SERIKALI IAINISHE HAYA MISAADA YA WAATHIRIKA WA TETEMEKO KAGERA
Na Happiness Katabazi
ITAKUMBUKWA Kuwa 10/9/2016 saa 9 Alasiri maeneo ya Kanda ya Ziwa na hasa MKoa wa Kagera yalipatwa na tetemeko la Ardhi linalokadiriwa Kuwa na ukubwa wa 5.9 Katika vipimo Vya Richter.
Tetemeko Hilo lilisababisha athari mbalimbali zikiwemo Vifo ,majeruhi,uharibifu wa makazi na miundombinu ya umma na watu binafsi . Jumla ya watu 17 wa lipoteza Maisha na 560 kujeruhiwa kutokana na maafa hayo.
Kwa siku Kadhaa sasa Kumekuwa na taarifa zikisambaa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya vyama Vya siasa Vya upinzani vimetoa matamko ya kupinga uamuzi wa Serikali kutumia Rasilimali zilizopatikana kwa michango ya kuwasaidia waathirika na kuendelea kuwarekebishia miundombinu muhimu kwa Maisha na manufaa ya wakazi wa Kagera.
Wanaopinga uamuzi huo wa serikali wengine wamediriki Kusema " serikali ya Rais John Magufuli imetafuna Fedha za Waathirika wa Tetemeko Kagera', ' serikali ya CCM imekula hela za Ubani' ,wengine wanasema serikali ingie tafuta Fedha zake zenyewe ndiyo ijengee miundombinu na siyo Kujenga miundombinu kwa kutumia Fedha za michango waliochangiwa waathirika wa tetemeko la Kagera.
Lakini Novemba 15 Mwaka huu ,serikali ilitoa tamko lake na kupinga Madai hayo na Kusema huo ni upotoshaji kuhusu Hatua zikizochukuliwa na zinazoendelea kuchukuliwa Katika kukabiliana na maafa hayo.
Serikali ikasema ukweli ni kwamba serikali kwa kushirikiana na wadau Imechukua Hatua kubwa za kuwasaidia waathirika na inaendelea kufanya Hivyo .
Ili kuleta uhalisia wa takwimu za Fedha ya maafa zilizotolewa kwa walengwa na wahisani mbalimbali,wananchi wangependa kupata data zifuatazo ili kuwaondoa wasiwasi ;
Jumla ya Majina ya watu 17 waliopokea Maisha pamoja na kutaja familia zao. Majina ya majeruhi 569 kwa kutaja kila kaya na Hospitali zilizotoa matibabu na tarehe waliopatiwa matibabu na aina gani ya matibabu. Gharama za Mazishi kwa Kila kilichochogharamiwa kwa watu 17.
Majina ya Wahanga waliyopewa Chakula kwa kutaja kiasi cha Chakula kwa kila Mhanga ,Madawa,nguo za aina gani na makazi yapi kwa kutaja kila Muhanga na kaya yake. Huduma za Tiba, Matunda aina gani na mangapi kwa kila mwathirika na vifaa gani na kwa kila shule na thamani.
Vyote Hivyo viwekwe Kwenye Tovuti ya serikali ili watu waone na wale wanaosambaza kile serikali inachoita ni upotoshaji waumbuke na hiyo ndiyo sifa Moja ya wapo ya serikali yoyote Duniani inayowajibika kwa uwazi.
Hata hivyo baadhi ya ndugu wa karibu wa marehemu niliyozungumza nao wamenitbitishia Kuwa kweli serikali ilitoa Sh.Milioni 1.8 kwa familia ya marehemu kama mkono wa pole .Ni jambo Jema.
Baadhi ya wananchi wangependa kufahamu tathimini ya maafa yaliyotokea ya
Yalifanywa Kwa watu gani ,majengo ya aina gani na kwa watu wa aina gani kama masikini ,wazee,matajiri,majeruhi .
Kwa mujibu wa taarifa ya serikali inaonyesha jumla ya Fedha taslimu iliyopo kelewa Katika Akaunti ya Benki ya Maafa ni Sh.5,412,984,934.82 na Sh 17,579,427.00 zilipo kelewa na serikali kwa njia ya mitandao ya simu.
Serikali ilisema imeishapokea misaada mingine yenye thamani ya Sh.bilioni 2.25 kama ifuatavyo : Unga Tani 58.12, Sukari Mifuko 1,150 , Mchele gani 133.96 ,Maharage Tani 19.666,mahindi Tani 70.1 na majani ya chai Tani 3.
Wananchi wangependa vilevile kupata orodha ya Majina waliyopatiwa vitu hivyo toka kila Wilaya ,Mkoa na Kaya na kiasia gani kwa kila mtu na vilevile wangetaka kujua kama kulikuwa na Tatizo la Maji Katika Mkoa wa Kagera hadi ukatolewa msaada wa Maji kwa walengwa.
Kuhusu miundo mbinu ya barabara Je ni barabara ngapi zimejengwa na Tenda ilifanyakazi lini gharama?gharama ya utengenezaji wa barabara ulifikiwaje na makandarasi na Wakandarasi wapi walipewa Kazi hiyo ?
Mifuko ya Saruji 2,300 yenye thamani ya Sh.39,000,000 iliyotolewa na Shirika la World Vision iligawiwa kwa akina nani Katika Kaya 460 zilizotajwa na kila mfuko uligharamia kiasia gani?
Wananchi wanataka kujua serikali ilivyokuwa ikiwaamasisha wachangie misaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi walioanisha Makundi ya watu Maskini ,wazee,wajane na walemavu? Au waathirika? Na tathimini ya kipato imefanyika lini?
Kama ndivyo Mbona serikali inapanga Kujenga Taasisi kwa kutumia Fedha za misaada badala ya kutumia Fedha za serikali?
Je serikali inawekwa katika kundi lipi Kati ya walemavu ,wajane na wazee au ni Maskini ?Kama ndivyo kwa nini msaada haukufikishwa kwa kila Muhanga?
Kama watu waathirika mtaji mkubwa ni nyumba zilizoharibika na hatakuwa na taarifa za Njaa kwa Sababu zilizoharibika ni nyumba za makazi na si Mazao
Kwa hayo machache baadhi ya wanachi tungependa kumjulishwa na kumfafanuliwa vizuri kuhusu jinsi gani misaada iliyotolewa ilivyogawiwa na Sababu ya kufanya msaada hiyo kugeuzwa Kujenga Taasisi za serikali wakati Taasisi hizo zinapaswa Kujengwa kwa Fedha za serikali.
Ikumbukwe Fedha hizi haziitaji Uhakiki kama Fedha za mikopo ya wanafunzi wa Elimu yaVyuo Vikuu ambazo Fedha za Bodi ya Mikopo zinataja vigezo wa wanufaika wa mikopo Kigezo Kimoja wapo ni watoto wa masikini .
Misaada na Fedha zilitolewa na makundi mbalimbali kwa waathirika wa Kagera zilitolewa kwa waathirika wote bila kubagua kundi lolote.
Mungu ibariki Tanzania
Chanzo:Facebook: Happy Katabazi
0716 774494
19/11/2016.
Sent from my iPad
0 comments:
Post a Comment