Mijadala ya kidini ni migumu sana kujadiliwa katika kadamnasi. Hivyo lazima kuwa mwangalifu mtu kuleta mjadala huo. Ninauleta.
Mara chache mimi hupenda kusikiliza mahubiri zaidi ya yale ninayoyashiriki kule ninakosali. Lakini nayasikiliza. Napenda sana kusoma Biblia. Japo sijiiti mtaalamu lakini naisoma.
Mungu alipoumba mwanadamu alifanya tofauti na alipokuwa akiumba viumbe wengine.(Mwanzo 1: 24) inaonyesha kuwa alitamka na viumbe hao wakawepo. Lakini kwa mwanadamu alifinyanga udongo na kupuliza pumzi (Mwa 2: 7). Lakini pia Biblia inatuonyesha kuwa Mungu alimuumba mwanadamu kwa majukumu maalum (Mwa 1: 26-30).
Pamoja na makusudi hayo ya Mungu wanadamu walivuruga kazi ya Mungu na (Mungu) akajitenga nao.
Mungu alimtuma Yesu aje ampatanishe mwanadamu na Mungu wake. Naogopa kuvijaza vifungu vya Biblia lakini ninajua wasomaji wa Biblia hawana tatizo na hilo.
Tunajua kuwa toka mwanzo mwanadamu hukosana na Mungu wake kwa ushawishi wa shetani. Inaaminika kuwa shetani alikuwa mmoja kati ya malaika wakubwa ambao waliasi na kutimuliwa mbinguni; (Ezekiel 28 11-19). Kwa neno hilo ibilisi alikuwa na mamlaka makubwa sana. Kwa neno hili alikuwa akitembea nyimbo zinaimbwa. Akikutana na moto hapiti pembeni. Lakini bado akaamua kulingana na Mungu. Akanyang'anywa yote. Ndivyo shetani alivyomwingia mwanadamu kwa kumdanganya kuwa wala hawezi kufa bali atakuwa kama Mungu (Mwa 3: 4-5).
Yesu licha ya kuwa Mungu, lakini kwa jinsi alivyojishusha na kuwa Mwanadamu, baada ya kuzaliwa kama mimi na wewe alijishusha ili awe mahala stahiki. Mtu mmoja alipomjia na kumwita "mwema" yeye alijibu kuwa "mwema ni Mungu tu". Maana yake nini? Yesu anawaandaa wanadamu ambao atawakabidhi wajibu wa kuifanya kazi zote baada ya yeye kutoka ulimwenguni kumuwekea Mungu heshima ya kipekee na kamwe kutojiinua.
Petro licha ya kupewa mamlaka makubwa na Bwana Yesu lakini tunajifunza neno kubwa la kujishusha. Baada ya kumponya kiwete na waumini wenzake kumuona kama Mungu yeye anajiweka pembeni na kazi iliyofanywa na Yesu kwa kumtumia (Mdo 3: 11-16).
Mitume Paulo na Barnaba walikwenda kijiji cha Listra na kumponya kiwete. Watu wakawaona kama wao ni Mungu. Lakini kwa jinsi walivyomjua Mungu walikataa na kuhakikisha watu wanaelewa tofauti kati ya Mungu na wao.(Mdo 14:14-18). Lakini nakumbuka kusoma habari za mfalme mmoja aliyesifiwa na kuitwa Mungu, nay eye kukubali sifa hizo. Alipigwa na Mungu mpaka akafa, (Mdo 12: 20-23).
Siku hizi viongozi wetu wa dini wameacha kabisa kumhubiri Kristo na kuanza kujihubiri wenyewe. Utukufu wa Mungu wameubeba na kuufanya wa kwao. Neno linasema "Mwawezaje kuamini ninyi mnaopokeana utukufu ninyi kwa ninyi na utukufu ule utokao kwa Mungu aliye wa pekee hamuutafuti?" Yoh 5:44. Mchungaji anamtukuza mwinjilist. Askofu anamtukuza shemasi basi. Viongozi wetu badala ya kuwatafutia waumini njia ya kuwapeleka mbinguni (Galatia 5: 19-23) wao wanahubiri magari, majumba mashamba, watoto na mengine ambayo mtu akifa anayaacha.
Mimi binafsi namjua kuwa Yesu ni Katapila. Alizing'oa dhambi ndani mwangu akaniacha mtupu. Mimi ninajua kuwa Yesu ni transformer. Kila anayenijua kabla sijawa transformed na baada, ni shahidi kuwa Yesu ni transformer. Kamwe siwezi kumwambia aliyenihubiri kuwa ni Transformer au katapila. Mtu mwenye ufahamu wa Mungu wawezaje kukubali kuitwa majina kama hayo? Neno hili (Mdo 14:14-18) lilifutika kwenye biblia yako? Kwa nini uende jehanam mchana kweupe kwa sababu ya kutaka kusifiwa na wanadamu?
Sijatumwa. Lakini kama ukifikiri nimetumwa, basi amua nani kafanya hivyo? Kubwa jni hili: umefaidi nini?
Elisa Muhingo
0767 187 507
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment