Sunday, 1 February 2015

Re: [wanabidii] Kwanini majambazi yanavamia na kupora silaha za polisi?

Majibu sahihi ya swali lako ni vigumu kuyapata lakini binafsi ninaweza kubashiri yafuatayo
1. Silaha zinazoporwa inawezekana ziko mikononi mwa majambazi kwa ajili ya kufanikisha ujambazi wao ndani na nje ya Tanzania
2. yawezekana silaha hizo zinaporwa kwa minajili ya biashara yaani kuuzwa kwa majambazi wengine
3. Yawezekana wakawepo watu waliochoka na kile wanachokiona ni uonevu wa serikali sasa wameamua kujidhatiti ili kupambana na serikali
4. Mwisho naona jeshi letu la polisi limewekeza sana kudhibiti maandamano zaidi kuliko kujidhatiti kujilinda wenyewe, raia na mali zao.

Binafsi napendekeza liundwe jeshi la sungusungu na lipewe bajeti kubwa  kwa ajili ya usalama wa raia na mali zao ili jeshi la polisi tulilonalo liweze kuconcentrate na udhibiti wa maandamano ya raia wasiokuwa na silaha. Kwa hali ya maisha iliyopo ya vijana kukosa mwelekeo na watawala kutaka kukaa madarakani millele hata bila ya uwezo kiuongozi sioni dalili za maandamano kuisha siku za hivi karibuni. Kama panya road wachache tena bila hata bunduki moja wameweza kutikisa jiji la Dar itakuwa hao wenye silaha tena zenye uewezo sawa na za polisi?

2015-02-01 12:06 GMT+03:00 Ephata Nanyaro <nanyaro04@gmail.com>:

Jan 27 wakati polisi wawili huko Tanga wanaporwa SMG mbili na risasi 60,na mmoja kujeruhiwa,wenzao huko Dar walikuwa wanafyatua risasi na mabomu kutawanya wafuasi wa CUF waliokuwa kwenye kumbukizi ya mauaji ya wenzao yaliofanywa na polisi huko Pemba.Kila uchao polisi wanajenga UFA kati yao na raia,na umma wenye haki zote za Kidemokrasia katika nchi yao HURU.

Jeshi la polisi kwa muda mrefu sana limejitoa kwenye wajibu wake wa kuwa walinzi wa maisha na mali za raia,badala yake limekubali kutumiwa kisiasa na CCM hadi kufikia kuitwa polisiccm.Kwa kukubali kuwa hivyo limejikuta siku hadi siku likipoteza uwezo wake,weledi,ustadi wake,badala yake limejikuta likiwa LANGO la majambazi,yaani lango la kukabidhi majambazi silaha zinazokusudiwa kulinda raia.Ni aibu ya mwaka,ni fedheha kubwa sana ,na jambo lisilokubalika kuwa KUPORWA kwa silaha na majambazi kwenye vituo vya polisi kunawezekana tu kwa majambazi kutumia silaha za jadi,yaani,marungu,mapanga,na visu.Ni aibu zaidi kuwa jeshi la polisi limegeuzwa nyenzo ya kisiasa,au tawi la ccm kiasi cha kubezwa na kufanya wananchi kutojua hatma ya chombo hiki cha ulinzi na usalama wa mali zao.

Swali la kujiuliza

Je bunduki,risasi na mabomu yanayoporwa vinaenda wapi?je vinaenda kuanzisha jeshi la wapi na kwa madhumuni gani?

--
Ephata Nanyaro
P.o.box 15359
Arusha
+255 754 834152
Skype.nanyaro.ephata

"truth shall set you free"

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment