuna
mashaka kwamba
waligundua kuwa ilitengenezwa maalum kwa
ajili ya kumbeba Lowassa katika harakati zake za
urais.Pamoja na ukweli kuwa
kila mwanasiasa anayetafuta madaraka ya uongozi wa umma
huwa
na njia zake mwenyewe za kutafuta
ushindi, lakini mbinu hiyo
ya Lowassa
haiwezi kuwadanganya walengwa ambao hasa ni
viongozi waandamizi wa CCM.Wabunge aliowatumia kutaka
kufanikisha mkakati wake huo wa kuitisha CCM
ili iogope kuwa
isipomteua kugombea urais
itaondoshwa madarakani na
wapinzani, kwamba
asipoteuliwa yeye ili kusimama katika
kinyang'anyiro hicho basi chama hicho kitashindwa kuna
wengine wamekubali kutumika kiasi hicho kwa
sababu inaelezwa
kwamba ana pesa
nyingi.Ukimwondoa mtu kama Ntukamazina
ambaye ameshasema kuwa hagombei tena ubunge mwaka huu,
Chatanda anajipanga kutaka kugombea ubunge wa
jimbo la
Korogwe Mjini huku Komba au
'Maji Marefu' nao
wakikabiliwa na hali
ngumu majimboni kwao.Ili waweze kupata ushindi kwanza
kwenye kura za maoni za ndani ya CCM, wabunge
hao inabidi
kila mmoja awe na kiwango
kikubwa kabisa cha pesa za
kampeni, fedha
ambazo hakuna hata mmoja aliyenazo.Wote wanategemea kiinua
mgongo
ambacho kila mmoja atalipwa na
serikali baada ya muda wao wa
sasa
kumalizika kiasi cha miezi mine ijayo, lakini
wanafahamu kwamba hazitoshi kuwapa ushindi
wanaoutafuta.Kwa mfano, Komba
amekuwa akitishiwa hadi kufilisiwa na benki anakodaiwa
mamia
ya mamilioni ya fedha alizokopa
pamoja na riba, deni
linalotishia hadi
kukamatwa kwa mali zake kwa sababu
ameshindwa kulipa.Wote
walijitolea mhanga
kumsifia hadharani mbele yake mwenyewe
siyo
kwa sababu eti wanamuunga mkono kwelikweli, bali
walifanya hivyo kwa sababu wanayataka
mamilioni ya pesa
zake.Wanataka kumdanganya
kwa
sababu wanataka fedha hizo ili nao pia
wakahangaikie ubunge
kwa muhula mwingine
kwenye majimbo yao. Walikuwa hawamsifu
eti
kwa sababu anatakiwa kiasi hicho kuwa Rais wa Serikali
ya Awamu ya Tano.Wote
wananyemelea mamilioni ya fedha anazodaiwa kufadhiliwa au
kwa yeye mwenyewe kujikusanyia kwa namna moja
ama
nyingine.NI MTAZAMO WANGU
--
Send
Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
for any legal consequences
of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree
to this
disclaimer and pledge to abide by
our Rules and Guidelines.
---
You received this
message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop
receiving emails
from it, send an email to
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send
Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to
this Forum bears the sole responsibility for any legal
consequences of his or her postings, and hence statements
and facts must be presented responsibly. Your continued
membership signifies that you agree to this disclaimer and
pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message
because you are subscribed to the Google Groups
"Wanabidii" group.
To unsubscribe
from this group and stop receiving emails from it, send an
email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment