Tuesday, 10 February 2015

Re: [wanabidii] Lowassa anadanganywa na wabunge wanaonyemelea mamilioni aliyonayo

Kama anagawa mamilioni ya bure hata mimi ningekuwa mbunge ningeomba mgao.
em

2015-02-10 6:12 GMT-05:00 'godfred mbanyi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:

Declare interest first! Upo kundi gani??? Membe, Makamba Jnr, Pinda, au???


--------------------------------------------
On Tue, 2/10/15, Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com> wrote:

 Subject: [wanabidii] Lowassa anadanganywa na wabunge wanaonyemelea mamilioni aliyonayo
 To: wanabidii@googlegroups.com
 Date: Tuesday, February 10, 2015, 1:10 PM

 Lowassa
 anadanganywa na wabunge wanaonyemelea mamilioni
 aliyonayoNa
 Mwandishi MaalumMAGAZETI
 kadhaa yatolewayo kila siku nchini, Jumatatu Februari 9,
 2015, yaliongozwa na habari kuu kuhusu
 Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa kwamba 'anang'ara
 katika mbio za urais'.Katika habari hiyo, magazeti hayo
 yote yalinukuu kauli za wabunge saba wa CCM wanazodaiwa kuwa
 walizitoa katika hafla iliyotajwa kuwa "ya aina yake" ya
 chakula cha jioni, Jumamosi iliyopita.Lakini katika hali isiyokuwa ya
 kawaida, hafla hiyo kamwe haikutaja ilikofanyika zaidi ya
 kuelezwa tu kuwa "nyumbani kwa kigogo mmoja wa CCM",
 Kilimani mjini Dodoma.Kwa
 nini kigogo huyo alifichwa utadhani hafla hiyo ilikuwa
 haramu au kwamba iliambatana na vitendo vya kihalifu?Wabunge waliotajwa na kunukuliwa
 wakizungumza ni Deogratius Ntukamazina (Ngara), Diana
 Chilolo (Viti Maalum – Singida), Stephen Ngonyani au
 'Profesa Maji Marefu' (Korogwe Vijijini) na Mary
 Chatanda ambaye pia wa Viti Maalum (Tanga) na Katibu wa CCM
 wa Mkoa wa Singida.Wengine ni
 Kapteni John Komba (Mbinga Magharibi), Mussa Azzan Zungu
 (Ilala) na Yahya Kassim Issa ambaye ni mbunge wa Chwaka,
 Zanzibar.Wote walinukuliwa
 wakimwelezea Lowassa ambaye pia ni Waziri Mkuu wa zamani
 kwamba "ni kiongozi bora, kiongozi makini, chaguo la
 Watanzania" na kadhalika.Ntukamazina kwa mfano alisema:
 "Kule kwangu Ngara wananiuliza yule waziri mkuu aliyeleta
 hizi shule za kata yuko wapi? Mimi nawajibu atarudi na kila
 mtu mitaani anataja jina lako, kwa hiyo sauti ya wengi ni
 sauti ya Mungu".Wasiwasi
 kuhusu habari hiyo
 Kila gazeti, licha ya habari hiyo kuandikiwa ukumbini na
 isiyokuwa ya uchunguzi, yote hayakutaja jina la mwandishi
 kwa kusema ni "Mwandishi Wetu, Dodoma", halafu zote
 zinafanana kwa kila kitu katika mambo yafuatayo:
 (i) Kutotaja jina la kigogo wa CCM aliyeandaa hafla hiyo
 kuwa ni nani;(ii) Idadi ya
 wabunge waliohudhuria hafla hiyo imetajwa na kila gazeti
 kuwa 150 utadhani kila mwandishi aliwahesabu au walihesabiwa
 mlangoni, kisha hesabu yao ikatangazwa hadharani;(iii) Wabunge waliotajwa kwenye
 magazeti hayo kuwa waliongea ni walewale; na(iv) Wabunge hao pia wametajwa kwa
 mtiririko uleule, nukuu zilezile, namna ileile huku kila
 kitu kikiwa kinafanana kama barua iliyopigwa photocopy na
 kusambazwa huko kote;Katika
 hali hiyo, yapo mambo kadhaa ya kutilia wasiwasi kwa
 wasomaji makini ambayo ni pamoja na haya yafuatayo:
 (i) Kuna kila mwelekeo wa kuwa hafla hiyo iliandaliwa kwa
 agizo au kwa gharama za Lowassa mwenyewe;(ii) Kuna kila mwelekeo wa kuwa
 hafla hiyo iliandaliwa maalum kwa ajili ya kampeni za urais
 za Lowassa, lakini ukakosekana umakini wa kutosha ili
 kufanikisha siri iliyolenga kuwadanganya Watanzania;(iii) Wabunge waliozungumza
 inaelekea kwamba waliandaliwa maalum, halafu inawezekana
 kuwa maneno waliyozungumza walipewa au walielekezwa na
 Lowassa mwenyewe ama na washauri wake; na(iv) Habari hiyo imeandikwa na
 mwandishi mmoja, kisha ikasambazwa katika magazeti hayo yote
 kwa gharama za mwanasiasa na mbunge huyo ikiwa ni sehemu ya
 kampeni zake za urais.Ili
 kuthibitisha vinginevyo, magazeti hayo inabidi yajibu
 maswali makubwa yafuatayo kwa wasomaji wake ambao ni pamoja
 na mimi kwamba ilikuwaje habari hiyo ifanane kwa zaidi ya
 asilimia 75 kuhusu:(i)
 Mpangilio wa wabunge walivyozungumza katika hafla
 hiyo?(ii) Ilikuwaje idadi ya
 wabunge waliozungumza na kunukuliwa na magazeti hayo yote
 iwe ileile?(iii) Ilikuwaje
 mtiririko wa habari hiyo ufanane kiasi hicho kwa magazeti
 yote na kuonekana kuwa imeandikwa na mwandishi mmoja kama
 kweli ni tofauti?(iv) Kama
 habari hiyo iliandikwa na waandishi tofauti, wapi
 walikokutana, kisha wakakubaliana kuwa nukuu zao zote ziwe
 ni zilezile?(v) Wapi
 waandishi hao walikokutana na kukubaliana kuwa vilevile
 mtiririko wa nukuu zote hizo ufanane kama mayai?Mfano ninaomaanisha ni kama pale
 Mbunge wa Ngara, Deogratius Ntukamazina aliponukuliwa na
 magazeti hayo yote akisema:"…Oktoba tutakuwa na uchaguzi
 mkuu wa kumchagua kiongozi atakayesukuma mbele nchi
 yetu."Sote tunafahamu chama
 chetu bado hakijatangaza utaratibu, lakini sisi wabunge
 marafiki zako tunakuomba muda ukifika uchukue fomu kwa
 sababu unatosha".Nukuu hiyo
 ya neno kwa neno ipo katika kila gazeti, halafu imeandikwa
 kwa staili ileile na kwa aya zinazofanana utadhani ilipigwa
 'photocopy' na kusambazwa huko kote.Mbali na hapo, habari hiyo pia
 inafanana kwa kila kitu katika magazeti hayo yote ambapo,
 pale palipoandikwa bila ya kunukuu neno kwa neno inakuwa
 hivyo kwa kila gazeti, na pia kila paliponukuliwa (quoted)
 napo panakuwa vilevile utadhani pamefanyiwa
 'scanning'.Aidha,
 magazeti hayo yote yamemwandika Chilolo kwa aya moja yenye
 maneno 22 tu kama ifuatavyo:"Kwa upande wake, Mbunge wa Viti
 Maalum, Diana Chilolo (CCM) aliunga mkono kauli ya
 Ntukamazina kwa kusema Lowassa ni chaguo la wengi".Wasomaji wote makini walioisoma
 habari hiyo ndani ya magazeti hayo au baadhi yake hakuna
 mashaka kwamba waligundua kuwa ilitengenezwa maalum kwa
 ajili ya kumbeba Lowassa katika harakati zake za
 urais.Pamoja na ukweli kuwa
 kila mwanasiasa anayetafuta madaraka ya uongozi wa umma huwa
 na njia zake mwenyewe za kutafuta ushindi, lakini mbinu hiyo
 ya Lowassa haiwezi kuwadanganya walengwa ambao hasa ni
 viongozi waandamizi wa CCM.Wabunge aliowatumia kutaka
 kufanikisha mkakati wake huo wa kuitisha CCM ili iogope kuwa
 isipomteua kugombea urais itaondoshwa madarakani na
 wapinzani, kwamba asipoteuliwa yeye ili kusimama katika
 kinyang'anyiro hicho basi chama hicho kitashindwa kuna
 wengine wamekubali kutumika kiasi hicho kwa sababu inaelezwa
 kwamba ana pesa nyingi.Ukimwondoa mtu kama Ntukamazina
 ambaye ameshasema kuwa hagombei tena ubunge mwaka huu,
 Chatanda anajipanga kutaka kugombea ubunge wa jimbo la
 Korogwe Mjini huku Komba au 'Maji Marefu' nao
 wakikabiliwa na hali ngumu majimboni kwao.Ili waweze kupata ushindi kwanza
 kwenye kura za maoni za ndani ya CCM, wabunge hao inabidi
 kila mmoja awe na kiwango kikubwa kabisa cha pesa za
 kampeni, fedha ambazo hakuna hata mmoja aliyenazo.Wote wanategemea kiinua mgongo
 ambacho kila mmoja atalipwa na serikali baada ya muda wao wa
 sasa kumalizika kiasi cha miezi mine ijayo, lakini
 wanafahamu kwamba hazitoshi kuwapa ushindi
 wanaoutafuta.Kwa mfano, Komba
 amekuwa akitishiwa hadi kufilisiwa na benki anakodaiwa mamia
 ya mamilioni ya fedha alizokopa pamoja na riba, deni
 linalotishia hadi kukamatwa kwa mali zake kwa sababu
 ameshindwa kulipa.Wote
 walijitolea mhanga kumsifia hadharani mbele yake mwenyewe
 siyo kwa sababu eti wanamuunga mkono kwelikweli, bali
 walifanya hivyo kwa sababu wanayataka mamilioni ya pesa
 zake.Wanataka kumdanganya kwa
 sababu wanataka fedha hizo ili nao pia wakahangaikie ubunge
 kwa muhula mwingine kwenye majimbo yao. Walikuwa hawamsifu
 eti kwa sababu anatakiwa kiasi hicho kuwa Rais wa Serikali
 ya Awamu ya Tano.Wote
 wananyemelea mamilioni ya fedha anazodaiwa kufadhiliwa au
 kwa yeye mwenyewe kujikusanyia kwa namna moja ama
 nyingine.NI MTAZAMO WANGU



 --

 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

  

 Kujiondoa Tuma Email kwenda

 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya
 kudhibitisha ukishatuma

  

 Disclaimer:

 Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
 for any legal consequences of his or her postings, and hence
 statements and facts must be presented responsibly. Your
 continued membership signifies that you agree to this
 disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

 ---

 You received this message because you are subscribed to the
 Google Groups "Wanabidii" group.

 To unsubscribe from this group and stop receiving emails
 from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

 For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment