Thursday, 1 November 2012

Re: [wanabidii] Nyerere hakuwa kitendawili - jibu

mh,bwana Matinyi,nakumbuka uliahidi kumjibu yule mwandishi..but siku imagine kama ungekuwa smart this way.thanks.Now,ni rahis kwa anayeutafuta ukweli kuupata.Cheers.Godfrey Ngupula.



------------------------------
On Thu, Nov 1, 2012 20:17 EET Mobhare Matinyi wrote:

>
>Jibu kwa aliyedai Nyerere alikuwa kitendawili
>Mobhare Matinyi, Washington DC Toleo la 266 31 Oct 2012 RAIA MWEMA
>NI kweli kwamba rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, si mtu rahisi kumwelewa hasa kama hukuwepo wakati akitawala, au ulikuwepo lakini hukumfuatilia au kama una mengine rohoni mwako.
>Inaweza kuwa vigumu kumwelewa pia iwapo unakumbana na watu wanaotaka kuiandika historia upya kama mwandishi wa makala iliyotangulia aliyedai kuwa Nyerere alikuwa kitendawili.
>Lakini basi, kwa vyovyote itakavyokuwa, hatuna budi kumchambua kwa kutumia ukweli na si porojo za alinacha. Wapo wasomi waliowahi kuonya kwamba ingawa kila mtu ana uhuru wa kuwa na maoni yake, lakini hakuna mwenye uhuru wa kuwa na ukweli wake yeye tu. Ndiyo, Nyerere kutokana na mengi aliyoyafanya, si rahisi kumwelezea kinagaubaga katika nafasi ndogo kama hii.
>Si kweli kwamba Watanzania eti wamekuwa wakishindwa kutafsiri yale yote aliyoyasimamia ingawa ni kweli kwamba yapo machache yaliyopindwa na viongozi waliokuja baadaye ama yaliyobadilishwa kama ilivyostahili. Mathalani kuuawa kwa Azimio la Arusha pamoja na maadili ya uongozi, kufutwa kwa mfumo wa chama kimoja huku yeye mwenye akiunga mkono, na kutetereka kwa Muungano kunachipukia kutoka kwenye makubwa aliyoyaasisi.
>Lakini kinyume na anavyodai mwandishi wa makala ile, Watanzania hawajashindwa kuelewa, mathalani, umuhimu wa kuishi kama Taifa na si kama mkusanyiko wa makabila yanayochukiana. Kadhalika, bado Watanzania wanapendelea kuishi bila kubaguana kidini ingawa viongozi wetu dhaifu hawalipendi hilo.
>Watanzania walizielewa falsafa zake na sera zake kwa kadri ilivyowezekana ingawa ipo moja iliyowauma, nayo ni Operesheni Vijiji vya Ujamaa. Wazo lilikuwa zuri ila utekelezaji ulikuwa mbaya. Lakini pia ni kukosa busara kudai kwamba tungeendelea kuishi vile vile kama nyumbu mbugani Serengeti.
>Ni uongo kudai kwamba hakuna anayekosoa mambo ya Nyerere wakati wanasiasa kama Edwin Mtei hufanya hivyo kwa heshima na wengine kama Christopher Mtikila hufanya kwa dhihaka. Watanzania wameandika kumkosoa Nyerere na sera zake, itikadi, falsafa na mengineyo nikiwemo miye binafsi lakini si lazima wawe wengi.
>Mtanzania Ludovick Mwijage anayeishi Udeni alipata kuandika kitabu chake mwaka 1994 huku Nyerere akiwa hai bado, "Dark Side of Nyerere's Legacy", yaani kwa kutumia lugha za wanajimu, "Upande Mweusi wa Urithi wa Nyerere". Mwaka 2008 alichapisha kingine, "Julius K. Nyerere: Servant of God or Untarnished Tyrant" akihoji iwapo Nyerere alikuwa mtumishi wa Mungu kweli au dikteta ambaye hakuchafuliwa.
>Lakini kuna ukweli mmoja kwenye kumwandika Nyerere; pale inapofikia kwenye kumlinganisha na viongozi wengine waliomfuatia au wengine barani Afrika. Hapo ndipo watu wanaposita kutokana na tofauti kubwa iliyopo kati yao. Profesa Anyang Nyong'o wa Kenya alisema mwaka 1999 kwamba Nyerere hakuwa na mwenzake miongoni mwa viongozi wa Afrika wakati Profesa Ali Mazrui alisema kwamba ingawa marehemu Rais Leopold Senghor wa Senegal alikuwa na akili, na Mzee Nelson Mandela wa Afrika Kusini alikuwa mwadilifu, lakini Nyerere alikusanya vyote viwili na hakuna aliyemfikia.
>Mwenyewe mwaka 1996 wakati akitunukiwa Tuzo ya Amani ya Kimataifa ya Mahatma Gandhi mjini New Delhi, India, alisema kwamba hakustahili kuipata kwa kuwa aliunga mkono harakati za ukombozi wa Afrika kwa kutumia bunduki. Hakupenda kujikweza na pengine ndiyo maana hakuandika wasifu wake, na hata mwanae aliwahi kuliambia Daily News kwamba kama baba yake angeulizwa kuhusu wazo la kumtafutia utakatifu angekataa.
>Kudai kwamba Nyerere aliwapumbaza Watanzania si sahihi ingawa ni kweli kwamba aliyashikilia mengi mwenyewe kutokana na hali yenyewe ilivyokuwa enzi hizo. Aidha, hapa Afrika hakuna aliyekuwa akiijua nadharia sahihi ya maendeleo viongozi walikuwa wakifanya majaribio ila wengi wao hakuwakufika mbali wakapinduliwa.
>Ni uongo wa dhahiri kudai kwamba Nyerere alistaafu mwaka 1985 kwa msaada wa masharti magumu ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF). Vyombo hivyo viwili viliivamia Tanzania baada ya Nyerere kuondoka madarakani na siku zote alivipinga. Ukweli ni kwamba Nyerere alishasema kwamba atastaafu tangu mwaka 1980 lakini mtikisiko wa Vita ya Kagera ukamfanya asogeze mbele uamuzi wake.
>Aidha, ushauri wa vyombo hivi vya kimataifa ulituingiza kwenye shida kubwa kuliko iliyokuwapo na takwimu zipo na ndicho Nyerere alichowauliza Benki ya Dunia siku moja mjini Washington na wakashindwa kumjibu. "Mlisema sisi tulishindwa, lakini ninyi mmefanya nini sasa?" Nyerere alisema watu wa Benki ya Dunia walibaki wameduwaa.
>Nyerere alipozungumza na waandishi wa kimataifa mjini London mwaka 1985 alisema kwamba anajiuzulu kwa kuwa Tanzania kuna uchaguzi, angependa kuona mtu mwingine anatawala na kwamba kama ameshindwa kuifanyia jambo nchi yake katika miaka 23 bado hataweza akipewa miaka mingine 23. Tulitaka nini zaidi ya uamuzi wake huu?
>Kwamba alikuwa mtoto wa chifu mmoja asiyejulikana kutoka madongo kuinama inasaidia nini kuhoji hivyo? Kwamba alikuwa mkristo aliyependa kuvaa baraghashia ya kiislamu, tatizo lake ni nini? Je, hiyo ni baraghashia ya kiislamu au kiarabu, au ndiyo yale yale ya kuchanganya Uarabu na Uislamu? Mbona Augustine Mrema naye huivaa?
>Kuhoji iwapo alikuwa mkomunisti aliyekuwa anakwenda kanisani na papo kudai kuwa aliungana na Zanzibar ili kuizuia isiingie kwenye ukomunisti ni kuchezea akili za watu. Kwamba eti huenda alikuwa muunganishi aliyetuachia Muungano wenye nyufa, je, nani kazuiwa kuziziba?
>Kwamba alikuwa mmajumui wa Afrika aliyekataa katakata kuanzishwa kwa serikali moja ya Afrika ni uzushi mwingine. Nyerere alisema kwamba kwa hali halisi ilivyokuwa haikuwa rahisi kuzilazimisha nchi zinazopata uhuru ziingie kwenye muungano wa Afrika kama alivyotaka Kwame Nkrumah wa Ghana. Alisema iwapo muungano utaanzia kwenye kanda itakuwa rahisi kuliko kuburuzana.
>Ni heri kwamba mwandishi amekiri kuwa Nyerere aliishi maisha ya kawaida, hakupendelea ndugu zake lakini ameshindwa kueleza upande wa pili wa faida za maamuzi yake aliyoyalaumu kama kufuta uchifu, serikali za mitaa, ushirika, vyama vya wafanyakazi na hata vyama pinzani vya siasa. Amelaumu utaifishaji wa mali binafsi, shule, hospitali na hatimaye na uanzishwaji wa vijiji vya ujamaa kwa mvurugano, kupiga marufuku maandamano na migomo na kuwasweka ndani wapinzani wake.
>Lakini hali ingekuwaje kama uchifu ungedumu na kelele za ukabila? Serikali za mitaa na ushirika vilirejea na kimsingi wafanyakazi walikuwa na chama chao ingawa kilikuwa chini ya chama tawala, lakini pia utaifishaji wa mali ulifanywa kwa minajiri gani kama siyo kumsaidia mnyonge?
>Ikumbukwe kuwa Waingereza hawakuacha kitu! Je, utaifishaji wa shule haukuwasaidia watoto wa Waislamu ambao waligomea shule za wamisionari wa kikrsto? Je, Watanzania masikini wangeweza kulipia gharama za matibabu kwenye hospitali za misheni bila serikali kutia mkono?
>Ndiyo, kulikuwa na sheria za kikandamizaji lakini ni vema kumlinganisha Nyerere na wenzake wengine kama Ahmed Sekou Toure aliyekuwa akiwaua wapinzani wake. Abdel Nasser aliyekuwa akiwaua waandamanaji. Nkrumah aliyekuwa kama mungu-mtu. Jaffery Nimeiry aliyegoma kuwasikiliza watu wake na kisha kuwaua. Jomo Kenyatta aliyeruhusu magazeti binafsi lakini akawatesa waandishi. Idi Amin aliyekuwa akiwaua watu eti baada ya kuota kwamba watampinga siku zijazo. Nyerere hakuwa mtakatifu lakini alikuwa na utu na hata pale alipotumia nguvu alifanya hivyo akiamini anailinda Tanzania.
>Madai kwamba nyaraka za Marekani zilizofunuliwa baada ya miaka mingi zinathibitisha kwamba Muungano wa Tanzania ulitokana na shinikizo la mataifa ya Magharibi ni utani mwingine. Mwaka 1966 Shirika Kuu la Intelijensia la Marekani (CIA), lilikamilisha utafiti juu ya Zanzibar katika juhudi za kuielewa na kujua Muungano ulikujaje. Mmoja wa watafiti alikuwa Helen-Louise Hunter ambaye baadaye aliandika muhtasari wa utafiti huo akisema kwamba Zanzibar haikuwa muhimu kwao. Hawakujua hata iliunganaje na Tanganyika.
>Mwandishi wa vitabu, Godfrey Mwakikagile, katika kitabu chake cha mwaka 2008, "The Union of

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment