Saturday 19 November 2016

Re: [wanabidii] Magufuli kasema yote: katiba mpya isubiri nchi inyooshwe

Uko sahihi Edgar, utekelezwaji wa katiba wakati mwingine inatakiwa kutumia nguvu kusukuma na kuwafanya watekelezaji wa katika katika ngazi mbalimbali kutokana na mazoea tuliojijengea kuwa hufanyi mpaka kwanza uone maslahi yako binafsi yanalindwaje (ruswa) na hiyo ndiyo imekuwa tabia kwa miaka mingi sana. Ili kutoka hapo kaka ndiyo ngoma hiyo hata kama ungekuwa ni wewe ni kazi kubwa. Huko nyuma ulikuwa ukiteuliwa posta yoyote ni ulaji na unapata pongezi nyingi sana.... Kweli muheshimiwa rais kazi anayo......

From: Edgar Mbegu <embegu@hotmail.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Saturday, November 19, 2016 3:18 PM
Subject: Re: [wanabidii] Magufuli kasema yote: katiba mpya isubiri nchi inyooshwe

Tusishabikie na ubabe wa ndani vile vile. Tusikubali nchi kuendeshwa kwa utashi wa mtu mmoja hata kama ana akili kiasi gani! Katiba iliyopo ifuatwe to the letter hata kama ni mbovu. Utawala wa sharia utamalaki kwa maslahi ya wote na siyo ya mtu au kikundi cha watu. 

Sent from Samsung tablet.

-------- Original message --------
From: 'Mashaka Makana' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Date: 19/11/2016 12:50 (GMT+03:00)
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Magufuli kasema yote: katiba mpya isubiri nchi inyooshwe

Watanzania tusishabikie ubabe wa nchi kigeni kuwa ndiyo suluhisho ya matatizo ya ndani ya nchi. Tunasiakia na kuona ya Libya na kule Iraq watu walishabikia wakidhani ingekuwa suluhisho ya tamaa ya mali na madaraka na kukubali kutumika na hawajapata chochote zaidi ya kuharibu miundombinu ya nchi yao na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Hii Demokrasia ya uchaguzi kila baada ya miaka mitano ukilinganisha na gharama za uchaguzi ni hasara tupu na matumizi mabaya ya pesa za umma, Wakati wa kampeni za uchaguzi raia hawafanyi kazi kungojea mikusanyiko ya kampeni. Je. ni hali ya namna hii na kwa nchi zenye utawala wa kifalme? Msaada hapo!

From: 'Lesian' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Saturday, November 19, 2016 11:39 AM
Subject: Re: [wanabidii] Magufuli kasema yote: katiba mpya isubiri nchi inyooshwe

Katiba iliopo ni'mbovu reuben.....inawapa watu mamlaka ya ajabu anateua hadi wajumbe wa nyumbakumi...hawa ma dcs wa n sasa kama si upotevu wa pesa......
Katiba iliopo ni nzr kwa watu kama kina reuben tu wqnaofagilia kila jambo ilmradi limesemwa na kusimamiwa na ccm
Hawanaga mawazo mbadala na hawatak,'na maana yake hawataki kuona mbele na trump kaja atawanyooshen subirin mnaokomaa madarakan navyma vyenu kaja komesha..teh teh

'Reuben Mwandumbya' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Mbegu;
Sio kwamba inji haina Katiba kabisa,itanyooshwa na katiba iliyopo.
Katiba iliyopo sio kwamba ni mbaya kabisa kwamba sawa na haipo, mabadiliko ya katiba yana sehemu chache za kuboresha na kuongeza.
Uhuni uliokuwepo/uliopo umetokana na kutofuata Katina, shaeria na kanuni zake i.e. lazier free
 
Reuben

On Thursday, November 17, 2016 7:42 PM, Edgar Mbegu <embegu@hotmail.com> wrote:

Nchi itanyooshwa kwa sheria zipi? Kwa utaratibu upi?  Kwa utashi wa mtu binafsi?  Ametumwa na nani?

Sent from Samsung tablet.

-------- Original message --------
From: 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Date: 17/11/2016 10:36 (GMT+03:00)
To: ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Subject: [wanabidii] Magufuli kasema yote: katiba mpya isubiri nchi inyooshwe

Serikali za Wanyama na ndege au Wadudu;

Ndani zina taadhima, kama kwamba maabudu;

Na watu wenye hekima, siku hizi hawamudu

Madaraka na heshima, heri mnyama na mdudu

Vinywa vimewaachama, tamu imekuwa ngwandu

Na heshima imehama baki taka na mashudu

Na madhara na dhuluma miungu ya kuabudu

(Shaaban Robert; katika "Kielelezo cha Fasili")

SHAABAN Robert katika shairi nililonukuu hapo juu, anaelezea madhara ya Uongozi na Viongozi wanapokosa maono, hekima na heshima kwa wananchi akisema, inapokuwa hivyo heri Serikali za Wanyama, Ndege au Wadudu zina taadhima kuliko za viongozi wenye kukithiri kwa dhuluma na kujigeuza miungu watu.

Japo gwiji hilo la ushairi Afrika Mashariki alikuwa akiandikia zama zake zaidi ya miaka 50 iliyopita ambapo fukuto la ufisadi, rushwa, kutoweka kwa uzalendo, uadilifu, maadili ya uongozi na ubinyaji wa demokrasia ilivyo sasa halikuwa jambo lililopevuka, lakini utabiri wake wa kinabii kwa yajayo hayo wakati huo ulikuwa sahihi na ndiyo yaliyoikaba koo nchi yetu hivi leo.

Ilivyo leo, na kama tunavyoambiwa na wataalamu wa siasa na sayansi ya jamii kwa ujumla, suluhisho la maovu haya ya kijamii ni kwa njia ya Katiba ya nchi itakiwayo na itokanayo na wananchi wahanga wa maovu hayo, kwa njia ya maoni na kura ya maoni.

Pengine ni kwa sababu hii miaka ya karibuni, na hasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015, kwamba suala la Katiba mpya lilikuwa ajenda moto, na zaidi kwa vyama vya upinzani vilivyodai kuwa Katiba iliyopo imepitwa na wakati kwa sababu iliandaliwa katika mazingira tofauti na ya sasa miaka 40 iliyopita.

Tangu mwanzo, Serikali, kupitia Mwanasheria wake Mkuu (AG) na mara nyingi pia kupitia waziri mwenye dhamana ya mambo ya Katiba na vigogo wengine wa chama tawala, ilitamka wazi kuwa, "Katiba mpya si ajenda ya serikali madarakani", tamko lililochukuliwa na wengi kama sawa na kujaribu kuzuia mafuriko kwa viganja vya mkono.

Hatimaye mwaka 2012, serikali ilisalimu amri kwa "mafuriko" hayo kwa kuteua Tume ya Kupendekeza "Rasimu ya Katiba", chini ya uenyekiti makini wa Jaji Joseph Sinde Warioba kwa matarajio kwamba Katiba hiyo mpya ingetumika kwa mara ya kwanza katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015.

Hadi kipindi hicho na mpaka sasa, nchi yetu ilikuwa na moja ya Katiba bora Afrika Mashariki – Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ambayo ukiondoa mapungufu machache kadhaa yaliyomo, likiwamo lile la harufu ya chama kimoja; madaraka makubwa ya Rais (Mhimili wa Utawala) dhidi ya mihimili mingine – Bunge na Mahakama na baadhi kuhusu Muungano, ilitosha na kwa utoshelevu mkubwa katika ujenzi wa demokrasia na utawala bora nchini.

Ni mwananchi gani mpenda demokrasia ya kweli bila kificho, anaweza kubeza ubora usio na mshindani wa Katiba hii kwa mambo muhimu inayotetea, kama vile, "malengo muhimu na misingi ya shughuli za serikali madarakani" (ibara 6 – 11); na "Haki ya Usawa na Wajibu wa Serikali kwa Raia" (ibara 12 – 30) ambayo Katiba za nchi nyingi hazina?.

Ibara hizi za Katiba zina umahiri wa pekee kutokana na ukweli kwamba zilitungwa na kupewa nguvu na msukumo enzi za utawala ulioweka mbele mambo kama vile uwajibikaji na maadili kwa viongozi; usawa wa binadamu na wa kijamii, utu na dhana nzima ya uchumi/utajiri wa nchi kuwa mikononi mwa wananchi kwa ajili ya na kwa manufaa ya wananchi wenyewe.

Kwa kuzingatia haya, nchi haikuhitaji, na bado haihitaji Katiba mpya kwa wakati huu, ila ipo haja isiyohojika ya kuifanyia marekebisho ya hapa na pale Katiba iliyopo kwa kuondoa ibara zinazopwaya au zinazokinzana (repugnant provisions) na mnyumbuliko wa demokrasia kwa mazingira ya sasa.

Serikali ya Awamu ya Nne ilitishika na kusalimu amri kwa "mungurumo" wa mbali wa kudai Katiba mpya bila sababu wakati ikijua ubora wa Katiba iliyopo, ila kwa sababu ya "uzembe" wake wa kuruhusu maovu ya kijamii tuliyoyataja kutamalaki.

Uzembe huo ulisababisha kujipaka matope na uchafu wa kila aina ama kwa kushiriki au kwa kunyamazia maovu hayo kufikia kile anachosema kila mara Rais wa awamu ya tano, John Pombe Joseph Magufuli (JPM), kwamba, "nchi iliendeshwa kihovyo hovyo tu kana kwamba hapakuwa na (viongozi) serikali".

Kazi kubwa na nzuri iliyofanywa na Tume ya Warioba kwa njia ya Rasimu ya Katiba ni kuboresha na kufafanua kwa fikra na "mantiki" pana zaidi ya yaliyo bora yaliyomo katika Katiba ya 1977 pamoja na namna ya utekelezaji kwa uthabiti, na kwa kuziba au kuondoa mapungufu tuliyokwishaelezea hapo mwanzo.

Ni Rasimu iliyohusisha "akili" bora za ainaaina zinazofahamika hapa nchini, zenye fikra za kimapinduzi, utu na usawa wa binadamu na wa kijamii na ambayo kama ingepita ilivyo, bila ya shaka yoyote ingetoa Katiba bora na ya aina yake kumfanya Mtanzania aishi bustani ya Edeni bila hofu wala mawaa, badala ya kuendelea kuishi kwenye "shamba la bibi" ilivyo sasa, kwa kila mtu kuishi kadri ya ukali wa meno yake kuweza kurarua na kupora kiharamia awezavyo, bila kujali wanyonge na mafukara wa nchi wa kufukarishwa na mfumo.

Rasimu hii ilikuwa tishio kwa maslahi ya mfumo wa kifisadi uliotaka kubakia na uliofanya nchi "kuendeshwa kihovyo hovyo tu kana kwamba hapakuwa na serikali".

Waingereza wana msemo, kwamba, "give a dog a bad name and it will be killed", yaani, "mpe mbwa jina baya na atauawa". Haraka haraka mafisadi wa nchini na wa kimataifa walivuta pumzi kukusanya nguvu kuiangamiza rasimu hii kwa kuipa tume na baadhi ya wajumbe wake majina mabaya mabaya ionekane ya "majahili" na rasimu hiyo kuwa haifai.

Kanuni na taratibu za kutunga Katiba zikapindwa bungeni kuhakikisha kwamba inanyumbulishwa na kusukwasukwa mithili ya meli ndani ya tufani na kupoteza mwelekeo wa Katiba iliyokusudiwa.

Kisha, kwa matumizi ya hoja za nguvu; ubaguzi wa kiitikadi wa kubumba; ushawishi wa kilaghai na matumizi ya pesa chafu kwa kushirikisha ubepari wa ndani na wa kimataifa, tabaka hili la kifisadi lililewesha bangi sehemu kubwa ya Bunge Maalum la Katiba kiasi cha kupanua midomo na kulishwa kila aina ya "mvinyo", vinywa vimewaachama mithili ya makinda ya ndege, huku likijipa bila uhalali wa kisheria, mamlaka ya kuandika lenyewe "Katiba Inayopendekezwa" kwa kutupilia mbali sehemu kubwa ya maoni ya wananchi.

Matokeo ya ubabe huu yalikuwa ni pamoja na kunyofolewa kwa sehemu kubwa, misingi ya usawa wa kijamii, tunu za taifa, maadili ya taifa, usimamizi wa rasilimali za taifa kwa manufaa ya wananchi wote na uwajibikaji wa viongozi ili kusimika kile kinachoweza kuitwa "jamii ya kitabaka".

Baada ya kunyofolewa kwa sehemu kubwa mengi mema kwenye Rasimu ya Tume ya Warioba, "Katiba Inayopendekezwa" ya wababe wa ufisadi na mawakala wa ukoloni mamboleo, si tu kwamba iliweka rehani demokrasia na uhuru wa nchi na raia kwa ubeberu mpya, bali pia inasaliti yaliyo mema katika Katiba ya sasa ya mwaka 1977 kuturejesha "utumwani" kwa Farao, Misri.

Pengine, na huenda JPM aliyaona mapema haya kiasi cha kupata ujasiri wa kuhoji kwenye mkutano wake na wahariri wa vyombo vya habari nchini hivi karibuni akisema, "Je, mliwahi kunisikia wakati wa kampeni zangu nikitaja lolote juu ya Katiba?".

Maadam wababe wa ufisadi bado wana ushawishi mkubwa wa kilaghai juu ya mkondo wa Katiba nchini kwa kushirikiana na vigogo wengi ambao bado wapo ndani ya mfumo wa serikali, mwendelezo wowote wa "Katiba Inayopendekezwa" hauna maana tena kwa sababu utaipeleka nchi pabaya kwa matakwa ya wababe hao.

Acha muda upite kwa jambo hili, hadi umma utakapofunguka macho kuona uchafu uliokuwa ukilishwa ili kuchangamkia mchezo huo wa kifo. Na maadam sehemu kubwa ya Katiba iliyopo ina mengi mazuri ila kwa sababu tu ilibezwa kwa maslahi ya kitabaka; JPM hana sababu ya kukosa usingizi juu ya "mwongozo" wa kufanyia kazi ila kwa kuzingatia na kuheshimu mema yaliyomo.

Wananchi (mimi nikiwa mmoja wao) baada ya kuona kuwa maovu ya kijamii yanavuma na kunyamaziwa wakati Katiba iliyopo ikivunjwa bila hofu kwa wavunjaji kuwajibishwa, walifikia kutamani kuwa na kiongozi "kichaa" kidogo, dikteta mwema (benevolent dictator) ainyooshe kwanza nchi japo kwa awamu moja tu kwa kuwashikisha adabu wote wenye kuchezea demokrasia, uhuru na haki za raia, hata kama ni kwa "kuweka pembeni" kidogo baadhi ya vifungu vya Katiba nzuri iliyopo.

Tangu mwanzo, serikali haikuwa na nia njema na suala la Katiba mpya ila kuziba ombwe la uongozi kwa njia hiyo kufuatia kutamalaki kwa ufisadi, rushwa na demokrasia duni na hivyo kuelekea kuipa nguvu kambi ya upinzani dhidi ya serikali iliyokwenda likizo kuchapa usingizi.

Ni wazi pasingekuwa na hoja ya upinzani juu ya maovu haya kama uongozi ungetekeleza wajibu wake vyema kwa kuongozwa na Katiba iliyopo, na hivyo pia pasingezuka hoja ya Katiba mpya.

Ndiyo maana, baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kuingia madarakani na kujitoa mhanga kupambana na maovu haya, kambi ya upinzani imeishiwa hoja na madai ya Katiba mpya kukosa mantiki. Hebu angalia mifano hii kuona ilivyokuwa.

Ukiona serikali madarakani inaatamia kwa mbawa zake maovu yenye kuhujumu nchi, kupora au kuibia serikali mapato na kuwakingia kifua wafanyabiashara wahujumu wa uchumi, wakishirikiana na wanasiasa ili wasiguswe; hapo elewa kwamba, serikali hiyo imejiweka rehani kwa wenye fedha, mafisadi na maharamia wa uchumi wa nchi.

Ukiona kuibuka kwa tabaka la wafanyabiashara kuchangamkia nafasi za uongozi wa chama na serikali kwa udi na uvumba na kwa kupenyeza nguvu ya fedha kupata uongozi, fahamu kwamba demokrasia, utawala bora na utawala wa sheria unayoyoma na kukaribisha utajiri (fedha) kununua madaraka na uongozi, na uongozi kuwa sehemu ya kundi la kimafia la kupora utajiri wa nchi, hata kama nchi itakuwa na katiba bora kupita zote duniani.

Chini ya awamu hii, yaonesha kama vile JPM anawaambia viongozi wa aina hii, wauze kwanza vyote walivyo navyo na kisha wamfuate katika kuutafuta ufalme wa kisiasa, kwa maana hawawezi kutumikia mabwana wawili kwa pamoja, yaani watu na mali.

Nakwambia, subiri uchaguzi mkuu ujao (2020) uone; zaidi ya nusu kati yao hawatachukua fomu, maana walizoea vya kunyonga na sasa vya kuchinja hawaviwezi. Hapo, iko wapi hoja ya Katiba mpya?.

Ukiona uchumi wa nchi unahama mikononi mwa wananchi kwenda mikononi mwa wajanja wachache; rasilimali za taifa kuporwa na "wawekezaji" wa kigeni bila hofu kwa kushirikiana na mawakala wao wa ndani; elewa kwamba nchi iko hatarini kugeuzwa "shamba la bibi", kwa kila mtu kurarua na kupora kadri ya ukali wa meno yake.

Ukiona viongozi wa kitaifa wakiutangazia umma kwa ulaghai kwamba uchumi wa taifa unapaa wakati wananchi wakizidi kufukarika kuliko mwanzo, na eti kwamba wasiokubaliana na uongo huo ni "wavivu wa kufikiri" au wapinzani wa chama na serikali; fahamu kwamba hizo ni dalili za serikali kujiweka mbali na wananchi wake na kuwa "mwenye shibe (viongozi) hamjui mwenye njaa".

Ukiona serikali inapuuza maoni ya wananchi na kusikiliza ya wenye pesa na wenye madaraka; elewa kwamba serikali hiyo imelewa madaraka; itanyanyasa vyombo vya habari na wanahabari kwa changamoto zao za "kuuamsha umma".

Lakini ilivyo leo, mambo yanaonekana kugeuka, kwamba kiongozi wa awamu ya tano (JPM), anaonekana kuongozwa na kauli mbiu na hekima ya Rais, mwanademokrasia wa zamani wa Marekani, Abraham Lincoln, kwamba "Kwa kuungwa mkono na umma (si na mafisadi na majambazi ya kisiasa) naweza kufanya jambo lolote; lakini bila hivyo na mbele ya upinzani wa umma, siwezi kufanya lolote".

Kauli mbiu hii inakidhi ule msemo wa Kilatini "Vox Populi, Vox Dei", yaani, "Sauti ya Wengi ni Sauti ya Mungu". Pengine ni kwa sababu hii, kwamba JPM mara nyingi hachoki kuwaomba wananchi wamwombee kwa Mungu amlinde katika harakati hizi. Kwa nini?.

Hapa tena, Shabaan Robert anaonekana kumpa sala JPM kwa shairi "NILINDE", linapokuja suala la kutetea na kulinda maslahi ya taifa katikati ya ufisadi uliotamalaki. Kwenye shairi hilo, Shaaban Robert anasema:

"Ni weledi wa kusema, watu wa leo

Na elimu na hekima, si haba kwao

Bali hawana huruma, katika moyo

Na fahari (kwa taifa) na heshima

ni chache kwao tamthili ya wanyama,

mfano wao kisha waweza kuuma, sumu wanayo

E Mungu mwenye uzima, nilinde nao".

Na tumuombee sote kwa Mungu afanikishe vita hii bila hoja ya Katiba mpya.

Raia mwema
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment