Friday, 28 November 2014

Re: [wanabidii] ESCROW:Majibu ya PROF MUHONGO ni aibu ya mwaka kwa PAC na wasaka tonge

I wish they were that much gentle, they should have kissed their beloved offices and say goodbye! But because of their greedy for power, here we are with their 'illogical' arguments.

Sio wasomi wote wameelimika, na haijalishi kiwango cha elimu alicho nacho! Ma, professor wetu kwenye hii soo, nao, hivihivi tu, hawajaelimika. This scandal is suicidal to their academic career. Hili sio jambo la kutafakari mara mbili, na huhitaji mtu akuambie, 'umejinyea' (samahani kwa neno hili); ila wangelikuwa werevu, na kwa vile walijijua kwa nanmna yoyote ile sakata hili, lingeliwataja, hawakuhitaji kusubiri, zaidi ya kuandika barua ya kujiuzulu, na kutafuta kijiwe kingine. Duh, hawa jamaa wana roho ngumu sana!

Baba wa Taifa hayati Mwl J. K. Nyerere alisema, tuhuma tu kwa kiongozi, hazifai, zinatosha kumfanya awajibike. Haya ndio maadili ya uongozi yanayoingoza hii nchi, na siku hizi, wamekuwa na tabia kwenye TV kutukaririsha wosia wa baba wa taifa. Hivyo, ni haki wananchi kuchachamaa, maana visu wamevinoa wenyewe au maarifa wametupatia, sasa tunayatumia, wanatuona wabaya, hapana, wawajibike. Hata kama baba wa kaya a,k.a Raisi, anahusika, I am sorry, I have not other morals than to advice him too to resign, and for him to remain dignified in the history of our mama land Tanzania.

Jamani, haiingii akilini kuwa fedha zote hazikuwa za umma! Kama sivyo, kwa nini zikaguliwe na Mkaguzi wa Serikali! Logically, this argument is flawned! Sawa, hata kama zingelikuwa za mtu binafsi, nchi hii ina mamilionea wengi, mbona siwasikii wakienda eneo kama Kariakoo na kuanza kuwagawia watu kama njugu? Haipo na wala ahaitakaa itokee, na kilichotokea, tena milungula mikubwa ya fedha kiasi hiki watu kugawana kama njugu, tena zikitokea taasisi mama tuliyopa dhamana ya kusimama fedha zetu, hatuwezi kukipa kitendo hiki jina lingine zaidi ya kiashiria kinachoonyesha kuwa serikali imeshindwa pamoja na viongozi wake. Kwa matumizi mabaya kiasi hiki, hatustahili kuaminika kwenye maswala ya fedha, ama kwa mkopo au kama msaada. Tena kwa sataili hii, nchi itegemee ukwepaji mkubwa wa kodi kuongezeka, maana zilizochotwa na kodi zetu, yangu mimi na wewe bila ya kujali unachangia kiasi gani.

Fedha hizi zilitosha kutengeneza madawati kwa shule zote za Tanzania popote pale zilipo pamoja na kutengeneza maabara za kisasa, tena zikiwa na vifaa vyote vya muhimu kwa nchi nzima, na ingelibaki. Hebu fikiria, fedha hizi zingelitumika kwa kazi hizi, ni vijana wangapi, na wakandarasi, wakiwemo mafundi mchundo na seremela ambao wangelipata kazi, na mzunguko kwenye uchumi wetu ungelikuwa kiasi gani! Ni nyuso za watanzania wangapi zingelikuwa na furaha, na hivyo kitakia nchi baraka? Nawashauri wahusika wote wakatubu kwa Mungu, la, wataanika na vizazi vyao, maana ni wengi wanateseka nchini kwa kukosa huduma muhimu, kwanza wagonjwa kukosa dawa, na wanafunzi kukalia mawe au kukaa chini, haiingii akilini hili, halafu viongozi wetu wanasema fedha sio za serikali, hivyo, ilikuwa halali kugawana kama njugu, lakini, hata, njugu zinanunuliwa, hakuna za bure!

Vijana kibao na wajasiriamali wameandika miradi, lakini hakuna fedha, leo mnagawana fedha, hata kama sio za serikali, wangeliwakopesha watu au SACCOS watu wakazifanyia kazi, na sio kugawana kama fedha zilizookotwa mahali zisizokuwa na mwenyewe. Hapana jamani, haliingii akilini hili. Serikali isijitete, iwajibike, hata kama angelikuwa baba yangu, kashindwa. To be human is to err and the noble persons are not the ones who excels alone but those who knows how to acknowledge their mistakes in due circumstances.

Serikali ingelichote fedha hizi zote, na wakatupatia mchakato kuwa asilimia fulani tulitengeneza madawati, maabara, na au kulipa mishahara ya waalimu na tukivitathmini vyote hivyo tukaona vinaoana na fedha iliyotumika, tusingelikuwa na ugomvi nao. Tatizo tunapumuliana wote hapa, ghafla, unamuona mwenzako kaibuka, ana hiki au kile na ukilinganisha na mshahara wake na muda aliokuwepo kazini havioani, hakuna jinsi, mwizi tu huyu. Sio maneno yangu bali ya Baba wa Taifa. Hata kama ulikuwa kazini kw miaka zaidi ya kumi na sio kwenye biashara, mali na samani za mabilioni unazipata wapi kama wewe sio mwizi?

Alafu tatizo la viongozi wetu, wanapenda kuiba au kula kwa mikono miwili, na hili ndilo linalowaumbua. Tuige kwa wenzetu, wao wanakula kamisheni au udalali, na una viwango vyake. Ukiwa ni mradi wa mabilioni, kiwango chake ni kati ya 1% hadi 2% na thamani ya mradi inapokuwa chini ya hapo, kiwango cha kamisheni nacho kinapanda, na ni tofauti kutoka nchi moja na nyingine, ila ni kati ya 5% na 10% na sii zaidi ya viwango hivi na huwa inakatwa kodi. Kwa wenzetu, Kitambulisho chako cha uraia, kina kuunganisha na huduma zote za kijamii, zikiwemo huduma za kibenki, kuwa wanaweza kufuatili kila senti inayoingia kwenye akaunti yako, na kila inapoingia, benki wanakata kodi, na kuipeleka serikalini. Serikali ikikusanya, inawarudishia wananchi kwa njia ya huduma, na wanapothaminisha hizi huduma, garama zinapaswa kuwiana na makusanyo, na kama kuna baki, hiyo inaweza kuchukuliwa kama faida, ndio hiyo wakati mwingine inaletwa kwetu kama msaada, lakini chanzo chake ni kodi. Kwanini nchi yetu ya 'tumbili' pamoja na ukweli kuwa temepelekwa ulaya kusoma, ili kupata ze best practices, tuje tuziweke kwetu kama zilivyofanya nchi za China, Singapore na Malaysia, jamani nauliza, nchi ya 'tumbili' tunalaana gani? Nimetumia neno tumbili maana, tumbili hata wafilisi mazao kiasi gani, huwa hanenepi! Na Tanzania ndivyo tulivyo.

Ninalizie tu kwa maneno haya, ambayo nayo yamezaliwa kwenye sakata hili, kuwa, kuna watu wanatania, kuwa, "kwenye mchongo wowote wa hela, ukiona Mchagga hayupo, usitie mkono, mtakamatwa tu!" Na mimi najiuliza, historia inawasema hawajamaa ni wazuri kufungua milango, inakuwaje walikosekana kwenye milungula hii? Kumbe hatujui 'falsafa ya mchagga na umahiri wa kufungua milango.! Katu hawa jamaa hawali mbegu, maana akifanya hivyo, kesho atafungua wapi? Na hawa wenzagu, hawakulijua hili, walikomba mpaka na ule udongo, yaani, kama ni shamba, lisikae lilimike tena.

Huu ni ujinga, na kwa ujinga huu, wanapaswa kuwajibika.

2014-11-28 10:09 GMT+03:00 Magora Hassan <magorah15@gmail.com>:

Kuna baadhi ya mambo hayahitaji hata darasa moja kichwani kujua nani muongo na nani mkweli. Kama kweli mlifuatilia vizuri hotuba ya Mh Mbowe mtajua kabisa kuwa Prf Muhongo ni muongo wa mwaka kwani aliumbuka vibaya juu ya habari ya mwanasheria wa Tanesco kufukuzwa kazi. Awali alisema kuwa alijiuzulu kwa kuhofia kufukuzwa kazi kwani alimdanganya mwajiri wake(tanesco) kuwa alitakiwa kwenda Maleysia akiambatana na ofisa kutoka ofisi ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali. Mh Mbowe alithibitisha uongo huu kwa kuonyesha barua iloandikwa na Mh Werema ikieleza juu ya azma ya mwanasheria huyu wa Tanesco kwenda Maleysia kikazi. Hapa utaona kuwa Serikali imejipanga kuudanganya uma wa Watanzania ilihali watu wanaujua ukweli.

Rgrds
Magora

On Nov 28, 2014 8:21 AM, "'Reuben Mwandumbya' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Mollel;
Ulichokisema hapa chini kina harufu hasi.
Unawashindanisha kwa vigezo gani?Hawa watu wote wanategemeana sawa na viungo vya mwili hakuna kisicho na umuhimu. japokuwa ushindanishi wako unaouongelea hapa ni wa kisiasa.
Mkulima anaweza kuishi vizuri tu bila uwepo wa Mfugaji.
 
Reuben

From: 'lesian mollel' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Thursday, November 27, 2014 12:43 PM
Subject: Re: [wanabidii] ESCROW:Majibu ya PROF MUHONGO ni aibu ya mwaka kwa PAC na wasaka tonge

mmmmh,lowasa na pinda mmmmh pinda hana ubavu bana, mkulima na mfugaji mmmm mkulima lazima atashindwa
 
From: 'john mushi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Thursday, November 27, 2014 11:21 AM
Subject: Re: [wanabidii] ESCROW:Majibu ya PROF MUHONGO ni aibu ya mwaka kwa PAC na wasaka tonge

Hivi wewe Emma unayejaribu kulijua sakata na kumsifu Muhongo na majibu yake unaelewa kweli nchi iliko?Hivi ramani nzima unaiona na kuielewa?THINK BEFORE YOU .....PESA HIZO HATA KAMA NI ZAKO WEWE  BINAFSI  ZILIVYOTOLEWA TOLEWA  USINGESHTUKA? KWA HALI HIYO UTAENDELEA KUCHANGIA MAABARA NA MADAWATI NA MUHIMBILI UTAENDELEA KUWACHUKUA MAREHEMU WAKO MPAKA UTAKAPOZINDUKA! MUNGU AKUBARIKI EMMA NA WENGINE WOTE WA STAILI YAKO.

From: 'jabir yunus' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Thursday, November 27, 2014 9:43 PM
Subject: Re: [wanabidii] ESCROW:Majibu ya PROF MUHONGO ni aibu ya mwaka kwa PAC na wasaka tonge

Emma unabakia na msimamo wako huo hata baada ya mchango wa Tundu Lissu, David Kafulila na Freeman Mbowe?

Utakuwa mtu wa ajabu sana.

Haya.

J

From: Emma Kaaya <emmakaaya@gmail.com>
To: Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Thursday, November 27, 2014 7:08 PM
Subject: [wanabidii] ESCROW:Majibu ya PROF MUHONGO ni aibu ya mwaka kwa PAC na wasaka tonge

Kwa aliyefatilia majibu ya waziri wa nishati na madini profesa Sospeter Muhongo leo bungeni akijibu hoja za kamati ya PAC atakubali kuwa kamati ya ZITTO KABWE imewadanganya watanzania. Muhongo ambaye amejibu hoja moja baada ya nyingine kwa kutoa ushahidi wa viambatanisho muhimu amedhihirishia bunge kuwa kamati ya bunge imetoa taarifa ya uongo. 

Katika majibu yake, profesa Muhongo amedhihirisha kwa ushahidi kuwa pesa za ESCROW hazikua za serikali. Pesa hizo ni za IPTL na kwamba serikali bado inadaiwa kiasi cha shilingi bilioni 94 na IPTL kama malipo ya kufua umeme. 
Aidha, Muhongo amemlipua mwanasheria Mkono ambaye aliingia mkataba na TANESCO wa kuwa mwanasheria wao na alidai na kulipwa kiasi cha bilioni 62 (robo ya pesa za ESCROW) kama malipo ya uanasheria. Mkataba huu ulivunjwa na TANESCO chini ya uongozi wa waziri Muhongo. 

Majibu haya ya Muhongo yameivua nguo kamati ya PAC na kuzua maswali mengi yasiyo na majibu. 
Kwanini PAC ilidanganya bunge? 
Kwanini PAC haikuonesha vielelezo hivyo? 
Nani yako nyuma ya PAC? 
Kwanini PAC haikutaja ufisadi huu wa Mkono? 
Taarifa kuwa wasaka Urais wa CCM ndio waliopika uongo huu tuziamini? 

Kwa muda sasa tangu sakata hili lianze, yako majina ya watu ambayo yamekua yakitajwa kuwa wana maslahi yao binafsi na sakata hili la escrow.
Hawa ni wafuatao:-

REGINALD MENGI:
Huyu alikua anatajwa kutaka kulipa kisasi cha ugomvi wake na Muhongo na Maswi kufuatia kunyimwa vitalu vya gesi na kutajwa na Muhongo kuwa ni dalali na si mfanyabiashara. Taarifa ya PAC imelitumia neno dalali sana, lakini si kwa Mengi safari hii. Bali kwa Prof Muhongo. Hatujui kama ndio kisasi cha Mengi au la. 

NIMROD MKONO:
Huyu ni mwanasheria maarufu ambaye aliingia mkataba wa kuwa mwanasheria wa TANESCO ambao ulivunjwa na Muhongo na katibu mkuu wake Maswi . Mkono hadi mkataba ulivunjwa alikua ameigharimu TANESCO kiasi cha bilioni 62, sawa na robo ya pesa za ESCROW. Akiwa nchini Uingereza Mkono alizusha uvumi wa kulishwa sumu, lakini mjumbe mwenzie wa kamati Halima Mdee alitilia shaka taarifa hiyo kwakuwa alikua na Mkono Uingereza. 
EDWARD LOWASSA :
Hawa walitajwa kuwa na mipango kwa wakati tofauti ya kumchafua waziri mkuu Pinda kila mmoja akilenga kupendekeza njia ya Urais. Lowassa anatajwa kumuona Membe kuwa si tishio (threat) tena katika mbio zake za u Rais. Badala yake anamtazama Pinda kama kikwako kikuu au mshindani mkuu kwa sasa. Lowassa anatajwa kutumia karata ya ESCROW ili kummaliza Pinda kisiasa kwa kumbana ajiuzulu. Katika kufanikisha haya, mpambe wa Lowassa ambaye pia ni mbunge Peter Serukamba anatajwa kusimamia bungeni mara kadhaa kutaka kamati teule iundwe kuchunguza sakata hili, kama karata ya kummaliza Pinda. Aidha Lowassa anatajwa kuwashawishi wabunge wa upinzani kwa mlungula ili waishabikie hoja hiyo. 

BERNARD MEMBE
Waziri huyu wa mambo ya nje yeye anaamini kuwa hadi miezi mitatu iliyopita kabla ya ujio wa Pinda kwenye mbio za urais, mpinzani wake mkubwa alikua mbunge wa Monduli na waziri mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa. Membe alibweteka akiamini kuwa Lowassa jina lake litakatwa na kamati kuu na lake kupita . Lakini baada ya ujio wa Pinda kwenye mchakato wa Urais, Membe alitikiswa sana. Akafikia hatua ya kulalamika kwenye magazeti juu ya harakati za Pinda. Alijua kuwa hesabu zake zimevurugika. Utafiti wa TWAWEZA ukamuumiza zaidi pale ulipoonesha kuwa Mizengo Pinda ndiye anayemfuatia Lowassa kwa karibu, huku Membe akizidiwa na Lipumba na Dr Slaa. Kama kawaida yake akalalamika kwenye vyombo vya habari. Karata pekee ambayo Membe aliiona ni kutumia ESCROW kummaliza Pinda na ikiwezekana kuiangusha serikali kwa maana ya baraza zima la mawaziri. Membe anaamini (sijui kama ni kweli) kuwa Jakaya anamtaka awe Rais baada yake. Hivyo kwa vyovyote angerudi kwenye nafasi yake. Katika kufanikisha hili, Membe anatajwa kuwatumia wabunge wa Upinzani kwa kuwashawishi na kuwahonga pesa kuipitia yeye Membe na wapambe wake. Wabunge hao walichukua pesa lakini walivujisha siri. Membe pia anadaiwa kuvujisha siri za sakata la ESCROW na kupika uongo kwa kupitia waandishi wa habari. Hapa anatajwa mwandishi wa gazeti moja la kiingereza (jina tunahifadhi) la hapa nchini. Pia Membe anatajwa kuwatumia marafiki zake wengine walioko ndani ya vyama vya Upinzani kuvujisha siri za vikao vya mienendo ya kujadili ESCROW. Baadhi yao ni vijana waliokuwa wanarusha mtandaoni habari hizo moja kwa moja wakati vikao vya CAUCUS YA CCM vikiendelea. Mmoja wa wapambe hawa anaeshukiwa ni Yeriko Nyerere ambae ni member mzuri wa jamii forums (rejea post za Yeriko Nyerere). 

Wananchi tulipuuza tukajua huu ni uongo, lakini leo hii baada ya majibu ya Muhongo tunashawishika kuamini kuwa ESCROW imetengenezwa na wachache kwa maslahi ya wachache huku wengi tukitumiwa kama daraja. Prof Muhongo kawaumbua PAC
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

-----------------------
Fratern Kilasara
,

P. O. Box - (Home): 62810; or (Office): 65300
Dar es Salaam - Tanzania.
Mobile (Personal): +255 (0)715 40 41 53 or +255 (0)754 40 41 53
Emails: kilasara.fratern@gmail.com or kilasara.fratern@yahoo.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment