Ndugu zangu,
Tarafa ya Pawaga na vijiji vyake kadhaa mkoani Iringa imeathiriwa na mafuriko makubwa.
Wananchi takribani mia tatu wakiwamo wanawake na watoto wamepoteza kijiji chao na mali zao. Hawana walichobaki nacho.
Taarifa zilizopo ni kuwa hali za wahanga wa mafuriko kule Pawaga bado ni mbaya. Kumekuwepo na magonjwa ya milipuko, watu kukosa chakula na hata nguo za kujisitiri.
Kwa nafasi yangu ya Uwenyekiti wa Jukwaa la Kwanza Jamii na kwa kupitia mtandao huu wa Mjengwablog.com na kipindi cha ' Nyumbani Na Diaspora kinachorushwa TBC1, tunahimiza Watanzania popote walipo, na wenye utayari na hiyari ya kuwachangia ndugu zao wa Pawaga kwa hali na mali, wafanye hivyo.
Michango yenu itaorodheshwa hapa na kwenye mtandao wamjengwablog.com kwa majina na kwa wasiotaka kuandikwa majina yao itafahamika hivyo pia.
Jumamosi ya Februari 20 nitasafiri kwenda eneo la tukio Pawaga na kuwakilisha kwa walengwa kitakachopatikana kutokana na michango yenu.
Tuma mchango wako kwa M-Pesa 0754 678 252, Tigo-Pesa 0715 900 717
Jina litakalosomeka ni Maggid Mjengwa. Kwa walio nje ya Tanzania mnaweza kutuma kwa Western Union, jina Maggid Mjengwa, Box 2414, Iringa. Michango yenu itaendelea kupokelewa hadi Februari 26.
Tukumbushane Harambee tulizozifanya kwa mafanikio huko nyuma:
Kwa pamoja, tulifanikisha kukusanya michango ya watoto wa Somalia na kuikabidhi UNICEF, Dar es Salaam. Ni zaidi ya shilingi milioni mbili.
-Tulifanikisha mchango wa kusaidia ukarabati wa maktaba ya Kijamii kijijini Mahango, Madibira. Zaidi ya shilingi milioni nne.
-Tulifanikisha kumchangia Mjane wa mwanahabari Daud Mwangosi. Takribani shilingi milioni tisa zilipatikana.
Michango yote hiyo ilikabidhiwa kwa walengwa kwa vithibitisho.
Ni wakati sasa kuwachangia ndugu zetu wa Pawaga.
Maggid Mjengwa,
Iringa.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment