Friday, 11 November 2016

Re: [wanabidii] Re: Mchakato wa katiba: Mwakyembe alinukuliwa sawasawa???

Muhingo kwa hili tuko wote. Tumetofautiana katika mengi hii hoja nakuunga mkono 100%
 
Jovin Bifabusha DIRECTOR KWFF LTD P. O. Box 313 Skype: jovin.bifabusha Karagwe, Tanzania +255 784 709200


On Thursday, November 10, 2016 11:10 PM, 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:


Majuzi Rais wetu aliposema Katiba haikuwahi kutajwa wakati wa kampeni ilitafsiriwa kuwa kwake Katiba sio kipaumbele. Sikukubaliana naye. Nitaandika makala kudhibitisha. Lakini mara nikakumbuka makala hii niliyoitoa siku hizo wakati Waziri wa Katiba aliponukuliwa akisema maneno kama hayo.
Nikaamua kusoma nilichokiandika ndiyo maana ipo hapa
--------------------------------------------
On Fri, 2/26/16, ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com> wrote:

Subject: Mchakato wa katiba: Mwakyembe alinukuliwa sawasawa???
To: wanabidii@googlegroups.com
Cc: "WANA BIDII" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Friday, February 26, 2016, 1:00 AM


Bahati mbaya mimi sikumsikia Dr Mwaakyembe akihojiwa na TBC aliposema Katiba si kipaumbnele cha Rais Magufuli. Nimepata habari hii kupitia Blog ya Udaku Special.
Katika Muhtasari   nilioupata kwenye blog ningetaka kujadili mambo matatu yaliyomo ndani ya maudhui mwandishi anayosema Dr Mwakyembe aliyasema. Nayo ni:
(1) Katiba mpya haina umuhimu mkubwa katika maisha ya kila siku ya watu.
(2) Katiba sio kipaumbele cha rais Magufuli
(3) Mchakato ukianza hautaanzia kwenye toleo la pili la Jaji Warioba

Hebu tuyajadili haya matatu:
1) Neno hili kuwa Katiba haina umuhimu katika maisha ya kila siku ya mwananchi mimi nadhani labda Dr. Mwakyembe
alinukuliwa vibaya. Neno hili halifanani naye. Tumekuwa na tatizo la matumizi makubwa kutokana na serikali kubwa kwa sababu Katiba inamruhusu rais kuunda baraza la mawaziri atakavyo. Katika Mswada wa Warioba rais alikusudiwa kubanwa mpaka mawazidi 18. Iweje Mwakyembe aseme eti katiba haina
umuhimu katika maisha ya mtanzania ya kila siku? Nimetaja moja tu lakini ni mengi. Yeye ni Waziri wa Sheria na katiba Kweli Magufuli anaweza kuunda wizara isiyo na maana na umuhimu katika maisha ya Mtanzania? Ingekuwa alitamka hivyo tuseme alikusudia kumwambia nini Rais aliyemteua na kuunda
wizara isiyo na maana kwa maishaa ya Mtanzania? Hakulisema yeye!

2) Katiba sio kipaumbele cha rais Magufuli
Nakubaliana na Mwakyembe kuwa kwa sasa Katiba sio Kipaumbele cha Rais. Lakini pia sio 'kipaunyuma'. Wakati Katiba sio kipaumbele cha Rais lakini kwa wizara ya Sheria na Katiba; Katiba ni kipaumbele. Baada ya Magufuli kurudisha nidhamu ya watendaji. Kuhakikisha uwajibikaji, kuhakikisha kodi zinaakusanywa na kutumiwa vizuri Wizara ya sheria na katiba itamletea Magufuli Katiba bora itakayolinda mafanikio yake baada yake. Siamini kuwa Mwakyembe anakusudia kuwa wizarani pale, halafu Rais wake afanye mema yote kwa myaka kumi tunayokusudia kumpa uongozi wa taifa hili, halafu
astaafu urais aingie mwingine avivuruge kwa sababu wizara ya Mwakyembe haikumsaidia Rais kuandaa Katiba itakayoyalinda mafanikia yake. Basi kama ndiyo maana ya Mwakyembe kuwa Katiba haina implication kwa maisha ya kila siku ya Mtanzania basi hapo wizarani kuna ombwe kutoliona hilo.

3) Mchakato ukianza hautaanzia kwenye toleo la pili la Jaji Warioba
Ikitokea mchakato wa Katiba ukianzia kwa kura ya maoni itakuwa ni kwa sababu rais hana mtu wa kumshauri katika wizara ya Sheria na Katiba. Katiba pendekezwa haiwezi kuyalinda mafanikio yanaayotarajiwa wakati wa uongozi wa Magufuli. Kama kuna kitu sitarajii Magufuli ashindwe ni kulipatia taifa hili katiba iliyoachwa na Bunge la Katiba na kufinyanga dudu. Itakuwa amefanya kazi bure kwa myaka yote atakayokuwa rais. Mkapa alilipa madeni nchi ikawa na hali nzurio ya kukopesheka. Baada yake nchi imevurundwa na sasa tunaona Magufuli anavyopata taabu kuirekebisha. Halafu naye aache nchi haaina Katiba itaakayolinda mafanikio aliyoyaancha? Na iwe hivyo wakati aliunda wizara ya Sheria na katiba? Na waziri aliapa mbele zetu kwa atamshauri vyema?
Wanaomkosoa Magufuli wanaposema ashughulikie mfumo watu wanaafikiri mfumo gani zaidi ya Katiba? Ukweli ni kuwa siamini kuwa  maneno haya aliyasema Mwakyembe. Naapa; hakuyasema.
Elisa Muhingo

 
  --
 
  Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
   
 
  Kujiondoa Tuma Email kwenda
 
  wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya
  kudhibitisha ukishatuma
 
   
 
  Disclaimer:
 
  Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
  for any legal consequences of his or her postings, and
hence
  statements and facts must be presented responsibly. Your
  continued membership signifies that you agree to this
  disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
 
  ---
 
  You received this message because you are subscribed to
the
  Google Groups "Wanabidii" group.
 
  To unsubscribe from this group and stop receiving emails
  from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
 
  For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment