Tuesday, 8 November 2016

[wanabidii] LUMBESA NA SHERIA YA LUMBEZA: KERO NI NINI?

Tanzania imekuwa ikirekebisha sheria ambazo badala ya kuwahudumia na kwastawisha watanzania sheria hizo zimegeuka na kuwa kero. Mifano ya sheria hizo zilizokwisha rekebishwa, kuondolewa au zinaendelea kurekebishwa ni mingi. Zamani kulikuwa na sheria inayoruhusu mfanya kazi wa benki kumtoa mhindi au mzungu kwenye foreni benki. Walioitengeneza sheria hiyo waliamini wahindi na wazungu ndio walikuwa wanastahili kuwahi kazini/biashara maana walijulikana kazi zao zina maana kuliko "wengine". Sikui kama sheria hiyo ilifutwa au mazingira yaliiua.

Kuna shida kubwa inayowakuta wakulima. Wao huonewa na walanguzi. Walanguzi huwavizia wakulima wakati mgumu na kuwapunja bei ya mazao wakati wa mavuno au mara baadaa ya kupanda. Wakati wa kipindi cha mavuno mazao huwa mengi kuliko soko. Kwa hiyo walanguzi wanaringa maana wao ni wachache kuliko kiasi cha mazao yanayouzwa. Au kipindi wakulima wameweka kila kitu ardhini na ndipo watoto wanaenda shule au mahitaji mengine. Walanguzi huja na vifedha vidogo na kuwakopesha wakulima kwa dhamana ya mazao yaliyo shambani kabla ya wakati wa mavuno.

Ni wajibu wa serikali kuweka mazingira ambayo makundi haya hayataumizana. Moja kati ya njia ambayo serikali imeweka ni kuwa na vipimo sahihi. Mfano kila kinachoweza kupimwa kwa uzito basi mizani sahihi itumike. Au kimiminika nacho vipimo sahihi vitumike. Tanzania tumecha kutumiaa ratili badala yake tunatumia kilograms/Litre.

Kipimo hiki kimekuwa kikikwepwa na wafanya biashara wanapomwendea mkulima. Badala yake wanatumia bakuli (ndonya), Debe (Plastiki) na magunia. Walanguzi hao wanapenda kununua kwa ujazo huku wao wakiuza kwa uzito. Ujazo wenyewe unakuwa wa ajabu. Mfano debe moja unakuta limejazwa na ziada ya robo debe iko juu ya debe hilo. Ikifika wakati wa ujazo wa mifuko au magunia utakuta gunia limejazwa gunia moja na nusu. Tunaiita LUMBESA.

Serikali inakuja na suluhisho. Ikikutana na mlanguzi amejaza lumbesa inamkamata na kuna wakati tumeshuhudia vyombo vya habari vikituhabarisha habari za wafanyabiashara kutelekeza viazi baada ya kubanwa na "watetezi" wa wakulima-wakala wa mizani.
Mimi sioni kama kwa kufanya hivyo wamemsaidia yeyote. Huenda wanawaumiza wote. Na mkulima unapomzuilia kuuza mazao yake au kuwabughudhi wanaokuja kuyanunua hujamsaidia, bali umemuongezea uchungu baada ya kipindi cha kilimo.

Twaweza kutumia technologia badala ya mabavu.
Kama mkulima akiwekewa mazingira ya kuwa na mikopo hatakuwa na haraka ya kuuza mazao yake. Majuzi katika kipindi cha shamba shape-up niliona utaalamu unaoweza kutunza viazi kutoka wiki moja baada ya kuvunwa mpaka myezi mitano. Ni kwa kutumia mkaa bandani.
Lakini katika mazingira bora kama hayo mkulima anakuwa amepewa ujasiri wa kuongea na walanguzi kama mshirika badala ya kutegemea nguvu za polisi na wakala wa vipimo wakati ana njaa.
Lakini pia na walanguzi hao wakisha nunua viazi wanavisafirisha kwa ujazo. Wanatozwa kwa gunia. Ukiwa na gunia nyingi utalipa zaidi. Kumfanya mlanguzi huyo apime kilo 100 kwa gunia ni kumfanya awe na magunia mengi ya kulipia. Akisha yanunua kwa kilo kutoka kwa mkulima, ana dhambi gani kujaza milumbesa yake hivyo akasafirisha kwa bei nzuri na hivyo na mlaji akapunguziwa bei?

Kama bei ya kilo ya viazi ni sh. 1000, mfanya biashara kupakia kilo 130 kwenye gunia ana kosa gani ili mradi ananunua na kuuza kwa uzito au ujazo sahihi?
Mimi siamini kuwa watendaji wetu hawalioni hilo. Kweli woga wa hotuba za majukwaani ndizo zinawafanya wasitumie bongo?

Elisa Muhingo
0767 187 507

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment