Rais "mtalii" kichomi, msaliti muuza uhuru wa nchi
UKIKUTA kiongozi wa nchi anapenda kurandaranda kwenye miji mikuu ya mataifa ya ughaibuni, fahamu kwamba mtawala huyo hana ajenda ya maendeleo kwa wananchi wake, maana kwake sera za kimataifa ndilo liwazo lake, badala ya ustawi wa taifa kwa mikono yake.
Hapendi kusikia kilio cha "wasio nacho", siku zote ana mzio (allergy) na jasho la wadunda kazi wa nchi yake, wenye kupanda bila kuvuna, kuwekeza jasho lao pasipo kupata kutokana na mfumo katili wa uchumi. Bali yeye huvutiwa na manukato ya ughaibuni, akaziba masikio kwa waliao nyumbani akiwaita "wavivu wa kufikiri", na eti waliolaaniwa kwa ufukara wa kutengenezewa.
Ukiondoa Serikali za Awamu ya Kwanza chini ya Mwalimu Julius
Nyerere, na ya pili chini ya Rais Ali Hassan Mwinyi, Serikali za
Awamu mbili zilizofuata ziliongozwa na marais "watalii" "kiguu na njia", wenye mitizamo ya "majuu" badala ya matatizo ya nchi, huku wakikaribisha nyang'au wa kimataifa kushambulia na kupora uchumi wa nchi kwa dhana potofu ya uwekezaji (usiojali) na uhusiano wa kimataifa.
Na hili la utamaduni ulioanza kujengeka, wa kuchagua kiongozi wa nchi kutokana na Mawaziri wa Mambo ya Nje, imeonesha dhahiri kwamba viongozi wa sampuli hiyo siku zote akili yao iko nje ya nchi zaidi kuliko kuwa ndani ya nchi na kwa wananchi wao.
Hawana muda na raia; ziara zao vijijini hufanana na za "flying doctors" – madaktari chonjo; misafara yao yenye ulinzi mkubwa, huenda kasi ya radi wasipate fursa ya kuongea na wanaowaongoza njiani, wakihofia "usalama" wao katikati ya wananchi wanaodai kuwaongoza, wakati hizo ni mbwembwe na makeke yenye gharama kubwa kwa wananchi na uchumi wa nchi.
Mbona Mwalimu Nyerere, alichanganyika kirahisi na wananchi shambani, akiwafundisha kilimo bora na bado hakudhurika?.
Mbona Rais John Pombe Magufuli leo anaweza kusimama njiani akahutubia wananchi bila hofu ya usalama?.
Ni serikali hizi mbili za mwisho (Awamu ya Tatu na Awamu ya Nne) zilizouza uchumi wa nchi kwa pamoja na kuua uzalendo, maadili na utamaduni wa taifa kwa kasi ya kutisha kwa ubepari wa kimataifa chini ya utandawazi (utandawizi) usiodhibitiwa wala kuratibiwa.
Ni awamu hizi mbili zilizoiingiza nchi katika mikataba hatari ya kimataifa kiwango cha kukaribisha ukoloni nchini kwa mshangao wa nchi nyingi za kiafrika, kama tutakavyoona hivi punde katika makala haya.
Wale wanaojaribu kumtupia madongo, Rais John Pombe Magufuli kwa kutogeuka "mtalii" ili aanze kurandaranda nje ya nchi akitumbua jasho la watu wake, badala ya kuumia nao pamoja katika "kutumbua majipu" waliyotuletea, wanatumika na ubeberu kutaka kumwondoa kipenzi huyu wa watu kwenye reli ya ukombozi wetu; na hao wakafie mbali.
Raia Mwema
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment