Saturday, 1 November 2014

[wanabidii] KUNUNUA KOMPYUTA MSIMU WA SIKUKUU 2014

KUCHAGUA LAPTOP ( MPAKATO ) MSIMU WA SIKUKUU 2014 

Tokea LAPTOP zimeanza kuingia sokoni zimekua sehemu ya maisha yetu ya kila siku . Mwanzoni hazikua zinapendeza sana , Kubwa na Gharama . Lakini siku hizi katika dunia ya ushindani mambo yamebadilika kwa sababu kuna kampuni nyingi zinazotengeneza Laptop kwahiyo zimekua na gharama nafuu na mtu anaweza kuchagua aina anayotaka kulingana na viwango au uwezo wake .

Kuna kampuni nyingi zinazotengeneza Laptop lakini kwa zinazouza sana ni hizi , DELL , ASUS , LENOVO , IBM , HP , SAMSUNG , APPLE , ACER ,CHILLBLAST , ALIENWARE , TOSHIBA ,SCHENKER , MSI , GIGABYTE ,SONY , SCAN .

Kama unataka kununua laptop msimu huu wa sikukuu za mwaka 2014 , huu ni muongozo unaoweza kukufaa katika kuchagua laptop , ingawa baadhi ya vitu vinaweza kubadilika kutokana na nchi na soko kwa ujumla .
Ukienda kwenye Maduka utakuta kuna laptop aina 3 , zile zenye Operating System haswa windows , ambazo hazina kabisa , na ambazo zimewekwa lakini za majaribio ukiingia kwenye mtandao unatakiwa kununua .

Bei za laptop zinategemea moja ya mambo hayo 3 ukiacha mengine yote , laptop ambazo hazina kitu kabisa bei yake ni ndogo inapungua zaidi ya dola 200 kuliko zile ambazo zimeshawekwa Programu kama ni za majaribio au ambazo zimeshasajiliwa kabisa .

Sasa hivi kuna Preview ya Windows 10 , unaweza kuingia dukani ukaambiwa ndio toleo jipya wewe ukakubali kuitumia kumbe ni preview tu baada ya muda itaweza kukusumbua , kwa sasa usitumie windows 10 , tafuta windows 7 au 8 .

Kabla ya kuamua kununua laptop hakikisha unajua kile unachotaka kufanya na laptop husika , kama ni kwa masuala binafsi tu madogo au ya kitaaluma ( kutegemea na taaluma ) . mfano kama unataka kununua ya kuchezea Michezo (Games ) unatakiwa kuchagua yenye viwango na uwezo mkubwa , kama CPU , RAM , zaidi hapo andaa bajeti kubwa .
Kama ni kwa ajili ya Kuandika vitu vyako tu , kutembelea tovuti mbalimbali unaweza kununua laptop ya viwango vidogo na utatumia gharama ndogo .
CPU ndio muendeshaji mkubwa wa Laptop yako kwa ujumla , udogo au ukubwa wa CPU ndio utaamua kasi ya laptop yako kutokana na matumizi . Kuna Kampuni nyingi zinazotengeneza CPU Kama Intel , AMD , Motorola na nyingine nyingi lakini INTEL na AMD ndio zinazonunuliwa zaidi sokoni na kutumika zaidi kwenye laptop , mwendo wake au Spidi inatakiwa iwe kuanzia 3.4 Ghz , Core i5 or i7 M .

Uwezo na Ukubwa wa kuhifadhi vitu wa Laptop yako ni muhimu sana , hii nayo inategemea na aina ya shuguli unazofanya na vitu vyako , kama unavideo nyingi , nyaraka , picha na vitu kama hivyo unashauriwa kua na laptop yenye uwezo na eneo kubwa la kuhifadhia vitu vyako hii inaitwa HDD – Hard Disk Drive , inatakiwa iwe na angalau GB 250 , iwe na mfumo wa SATA .

HDD Kubwa inaendana na RAM wengine huita Memory kubwa , hii inatakiwa kuanzia GB 4 na kuendelea , kutegemeana pia na shuguli unazofanya , laptop inapofanya kazi vitu vyote huhifadhiwa kwenye hii RAM .

Kwa watu wanaopenda michezo ya Kompyuta , kuchora , kutengeneza filamu kutumia Kompyuta , suala la VGA , GPU au Graphic Card ni muhimu sana , uzuri wa Video unayoiona kwenye kioo unategemea sana hii kadi , Kuna kampuni nyingi zinazotegeneza hizi kadi kwa ukubwa na viwango tofauti .

Huwezi kutumia laptop bila ulinzi dhidi ya mashambulio kutoka nje labda kwenye internet au vitu unavyochomeka kama flash , au unavyoingiza kama CD/DVD , hapo ndio tunakuja kwenye suala zima la ANTIVIRUS .Mpaka sasa hivi kampuni nyingi zimeshatoa matoleo mapya ya ANTIVIRUS Zao , kama Kaspersky 2015 , AVIRA , AVG 2015 , AVAST 9.0 , NORTON , SYMANTEC , MCAFEE na Nyingine nyingi . 

Ufanyaji mzuri wa ANTIVIRUS unategemea sana ukubwa na uwezo wa LAPTOP yako na zaidi ni jinsi unavyoiboresha kwa kuingiza kwenye internet kwa ajili ya kufanya updates ( boresha )

Kwa wale wanaopenda kusafiri au sehemu zenye shida ya umeme suala la betri ni muhimu sana kwenye laptop mpaka mwaka mmoja uliopita betri zilikua zinadumu kwa saa 4 lakini sasa hivi kuna mpaka saa 8 kutegemea na aina ya Laptop na Ukubwa wake , betri inayokaa muda mrefu itaweza kukusaidia kwa muda mrefu zaidi .

Screen au Kioo ni muhimu kwa watumiaji wa laptop hili nalo hutegemea shuguli unazofanya , kwa mtumiaji wa kawaida anaweza kuamua kutumia kioo cha kawaida ila kwa mchoraji wa ramani yeye atahitaji laptop yenye kioo kikubwa ili aweze kuona kazi zake na kuchora vizuri zaidi .

Kwenye laptop zote za sasa hivi zinavitu ambavyo ni lazima kama NIC (Sehemu ya Kuchomeka waya wa Mawasiliano ) , WIFI ( Wireless ) , USB , Speaker na Mic , Cardreader , webcam , FingerPrint .

Warranty ni kitu muhimu sana kwenye bidhaa yoyote unayonunua sio kwenye Laptop tu , hii ndio inaeleza jinsi utakavyorudisha laptop dukani kama imeharibika ndani ya muda Fulani na kitu gani kikiharibika ndio urudishe .

Kwenye Laptop na Vifaa vingi warranty inakua ndani ya miaka 3 lakini kwa nchi nyingi za afrika , Tanzania ikiwemo ni mwaka mmoja .

Mwisho kabisa ni kuongea na muuzaji wa bidhaa kuhusu shuguli unayoenda kufanya na kifaa chako kabla ya kununua , ataweza kukushauri zaidi na hata kukuonyesha bidhaa zilizopo ili uweze kuchagua ili usije kupata taabu baada ya kununua .

YONA FARES MARO
0786 806028 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment